Yaliyosemwa katika kampeni ya kumnadi mgombea ubunge wa CCM Kinondoni 12/02/2018

Egnecious

JF-Expert Member
Jul 8, 2015
871
1,000
YALIYOSEMWA KAMPENI ZA CCM KUMNADI MGOMBEA UBUNGE (CCM) KINONDONI 13 FEB

"Nakupongeza sana Mtulia kwa uwezo mkubwa ulioonyesha wa kunadi sera za kimaendeleo kuliko wagombea wote" - Mussa Azan Zungu, MB (Ilala)

"Wanasema Mtulia angemuunga mkono Rais Dk. Magufuli akiwa huko huko upinzani. Hivi unawezaje kushangilia timu ya Yanga ukiwa kwenye jukwaa la Simba?" - Nitha Stanley Lameck, Mwenyekiti Chipukizi Taifa

"Mchague Mtulia kwa sababu amekataa kuwa Mbunge wa kutukana, kuziba mdomo na kutoka nje ya Bunge. Mtulia ni Mwakilishi wa kweli wa Wananchi, hakubali kuburuzwa" - Martha Mlata, MB

Tsh. Milioni 55 za kujenga barabara zipo tayari Diwani amezizuia; Zipo pia pesa Tsh. Milioni 45 za kuchimba mifereji, Diwani amezizuia. Mchagueni Mtulia akahakikishe pesa zinaachiwa mnapata maendeleo" - Iddi Azzan

"Uchaguzi huu hamchagui ilani kwa sababu ipo, hamuendi kuchagua sera kwa sababu zilishachaguliwa 2015, awamu hii mnaenda kuchagua mtu sahihi kwa wana Kinondoni ambaye ni Mtulia" - Sixtus Mapunda, MB

"Mtulia alikuwa kila akifanya jambo la kimaendeleo, alikuwa akirudishwa nyuma. Akaona bora ahame kwenye timu ya upinzani maana inawacheleweshea maendeleo wana Kinondoni" - Sixtus Mapunda, MB

"Msitegemee hata siku moja Wapinzani watasema neno jema kwa Mtulia, maana Mtulia anajali maendeleo ya Watu ambayo wapinzani hawapendezwi nayo" - Sixtus Mapunda, MB

"Mtulia ametulia, ni Mwaminifu nyakati zote" - Sixtus Mapunda, MB

"Niligombea jimbo la Kinondoni ili niwe mtetezi wa Wanyonge na si wa posho wala mshahara" - Mtulia

"Maulid Mtulia ni Mbunge ambaye kazi yake ni kuleta maendeleo" - Mtulia

"Lengo la Ubunge wa Mtulia ilikuwa si kupokea mshahara, si kupokea posho, si kupokea kiinua mgongo. Lengo la Ubunge wangu ni kuwaletea maendeleo kwa wana Kinondoni" - Mtulia

"Wakati wa Ubunge wangu niliishi kwenye wakati mgumu kutokana na chama kugawanyika pande mbili. Kila niliyekuwa nikifanya nae kazi, upande mwingine ulikuwa unanilaumu" - Mtulia

"Nilikataa kuwa Mbunge wa chama, Ubunge wa kufuata maagizo. Kuwatumikia Wananchi bado ninataka, tatizo lilikuwa kwenye chama kile nilichokuwepo" - Mtulia

"Wakati najiuzulu nilijua fika Ubunge utaenda kwa CCM kwa sababu CCM ni Chama Cha Kimaendeleo" - Mtulia

"Uteuzi niliopewa na CCM kugombea tena Ubunge umenisaidia sana kuweza kufikia malengo yangu ya kufikisha maendeleo kwa wana Kinondoni" - Mtulia

"Serikali inaposhirikiana na Maulid Mtulia, wewe utakosa maendeleo? Huo ndio usaliti? - Mtulia

"Mimi ndio mgombea pekee mwenye mahusiano mema na viongozi na Serikali. Hii itasaidia kuleta maendeleo kwenu kwa haraka" - Mtulia

"Pesa za barabara, Zahanati, kuchimba mifereji na kuboresha masoko zipo tayari. Nichagueni niende kuzisimamia ufanisi uonekane, mpate maendeleo" - Mtulia

"Baada ya kusikia nalalamika mno juu ya kamata kamata ya bodaboda, Mkuu wa Mkoa Paul Makonda amezuia aina yote ya kamata kamata kwa bodaboda" - Mtulia

"Mkinichagua Vijana na akina Mama nitahakikisha ile mikopo ya asilimia 10 toka Manispaa inawafikia kwa wakati" - Mtulia

"Mkinichagua nitaenda kuboresha zaidi upatikanaji wa huduma bora za kiafya ikiwemo kuhakikisha Wazee wote wanapewa Bima za afya za matibabu bure" - Mtulia

"Nazidi kuwasisitiza muende mkaniombee kura kwa walio majumbani na Februari 17 muwahi vituoni muende mkanipigie kura za ndiyo. Ushindi kwa Mtulia ni lazima" - Mtulia
IMG-20180213-WA0025.jpg

IMG-20180213-WA0024.jpg
 

Mshuza2

JF-Expert Member
Dec 27, 2010
7,939
2,000
Uchi wa akili ni mbaya kuliko uchi wa nyama..hiki kinaenda kuwa kipimo halisi cha akili za watanzania!
 
  • Thanks
Reactions: Nzi

Moisemusajiografii

JF-Expert Member
Nov 3, 2013
14,332
2,000
Wanamnadi huku ndani kabisa mioyoni wanahisi aibu sana.Lakini,ukiwa CCM hivi akili huwa wanaziacha zipumzike wapi?Terrible, huh!?
 
  • Thanks
Reactions: Nzi

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom