Yametimia - Serikali legelege sasa ni maradhi ya degedege | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Yametimia - Serikali legelege sasa ni maradhi ya degedege

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Jul 21, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Jul 21, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kashfa kubwa ya kuibuliwa kwa rushwa bungeni inayomhusu Katibu Mkuu wa Serikali Jairo, pamoja na wabunge wa CCM kuifichua na kumtaka aachie ngazi jambo ambalo limesababisha hata makadirio ya wizara hiyo kutokukubaliwa na kuwekwa kwapani na serikali hadi baada ya wiki tatu ili ifanyiwe marekebisho, ni jambo ambalo litaigharibu serikali baadaye na Chama Cha CCM.

  Pamoja na Waziri Mkuu kuguswa sana na jambo hilo na kumweleza Rais juu ya matukio yaliyoko sasa Dodoma, kauli ya Rais kwamba jambo hilo lisubiri yeye hadi atakapomaliza ziara yake ndipo aje aone afanye nini si kauli yenye uzito stahiki kwa kiongozi wa nchi kwa kiwango cha jambo lililopo.

  Kikwete kwake umuhimu ni safari zake lakini matatizo ya taifa ni jambo la ziada ambalo halina usito stahiki. Je hii ni dharau kwa wananchi waliomchagua au ni serikali kupata ugonjwa wa degedege?

  Kwa hali ilivyo namwunga mkono Mbunge wa Nzega Dr. Kingwangala kwamba serikali hii ni legelege.
   
 2. fikramakini

  fikramakini JF-Expert Member

  #2
  Jul 21, 2011
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 247
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Utata upo kwenye hiyo red. Hii si dharau bali ni adhabu kwa wananchi ambao hawakumchagua maana matokeo ya uchaguzi yalichakachuliwa ...
   
Loading...