Yaliyosemwa kampeni za CCM kumnadi mgombea ubunge (CCM) Kinondoni mhe. Mtulia kata ya Mwananyamala tar. 15 Feb, 2018

JINOME

JF-Expert Member
May 29, 2017
958
1,000
*

"Nawaomba sana mumpigie kura za ndiyo Mtulia kwa sababu anaweza na ni Mtu sahihi anayewafaa Vijana na Wana Kinondoni wote." - Tabia Mwita, Makamu Mwenyekiti UVCCM Taifa

"Mtulia ni Mtu sahihi kwa maendeleo ya wana Kinondoni." - Tabia Mwita, Makamu Mwenyekiti UVCCM Taifa

"Mtulia anatokana na chama kilichopo madarakani na chenye Serikali. Atawaletea maendeleo, anafaa mpe kura yako ya ndiyo" - Muslim Hassanali

"Mgombea wa Chadema ni miongoni mwa wapiga kura wenu? Atakuwaje Chaguo la wana Kinondoni" - David Kafulila

"Sina mashaka na uwezo wa Mtulia kwa sababu amepikwa vyema, mwaka 2008 alipelekwa Marekani kwenda kupikwa kuwa kiongozi. Ninajua ana uwezo wa kiuongozi" - David Kafulila

"Kama kigezo cha kuchagua chama bora, Chama Cha Mapinduzi ni chama cha kwanza Afrika na cha pili kwa ubora Duniani. Chagueni Chama bora cha CCM" - David Kafulila

"Mtulia amekuwa Mbunge kwa miaka 2, ukimchagua hatakuwa mgeni kiutendaji Bungeni" - David Kafulila

"Mtulia anavyogombea shida yake si mshahara wala posho kwa sababu alikubali kuviacha kwa kujiuzulu. Mtulia ana kiu ya kuwaletea maendeleo wana Kinondoni" - Mhe. Livingstone Lusinde, MB (Mtera)

"Kama ni usaliti, Mtulia hajakusaliti bali ameisaliti familia yake kwani kwa miezi zaidi ya mitatu hapokei mshahara." - Mhe. Livingstone Lusinde, MB (Mtera)

"Ukimchagua Mtulia Serikali itajitahidi kuleta maendeleo Kinondoni ili uchaguzi wa mwaka 2019 na wa mwaka 2020 CCM iweze kushinda kwa kishindo." - Mhe. Livingstone Lusinde, MB (Mtera)

"Wakati Wabunge wa upinzani wakitoka nje, Mtulia ni Mbunge pekee wa upinzani aliyebaki Bungeni kupitisha Bajeti ya nchi. Mtulia anawafaa wana Kinondoni" - Mhe. Suleiman Jaffo, MB (Kisarawe)

"Nyie ni mashahidi namna Mtulia anavyoshirikiana nanyi kukabiliana na mafuriko" - Mhe. Suleiman Jaffo, MB (Kisarawe)

"Mtulia anajua magumu aliyokutana nayo akiwa Mbunge upinzani, ameamua kubadili gia angani na kupanda basi linaloelekea kwenye maendeleo." - Ridhiwani Kikwete, MB (Chalinze)

"Mawaziri, Wabunge, na viongozi wa Serikali waliokuja hapa ni dalili ya ushirikiano tosha atakaoupata Mtulia kuwaletea maendeleo wana Kinondoni. Mchagueni Mtulia" - Dk. Tulia Ackson, NS

"Nimekuwa Mbunge kwa miaka miwili, kuwa Mbunge upinzani ni kazi ngumu sana." - Mtulia

"Namwomba sana Waziri Jaffo atusaidie kutupatia pesa za kusaidia ujenzi wa soko la Mwananyamala" - Mtulia

"Tunaomba Serikali sikivu isamehe deni la Marehemu. Nichagueni nikasimamie hilo" - Mtulia

"Nichagueni nikasimamie Vijana na akina Mama wanapata mikopo ya asilimia 10 toka Manispaa" - Mtulia

"Nichagueni nikaungane na timu kubwa ya Serikali iliyopo madarakani kuwaletea maendeleo" - Mtulia

"Nawaombeni sana Ndugu zangu nyoote mniombee kura na Jumamosi Februari 17 mjitokeze kwa wingi, mapema vituoni mnipigie kura za ndiyo" - Mtulia
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom