Yameanza kutimia: Bandari kavu zalia kukosa mizigo

Kama mizigo ilikuwa inaingia lakini hela ilikuwa haionekani nini faida yake? Bora tuwe na mizigo michache lakini inayoleta tija kwa taifa.
Magufuli alipaswa kwenda taratibu na sisi wengine tulishauri kupitia hapa JF nini kinaweza kutokea siku za usoni.Ngoja ni-quote hiyo post kwa kuinakili kwako.
 
Wenye mahaba mbona wanajulikana dunia nzima, labda kama wewe umezaliwa jana ndio huwafahamu. Wanatunga uongo na uzandiki kama wako kufurahisha nyoyo zao. Mtu mgonjwa wanasema anakimbia kilomita elfu tano
 
Hiii hapa
665187678b8dabc0ada61f2451671a3c.jpg
Moderator tunaomba muiweke hii picha hapo juu kwenye huu uzi.
 
Kama sukari tu iliwashinda wataweza biashara kubwa kama magari yanayopita bamdarini?
 
acha mpunguzwe tu maana kazi zenyewe mlikuwa mnapeana kwa kujuana................mje muone maisha halisi yalivyo sio ya mkatomkato.
Nadhani hujaelewa hatupunguzi kwakuwa kuna mamluki bali mdororo
 
Wenye mahaba mbona wanajulikana dunia nzima, labda kama wewe umezaliwa jana ndio huwafahamu. Wanatunga uongo na uzandiki kama wako kufurahisha nyoyo zao. Mtu mgonjwa wanasema anakimbia kilomita elfu tano

Ya kwako yamezidi
 
Aisee hii maana yeke hali itazidi kuwa mbaya kwa hao wanaoachishwa na familia zao. Tz mfanyakazi unakuta anafamilia inamtegemea tena family ni extended family hadi ndugu wanamtegemea....hii crisis serikali isipotafuta ufumbuzi haraka itavuruga uchumi wa nchi zaidi. Kupunguza wafanyakazi haitaishia hapo.....itaendelea na kwingine coz mdororo wa uchumi umeenea kila sehemu.
 
Na bado ile Bandari itageuka kuwa fukwe ya watoto kwenda kucheza siku za weekend na "kudiba" maana meli zitakoma kutia nanga! Ikitia nanga moja kwa week inatosha! Uone utakusanya nini na ma vat yenu kwa mizigo ya transit! Pia tusisahau ukitaka kuagiza kitu chochote nje unalipa kwanza kodi fulani pale tra baada kupewa ruksa wizara fedha....wakitekeleza huo upuuzi ndio kabisa...tutanunua magari chakavu ya ndani waone jeuri yao! Hata mishahara watakopa weee hadi nchi itawashinda!! Uongozi sio njozi!!
 
Tutafika tu wapendwa! Uchumi Mzuri mbeleni uanza na Maisha magumu! Yote ili kufika mahari pazuri!. Tusiogope!! Makampuni yatapunguza kwa sasa lakini punde yataongeza ufanisi na kuajiri wengi! Tanzania mpya inakuja, onja taabu ufanikiwe!
 
Aisee hii maana yeke hali itazidi kuwa mbaya kwa hao wanaoachishwa na familia zao. Tz mfanyakazi unakuta anafamilia inamtegemea tena family ni extended family hadi ndugu wanamtegemea....hii crisis serikali isipotafuta ufumbuzi haraka itavuruga uchumi wa nchi zaidi. Kupunguza wafanyakazi haitaishia hapo.....itaendelea na kwingine coz mdororo wa uchumi umeenea kila sehemu.

Mkuu halafu unasikia mtu anapanda jukwaani anasema ana watumikia wananchi!! Sasa sipati picha eti tunaambiwa tutaumia kwa muda kidogo kisha mambo yatakuwa mazuri, nakuhakikishia huenda uchumi ukazidi kudorora na itachukua muda kurudi ulivyokuwa.
 
Uongozi wa kibri,dharau na ubabe haukuwahi kufanikiwa tangu kuanza kwa dunia. Unataka utukufu kuliko Mungu kisha unamtegemea... Hahahaa.. Naona maprofesa wengi wameteuliwa lakini bahati mbaya sana wamemaliza vyuo wakaanza kufundisha wengine hawajawahi hata kusimamia biashara ya duka wanafundisha ambacho hawajawahi kukifanya kisha leo unawapa uongozi wa kitaifa. Sinema nyingi zinakuja na utaendelea kushangaa hivyohivyo. Ya sukari imeisha na bei imepanda na ile ya nje ndo nyingi sana. Ngoja tuone hii ya mafuta sijui itaishaje. Ya bandari nadhani ni wadhamini tu.
 
Ili dhahabu iwe safi lzm ipite kwenye tanuru la moto. Tanzania tunapita na tutapita kwny kipindi kigumu kwa uchumi lkn miaka ijayo nchi itakuwa bomba

Acha ndoto za mchana ndugu yangu. Ni lazima uchumi uharibike ndio uwe mzuri? hivi ni formula gani hiyo mnatumia ndugu zetu? Nyie bebeni maneno ya ushabiki wa kisiasa lakini kwa sisi tulioona enzi za Nyerere ilikuwa hivi hivi kwamba tufunge mikanda, lakini tulivaa viraka na huduma muhimu ilibidi tupange mstari kuzipata. JK alizurura dunia nzima na kujifanya ni rafiki wa nchi za nje lakini hivyo viwanda vilivyojengwa na hao marafiki viko wapi? Ni maendeleo gani ya maana tumepata kutokana na urafiki ule wa JK na nchi hizo zaidi ya deni la taifa kupanda? Leo huyu anaongea lugha za kujifanya hataki msaada wa masharti huku akitegemea wachina kufanya maajabu, wakati urafiki wetu na china haujawahi kuharibika lakini bidhaa fake toka uchina ndio zimejazana hapa nchini.
 
Back
Top Bottom