Yaliyotokea mpakani na Kenya, Zambia na Rwanda yanaonyesha haja ya umakini kwa Magufuli kuteua wakuu wa mikoa ya mipakani wenye uwezo wa kidiplomasia

Hilo ndilo ninaloshauri kwamba watu wenye mtazamo kama wako kamwe wasije kuteuliwa kuwa wakuu wa mikoa ya mipakani - ni wazi watu wa aina yako mpo wengi!
Unajuaje kama mimi si mkuu wa mkoa? Wewe hujui haya mambo, diplomasia itafuata lakini huu uhuni wa kutuchezea ukomeshwe kwanza. Kama kwa mfano Kenya wanafahamu diplomasia basi wasingekuwa wanasema watanzania wana corona. Yaani wanapima Wakenya na Watanzania wanaotoka Tanzania ati unakuta Watanzania tu ndio wana corona!!! Utadhani Wakenya wakiwa Tanzania hawaongei na hao wenye corona. Waache uhuni.
 
Ndio chama kuongozwa na wasomi kuna professionalism

Angalia Sera waluzonadi chadema kipindi cha uchaguzi walisema kipaumbele chao cha kwanza in elimu cha pili ni elimu na cha tatu ni elimu inafika kuchagua mwenyekiti Wa chadema taifa wanachagua form six division zero!!! Tatizo hawana professionals kwenye chama
Na CCM katika kipindi cha uchaguzi ilani yao ilisema wanafunzi wakipata mimba wataendelea na masomo! Professionalism?
 
Na hao watalii wangekujaje Tanzania wakati tulikuwa tumefunga safari za kimataifa? Wakati bifu hizi zinatokea uliona ndege zinatua pale JKIA? Sasa Wakenya wangekuwa wanazuia watalii hewa? Hao watalii wana lockdown kwao kuliko hata ya Kenya

Acheni theory zisizo na mshiko.
Kwani athari za corona zitaisga leo?chini kabisa maumivu mpaka miaka mitafu ijayo
 
Nakumbuka katika kuteua wakuu wa mikoa muda fulani uliopita, Raisi Magufuli alisema kwamba alikuwa akiteua wakuu wa mikoa ya mipakani wengi wakiwa wanajeshi ili kusaidia katika suala la ulinzi mipakani. Lakini sasa, migongano na nchi jirani za Kenya, Zambia, Rwanda na hata Uganda zimetufundisha na kutupa onyo juu ya umuhimu wa kuhakikisha kwamba wakuu wa mikoa ya mipakani wanapaswa kuwa watu wenye uwezo mkubwa wa kidiplomasia.

Ukichukulia Tanga na Kilimanjaro kwa mfano, tumeshuhudia wakuu wa mikoa wakichochea badala ya kuzima moto wa jazba uliojitokeza kati yetu na Kenya, hadi kufikia hatua ya kuwakejeli viongozi wakuu wa nchi jirani! Sasa hii ni hatari sana, na tusipoangalia inaweza kuleta machafuko kufikia wananchi wa mipakani kuanza kupigana na watu wa nchi jirani na hata kuuana. Na mazingira kama hayo yanaweza kufikia hatua ya polisi au jeshi kuingilia kati, na hata risasi kupigwa dhidi ya nchi jirani na kuzua mpambano wa askari wenye silaha.

Sio vibaya kuweka wanajeshi kama wakuu wa mikoa ya mpakani, kwa kuwa wapo wanajeshi wanaojulikana kuwa mahili katika masuala ya diplomasia. Hata hivyo, kama ni suala la ulinzi mipakani ni vema kuwa na kambi za jeshi katika kila mkoa wa mpakani, na wakuu wa kambi hizi wakawa sehemu ya kamati za ulinzi za mkoa ambazo zinasimamiwa na wakuu wa mikoa.

Hata hivyo, kipaombele kiwe kuteua wakuu wa mikoa ya mipakani ambao ni raia na watu wenye uwezo mkubwa katika masuala ya diplomasia. Na ikibidi, wakuu wa mikoa ya mipakani wawe wanapitia mafunzo maalumu ya diplomasia kabla ya kuripoti kwenye vituo vyao vya kazi.

Ningependa kushauri kwamba mabadiliko haya yafanyiwe kazi haraka iwezekanavyo.
Kwani kufunga mpaka wa eneo lake ni kosa? Mbona wao wanafunga ya kwao? Kwa nini kitu kikifanywa na Tanzania inakuwa nongwa mnaanza kuleta siasa za maji taka? Jino kwa jino tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakumbuka katika kuteua wakuu wa mikoa muda fulani uliopita, Raisi Magufuli alisema kwamba alikuwa akiteua wakuu wa mikoa ya mipakani wengi wakiwa wanajeshi ili kusaidia katika suala la ulinzi mipakani. Lakini sasa, migongano na nchi jirani za Kenya, Zambia, Rwanda na hata Uganda zimetufundisha na kutupa onyo juu ya umuhimu wa kuhakikisha kwamba wakuu wa mikoa ya mipakani wanapaswa kuwa watu wenye uwezo mkubwa wa kidiplomasia.

Ukichukulia Tanga na Kilimanjaro kwa mfano, tumeshuhudia wakuu wa mikoa wakichochea badala ya kuzima moto wa jazba uliojitokeza kati yetu na Kenya, hadi kufikia hatua ya kuwakejeli viongozi wakuu wa nchi jirani! Sasa hii ni hatari sana, na tusipoangalia inaweza kuleta machafuko kufikia wananchi wa mipakani kuanza kupigana na watu wa nchi jirani na hata kuuana. Na mazingira kama hayo yanaweza kufikia hatua ya polisi au jeshi kuingilia kati, na hata risasi kupigwa dhidi ya nchi jirani na kuzua mpambano wa askari wenye silaha.

Sio vibaya kuweka wanajeshi kama wakuu wa mikoa ya mpakani, kwa kuwa wapo wanajeshi wanaojulikana kuwa mahili katika masuala ya diplomasia. Hata hivyo, kama ni suala la ulinzi mipakani ni vema kuwa na kambi za jeshi katika kila mkoa wa mpakani, na wakuu wa kambi hizi wakawa sehemu ya kamati za ulinzi za mkoa ambazo zinasimamiwa na wakuu wa mikoa.

Hata hivyo, kipaombele kiwe kuteua wakuu wa mikoa ya mipakani ambao ni raia na watu wenye uwezo mkubwa katika masuala ya diplomasia. Na ikibidi, wakuu wa mikoa ya mipakani wawe wanapitia mafunzo maalumu ya diplomasia kabla ya kuripoti kwenye vituo vyao vya kazi.

Ningependa kushauri kwamba mabadiliko haya yafanyiwe kazi haraka iwezekanavyo.
Wewe wa ajabu sana, wakenya wameihubiria dunia kua wa Tz tuna korona, na wao ndio wa kwanza kufunga mpaka, halafu unakuja hapa eti ooo bla bla blaa, nina hakika wewe sio mtanzania, shame on you, diplomasia gani utumie kwa mtu ambae ame ku underrate
 
Unajua uungwana ni sifa, sio udhaifu. Ukikumbuka hilo maisha yako nyumbani, kazini hata na jirani zako yatakuwa mazuri sana
Na wao wakiwa waungwana ndio vizuri. Sio unaonewa unajifanya malaika. Tunapambana hatumwachii Mungu.
 
Wajinga sana Kenya wao ndio walikuwa wakituchafua kimataifa kuwa tumejaa mi corona kila kona kwenye press hadi za kimataifa ohh imebaki sehemu moja tu ndio inatuletea corona ambayo ni Tanzania wakawa wanatuataja kabisa heri wangechukua tu measures lakini sio kupiga tarumbeta kuwa mitanzania imejaa mi corona
Sisi tuna ma carona mengi tu watanzania kwani uongo
 
Nakumbuka katika kuteua wakuu wa mikoa muda fulani uliopita, Raisi Magufuli alisema kwamba alikuwa akiteua wakuu wa mikoa ya mipakani wengi wakiwa wanajeshi ili kusaidia katika suala la ulinzi mipakani. Lakini sasa, migongano na nchi jirani za Kenya, Zambia, Rwanda na hata Uganda zimetufundisha na kutupa onyo juu ya umuhimu wa kuhakikisha kwamba wakuu wa mikoa ya mipakani wanapaswa kuwa watu wenye uwezo mkubwa wa kidiplomasia.

Ukichukulia Tanga na Kilimanjaro kwa mfano, tumeshuhudia wakuu wa mikoa wakichochea badala ya kuzima moto wa jazba uliojitokeza kati yetu na Kenya, hadi kufikia hatua ya kuwakejeli viongozi wakuu wa nchi jirani! Sasa hii ni hatari sana, na tusipoangalia inaweza kuleta machafuko kufikia wananchi wa mipakani kuanza kupigana na watu wa nchi jirani na hata kuuana. Na mazingira kama hayo yanaweza kufikia hatua ya polisi au jeshi kuingilia kati, na hata risasi kupigwa dhidi ya nchi jirani na kuzua mpambano wa askari wenye silaha.

Sio vibaya kuweka wanajeshi kama wakuu wa mikoa ya mpakani, kwa kuwa wapo wanajeshi wanaojulikana kuwa mahili katika masuala ya diplomasia. Hata hivyo, kama ni suala la ulinzi mipakani ni vema kuwa na kambi za jeshi katika kila mkoa wa mpakani, na wakuu wa kambi hizi wakawa sehemu ya kamati za ulinzi za mkoa ambazo zinasimamiwa na wakuu wa mikoa.

Hata hivyo, kipaombele kiwe kuteua wakuu wa mikoa ya mipakani ambao ni raia na watu wenye uwezo mkubwa katika masuala ya diplomasia. Na ikibidi, wakuu wa mikoa ya mipakani wawe wanapitia mafunzo maalumu ya diplomasia kabla ya kuripoti kwenye vituo vyao vya kazi.

Ningependa kushauri kwamba mabadiliko haya yafanyiwe kazi haraka iwezekanavyo.

Upuuzi mtupu, ulitaka wakuu wa mikoa ndo waende kulialia kwa wakenya ambao wanatunyanyasa? Mbona hukuwashauri hao wakenya wakati madereva wetu wkilalamika kunyanyaswa?
Sisi pia tumechukua hatua kama taifa huru, kama wao walivyoona ni vema kutuzuia,
Kama ni uhitaji kila mtu anamtegemea mwenzake, dipromasia sio mmoja aumie tuu,
Ndo maana KIM JONG UN, hataki ujinga ujinga.
 
Nadhani Tanga, Kilimanjaro huyu mama sidhani kama alishakuwa mwanajeshi. Lakini hiyo ilikuwa kauli ya ujumla, hakuna tuliposema Mkuu wa mkoa Tanga na Kilimanjaro ni wanajeshi. Ila Magufuli alisema anataka kuweka wanajeshi mikoa ya mipakani kama Kigoma na Kagera ili wasaidie masuala ya ulinzi mipakani
Bora hata Mama Mghwira alipitaga JKT kwa mujibu wa sheria enzi zake lakini Shigela hata JKT hajapita, mwanajeshi wapi? Shigela ni raia wa kawaida tu
 
Back
Top Bottom