Yamenikuta, maji yapo shingoni, naomba ushauri wapendwa plse!

summary
hapendi ndugu
hapendi mtoto
kuzaa mpaka operation
kiburi

ushauri

achana nae ( straight fowad)..huyo atasababisha uzee wako uwe wa manung'uniko.....utazeeka vibaya sana ndugu yangu....kwa kuwa ana matatizo ya uzazi alipaswa kukuheshimu wewe na ndugu zako....huyo hakupendi hata kama anakupikia......lol..halafu kamanda kuna mahali huwa unapuuzia maneno ya ndugu zako...najua wazazi wako wameshakwambia.....lakini leo kwa kuwa umeona maji yako shingoni na hii nadhani ni baada ya wewe kukaa mda mrefu bila kwnda ughaibuni....... angalia maisha yako mkuu na huyo mtoto na hizi mali ndizo zinakufanya uogope kuachana nae, jenga hoja mkuu wangu then mwache aende.....


 
No way,kwa mlio lelewa kwenye familia za kizungu sawa!
Ila mimi niliye lelewa familia za mlo mmoja tena na mama peke yake,kazi yenyewe amefanya u-house gal,ukondakta full kudhalilishwa afu leo mke wangu awe na maana kuliko mama?

Nihukumiwe kwa hilo,ila mke ntapata mwingine na sio mzazi alo nipigania toka navaa nguo moja mwaka mzima hadi leo nilipo!

Uzungu huu ndo unafanya mnaoa wake zenu wana waambia wazazi kitu cha mwisho,tuangalie maisha yetu mnakubali na kuwatosa wazazi wakiwa na shida,but for me......never,my mama is every thing to me!
The Following User Say Thank You to Speaker For This Useful Post:

 
No way,kwa mlio lelewa kwenye familia za kizungu sawa!
Ila mimi niliye lelewa familia za mlo mmoja tena na mama peke yake,kazi yenyewe amefanya u-house gal,ukondakta full kudhalilishwa afu leo mke wangu awe na maana kuliko mama?

Nihukumiwe kwa hilo,ila mke ntapata mwingine na sio mzazi alo nipigania toka navaa nguo moja mwaka mzima hadi leo nilipo!

Uzungu huu ndo unafanya mnaoa wake zenu wana waambia wazazi kitu cha mwisho,tuangalie maisha yetu mnakubali na kuwatosa wazazi wakiwa na shida,but for me......never,my mama is every thing to me!
Well said man! nadedicate kwako ule wimbo unaosema...mamaaa you are the queen of my heart.....
 
ningekuwa mimi ningemuacha na hizo mali tugawane maanaFuraha yangu ni kuona watu wangu wa karibu wanafurahi.
Mali inatafutwa ila furaha ni wewe mwenyewe kama utaamua kujipa furaha au lah.
 
achana nae huyo m/mke najua unaweza ukawa unampenda sana huyo mchumba wako lakini kwa nn aanze kukuonyesha red light mapema kiasi hiki wakati hata bado hakujapambazuka? Nina mfano wa ndg yangu mmoja alikuwa na kesi kama yako na walipoishia ni jamaa kuacha kila kitu kwa mkewe na akaenda kuanza moja, Bora wewe bado hata hamjafunga ndoa huyo ndg yangu yy alikuwa ameoa ila mkewe alikuja kumfukuza mama mkwe wake wakati jamaa yuko safarini.

Suala la mali sio issue kwanza hamjaoana mtagawana vp mali? nani ana ushahidi kuwa mliishi pamoja, timua huyo mapema au kama vp uza hivyo vitu mtimue halafu nunua vipya. Nakushangaa unashindwa kumtimua kwa kuofia mtagawana mali wakati sio mke wako?

Amka huyo si mke nakwambia na kama ukimuoa utapata laana ya ndugu, marafiki, wazazi na wafanyakazi wenzio hicho ni kimeo MUNGU amekuonyesa tu mapema

hebu kasome tena maelezo yake.
 
Vipi huyo mchumba wako ni Yatima au amekulia kwenye mazingira magumu?? Wanawake wenye tabia hizo au mama wakwe huwa wamezaliwa kwenye mazingira magumu sana. Imagine unachukiaje ndugu wa mumeo? Yaani unajua hata huyu shetani nafikiri tunamsingizia mambo mengi sana.

Nakushauri umwache aendelee na majinamizi yake ya kishetani, kuchukia watu bila sababu, kama yuko tayari kubadilika sawa ila kabla ya kumuoa mpe tena miaka 3 uangalie kama amerudisha mapenzi kwa ndugu zako. othewise I advice you to leave her alone, wake wema wako wengi watakaokuja na upendo kwa familia yako na wanaokkuzunguka pia.
 
Huyo mwanamke ni mkorofi inavyoonekana maana angekua na utu na ubinadamu wa kweli angekupenda wewe na familia yako na hata kama ni kutokuelewana na ndugu ingikua kwa baadhi yao tu na si hivyo

CHA KUFANYA
MWACHE AEENDELEE NA MAISHA YAKE KAMA VILE HUJAWAHI KUKUTANA NAE
, MUONDOE NDANI YA MAWAZO YAKO YEYE PAMOJA NA YOTE MLOWAHI KUSAIDIANA YASAHAU
, ANZA UPYA USIMUULIZE CHOCHOTE TAFUTA KILA KITU UPYA maisha ni kitu cha kupita tu haina maana kuishi na mtu anaekutesa MOYO wako mwisho upoteze ndugu, wazazi, mtoto na marafiki hata na uhai wako
 
Maty hapo juu mama mi ninavyodha huyu kaka tayari kashaona ndugu zake ni bora kuliko mke wake, na kashafikia uamuzi wa kumwacha tatizo ni mali zake tu. Kuna kitu nakiona hapo, kuna uhusiano mkubwa kati ya mali zake na wazazi wake pia, sio bure hii spirit ya mali aliyonayo huyu ya kaka yawezekana na hawa ndugu zake wanayo. So wanaona mali kuliko mtu/utu. r
Sijaona sehemu kasema tabia ya huyu dada, naona wazazi na mali. Khaaa sijui lkn kwa vyovyote vile hata mi nikichoka ntasema kama wanichoka...sio bure
 
tatizo kama hili la jamaa mi ilinipata baada tu ya kuoa: lkn mi nilifanya kiakili sana mpaka akaamua kukimbia mwenyewe. tofauti na huyu mi tayari nilzaa naye mtoto mmoja. Nilichofanya niliamua kumfanyia visa mara sirudi nyumbani, mara nafika nyumbani na mwanamke namtambulisha kama rafiki then natoka naye halafu sirudi siku hiyo, akilalamika nakaa kimya simjibu, simgombezi, sikumtukana ila vituko hivi tu vilitosha. Nilifanya hivi kwa miezi miwili tu akachapa lapa mwenyewe, wala mali hatukugawana. Baada ya kujivunza kupitia kwa huyu wa kwanza sasa ni mke anayestahili kweli kuitwa mke na ninaenjoy kweli maisha ya ndoa
kwaangw laway!
 
MWANAMKE NI SAWA NA JEZI YA MPIRA UKIUMIA,ANAPEWA MWINGNE AITETEE TIMU,WANAWAKE WENGI WALIOSOMESHWA NA WENZI WAO HUA HAWANA CHA KULIPA ZAID YA MAUMIVU KAMA UYAPATAYO.KUHUSU SWALA LA MKEO INAHITAJIKA UFANYE MAAMUZI MAGUM.MFANO, UTAJISIKIAJE MIAKA IJAYO MWANAO WA KUMZAA AKUTUPIE LAWAMA KUA ULISHINDWA MTUNZA JAPOKUA UNAUWEZO KIFEDHA?↲Pili NI MKE YUPI DUNIANI ANAEKUA NA SIFA NJEMA NA ROHO NZURI KWA KUWACHUKIA NDUGU NA WAZAZI WA MUMEWE?↲MALI NI KITU GAN BILA FURAHA YA NAFSI?CHUKUA MFANO UMETUOMBA USHAURI ILI NAFSI YAKO ITULIE,MBONA HUKUTUOMBA HELA ILI MALI YAKO ISIPUNGUE? WEWE NI M2 WA AINA GANI UNAEKUBALI MWANAO AENDE KIJIJIN ILIHAL WAJUA FIKA NI UGUMU GANI ULIOPO UKO,KAMA NI MSOMI INABDI UPIME KAMA ELIMU YAKO IMEKUSAIDIA AU LA.THENK U.
 
Mkuu, pole sana na hizo changamoto.
Najua wengi wameshauri kwa kadiri ya uwezo wao, lakini kwa upande wangu ningeshauri wazo la 'KUVUNJA NDOA' ondoa kabisa.
Hebu fuata ushauri uliotelewa na wadau hawa


Ndugu Lumecha

wachunguze hao ndugu zako, watakuwa wana tatizo ndio maana mkeo anawachukia. Labda wanamsimanga na kumpiga majungu kwa vile hajapata mtoto na wewe.

Ndugu wa baadhi ya wanaume wamekuwa wakiwafanyia visa wake za ndugu zao kwa sababu nyingi ikiwapo kuwa na tofauti ya makabila, life style, kukosa watoto, mali etc.

Kama mwanaume usipotumia busara na uchunguzi usiokuwa biased, unaweza vunja ndoa yako.

Usizungumze na kila upande kivyake, usitumie mshenga, babu, bibi au mjomba. Subiri hadi utakaporudi myazungumze kwa pamoja, mke na nduguzo.


Labda uliwaringishia ndugu zako kuwa mke wangu nimemsomesha mwenyewe, ni mwema sana, atawasaidia. Ukawapa expectations za uu kuliko mkeo alivyoweza kuwatimilizia, wakaanza kumchukia na kumfanyia visa. Na yeye anajiona ni mke na anastahili heshima kutoka kwao pia. Lugha au vitendo vikagongana.

Waambie nduguzo kuwa huyo ni mkeo, ni familia yako na anastahili heshima kama wanayokupa wewe, wakimdharau wamekudharau wewe.
Mwambie mkeo hao ni nduguzo na wanastahili heshima kama anayokupa, akiwadharau kakudharau. Hivyo hivyo na kuhusu chuki.
Mwanaume lazima uwe na msimamo sio kulegalega na kukimbilia kuvunja ndoa.

USITOE SIRI ZA MKEO AU UBAYA AU UZURI WA MKEO KWA NDUGUZO, LAZIMA WATAMCHUKIA.


Dah dunia hii bwana kweli tu wasafiri. Hebu mshirikishe Mungu kwa nia moja hilo tatizo, hebu jaribu kuongea naye kwa lugha ya upendo, mweleze muulize ujue kwa nini anafanya hivo. Hebu tulia ili upate kujua kiini cha matatizo hayo nini? Haiwezekani awachukie wazazi na ndugu zako bila sababu. Na sababa inaweza kutokana na yy mwenyewe, mf. uchoyo nk nk, au ikatokana na hao wazazi/ndugu. Pengine ndugu hao wanamuona kauzibe kwa yale unayo/uliyokuwa unawafanyia na sasa hufanyi au unafanya kidogo.


Mtu ataachana na mama yake na baba yake, nao watakuwa mwili mmoja, alichokiunganisha Mungu mwanadamu akiwepo mzazi na ndugu wasitenganishe. Chonde chonde kaka angu Mama yako hata pamoja amekuzaa asikutenganishe na mke wako. Tafuta jinsi ya kuishi na mkeo kwa akili kamwe mama hawezi chukua nafasi ya mke moyoni mwako, atabki mama tu milele, fikiria kk ukimuacha huyo ukamuoa mwingine wazazi wakamchukia tena utamuacha? Dah bwana labda kuna sababu ingine, hicho cha kujibu inategemea na mazingira. Nakuja!!

Siku zote lazima tujifunze kutatua na sio kukimbia matatizo. Kama ndoa yako ni ya KIKRISTO, basi imekatazwa kabisa kwa wanandoa kuachana isipokuwa kwa sababu ya uzinzi.
Kwa vile tatizo lako linaweza lisihusiane na uzinzi hivyo basi, yakupasa kutatua tatizo, labda ukirudi kutoka kubeba box.
Kaa na watu wenye busara, watu wa kanisa kama wachungaji jaribu kupata ushauri wao. Pia jaribu kutafuta nafasi nzuri ya faragha kuzungumza na mwenzio. Hayo matatizo yote yanasuluhisho... Hebu weka moyo wako na uamini kuwa utayapatia ufumbuzi matatizo yako na sio kuyakimbia, kwa sababu huna hakika utakutana na mtu wa namna gani.
Kama mliweza kupanga na kufunga ndoa pamoja na changamoto zote zile huoni kuwa unaweza kupata suluhisho??
Ndoa yako ni changa sana, haina hata mwaka,hivyo nafasi ya kupata solution ni kubwa sana. Mkae chini mzungumze
Labda angalizo kwa wasomaji wengine, mojawapo ya vitu vilavyoleta matatizo katika ndoa ni WATOTO wa nje kuletwa ndani ya ndoa. ni wanawake wachache sana wanaweza kuvumilia kwa moyo mmoja, lakini kama ikiwezekana watoto wa nje uwahudumie kivyao vyao..

Asante
 
Mkuu, pole sana na hizo changamoto.
Najua wengi wameshauri kwa kadiri ya uwezo wao, lakini kwa upande wangu ningeshauri wazo la 'KUVUNJA NDOA' ondoa kabisa.
Hebu fuata ushauri uliotelewa na wadau hawa













Siku zote lazima tujifunze kutatua na sio kukimbia matatizo. Kama ndoa yako ni ya KIKRISTO, basi imekatazwa kabisa kwa wanandoa kuachana isipokuwa kwa sababu ya uzinzi.
Kwa vile tatizo lako linaweza lisihusiane na uzinzi hivyo basi, yakupasa kutatua tatizo, labda ukirudi kutoka kubeba box.
Kaa na watu wenye busara, watu wa kanisa kama wachungaji jaribu kupata ushauri wao. Pia jaribu kutafuta nafasi nzuri ya faragha kuzungumza na mwenzio. Hayo matatizo yote yanasuluhisho... Hebu weka moyo wako na uamini kuwa utayapatia ufumbuzi matatizo yako na sio kuyakimbia, kwa sababu huna hakika utakutana na mtu wa namna gani.
Kama mliweza kupanga na kufunga ndoa pamoja na changamoto zote zile huoni kuwa unaweza kupata suluhisho??
Ndoa yako ni changa sana, haina hata mwaka,hivyo nafasi ya kupata solution ni kubwa sana. Mkae chini mzungumze
Labda angalizo kwa wasomaji wengine, mojawapo ya vitu vilavyoleta matatizo katika ndoa ni WATOTO wa nje kuletwa ndani ya ndoa. ni wanawake wachache sana wanaweza kuvumilia kwa moyo mmoja, lakini kama ikiwezekana watoto wa nje uwahudumie kivyao vyao..

Asante
We mamayo c ajapata bahati ya kudharauliwa na mke wa mtoto wake,kwanza mtoa mada anajua tatizo ni mkewe,na anahofia sana mali zake kuliko ki2 kingne.
 
freema: nawasiwasi na wewe mbona kama unamtetea sana au na wewe ndio tabia zako??

Kama wasiwasi wako ni kutetea, basi hata mim nakuwa na wasiwasi na wewe, umeshaacha mke kwa sababu kama hii?

Ukifanya kazi ya ushauri, matatizo haya hasa kwenye extended families kama za Kitanzania, ni mengi mno. Asilimia kubwa ya matatizo ya ndoa yanachangiwa na ndugu wa mume/mke kuingilia wana-ndoa. Hii humfanya mmoja wao ajione out of place.....ndipo vurugu zinapoanza.

Fikiria unaishi na shemeji yako, halafu anaanza kupeleka salamu za lawama kijiji, shemeji hanipikii, shemeji ananituma sana nakosa muda wa kujisomea, shemeji ananiangalia wakati nakula, shemeji haninunulii nguo, shemeji ananipa pocket money kidogo, shemeji anamchapa mtoto, hampi chakula, anamfokea....etc. Kinachofuatia ni ndugu wote kumwona huyo mwanamke mbaya, ana roho mbaya bila kuuliza chanzo cha yote. Tena ukute shemeji alikuwa anaishi na brother kabla hajaoa, ndio kabisa kwa sababu akija mwanamke ataleta sheria mpya. Shemeji anaona tabu. Kaka anapigiwa simu huko majuu, mkeo hivi, mkeo vile. Mambo yanaenda yakikua, mwisho wa siku yanafikia hapo yalipofikia.

Sisemi mwanamke yuko right, ila na ndugu wa wanaume, hasa wanapokuwa tegemezi kwa kijana wao, huleta vurugu na kashikashi kwenye ndoa, hasa changa na isiyo na mtoto.
 
mkeo akigundua kuwa mama yako ni bora kuliko yeye huoni kuwa ndoa itakuwa shakani na lazima wataoneana wivu na kuanza kununiana??
mimi mke wangu ana nafasi ya pakee na mzazi ana nafasi yake nyingine tofauti na sitaki mzazi aniingilie kwenye ndoa yangu kabisa. Kuja wazazi waje kwa miadi sio wanakurupuka na kuja kushinda kwangu. Pia sio lazima wawasiliane na mke wangu kila siku, hawana cha maana cha kufanya? Mie nachukia sana ndugu wanaoingilia uhusiano wa mtoto wao.

Okey,siwezi kukulaumu sana!
Inategemea ulikuwa na uhusiano gani na wazazi wako wakati unakua,....
Kwenye amri za Mungu nizijuazo,...hakuna amri yoyote inayo ongelea mke (simaanishi kumdharau)!
Ila kuna amri inayo ongelea wazazi na ndiyo amri pekee yenye ahadi!,...utazidishiwa siku za kuishi.
Kwenye kitabu kitakatifu kuna sehem unaambiwa ikilazimika basi utaachana na mkeo,lakini hakuna sehemu inasema kwa namna yoyote ile umuudhi au kumsahau mzazi wako.

Simaanishi usimpende mkeo,..(imeamriwa umpende),..na tusitumie kigezo cha mme kuachana na wazazi wake kwenda kuwa mwili mmoja na mke wake kama sababu ya kuwasahau wazazi,...NI LAANA

Lakini mke anapokuwa sababu ya wewe kuvunja amri ya Mungu,..(waheshimu baba na mama upate heri na miaka mingi duniani),...huyo mke ana faida gani?
 
Kama wasiwasi wako ni kutetea, basi hata mim nakuwa na wasiwasi na wewe,a. Hii humfanya mmoja wao ajione out of place.....ndipo vurugu zinapoanza.

Fikiria unaishi na shemeji yako, halafu anaanza..etc. Kinachofuatia ni ndugu wote kumwona huyo mwanamke mbaya, ana roho mbaya bila kuuliza chanzo cha yote. Tena ukute shemeji alikuwa anaishi na brother kabla hajaoa, ndio kabisa kwa sababu akija mwanamke ataleta sheria mpya. Shemeji anaona tabu. Kaka anapigiwa simu huko majuu, mkeo hivi, mkeo vile. Mambo yanaenda yakikua, mwisho wa siku yanafikia hapo yalipofikia.

Sisemi mwanamke yuko right, ila na ndugu wa wanaume, hasa wanapokuwa tegemezi kwa kijana wao, huleta vurugu na kashikashi kwenye ndoa, hasa changa na isiyo na mtoto.
umezungumza uzuri,ila katka familia wote hamuwez kua na uwezo sawa,sasa m2 akisaidia ndugu mkewe alete mgogoro then uyo ni mke ambaye anafundsha sekondari na ni m2 mwenye elimu ya chuo,sasa anawafundisha nini wanafunzi huko shuleni? Mana kama wasifu wake wa ndani ndo huo,je unataka kusema utatofautiana na wasifu wake wa nje kiutendaji?
 
Ni hivi Dada Lizzy,

Hayo hayakuwepo hapo mwanzo, imagine hata mtoto wangu aliishi nami pamoja na yeye na kuanza shule hapa mjini hadi darasa la 3 lkn mwaka huu mie narudi field ananiambia mtoto nimempeleka kijijini coz jeuri nataka akajifunze tabia huko rural. Nina mdogo wangu wa mwisho namsomesha na yupo day school, hawaongei hata akimwamkia hajibu hapo mimi nipo je nikiondoka inakuwaje mpendwa? Yaani baada ya ndoa tu tabia imebadilika sana, na sasa ndo ameajiriwa akitoka asubuhi kurudi jioni akifika tu kulala kisa amechoka, mie ndo niingie jikoni au huyo mdogo wangu. Da lizzy nipe ushauri plse
Huyo dada asiye na mzuka wa kumpikia mume wake kwa sababu ya 'kuchoka' amezidi. Hata kama ingekuwa ndugu zako ndo wabaya asingefikia hatua hiyo. Ukiwa nje unamiss misosi ya home vibaya, umerudi hakuna mapishi ya mkeo... dah! hiyo michosho si kawaida.
 
...natamani nikujibu kwa experience yangu, lakini sdidhani ni busara.

Fuata moyo wako, usifuate akili yako. Sikiliza kwa makini nini moyo wako unakushauri.
Ukiwa tayari, fanya maamuzi magumu na uyasimamie mpaka mwisho wa maisha yako.


Kila la heri.
 
kinachotakiwa ni mke na mume kukaa na kupanga sheria wazazi/ndugu waje kwa mtindo gani, kugombana na ndugu wa mume wakati mume hayupo halafu akiuliza unamwambia sio lazima kuishi na wewe badala ya kueleza chanzo hiyo ndio nini? Sasa yeye atajuaje kama wewe huna makosa? Maana nduguze akiwauliza wanasema tatizo wewe ukiulizwa unakuja juu na kusema sio lazima kuishi na wewe

Vunja ukimya ongea na mwenzako!
 
Ndugu Lumecha

wachunguze hao ndugu zako, watakuwa wana tatizo ndio maana mkeo anawachukia. Labda wanamsimanga na kumpiga majungu kwa vile hajapata mtoto na wewe.

Ndugu wa baadhi ya wanaume wamekuwa wakiwafanyia visa wake za ndugu zao kwa sababu nyingi ikiwapo kuwa na tofauti ya makabila, life style, kukosa watoto, mali etc.

Kama mwanaume usipotumia busara na uchunguzi usiokuwa biased, unaweza vunja ndoa yako.

Usizungumze na kila upande kivyake, usitumie mshenga, babu, bibi au mjomba. Subiri hadi utakaporudi myazungumze kwa pamoja, mke na nduguzo.
hii inawezeka kabisa, lkn ndio hata mtoto aliyemkuta hapo kamfanyia visa!!??
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom