*YALIYOSEMWA KAMPENI ZA CCM KUMNADI MGOMBEA UBUNGE (CCM) KINONDONI MHE. MTULIA KATA YA NDUGUMBI TAR. 14FEB*
"Mtulia asubuhi alikutana na Waziri Mkuu Majaliwa akapewa fursa ya kuwasilisha shida za wana Kinondoni. Ameshaanza kufanya kazi ya Ubunge hata kabla ya kupigiwa kura" - Mussa Azzan Zungu, MB (Ilala)
"Mtulia ni Kiongozi makini, anafaa kuwa Mbunge wenu" - Zainabu Katimba, MB
"Mtulia alipenda sana kuwatumikia Watu wake ila tatizo lilikuwa kwenye timu yake ya usajili ilikuwa mbovu, haina nguvu" - Abdallah Ulega, MB (Mkuranga)
"Nimefanya kazi na Mtulia mara nyingi, ni Mtu makini anafaa kuwa Mbunge wenu" - Suleiman Jafo, MB (Kisarawe)
"Mtulia tuna mkubali sana, naomba mtuletee Mtulia tufanye nae kazi za kimaendeleo." - Dk. Tulia, NS
"Mtulia ameingia kwenye chama chenye ilani ambacho kinakaa vikao vyake mara kwa mara vya kimaamuzi vya kuleta maendeleo" - Dk. Tulia, NS
"Wanaosema kurudia uchaguzi ni gharama, wanataka kuturudisha kwenye mfumo wa chama kimoja" - Hussein Bashe, MB (Nzega Mjini)
"Sisi Wabunge tuliokuja hapa tupo tayari kuwa sauti ya Mtulia, sauti ya wana Kinondoni kwenye shida, kero na karaha zenu" - Hussein Bashe, MB (Nzega Mjini)
"Benki ya Dunia imeshatoa pesa za kutengeneza Mto wa Ng'ombe, mchagueni Mtulia akasimamie ufanisi wake" - Idd Azzan
"Mwenyekiti wa Mtaa amekula pesa za kulipia maji ndio maana maji hayatoki. Mchagueni Mtulia akamalize tatizo hilo muanze kupata huduma ya maji kama awali" - Idd Azzan
"Mtulia ni Mchezaji mzuri mwenye maono na fikra nzuri, anawafaa wana Kinondoni" - Sixtus Mapunda, MB (Mbinga)
"Mtulia alikuwa na wakati mgumu wakati yupo upinzani kutokana na kukwamishwa na wenzake waliokuwa hawataki Serikali ipate sifa ya kuwaletea maendeleo Wananchi." - Sixtus Mapunda, MB (Mbinga)
"Nilipata nafasi ya kuwa Mbunge. Ulikuwa Ubunge wa mashaka, wenye masharti na lawama tele." - Mtulia
"Timu kubwa ya viongozi wa kitaifa wakiwemo Wabunge, Naibu Spika na Mawaziri ni ishara tosha ya kuwapata wenzangu wapya wenye ushirikiano. Maendeleo lazima yatapatikana" - Mtulia
"Mto wa Ng'ombe na Mto Mwangosi, barabara za Argentina na Sinza nitahakikisha zinajengwa. Pesa zipo tayari" - Mtulia
"Nitahakikisha Vijana wanakopeshwa Pikipiki toka asilimia 5 ya Manispaa" - Mtulia
"Akina Mama nao pia sijawasahau, kuna pesa asilimia 5 toka Manispaa nitahakikisha mnapatiwa mikopo ya ujasiriamali" - Mtulia
"Waziri wa Tamisemi yupo hapa, naomba atusaidie kufanya marekebisho ya kimiundo mbinu kwenye shule za jimbo la Kinondoni" - Mtulia
"Mwenyekiti aliyeshindwa kulipa bili ya maji, deni hilo linakwenda kulipwa na Wananchi muendelee kupata maji safi na salama kama awali" - Mtulia
"Mnanijua sana, mnaujua uwezo wangu kiuongozi. Nawaombeni sana mkaniombee kura kwa waliopo majumbani na tarehe 17 muwahi vituoni mapema mkanipigie kura ya ndio niwe Mbunge wenu. Naombeni sana kura zenu za ndiyo." - Mtulia