Yaliyonipata Muhimbili baada ya kifo cha mwanangu siku ya tar03.03.2012!!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Yaliyonipata Muhimbili baada ya kifo cha mwanangu siku ya tar03.03.2012!!!!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by CHAI CHUNGU, Mar 5, 2012.

 1. CHAI CHUNGU

  CHAI CHUNGU JF-Expert Member

  #1
  Mar 5, 2012
  Joined: Feb 20, 2012
  Messages: 7,160
  Likes Received: 107
  Trophy Points: 160
  Ndg zangu wana JF nadhani niliwapa taarifa juu ya kifo cha mwanangu mpendwa "MARIAM ALLY"aliyefariki siku ya j,mosi usiku.
  Mwanangu alikua na umri wa miezi 9 hv,alianza kuugua malaria siku ya tar 29.02,usiku,tukampeleka dispensary alfajiri ya tar 1.3 na akapata vipimo na kuandikiwa doz ya malaria bcoz alikua na malaria "2".

  Aliendelea na doz mpaka siku ya tar 3 asubuhi nilipogundua kama anaupungufu wa maji mwilini,tukamrudisha dispensary ile ile kwa ajiri ya kumcheki tena,baada ya kumcheki dk alisema amepungukiwa maji kwahiyo anatakiwa kupewa drip,alitundikiwa drip kuanzia majira ya saa 5 asubuhi,ilipofika majira ya saa 12 jioni dr akatupa rufaa kwenda muhimbili, nilikodi tax na tukafika muhimbili ndani ya muda muafaka,nilipokelewa na dr1 hv bwana mdogo na alijaribu kunisaidia ili tumuwaishe kwenye oxsijen lakini ilishindikana maana madaktari walikua na kikao cha kupanga mgomo mpya.

  So mwanangu akawa amefariki kwenye mikono ya mamake,nilishukuru mungu kwa yote, sasa nikaanza utaratibu wa kutoa maiti kuipeleka mochwari,ilituchukua kama dk 40 hv kupewa kibali cha kuipeleka mochwari,still bado haikua problem sana kwangu.

  Sasa kilichonikera na kunisikitisha ni baada ya kufika mochwari sikumkuta muhusika wa mochwari na sasa ikanibidi kuzunguka kumtafuta muhusika huku nikiwa nimeibeba maiti ya mwanangu mikononi,punde alifika ndg yangu mmoja niliyekua nimempigia simu aje kunichukua na gari yake bcoz wife tayari alikua ameshachanganyikiwa,so ilibidi mimi nikae kwenye mrango wa mochwari kwa takribani masaa hv ili kumsubili muhusika na ndg yangu huyo pia akaanza kumtafuta na kumpata baada ya masaa 2 hivi.

  Baadae niligundua kwamba madaktari walikua bado wanaendelea na kikao cha mgomo uliopangwa kuanza j5 nchi nzima,
  Sasa ni swali kwa wana JF, Jee kama hayo yanatokea muhimbili jee sisi tusio na uwezo wa kwenda INDIA tutapona kweli???

  Naombeni comments.
   
 2. g

  gambagumu JF-Expert Member

  #2
  Mar 5, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 699
  Likes Received: 296
  Trophy Points: 80
  yatosha baba mshukuru mungu kwa kila jambo..pole sana.
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Mar 5, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Mkuu,
  Pole sana kwa masahibu hayo...Haya ni matokeo ya serikali mbovu inayosababisha madaktari wasifanye kazi inavyopasa, bali wakusanyike kuongelea maslahi wanayopunjwa.
  Anyway, mshukuru Mungu kuwa angalau HATIMAYE ulifanikisha suala lako...!...pOLE sana mkuu!
   
 4. papason

  papason JF-Expert Member

  #4
  Mar 5, 2012
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 2,317
  Likes Received: 634
  Trophy Points: 280
  YAANI NI HIVI!

  KUANZAIA LEO SIKUBALIANI KABISA NA MGOMO WA MADAKTARI NA WAUGUZI!

  Mkuu Sika pole sana sana na maswahibu yaliyo kupata, mwenyezi MUNGU ampumzishe kwa amani mtoto Mariam!
   
 5. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #5
  Mar 5, 2012
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,640
  Likes Received: 1,428
  Trophy Points: 280
  So sad, Pole kwa yaliyokukuta.. Hakika hatutoweza kubadili chochote kwa kuendelea kujificha kwenye keyboard na screen za laptop zetu! hii ndio inawafanya wanasiasa na watawala kuendelea kutuona mapimbi! wengine wakisikia mgomo ndio kwanza wanatafuta safari ya kwenda kutalii nje,, we need to change and demonstrate openly!

  Pole sana na msiba
   
 6. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #6
  Mar 5, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,274
  Trophy Points: 280
  Binafsi nilishakupa pole zangu kwenye thread ya taarifa ya msiba wa Mwanao, ila ili kuweka kumbukumbu sawa ni kwamba hakuna Dispensary inayotoa Rufaa kwenda Muhimbili, nadhani hapa umejichanganya labda kutokana na msiba.
   
 7. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #7
  Mar 5, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,020
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  mkuu pole sana.but naomba kukueleza kwamba daktari sio muhudumu wa mochwari
   
 8. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #8
  Mar 5, 2012
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 720
  Trophy Points: 280
  pole kwa msiba....maliza kwanza msiba, kaa utulie.
   
 9. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #9
  Mar 5, 2012
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Pole sana ndugu yetu, endelea kuomba mungu akupe nguvu....... haya ya migomo yanasikitisha sana kwa wahusika kushindwa kuchukua hatua sahihi
   
 10. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #10
  Mar 5, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,566
  Likes Received: 18,527
  Trophy Points: 280
  Pole sana kwa msiba!.

  Kila kitu hupangwa na Mungu. Yule malaika mtoa roho, "Israel", huipitia kila nafsi mara sabini fii saba kwa siku ili kuhakikisha ile saa iliyopangwa, haipiti hata sekunde moja!. Hivyo naomba nikupe pole kwa kukumbusha uzingatie kilichomtokea mwanao mpenzi ndio ilivyokuwa mipango ya Mola!.

  Tuendelee kujikabidhi kwa Mungu na kuwaombea al marhum wote walioitwa na umaut kwa namna yoyote ile ikiwemo mgomo na kumuomba atuepushie shari la mgomo mwingine ili kuzisijihisha nafsi zetu kuwa vifo hutokana na Mola na sio binadamu!

  Poleni tena wafiwa!
  RIP Mwanetu Marriam Ally!
   
 11. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #11
  Mar 5, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Tutaponea wapi ndg yangu Spika?
  Bado nakupa pole yangu binafsi pole sana spika!
  Na haya yote yanasababishwa na uongozi legelege uliopo madarakani mpk sasa!
  Nasema hivyo kwa sababu ni juzi tu kulikuwepo na mgomo wa madaktari na mgomo ule waziri mkuu pinda alidanganya umma kwa kuwahakikishia ya kwmb umekwisha na hautarudi tena,

  Na hata akadiriki kuwafukuza baadhi ya watumishi wa wizara ya afya kazi na kumbe ile ilikuwa geresha tu kwn wale watumishi bado wako kwenye maofisi ya6 wanapata AC tu!
  Na sasa kati ya madhara yanayoonekana wazi wazi ni mmoja kt ya kwako ndg yetu spika.

  Lawama yote ni ya serikali legelege ya jk na yule mwenzake anayejiita mtoto wa mkulima.
  Nasema hivyo kwa sababu hii,kama angewafukuza kazi wale watumishi legelege wa wizara ya afya kwn madaktari wangekuwa na mikutano ya hovyo kama wanavyoendelea navyo sasa hivi.
  Pole sana ndg yetu spika na MUNGU atakurejeshea nguvu hakika!

  Lawama yote pelekea serikali legelege ya jk!
   
 12. CHAI CHUNGU

  CHAI CHUNGU JF-Expert Member

  #12
  Mar 5, 2012
  Joined: Feb 20, 2012
  Messages: 7,160
  Likes Received: 107
  Trophy Points: 160
  Oh yes,offcourse,alituomba tumpeleke muhimbili!
   
 13. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #13
  Mar 5, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Pole mkuu!
  Personally najipa moyo one day tutapata suluhisho la yote haya!
  RIP Mariam
   
 14. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #14
  Mar 5, 2012
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,757
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  Pole tena Kaka... Mungu azidi kukutia nguvu.
   
 15. RICH OIL SHEIKH

  RICH OIL SHEIKH JF-Expert Member

  #15
  Mar 5, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 882
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
   
 16. babukijana

  babukijana JF-Expert Member

  #16
  Mar 5, 2012
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 4,814
  Likes Received: 1,147
  Trophy Points: 280
  pole sana mzee,kwa ujumla inaonekana ulichelewa muda mwingi pale dispensary,ilitakiwa umuwahishe moja kwa moja muhimbili maana inaonekana alikua katika hali mbaya sana
   
 17. K

  KAPONGO JF-Expert Member

  #17
  Mar 5, 2012
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,374
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Pole sana. Ni matokeo ya mambo mengi. Mosi ni ukiukwaji wa maadili na miiko ya kazi...vikao vya kujadili maslahi binafsi vingefanyika huku baadhi yao wakiachwa kuhudumia wagonjwa wa dharura..kinyume cha hapo ni ukiukwaji mkubwa na ubinafsi uliopitiliza wa kuthamini zaidi matumbo yao na si huduma kwa wananchi... kwa hilo madaktari hao 'uchwara' hawana tofauti na wabunge wetu 'wapiga mbonji' wanaojali zaidi matumbo yao kuliko kero za wananchi. Na serikali haikosi kulaumiwa kwa kudekeza mafisadi na viongozi wachumia tumbo. Kama ingekuwa na meno kero nyingi zingedhibitiwa.
   
 18. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #18
  Mar 5, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Mkuu, pole sana.
  Hivi ndivyo wafanyakazi wa serikali sehemu yeyote ile wanavyofanya kazi.

  Sio hispitali peke yake.........Ukienda manispaa, mtindo ndo huohuo; wizarani ndo usiseme.

  Pole sana mkuu.
   
 19. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #19
  Mar 5, 2012
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Mkuu, ndugu mmmoja kakuomba umalize msiba kwanza.

  Kwenye sehemu nilizoweka rangi au bold kunamaswali mengi sana kutokana na utata wake.
   
 20. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #20
  Mar 5, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,274
  Trophy Points: 280
  Muhimbili kwa ajili ya ugonjwa wa marelia tu, hivi mnafahamu maana ya Hospital ya rufaa? unalazimisha Jaji aje kusikiliza kesi kwenye mahakama ya mwanzo?
   
Loading...