YAMETIMIA! Nini Hatma ya wagombea Urais wa CHADEMA?

Sadoseba

JF-Expert Member
Feb 17, 2013
243
91
Hata Yona alikuwa nabii. Alitabiri kuangamizwa
kwa Ninawi ila unabii wake ulibadilika.

Mambo yote yatapita lakini neno litasimama.

KUTOKA 18 :21
21 Zaidi ya hayo utajipatia katika watu hawa
watu walio na uwezo, wenye kumcha
Mungu, watu wa kweli, wenye kuchukia
mapato ya udhalimu (rushwa); ukawaweka juu
yao,
wawe wakuu wa maelfu, na wakuu wa mia,
na wakuu wa hamsini, na wakuu wa kumi;


Yeremiah 23:-
16 Bwana wa majeshi asema hivi, Msisikilize
maneno ya manabii wakiwatabiria;
huwafundisha ubatili; hunena maono ya
mioyo yao wenyewe; hayakutoka katika
kinywa cha Bwana.

31 Tazama, mimi ni juu ya manabii, asema
Bwana, wanaotumia ndimi zao na kusema,
Yeye asema,
32 Tazama, mimi ni juu ya hao wanaotabiri
ndoto za uongo, asema Bwana, na kuzisema,
na kuwakosesha watu wangu kwa uongo
wao, na kwa majivuno yao ya upuzi, lakini
mimi sikuwatuma, wala sikuwapa amri; wala
hawatawafaidia watu hawa hata kidogo,
asema Bwana.

KUTOKA 18 :-
21 Zaidi ya hayo utajipatia katika watu hawa
watu walio na uwezo, wenye kumcha
Mungu, watu wa kweli, wenye kuchukia
mapato ya udhalimu (rushwa); ukawaweka juu
yao,
wawe wakuu wa maelfu, na wakuu wa mia,
na wakuu wa hamsini, na wakuu wa kumi;

MAWAZO YA MUNGU SI YA MWANADAMU

#HAPA KAZI TU!
 
Hahaaa kuelimisha umma nayo kazi. Ni kuwapa maarifa wasio na ufahamu . Sawa na ualimu = Kazi.
# Hapa kazi tu!!
 
Hata Yona alikuwa nabii. Alitabiri kuangamizwa
kwa Ninawi ila unabii wake ulibadilika.

Mambo yote yatapita lakini neno litasimama.

KUTOKA 18 :21
21 Zaidi ya hayo utajipatia katika watu hawa
watu walio na uwezo, wenye kumcha
Mungu, watu wa kweli, wenye kuchukia
mapato ya udhalimu (rushwa); ukawaweka juu
yao,
wawe wakuu wa maelfu, na wakuu wa mia,
na wakuu wa hamsini, na wakuu wa kumi;


Yeremiah 23:-
16 Bwana wa majeshi asema hivi, Msisikilize
maneno ya manabii wakiwatabiria;
huwafundisha ubatili; hunena maono ya
mioyo yao wenyewe; hayakutoka katika
kinywa cha Bwana.

31 Tazama, mimi ni juu ya manabii, asema
Bwana, wanaotumia ndimi zao na kusema,
Yeye asema,
32 Tazama, mimi ni juu ya hao wanaotabiri
ndoto za uongo, asema Bwana, na kuzisema,
na kuwakosesha watu wangu kwa uongo
wao, na kwa majivuno yao ya upuzi, lakini
mimi sikuwatuma, wala sikuwapa amri; wala
hawatawafaidia watu hawa hata kidogo,
asema Bwana.

KUTOKA 18 :-
21 Zaidi ya hayo utajipatia katika watu hawa
watu walio na uwezo, wenye kumcha
Mungu, watu wa kweli, wenye kuchukia
mapato ya udhalimu (rushwa); ukawaweka juu
yao,
wawe wakuu wa maelfu, na wakuu wa mia,
na wakuu wa hamsini, na wakuu wa kumi;

MAWAZO YA MUNGU SI YA MWANADAMU

#HAPA KAZI TU!

Kumbe kuhangaika kote huku, ulitaka kusema HAPA KAZI TU?
 
Una uhakika ushindi wa ccm hauna hila na ubatili? Kama unaongelea haki hakikisha haki imetendeka pande zote mbili. Vinginevyo na wewe utakua unalitumia vibaya neno.
 
Ni kweli hapa kazi tu na kazi ndo imeshaanza, mamabo yako mahakama za kimataifa kwa kuwa tumejifunga midomo na kitanzi katika mahakama zetu za ndani, sasa kazi tu pale uholanzi tukiongozwa na mawakili wetu wazalendo wa Chadema, haki ikitendaka slogani iwe kazi tu kuchomoka na kupisha wale wenye ridhaa ya watanzania nakubaliana na wewe sasa ni kazi tu na ishaanza kule Uholanzi
 
Una uhakika ushindi wa ccm hauna hila na ubatili? Kama unaongelea haki hakikisha haki imetendeka pande zote mbili. Vinginevyo na wewe utakua unalitumia vibaya neno.

Farao aliwafanyia hila wana wa Israel., hazikufanikiwa coz ulikuwa mpango wa Mungu watoke Misri. Kwa nn aziruhusu Tanzania?
# MUNGU SI KIGEUGEU & NENO LAKE LITASIMAMA!
 
Farao aliwafanyia hila wana wa Israel., hazikufanikiwa coz ulikuwa mpango wa Mungu watoke Misri. Kwa nn aziruhusu Tanzania?
# MUNGU SI KIGEUGEU & NENO LAKE LITASIMAMA!

Kumbe hata hauelewi unachojaribu kukisema. Wakati mwingine jaribu kutenganisha mawazo/hisia zako na neno la Mungu.
Nimekuuliza haki unaijua? Na imetendeka haki kwa pande zote? Unakuja na hadithi nyingine.
 
mijitu imekwiba kura afu inamdhihaki Mwenyezi Mungu kupitia biblia takatifu!!

alaniwe mtu yule alitumie neno la Mungu wa ibrahim, isaka na yakobo kuhalalisha uovu na dhuluma!!!

Tazama utawala huu wa Pombe utaparaganyika tu kwakuwa haukuingia madarakani kwa haki!!!
 
Shalom mkuu, unaonekana una idea kitu kizuri tatizo ni namna ya kutuwasilishia. Muktadha wa topic yako hauendani. Ndiyo, Yona alikuwa nabii & unabii ule haukutoka kwake ila kwa Mungu Mwenyewe. Je! Unafahamu kwa nini Mungu aliubatilisha ubabii aliompa Yona? Je! Unafahamu kwa nini Yona Alikasirika baada ya Mungu kuubatilisha unabii ule?

Turudi, tujenge msingi;

Maandiko yanasema neno la BWANA likamjia Yona;

"Ondoka, uende Ninawi, mji ule mkubwa; ukaihubiri habari nitakayokuamuru (Uovu wao umefika juu)" - Yona 3:2

Angalia alichohubiri Yona;

"Ni nani ajuaye kwamba Mungu HATAGEUKA na KUGHAIRI, na kuiacha hasira yake kali, ili msiangamizwe?"- Yona 3:9, na ndicho alichofanya Mungu, alighairi kuwaangamiza watu wa Ninawibkwa sababu walitubu na kuacha njia zao mbaya. Hii ndiyo dhima kuu ya unabii, kugeuza mioyo ya waovu kumuelekea Mungu. Unabii hutolewa tu kwa faida ya watu, katika kulijenga kanisa au Taifa na siyo kwa faida ya mtu binafsi.

Turudi Nyuma zaidi;

Katika siku za nabii Eliya, kuliibuka kundi la watu waliojulikana kama "Wana wa manabii." Watu hawa walizunguka sehemu mbalimbali za dunia wakipambana na nguvu za giza, na kuzivunja falme zilizojaa uovu. Hawakuweza kuvumilia tabia za uharibifu za wafalme waovu, lakini waliwabadilisha wengi kwa kuwaletea haki. Walifufua wafu, kuponya wagonjwa, kugawanya mito, kuharibu manabii wa uongo, na kuleta uhuisho/urejesho/uamsho kwenye maeneo hayo. Waliogopwa na wengi na Kuheshimiwa na wote. Walitembea katika njia ya usafi; na Mungu alikuwa rafiki yao.

Katika siku za Musa, Mungu alidhihirisha nguvu zake kwa Farao, lakini Farao alizipinga nguvu za Mungu kwa kujaribu kutumia wachawi na wapiga ramli. Ndipo, Mungu wa Mbinguni, aliye na nguvu zote, alifanya miujiza ya kustaajabisha hata wale wachawi na waganga wa Farao wakasema, "Huyu atakuwa Mungu. Hatuwezi kufanya miujiza ya namna hii." Na Farao akashindwa na kuwaachia huru wana wa Israeli (Kutoka 7-12).

KARAMA YA UNABII :

Karama ya unabii ni moja ya karama tisa/9 za Roho Mtakatifu:

"4 Basi pana tofauti za karama; bali Roho ni yeye yule. 8 Maana mtu mmoja kwa Roho apewa neno la hekima; na mwingine neno la maarifa, apendavyo Roho yeye yule; 9 mwingine imani katika Roho yeye yule; na mwingine karama za kuponya katika Roho yule mmoja; 10 na mwingine matendo ya miujiza; na mwingine UNABII; na mwingine kupambanua roho; mwingine aina za lugha; na mwingine tafsiri za lugha; 11 lakini kazi hizi zote huzitenda Roho huyo mmoja, yeye yule, akimgawia kila mtu peke yake kama apendavyo yeye." - 1 Wakorintho 12:4-11

Mungu anatuomba tuzitake karama za Rohoni;

"1 Ufuateni upendo, na kutaka sana karama za rohoni, lakini zaidi kwamba mpate kuhutubu (Unabii). 2 Maana yeye anenaye kwa lugha, hasemi na watu, bali husema na Mungu; maana hakuna asikiaye; lakini anena mambo ya siri katika roho yake. 3 Bali yeye ahutubuye (atoaye unabii), asema na watu maneno ya kuwajenga, na kuwafariji, na kuwatia moyo." - 1 Wakorintho 14:1-3

Kwa hiyo unabii ni karama inayoweza kutakiwa/ kuombwa na mtu kwa Mungu. Lengo la karama ya unabii sio "kukosoa mwili wa Kristo" bali ni kulitia moyo kanisa/Taifa na kulijenga;


MAANA YA UNABII:

1. Kujua kuhusu wakati ujao.

"Na tulipokusanyika akasimama mmoja wao, jina lake Agabo, akaonyesha kwa uweza wa Roho Mtakatifu kwamba njaa kubwa itakuja karibu katika dunia nzima, nayo ikatukia katika siku za Klaudio." - Matendo ya Mitume 11:28

2. Kusababisha kitu kitokee katika wakati ujao.

"Basi nikatabiri kama alivyoniamuru; pumzi ikawaingia, wakaishi, wakasimama kwa miguu yao, jeshi kubwa mno." - Ezekieli 37:10

SEHEMU KUU 3 ZA UNABII:

1. Ufunuo
2. Ufafanuzi wa ufunuo
3. Kufanyia kazi ufunuo

Nitatoa mfano mmoja hapa:

Ukisoma kitabu cha MATENDO YA MITUME 27 utaona ni habari inayomhusu Mtume Paulo; Ni kipindi ambacho alikuwa anasafiri kwenda Rome pamoja na wafungwa wengine. Upepo ulivuma & Merikebu waliyopanda ilikuwa kwenye hatari ya kuzama; Ndipo Paulo akatoa UNABII ufuatao;

"...akawaambia, Wanaume, naona kwamba safari hii itakuwa na madhara na hasara nyingi, si ya shehena na merikebu tu, ila na ya maisha yetu pia." - Matendo ya Mitume 27:10

Hapo Paulo anatabiri kuangamia kwa merikebu & watu waliomo.

Lakini baada ya siku 3, Paulo huyo huyo akaja na UNABII ufuatao;

"...Sasa nawapeni shauri, iweni na moyo mkuu, kwa maana hapana hata nafsi mmoja miongoni mwenu atakayepotea, ila merikebu tu. Kwa maana usiku huu wa leo malaika wa Mungu yule ambaye mimi ni wake, naye ndiye nimwabuduye, alisimama karibu nami, akaniambia, Usiogope, Paulo, huna budi kusimama mbele ya Kaisari; tena, tazama, Mungu amekupa watu wote wanaosafiri pamoja nawe. Basi, wanaume, changamkeni; kwa sababu namwamini Mungu, ya kwamba yatakuwa vile vile kama nilivyoambiwa." - Matendo ya Mitume 27:22-25

Hapa juu, Paulo anawaambia tena Hakuna nafsi ya mtu itakayopotea tofauti na alichosema mwanzo. Tunajifunza nini? Unabii ni kupata ufunuo, kuufuatilia ufunuo & kuutolea ufafanuzi. Kama Paulo asingeenda kumuuliza Mungu zaidi kuhusu unabii wa awali, angeonekana Muongo.

Ndicho kilichotokea Tanzania. Huenda ni kweli watu walipata ufunuo kuhusu Taifa, Je! Wametafuta uso wa Mungu zaidi kupata ufunuo zaidi kama alivyofanya Paulo? Au Mungu ameghairi kuindoa CCM kama alivyofanya kwa watu wa Ninawi & sababu ni nini? Hapa tutapata majibu kwa kwenda kumuuliza Mungu pekee & sio kuleta ushabiki.

Kwa leo Naomba nikomee hapa! Mungu ni Mwema.
 
Back
Top Bottom