Yaliyosisimua hotuba ya rais mwisho wa mwezi january. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Yaliyosisimua hotuba ya rais mwisho wa mwezi january.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kiby, Feb 1, 2011.

 1. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #1
  Feb 1, 2011
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,197
  Likes Received: 1,003
  Trophy Points: 280
  Nimeanza na kichwa cha habari cha kusisimua zaidi kama ilivyo kwa kawaida ya baazi ya magazeti yetu kuandika kichwa cha habari kizito kwa habari nyepesi na wakati mwingine habari kutokuwa na mahusiano na kichwa chenyewe. Dhumuni likiwa la kibiashara zaidi yaani kuuza gazeti.
  Kutokana na kawaida ya rais jk kujiwekea utaratibu wa kuhutubia taifa kila jioni ya tarehe ya mwisho wa mwezi. Jana nilijiandaa na kuwahi kwenye TV yangu kumsubiria rais wangu aanze kushusha data bahati mbaya sana nilibadili stesheni kuanzia tbc, itv, star tv, chanel ten na mpaka kwa kina Fernandes na mwingira bila mafanikio. Nilikuwa na shauku kubwa ya kumsikia mkulu hasa kuusikia ufafanuzi wake juu ya mengi yaliyojiri januari hii kuanzia na la Arusha, mbeya, mwanza, vyuo vikuu, giza lililotanda nchini kwa kukosa umeme, tuzo ya dowansi, uchakachuaji wa mishahara ya maafande, maandamano ya uvccm, Tunisia, evory cost na Misri.
  Kweli baada ya mkulu kutotokea nililala kama mpweke fulani hivi. Jamani wana JF naomba tusaidiane kwa mwenye taarifa za kilichomsibu mkuu wetu asionekane atujuze ili kama kinahusiana na maradhi tuanze kazi ya kumwombea afya njema haraka kwa Mnyazii Mungu. Kama ni mbinu ya kuahirisha matatizo tumkumbuahe kuwa mwisho wa mwezi wa pili yatakuwa yangali yakimsubiri hata kama ataamua kuyaahirisha mpaka desember yatakuwa yangali yakimsubiria. Labda njia pekee ya kuyakwepa ki-short cut ni kuikimbia nchi kama mwenzake wa Tunisia.
  .
   
 2. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #2
  Feb 1, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  ametingwa na maandalizi ya sherehe ya cmm tarehe 5.Kwahio hotuba ya taifa ataitoa kwenye hio siku hili aweze kutangaza chama zaidi.
   
 3. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #3
  Feb 1, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Anajua hadi zije siku 30 nyingine mtakuwa mmesahau au wataibua skendo nyingine ili kufunika hizo ulizotaja.
   
 4. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #4
  Feb 1, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Hongera kwa ubunifu wa kichwa cha habari hii, huyu bwana ana matatizo kuliko matatizo yenyewe.......we msubirie tu tutafika siku moja....tutafika mazima!
   
 5. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #5
  Feb 1, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,816
  Likes Received: 10,106
  Trophy Points: 280
  Dah, nimekugongea thanks maana hata mimi umenichanganya, huyu mkwere hajasikika haapa nyumbani kabisa, hana jipya vyote vya moto sasa, anasubiri akazungumzie hukooooo mbali
   
 6. I

  Ijuganyondo Member

  #6
  Feb 1, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 62
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Yuko addis ababa anahudhuria mkutano wa 21 wa AU!
   
 7. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #7
  Feb 1, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,816
  Likes Received: 10,106
  Trophy Points: 280
  Jamani msii-quote habari nzima, ili mtusaidie sie tunaotumia cm, yaani una-scroll hadi dole linauma!
   
 8. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #8
  Feb 1, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,816
  Likes Received: 10,106
  Trophy Points: 280
  Pengine kajifungia mahali anapanga jinsi ya kuburudisha jeshi lisijekumsaliti kama huko Egypt maana naskia wakimaliza huko na hapa
   
 9. menyidyo

  menyidyo JF-Expert Member

  #9
  Feb 1, 2011
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 1,339
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  kazi imemshinda!
   
 10. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #10
  Feb 1, 2011
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,197
  Likes Received: 1,003
  Trophy Points: 280
  .
  Mkuu kwani tanzania yote ni wana ccm? Hiyo tarehe tano asherehekee na makada wenzake wa chama na kuwahutubia. Lakini kwa habari ya urais tuna haki ya kumsikia kama rais wetu sote yaani wanachama wa vyama vya siasa, wasio wanachama, dini zote na jinsia zote.
  Hatuhitaji hutuba itakayotokana na mchemko wa hamaniko la ushabiki wa chama chake cha siasa.
  .
   
 11. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #11
  Feb 1, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,127
  Likes Received: 1,083
  Trophy Points: 280
  Kweli inaonekana ni Raisi wako pole sana na uendelee kumsubiri akuhutubie!
   
 12. m

  matawi JF-Expert Member

  #12
  Feb 1, 2011
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 2,055
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Samahani Kiby mimi rais wangu ni Slaa huyu Mkwere ni wa ccm
   
 13. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #13
  Feb 1, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  Tangu Dr W.Slaa aongee wakati wa kampeni na kuvutia audiance jamaa anagwaya sana ataongea nini watu wamsikilize?
   
 14. S

  Sebo Member

  #14
  Feb 1, 2011
  Joined: Feb 17, 2009
  Messages: 47
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 15
  :laugh:
   
 15. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #15
  Feb 1, 2011
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,197
  Likes Received: 1,003
  Trophy Points: 280
  .
  Kwani Dr Slaa ni wa chama gani? Kama tutakwenda hivyo basi na wana ccm watasema Slaa ni rais wa Chadema.
  Kimsingi tunamhitaji rais wa watanzania wote yaani wenye vyama na wasio na chama.
  Hata hivyo kwangu mimi binafsi ukiniletea Slaa na Jk ili nichague rais wa watanzania wote nitamchagua Dr Slaa kwani ana kila sifa na uwezo wa kuliongoza Taifa.
  .
   
 16. MartinDavid

  MartinDavid JF-Expert Member

  #16
  Feb 1, 2011
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 876
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  Jk hayuko bongo nadhani alikuwa uswisi na sasa yuko addis ababa ethiopia..

  Halafu atasema nini???? Wakati yeye ndiye mmiliki wa dowans...
   
 17. Ernesto Che

  Ernesto Che JF-Expert Member

  #17
  Feb 1, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,117
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Kwani mmemsahau kwa kukwepa hoja nzito,, kumbuka Znz walipodai ni nchi yeye alikaa kimya mpaka sakata likaisha,, pia KAGODA, MEREMETA, TANGOLD, CHENGE, MRAMBA, n.k kimsingi he is very weak when dealing with serios issues. Mnamuonea kutaka azungumzie mambo yaliyo makubwa kuliko yeye. Nchi hii haina Rais ila ina mfalme asiye na mamlaka ya utendaji kama Uingereza vile.
   
 18. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #18
  Feb 1, 2011
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,197
  Likes Received: 1,003
  Trophy Points: 280
  .
  Basi kama issue yenyewe ndo hii itabidi katika katiba mpya tunayoiendea nitoe mapendekezo ya kuwa na marais wawili. Mmoja awe ni wa sherehe na starehe na wapi awe ni wa kushughulikia matatizo ya wanachi.
  Wakuu hili nalo sii neno??
  .
   
Loading...