Yaliyonishangaza kwenye sikukuu ya mapinduzi mwaka huu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Yaliyonishangaza kwenye sikukuu ya mapinduzi mwaka huu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Congo, Jan 14, 2012.

 1. Congo

  Congo JF-Expert Member

  #1
  Jan 14, 2012
  Joined: Mar 13, 2008
  Messages: 1,272
  Likes Received: 559
  Trophy Points: 280
  Sikukuu ya Mapinduzi huja na kupita kila mwaka tangu yalipofanyika mwaka 1964. Jambo moja huwa nalishangaa kila mwaka. Gwaride huandaliwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na kukaguliwa na Rais wa Zanzibar. Hili hunishangaza sana kwa sababu Rais wa Zanzibar sio Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Rais wa Zanzibar angetakiwa kukagua gwaride la vikosi vya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, (KMKM, Valantia, Chuo cha Mafunzo n.k.). Kwangu mimi hivyo ndivyo vikosi sahihi ambavyo vingestahili kukaguliwa wakati wa Sherehe za Mapinduzi. Pili, Pemba kuna timu ya mpira wa Miguu inaitwa Jamhuri. Sasa, wakati wote wa mashindano ya kombe la Mapinduzi timu hiyo ilikuwa ikiitwa JAMHURI YA PEMBA. Nilipokuwa natafakari nilidhani Pemba ni nchi tena Jamhuri na nchi hiyo imeleta timu kucheza kwenye mashindano ya Mapinduzi. Kumbe ni timu iitwayo Jamhuri na inatoka Pemba. Nikakumbuka wakati wa malumbano huko visiwani (sina uhakuka ni mwaka gani) wakati wa mashindano ya klabu bingwa ya Afrika ilikuwa ni marufuku Sauti ya Zanzibar au TVZ kutamka shirikisho la mpira wa miguu barani Africa kwa kifupi. CAF (sema kafff). hii ingekuwa sawa na kukipa ujiko chama cha siasa kiitwacho CUF (kwa matamshi kafff). Sasa sijui kama hiyo timu iitwayo Jamhuri ya Pemba ni bahati mbaya au ni makusudi ili kupalilia ujio wa Jamhuri ya Pemba kisiasa kama baadhi wa wenzetu wa Pemba wanavyotaka.
   
 2. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #2
  Jan 14, 2012
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,640
  Likes Received: 2,872
  Trophy Points: 280
  Hivi Zanzibar ni mwanachama wa CAF au CUF?
   
 3. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #3
  Jan 14, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Aisee hapo kwenye heading kuna neno 'KIKUKUU' linaumiza sana kichwa mkuu. Jaribu kurekebisha.
   
 4. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #4
  Jan 14, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Liwe na liwalo kwani muungano sioni hata faida yake
   
Loading...