Yaliyonipata Muhimbili baada ya kifo cha mwanangu siku ya tar03.03.2012!!!!!

nimesoma thread hii nahisi kama napata mshutuko mkubwa,kweli 2mefikia hapa,haya mtoto wa Mkulima na Nape NNauye
 
pale muhimbili kuna kitengo cha emergence,kama mgonjwa ni mahututi huna kipingamizi kumpeleka,wangu alikua anahitaji hewa ya oxjeni.
Umeweka read kama kuonyesha huamini kama kweli likukua nazunguka na mwanangu kumtafuta muhusika,naomba uje kwangu banana nikuonyeshe picha nilizopiga kupitia simu yangu ya mkononi nikiwa nimebeba maiti ya mwanangu,kuhusu kikao chao mm sijui na wala siitaji kujua kiliisha saa ngapi,mwisho kabisa nawe ipo siku yatakukuta haya.

Spika, tafadhali elewa vitu ukiwa unashauriwa na wenzako. Umeombwa/umeshauriwa kumaliza msiba kwanza. utakapoisha utajua/utakua na nguvu ya kujua kipi cha kutamka na kipi hakipasi. Unaweza kukosea ama ukawaona watu wengine wanakukosea, tatizo ni wakati.

Hapa unachuandika kinamchanganyiko wa majonzi ya kufiwa mtoto (ambalo kiukweli linauma mno hasa pale anapokufa mbele yako au mikononi mwako). Ni jambo zito sana. Ndiyo sababu kama katika ile thread ya kwanza kuhusu kufiwa kwako, watu wengi wakawa wanakumbea Mwenyezi Mungu akuvushe kipindi hiki kigumu au akufaji ama akutie nguvu. hawakufanya hivyo ili waonekane wameandika la, kuna maaan kubwa sana. Rudi kasome moja baada ya nyingine na kutafakari ujumbe waliokuwa wanakuachia.

Tafadhali, naomba spika utulie kwanza hili lipite. Maliza msiba kwanza JF ipo. Huko baadaye twaweza jadili.

Si unaona ulivyomkosea mwenzako kama kumtakia na yeye sikumoja aje afiwe na mtoto wake. Maana hiyo ndiyo tafsiri ya sentensi yako ya mwisho niliyotia rangi nyekundu.
 
Hivi sisi tumerogwa?? hii story imenifanya nikumbuke mjomba wangu aliyepoteza maisha kipindi cha mgomo. Nduguzangu Tatizo hapa ni CCM sio madaktari. Halafu utakuta 2015 bado mijitu inakipigia Kura kirudi madarakani nafikiri imefikia hatua tuungane tubadili uongozi wa nchi hii. ili chama chochote kitapokuwa madarakani kijue kinaweza badilishwa na wananchi. Na utashangaa Arumeru Washili wanakirudisha CCM kwa kumchagua mbunge wao. Please endapo umewekwa kama msimamizi wa chama cha upinzani usikubali rushwa ili waibe kura. Hii imeniuma sana. Watz wenzangu CCM ni tatizo hebu tuweke hii dhana ya Mungu kaandika na siku imetimia pembeni maana kwanini kwa wenzetu wasioabudu Mungu maisha bado ni marefu ni kawaida kumkuta mzee wa miaka 80 na zaidi.

Hebu tujue tatizo na hili liwe mfano tosha kuwa ndugu zetu watoto wetu wapendwa wake zetu waume zetu wanakufa kisa mfumo mbovu. Wewe ndugu unayevaa fulana na kofia na kuona CCM ndio yenyewe badilika tafadhali
 
yatosha baba mshukuru mungu kwa kila jambo..pole sana.

siku zote mnaambiwa kuweni makini na afya za watoto. Mtoto mdogo sio sawa na watu wazima,huwezi jua nini kinamsumbua. Three days delay kwa mtoto ni sawa na death sentence kwa mtuhumiwa. Naomba kikao cha jumamosi kisihusishwe kabisa! Kulikuwa na madaktari wachache sana kutoka muhimbili,aafu wale waliokuwa zamu walikuwa kazini. Kutokana na maelezo yako inaonesha huyo mwanao alikuwa na severe pnemonia na hakutakiwa kuwa delayed mpaka siku tatu. Hao watu wa dispensary huwa wanagues tu ndo maana wakammismanage mwanao. Ulitakiwa uchukue hatua ya kwenda hospitali siku ya kwanza tu. Aafu upo dar,hizo dispensary ni sehemu ya first aid hapa mjini! Pole kwa kufiwa ila mgomo haukuwepo mwanao alishafika kwenye end stage ndo ukaenda naye muhimbili.
 
Binafsi nilishakupa pole zangu kwenye thread ya taarifa ya msiba wa Mwanao, ila ili kuweka kumbukumbu sawa ni kwamba hakuna Dispensary inayotoa Rufaa kwenda Muhimbili, nadhani hapa umejichanganya labda kutokana na msiba.
kaka unataka kutuambia katunga? sidhani kama inawezekana mtu kujitungia kitu hapa jf ili iweje. afu useme mwanao, maiti yake umekaa nayo mikononi masaa mawili. utakuwa ni ujinga. kama ni kutunga stoli basi angesema mtoto wa rafiki yake na n.k. ila pole mkubwa ndo tanzania yetu hiyo.
 
Mkuu, pole sana kwa masaibu yaliyokukuta na pole sana sana kwa kuondokewa na mwanao kipenzi.

Tutafanikiwa kuyaondoa hayo kwenye jamii yetu endapo tutaiondoa ccm na serikali yake madarakani na kuweka serikali ya wananchi, na itakayojali maslahi ya wananchi. Serikali itakayolinda haki za watu wote kwa usawa. Serikali itakayowalipa madaktari haki zao ili wafanye kazi zao, na serikali itakayotuhakikishia sisi wananchi haki yetu ya kutibiwa na madtari wanaolipwa kwa kodi zetu, badala ya kuachwa tukifa bila huduma.
 
Pole sana. Ni matokeo ya mambo mengi. Mosi ni ukiukwaji wa maadili na miiko ya kazi...vikao vya kujadili maslahi binafsi vingefanyika huku baadhi yao wakiachwa kuhudumia wagonjwa wa dharura..kinyume cha hapo ni ukiukwaji mkubwa na ubinafsi uliopitiliza wa kuthamini zaidi matumbo yao na si huduma kwa wananchi... kwa hilo madaktari hao 'uchwara' hawana tofauti na wabunge wetu 'wapiga mbonji' wanaojali zaidi matumbo yao kuliko kero za wananchi. Na serikali haikosi kulaumiwa kwa kudekezaacheni unafiki mtoto anayesema huwa anapokelewa emergency wanamstabilize kwanza ndo anaenda wodini. Na emergency siku ile hazikufungwa na madaktari wa mnh kikaoni walikuwa wachache sana,wengi walikuwa kazini siku ile. Ameshakuambia mtoto alifariki wakiwa kwenye harakati za kumuwekea oksijen ambayo inaonesha alishafika kwenye hali mbaya baada ya kucheleweshwa. Huyo kijana anayesema mdogo ndo daktari aliye kuwepo zamu,yawezekana alitegemea kukutana na watu wenye vipara ndo maana anasema madaktari hawakuwepo. Mtoto alicheleweshwa kwa delay ya mzazi na dispensary alikoanzia. Ni ngumu kuanza kukuelekeza kwenye key board ila kwa anayejua ameshatambua tatizo liko wapi. Ujue grieving inasababisha mtu awe anaconvict wengine kuwa ndo wenye makosa
 
Hivi wadau tumfanye nini huyu png..ani Vasco da Gama akienda kuvumbua nchi za mbali na huku nyuma atuachie mgomo wa madk? Yaani hili punga lina kiburi nyie mtajionea wenyewe! Kama halitaenda safari, litakaa kimya!
 
Ndg zangu wana JF nadhani niliwapa taarifa juu ya kifo cha mwanangu mpendwa "MARIAM ALLY"aliyefariki siku ya j,mosi usiku.
Mwanangu alikua na umri wa miezi 9 hv,alianza kuugua malaria siku ya tar 29.02,usiku,tukampeleka dispensary alfajiri ya tar 1.3 na akapata vipimo na kuandikiwa doz ya malaria bcoz alikua na malaria "2".

Aliendelea na doz mpaka siku ya tar 3 asubuhi nilipogundua kama anaupungufu wa maji mwilini,tukamrudisha dispensary ile ile kwa ajiri ya kumcheki tena,baada ya kumcheki dk alisema amepungukiwa maji kwahiyo anatakiwa kupewa drip,alitundikiwa drip kuanzia majira ya saa 5 asubuhi,ilipofika majira ya saa 12 jioni dr akatupa rufaa kwenda muhimbili, nilikodi tax na tukafika muhimbili ndani ya muda muafaka,nilipokelewa na dr1 hv bwana mdogo na alijaribu kunisaidia ili tumuwaishe kwenye oxsijen lakini ilishindikana maana madaktari walikua na kikao cha kupanga mgomo mpya.

So mwanangu akawa amefariki kwenye mikono ya mamake,nilishukuru mungu kwa yote, sasa nikaanza utaratibu wa kutoa maiti kuipeleka mochwari,ilituchukua kama dk 40 hv kupewa kibali cha kuipeleka mochwari,still bado haikua problem sana kwangu.

Sasa kilichonikera na kunisikitisha ni baada ya kufika mochwari sikumkuta muhusika wa mochwari na sasa ikanibidi kuzunguka kumtafuta muhusika huku nikiwa nimeibeba maiti ya mwanangu mikononi,punde alifika ndg yangu mmoja niliyekua nimempigia simu aje kunichukua na gari yake bcoz wife tayari alikua ameshachanganyikiwa,so ilibidi mimi nikae kwenye mrango wa mochwari kwa takribani masaa hv ili kumsubili muhusika na ndg yangu huyo pia akaanza kumtafuta na kumpata baada ya masaa 2 hivi.

Baadae niligundua kwamba madaktari walikua bado wanaendelea na kikao cha mgomo uliopangwa kuanza j5 nchi nzima,
Sasa ni swali kwa wana JF, Jee kama hayo yanatokea muhimbili jee sisi tusio na uwezo wa kwenda INDIA tutapona kweli???

Naombeni comments.
pole sana kwa kumpoteza mwanao, nachelea kusema kua hiyo ni kazi ya Mungu kama tulivyozoea kusema waafrika. Pengine kifo hicho kingeweza epukika,lakini .......Wasiwasi wangu katika taarifa yako ni mtiririko wa matukio,na muda uliofika muhimbili kikao cha madaktari kilichofanyika water front kilikua kimeshakwisha hata taarifa zimesha sambazwa kwenye vyombo vya habari( mi nilizipata mida ya saa kumi hivi) sasa hicho kikao gani tena mida hiyo (suppose) saa moja usiku?? story inatia shaka,japo inasikitisha
 
Pole sana mdau..madakitari na system nzima imekuangusha na kusababisha mauti na usumbufu. Kutokujali afya ni kutokujali uhai, wahusika wanafahamika na hawawajibishwi wala kutikiswa, nisiseme mengi na kuzidi kukutia machungu.
 
pole sana kwa kumpoteza mwanao, nachelea kusema kua hiyo ni kazi ya Mungu kama tulivyozoea kusema waafrika. Pengine kifo hicho kingeweza epukika,lakini .......Wasiwasi wangu katika taarifa yako ni mtiririko wa matukio,na muda uliofika muhimbili kikao cha madaktari kilichofanyika water front kilikua kimeshakwisha hata taarifa zimesha sambazwa kwenye vyombo vya habari( mi nilizipata mida ya saa kumi hivi) sasa hicho kikao gani tena mida hiyo (suppose) saa moja usiku?? story inatia shaka,japo inasikitisha
Binafsi nimetoka kwa bwana spika leo jioni mida ya saa 3 pale maeneo ya KIPUNGUNI banana ukonga,ni kweli kabisa huyu bwana kafiwa na wamezika jana,nilipita pale wakati nikitokea kitunda.
Na pia kanionyesha picha 2 ambazo amepiga akiwa maeneo ya mochwari muhimbili uku akiwa amemkumbatia maiti ya mwanae aliyoifunga kwenye kitenge.
Nimejaribu kumuomba ili tuiweke picha hiyo hapa ili watu waione lakini amekataa na kusema kua kwa mujibu wa dini yake hairuhusiwi kumuonyesha maiti hadharani maana ni sawa na kumdhalilisha.
Kwa yeyote atakayetaka kufika kwake ili akashuhudie mwenyewe ni vema akaenda kesho maana kutakua na kisomo cha kuhitimisha shughuri nzima!
Nimeacha maandalizi yanaendelea!!!!!
 
pole sana,i can feel your pain.maana kufiwa na mtoto ni maumivu yasiyoelezeka
 
pole sana mkuu....jumamosi walio kazini ni madktari wa zamu na walikuwepo.kikaoni walikuja ambao hawakuwa zamu.kazi ya Mola haina makosa.be strong kaka
 
Ndg zangu wana JF nadhani niliwapa taarifa juu ya kifo cha mwanangu mpendwa "MARIAM ALLY"aliyefariki siku ya j,mosi usiku.
Mwanangu alikua na umri wa miezi 9 hv,alianza kuugua malaria siku ya tar 29.02,usiku,tukampeleka dispensary alfajiri ya tar 1.3 na akapata vipimo na kuandikiwa doz ya malaria bcoz alikua na malaria "2".

Aliendelea na doz mpaka siku ya tar 3 asubuhi nilipogundua kama anaupungufu wa maji mwilini,tukamrudisha dispensary ile ile kwa ajiri ya kumcheki tena,baada ya kumcheki dk alisema amepungukiwa maji kwahiyo anatakiwa kupewa drip,alitundikiwa drip kuanzia majira ya saa 5 asubuhi,ilipofika majira ya saa 12 jioni dr akatupa rufaa kwenda muhimbili, nilikodi tax na tukafika muhimbili ndani ya muda muafaka,nilipokelewa na dr1 hv bwana mdogo na alijaribu kunisaidia ili tumuwaishe kwenye oxsijen lakini ilishindikana maana madaktari walikua na kikao cha kupanga mgomo mpya.

So mwanangu akawa amefariki kwenye mikono ya mamake,nilishukuru mungu kwa yote, sasa nikaanza utaratibu wa kutoa maiti kuipeleka mochwari,ilituchukua kama dk 40 hv kupewa kibali cha kuipeleka mochwari,still bado haikua problem sana kwangu.

Sasa kilichonikera na kunisikitisha ni baada ya kufika mochwari sikumkuta muhusika wa mochwari na sasa ikanibidi kuzunguka kumtafuta muhusika huku nikiwa nimeibeba maiti ya mwanangu mikononi,punde alifika ndg yangu mmoja niliyekua nimempigia simu aje kunichukua na gari yake bcoz wife tayari alikua ameshachanganyikiwa,so ilibidi mimi nikae kwenye mrango wa mochwari kwa takribani masaa hv ili kumsubili muhusika na ndg yangu huyo pia akaanza kumtafuta na kumpata baada ya masaa 2 hivi.

Baadae niligundua kwamba madaktari walikua bado wanaendelea na kikao cha mgomo uliopangwa kuanza j5 nchi nzima,
Sasa ni swali kwa wana JF, Jee kama hayo yanatokea muhimbili jee sisi tusio na uwezo wa kwenda INDIA tutapona kweli???

Naombeni comments.
Pole sana kwa kufiwa na pia kwa ujasiri wa kuandika kwa yaliyokusibu.
Ndani ya msiba huu kuna mafunzo ambayo inabidi tuyapitie kwa pamoja.
Kwanza ni kuhusu zahanati hasa za binafsi.Hizi zimekuwa kila wakati zikitoa majibu ya malaria parasite 2/200WBC,huu ni utapeli mkubwa.kuhusu zahanati hizi tena ni kuwa haziendeshwi kwa maadili na hii inatokana na Tanganyika Medical Board kutokufanya kazi zake vizuri.
Ukiangalia muda alowekewa dripu si ajabu alipata circulation overload na hii inaweza kuwa sababu za kifo chake.Intravenous fluid zina heasabu zake hasa kwa mtoto si suala la kuweka tu.
Jambo lingine ni kuhusu mortuary ya Muhimbili.Unaliliona hapoa Muhimbili ndivyo ilivyo kwa idara zote za serikali.System yote imeoza,watu wansoma magazeti asubuhi,wanfurahia kuona foleni,wanakwenda kunywa chai one hour.
Ninakupa pole sana lakini epuka zahanati za mitaani kwani kama sio malaria +2 basi ni typhoid.
 
Kuna member kaandika kuhusu MADAKTARI UCHWARA n WABUNGE WAPIGA MBONJI ambao kwa pamoja wanajali maslahi yao kuliko AFYA ZA WALIO WENGI huku wote hao wakipewa sapoti na wengi wetu....! Tumepotea wote kwa kusapoti pande husika!!! "WAPIGANAPO TEMBO WAWILI,ZIUMIAZO NYASI"
 
Back
Top Bottom