Yameanza kutimia: Bandari kavu zalia kukosa mizigo

Wanasema pamoja na mizigo kupungua lakini mapato yameongezeka sijui kwa kutumia formula gani.
It's simple.... Manake kulikuwa na upigaji wa kutisha.. Ni sawa na kuchota maji kwa tenga... Unachota mengi, yanapotea mengi
 
Lipeni kodi!
Mlishazoea kutoa mizigo kinyemela,hamtoi risiti mnapata super profit.Mtaa wa congo uchochoro tu pango ni milioni 4 kwa mwezi,unalipa kodi ya mwaka cash,kwa kujua unapata faida ya 250%,na mwenye nyumba wako nae halipi kodi
Bora mizigo ipungue lakin kitakachopatikana kiingie serikalini,kuliko mtu analeta kontena 40,analipia 2 nyingine anagawana na watu wa TRA.
Ndio maana kuna mtu kakutwa na nyumba 70!za nini zote hizo au amekuwa national housing?

je unafahamu effect yake kiuchumi na kijamii? ukikokotoa faida iko kwa nani na nani
 
Mizi
Wanasema pamoja na mizigo kupungua lakini mapato yameongezeka sijui kwa kutumia formula gani.
go mingi ilikuwa inapita bure
Na ndo maana zile meli za kiujanja ujanja hazionekani tena
 
Tafakuri ya uchumi wetu
Mara kadhaa nikitafakari uchumi wa nchi hii huwa siishiwi na tafakuri.
Nazikumbuka Juhudi za Mwalimu Nyerere kuifanya Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati lakini kwa bahati mbaya Mwalimu alikuwa akipambana peke yake na viwanda alivyoanzisha leo vingi ni ma ghala na nyumba za Bundi.
Najaribu kuwaza kulingana na Taarifa ya mkurugenzi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania.. Kwa sasa wanakusanya sh bilion 458 kutoka bandari ya Dar es Salaam pekee na hii ni baada ya kuziba mianya ya rushwa. Mapato ya Mwezi Juni ni trilion 1.3 wakati mapato ya mwaka jana wa fedha ni trilion 13.31.
Hapo ndiyo mahesabu yanapishana na dhamira ya kuelekea uchumi wa kati.
Ukiangalia kimahesabu utakuta nusu ya mapato ya nchi yanatokana na bandari. Kwani ktk trilion 1.3 bilion 458 zinatoka bandari ya Dar es salaam kwa mwezi Juni. Kama mapato ya bandari ya Tanga, Mtwara,Mwanza na Kigoma yanaweza kuleta bilion 50 kwa mwezi hii itakuwa na maana 50% ya mapato yote nchini hutokana na bandari. Na 50% nyingine hotokana na tozo katika tasnia nyingine kama reli, madini,gesi, kilimo, kodi kwa wafanyakazi na wafanya biashara zingine nje ya bandari,
Napata shida kuamini safari yetu kwani hata secta kubwa na rasmi kama gesi, madini, kilimo na usafirishaji bado hazijaweza kutupatia bilion 800 kwa mwezi. Huku matumizi ya serikali yanakisiwa kufika zaidi ya bilion 500 kwa mwezi. Unaweza kusema hela yote ya bandari hurudi katika matumizi ya serikali kwa mwezi, (running expenses) na zinazobaki zinaenda katika miradi ya maendeleo. Hivyo bajeti yetu ya maendeleo inategemea chenji ya bilion 600 na kidogo. So hii ndiyo hela tujenge reli, tununue Ndege, tuijenge Tanesco mpya, kiwanda cha kuchakata gesi, mbolea, barabara, nk.
Sitaki kuamini kama hatuna matatizo kitaasisi. Yapo tena makubwa.
Suluhisho la tatizo hili ni mtambuka halimtegemei raisi peke yake, bali taasisi imarakatika serikali, katiba nzuri na vyombo vya kusimamia sheria imara na mwananchi mwenye moyo wa uzalendo na mwerevu.
Mwisho uchumi ni mchezo wa hesabu na maendeleo ni kupanga na kupanga ni kuchagua. Kipi kianze kwa manufaa yapi na kipi kianze km kichocheo kwa tasnia nyingine. Viwanda ni dhamira ya muda mrefu lakini dhima ilipaswa kuwa huduma mtambuka (cross factors) na kuimarisha taasisi zetu kujiendesha bila msukumo na kwa weledi ulio automated.

Akhsanteni
 
Back
Top Bottom