Yamenikuta ndugu zangu. Je, nilichokifanya ili kumsaidia Bwana harusi nilikuwa sahihi?

JE, NILICHOKIFANYA NI SAHIHI?

Nilichaguliwa kuwa ktk kamati ya harusi ya jamaa yangu mmoja hivi, katika kamati hiyo mimi nilikuwa muweka hadhina ,
Kikao cha kwanza tulikaa na kupanga bajeti ya sherehe nzima ya harusi hiyo, bajeti yetu ilikuwa inatakiwa tupate 12,500,000/= (milion kumi na mbili na laki tano) ili kufanikisha sherehe hiyo.

Tukapanga viwango vya michango, tukatengeneza card na kuanza kusambaza kwa ndugu, jamaa, na rafiki. Kwa bahati nzuri watu walitoa michango kwa wakati, na kuvuka malengo ya bajeti yetu hadi tukafikia 13,200,000/= (milioni kumi na tatu na laki mbili)

Baada ya kukusanya michango na kupata kiasi hicho cha pesa , mimi binafsi nilimuangalia

(1) Bwana harusi je ana kazi? Jibu hana kazi.
(2) Bwana harusi ana biashara? Jibu hana biashara.

Mimi ninavyo mjua bwana harusi maisha anayoishi ni ya kudanda danda tu ili siku zisonge mbele.

Nikajiuliza kama bwana harusi maisha yake ndiyo haya kwanini tupoteze pesa nyingi kiasi hicho kwa starehe ya siku moja na kuacha bwana harusi akitaapita katika maisha?

Ilipofika siku ya kikao cha mwisho ili tupange na kuzigawa zile pesa katika kamati ndogo ndogo ili kila kamati pesa zao mfano: chakula, vinywaji, usafiri, n.k

Mimi ndio muweka hadhina na pesa zote ninazo mimi, sikutokea katika kikao, simu nikazima na nikasafiri kabisa, pesa zote nikaziweka katika account yangu.

Tarehe ya harusi ilifika bila ya mimi kuonekana sura yangu, ikawabidi wafanye mchango mwingine mdogo wa dharura na kupitisha sherehe ndoa tu.

Niliposikia ndoa imeshapita, nilirudi mjini na nikamtafuta bwana harusi nikamuomba msamaha ila nilimueleza nia na dhumuni la mimi kutoroka na zile pesa. Nia yangu yeye (bwana harusi) apate mtaji.

Nikamkabidhi pesa zake zote 13,200,000/= nikamwambia dogo fanyia biashara uendeshe maisha yako; sherehe ni kitu cha kupita tu.

Maoni yako kwa nilicho kifanya.

Sent using Jamii Forums mobile app
Huu ni uwongo mkubwa kabisa,huwezi kukimbia na hela ya harusi na ubakie salana
 
If at all this is true.

Kama ulikuwa na wazo hilo, la kumchangia bwana harusi oesa za kufungua biashara, ungemwambia bwana harusi, ungewaambia wajumbe wa kamati, ungewaambia walioombwa michango.

Kitu uichokifanya ni fraud.

Kuna kijana mmoja wa Upanga siku hizi maarufu sana, alishawahi kuwachangisha watu mchango wa harusi, halafu akaondoka Tanzania bila kuoa.
 
Kama ni kweli ulifanya hivyo, niamini mm, bado kuna watu wanakuwinda.
 
JE, NILICHOKIFANYA NI SAHIHI?

Nilichaguliwa kuwa ktk kamati ya harusi ya jamaa yangu mmoja hivi, katika kamati hiyo mimi nilikuwa muweka hazina ,
Kikao cha kwanza tulikaa na kupanga bajeti ya sherehe nzima ya harusi hiyo, bajeti yetu ilikuwa inatakiwa tupate 12,500,000/= (milion kumi na mbili na laki tano) ili kufanikisha sherehe hiyo.

Tukapanga viwango vya michango, tukatengeneza card na kuanza kusambaza kwa ndugu, jamaa, na rafiki. Kwa bahati nzuri watu walitoa michango kwa wakati, na kuvuka malengo ya bajeti yetu hadi tukafikia 13,200,000/= (milioni kumi na tatu na laki mbili)

Baada ya kukusanya michango na kupata kiasi hicho cha pesa , mimi binafsi nilimuangalia

(1) Bwana harusi je ana kazi? Jibu hana kazi.
(2) Bwana harusi ana biashara? Jibu hana biashara.

Mimi ninavyo mjua bwana harusi maisha anayoishi ni ya kudanda danda tu ili siku zisonge mbele.

Nikajiuliza kama bwana harusi maisha yake ndiyo haya kwanini tupoteze pesa nyingi kiasi hicho kwa starehe ya siku moja na kuacha bwana harusi akitaapita katika maisha?

Ilipofika siku ya kikao cha mwisho ili tupange na kuzigawa zile pesa katika kamati ndogo ndogo ili kila kamati pesa zao mfano: chakula, vinywaji, usafiri, n.k

Mimi ndio muweka hadhina na pesa zote ninazo mimi, sikutokea katika kikao, simu nikazima na nikasafiri kabisa, pesa zote nikaziweka katika account yangu.

Tarehe ya harusi ilifika bila ya mimi kuonekana sura yangu, ikawabidi wafanye mchango mwingine mdogo wa dharura na kupitisha sherehe ndoa tu.

Niliposikia ndoa imeshapita, nilirudi mjini na nikamtafuta bwana harusi nikamuomba msamaha ila nilimueleza nia na dhumuni la mimi kutoroka na zile pesa. Nia yangu yeye (bwana harusi) apate mtaji.

Nikamkabidhi pesa zake zote 13,200,000/= nikamwambia dogo fanyia biashara uendeshe maisha yako; sherehe ni kitu cha kupita tu.

Maoni yako kwa nilicho kifanya.
Ujasiri wa kufanya hivyo najua huna ila unatufundisha kitu hapo hizi harusi za siku hizi ni gharama mno na mwisho wa siku zinawanufaisha wachache hasa waliopata tenda huku zikiwaacha wahusika kwenye wakati mgumu
 
Hicho kitu hakiwezekani... Ni ngumu sana.. umeongea kitu chenye point lakini execution yake ni ngumu mno... maana hiyo michango si ya wanafamilia ya Bwana harusi bali ya watu mbalimbali...

Ingependeza kama ungetuambia wakati unamkabidhi hizo pesa harakati za kumtoa magereza Mwenyekiti wa kamati ya harusi zinaendeleaje...
 
WATU KAMA NYINYI NDIYO MNASTAHILI KUISHI DUNIANI SIO HAWA WENGINE WASIOJUA KUWAZA KUHUSU KESHO YA WENZAO. HONGERA SANA
 
Back
Top Bottom