Yaliyosemwa na mgombea ubunge Kinondoni mhe. Mtulia kata ya Tandale Jumanne Februari 6, 2018

wandamba

JF-Expert Member
Apr 29, 2014
465
1,000
*YALIYOSEMWA NA MGOMBEA UBUNGE KINONDONI MHE. MAULID SAID MTULIA KATA YA TANDALE JUMANNE FEBRUARI 6, 2018*

"Nikipita Tandale najiona mimi nilisoma Tandale Shule ya msingi na hata Madrasa nimesomea hapa pale AZARIA nafarijika sana kuwaona hapa mmejitokeza kwa wingi kunisikiliza." - Mtulia

"Niliguswa kujiingiza kwenye siasa ili niwasaidie Watu" - Mtulia

"Mwaka 2015 niligombea nikitarajia Wapinzani tutapata Serikali. Iliposhindikana ilani yetu ikawekwa pembeni. Tulikuwa hatuna ujanja wa kuleta maendeleo" - Mtulia

"Mpinzani hana Serikali, hana pesa, hana ilani inayoendesha dola. Huyo Mpinzani ataleta vipi maendeleo?" - Mtulia

"Unapomchagua Mtu uhakikishe anayajua, anaumwa na kuguswa na shida zako. Unapochagua hakikisha unamchagua aliye pamoja nawe" - Mtulia

"Kazi za Mbunge ni nyingi lakini kubwa zaidi ni Utashi! Je anaguswa na matatizo yenu, Mafuriko yakija anatoa msaada, Mimi nimezaliwa Bondeni mvua zikinyesha kilio zikigoma nabeba mchanga nikauze nipate viatu vya Shule hivyo matatizo nayafahamu sana ya hapa." - Mtulia

"Tandale ni Kata yenye mifumo mibovu ya maji safi na taka, hili ni suala dogo nikiingia madarakani ntakaa na Dawasco tulimalize.!" - Mtulia

"Ni lazima ujue Mtulia yupo kwenye chama alicho Rais Magufuli, alipo Mkuu wa Mkoa Makonda, alipo Mkuu wa wilaya Salum Hapi. Hawa wote ni Watu wa kimaendeleo, nichagueni nikashirikiane nao kuwaletea maendeleo" - Mtulia

"Leo hii mnataka mabasi yapite Tandale, barabara zisizo pitika ziwekwe vifusi na lami zipitike, leo hii mnataka mabomba ya maji yawekwe sawa. Hii ni kazi nyepesi ndani ya CCM" - Mtulia

"Wewe wa Tandale mwenzangu ukinikataa si umekataa maendeleo?" - Mtulia

"Naomba mnipigie kura za ndiyo Februari 17 na mkitoka hapa muende mkaniombee kura kwa waliopo majumbani. Nikopesheni imani, niwalipe maendeleo." - Mtulia

Maulid Said Mtulia ni Mgombea Ubunge jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya CCM
FB_IMG_1517933913559.jpg
FB_IMG_1517933916984.jpg
FB_IMG_1517933985961.jpg
FB_IMG_1517933920339.jpg
FB_IMG_1517933924025.jpg
FB_IMG_1517933927484.jpg
 

kigogo warioba

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
5,595
2,000
Anaomba kukopeshwa imani! aisee.. kumbe inaonekana hana imani kabisa huyu! amesahau kua anadaiwa imani aliopewa na wana cuf!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom