Yaliyotokana na Kikao cha Kamati Kuu ya Chadema | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Yaliyotokana na Kikao cha Kamati Kuu ya Chadema

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Regia Mtema, Dec 4, 2009.

 1. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #1
  Dec 4, 2009
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Wakuu nimeona nivema nikawapa majina ya kamati kuu mpya ya CHADEMA ili wale wasioifahamu basi waifahamu.

  1.Freeman Aikael Mbowe -Mwenyekiti
  2.Said Amour Arfi (MB)- M/Mwenyekiti Bara
  3.Said Issa Mohamed- M/mwenyekiti Zanzibar
  4.Dr Wilbrod Peter Slaa- Katibu Mkuu
  5. Zitto Zuberi Kabwe- Naibu Katibu Mkuu Bara
  6.Hamad Mussa Yusuph-Naibu Katibu Mkuu Zanzibar
  6. Edwin Mtei- Mwenyekiti Mstaafu
  7.Bob N Makani- Mwenyekiti Mstaafu
  8.Philemon Ndessamburo(MB)
  9.Mhonga Said Ruhanywa (MB)
  10.Shaban Mambo-Mwenyekiti Umoja wa Madiwani
  11.Lazaro Massai-Mwenyekiti wa Halmashauri Karatu
  12.Philip Shelembi
  13.Susan Lyimo(MB)
  14.Mwanamrisho Abama-Zanzibar
  15.Prof Mwesiga Baregu
  16.Dk Kitilla Mkumbo
  17.Nassor Ally Salim -Zanzibar
  18.Regia Estelatus Mtema- Mjumbe mdogo kuliko wote kwa kuchaguliwa
  19.Shida Salum Bitaliho
  20.Leticia G Mosore-Mwenyekiti -Baraza la Wanawake CHADEMA(BAWACHA)
  21.Susan H Kiwanga
  22.Grace Kiwelu(MB)
  23.Paul Herman Sule- Katibu wa Umoja wa Madiwani
  24.Charles Mwera(MB) na Mwenyekiti wa Halmashauri Tarime
  25.Nyangaki Silungushela- Mwenyekiti Baraza la Wazee CHADEMA
  26.John Mnyika-Mkurugenzi
  27.John Mrema-Mkurugenzi
  28.Benson Kigaila-Mkurugenzi
  29.Msafiri Mtemelwa-Mkurugenzi
  30.Victor P Kimesera-Mkurugenzi

  N.B
  Kwa mujibu wa Katiba ya CHADEMA
  1.Viongozi sita wa mwanzo wanaingia kwa kofia zao
  2.Wenyeviti wastaafu wanaingia kwa kofia zao
  3.Wenyeviti wa halmashauri zinazoongozwa na CHADEMA wanaingia kwa kofia zao
  4.Mwenyekiti na Katibu wa Umoja wa Madiwani wanaingia kwa kofia zao
  5.Wawakilishi watano wa wabunge-wanajichagua miongoni mwa wabunge
  6.Wenyeviti wa Mabaraza ya chama yaani Baraza la Vijana CHADEMA(BAVICHA),Baraza la wazee na Baraza la Wanawake
  7.Wakurugenzi wanaingia kwa kofia zao lakini ni wajumbe wasio na kura.
  8.Waliobaki kwa upande wa wanaume waligombea kupitia baraza kuu-hizi ni nafasi tatu tu Bara na moja Zanzibar
  9.Waliobaki kwa upande wa wanawake waligombea kupitia baraza kuu-nazo ni nafasi tatu tu Bara na moja ni Zanzibar-Kati ya hao watatu wawili ni watu wenye ulemavu yaani Regia Mtema na Shida Salum
   
 2. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #2
  Dec 4, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Lete habari pia za vyama vingine why CHADEMA tu
   
 3. Sinkala

  Sinkala JF-Expert Member

  #3
  Dec 4, 2009
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 1,505
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Amepata ya CHADEMA, na wewe kama unayo ya NLD iweke hapa, sidhani kama itaondolewa.
   
 4. M

  Mkulima JF-Expert Member

  #4
  Dec 4, 2009
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 698
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 60
  Muundo wa hiyo kamati kuu itafikiri unasoma kamati ya CCM.

  Kwanini vyama vya upinzani viige muundo ule ule wa CCM? Ningetegemea hii kamati ingelikuwa na watu wachache sana ambao ndio wangelikuwa vichwa wa CHADEMA.

  Mafanikio mema kamati kuu mpya ya CHADEMA.
   
 5. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #5
  Dec 4, 2009
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Nimeleta taarifa hizi kwa kuwa ndio habari nilizonazo na chama pekee kilichoifanya uchaguzi hivi karibuni.
   
 6. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #6
  Dec 4, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,543
  Likes Received: 18,174
  Trophy Points: 280
  Asante, good composition, inapunguza kidogo ile dhana ya Uchagga Chadema, ila I'm not comfortable kwa Kichwa Wilfred Lwakatare kuachwa nje just as ordinary member, wakati kwenye timu yao ni vichwa kadhaa na makapi kibao!.
   
 7. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #7
  Dec 4, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Ni Habari njema sana .Nangojea kusikia wale wanaosema kwamba Chadema ni kampuni mali ya wachaga . Sasa kamati kuu ni hiyo hebu tuanze sasa .
   
 8. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #8
  Dec 4, 2009
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Pasco
  Moja Asante kwa maoni mazuri. Kama nilivyoeleza kwenye thread yangu kwamba kuna walioingia kwa kofia zao na kuna waliogombea,Mpaka sasa sijafahamu kama Lwakatare ananafasi yeyote ndani ya CHADEMA itakayomfanya aingie kwa kofia yake kwani hakugombea kwenye uchaguzi uliopita labda alihofia kuwa mgeni ndani ya CHADEMA hivyo kama angegombea ingeleta picha mbaya kisiasa kwake na kwa chama. Pili naomba unifafanulie hapo nilipoweka RED sijakupata.
   
 9. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #9
  Dec 4, 2009
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,847
  Likes Received: 2,422
  Trophy Points: 280
  wote ni wachagga hao!!! Du si wanasemaga... Wote wachagga!!...propaganda bwana is another thing...!
   
 10. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #10
  Dec 4, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  Halima mdee??????????
   
 11. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #11
  Dec 4, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Nini nafasi ya Chadema Zanzibar?
   
 12. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #12
  Dec 4, 2009
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Sio mjumbe wa Kamati Kuu
   
 13. K

  Keil JF-Expert Member

  #13
  Dec 4, 2009
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hicho kipengele cha wenyeviti wa halmashauri kinahitaji mabadiliko. Tanzania tuna Halmashauri zaidi ya 100, suppose CHADEMA wakishinda kwenye halmashauri 10 tu kati ya hizo zote, je, wote wataingia kwenye Kamati Kuu kwa kofia zao?

  Kufanya mabadiliko baada ya kuona kuna wenyeviti wengi hiyo ndiyo huwa inapelekea kusabisha migogoro kwenye chama kwa kuwa njia ya kuwapata representatives wa hao wenyeviti inaweza "kuonekana inawapendelea" watu/mtu fulani na kuwaonea wengine. Ni vyema mabadiliko hayo yakafanyika mapema ili kuondoa hiyo notion.
   
 14. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #14
  Dec 4, 2009
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Samahani labda sikufafanua vizuri.Ni hivi katika kipengele cha wenyeviti wa halmashauri....Inasomeka hivi Wawakilishi watano wa Madiwani,wawili wakiwa ni madiwani wa kawaida na watatu wawe ni wenyeviti wa halmshauri zinazoongozwa na CHADEMA.Wajumbe hawa watachaguliwa na Umoja wa Madiwani wa CHADEMA....Nadhani nimeeleweka vizuri...
   
 15. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #15
  Dec 4, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,562
  Likes Received: 3,858
  Trophy Points: 280
  Chadema ina watu potential wengi, ila mwambieni Mtei akae kimya, Bob makani katulia na ukimya wake unaheshima, akina Baregu poa ila hawezi kujibu mswali magumu!.Kitila naye aache kuwa biased wote wanatakiwa kuwa neutral kabisa , hata kama wana lao it is better to keep silent to let party moving.
   
 16. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #16
  Dec 4, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Samahani wakuu nina swali. Kamati kuu ina members thelathini. Je hao wote wana lipwa mshahara na chama? Je members ambao wana vyeo vingine kama ubunge na wao wana mshahara wa kamati kuu?
   
 17. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #17
  Dec 4, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145

  Nafasi ya Chadema Zanzibar ni sawa na ile nafasi ya CUF Bara na CCM zanzibar
   
 18. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #18
  Dec 4, 2009
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Kwanini wawe hivyo kwani hawana haki?kwanini Mtei awe kimya?Sio kweli kwamba Prof Baregu hawezi kujibu maswali magumu...anyway huo ni mtazamo wako.....Sidhani kama kuna mwanaharakati au mwanasiasa yeyote anayeweza kuwa neutral labda awe anafanya unafiki,kwa vyovyote vile atakuwa na upande tu...Any way Kitilla ni mwezetu humu JF naomba nisimsemee....Ataeleza mwenyewe.
   
 19. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #19
  Dec 4, 2009
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Yaani wakae kimya au neutral kwa sababu waberoya amesema au kwa sababu ni kiongozi mmoja tu anayetakiwa kuongea chadema (zitto wa dowans)?
   
 20. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #20
  Dec 4, 2009
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  MwanaFalsa1

  CHADEMA hailipi mishahara viongozi wake mishahara.Si wajumbe wa Kamati Kuu,si Baraza Kuu wala si Mkutano Mkuu isipokuwa hulipwa posho ndogo sana za vikao kwaajili ya kujikimu na nauli. Wabunge na Viongozi Wakuu wale wa Bara hawalipwi hata hizo posho za vikao kwa kuwa wameamua kujitolea ingawa ni haki yao kupata. CHADEMA ni chama chenye mapato kidogo hivyo hakina budi kupunguza matumzi yasiyo ya lazima..Viongozi wote wa CHADEMA katika ngazi zote hakuna anyelipwa mshahara kwa sasa isipokuwa watendaji wa Makao Makuu tu.ndio wanapata posho kidogo za kujikimu kwa mwezi.
   
Loading...