Yaliyonikuta leo asubuhi

Jephta2003

JF-Expert Member
Feb 27, 2008
6,499
6,197
Basi leo asubuhi nimemuona mrembo mzuri masikini hata hawezi kugombania gari, nikaona hapa hapa ndio pa kuchukua ujiko!
Nikapanda fasta nikawahi siti ya watu wawili halafu nikakaa katikati ili akija nimpishe, dah! Si likatokea libabu moja limevaa miwani kubwaa kama ya
kukatia vitunguu likaa! Duh linanuka tu sigara, Yule Mrembo akasimama, limoyo likauma kweli!,
Daladala ilipofika Makumbusho nikaona lile Babu linashuka, aisee kama zali na Mrembo akakaa!
Jaman Bahati iliyoje,nikalianzisha,
MIMI : Mambo Mrembo.
MREMBO : poa,
MIMI : Karibu Karanga (nikatoa viujugu vya kuzugia)
MREMBO : silagi huo Uchafu,labda Pop Corn na Clips.
MIMI : Ok naitwa Chogomundu
Pangalashaba, mwenzangu?
MREMBO : He he heee! Jina kama
dawa!, mi naitwa Princess Rihanna!,
Wakati naendelea kupata majibu
Machungu ghafla Nikaona Gari
imefika Namanga, kwa kweli kama huyu mrembo angekuwa anatoa majibu ya kuridhisha ningeenda kushuka nae popote nikamwambia konda "Shusha Namanga" , sasa wakati nashuka nikashangaa kumbe na yeye anashuka hapo hapo!
MIMI : haa kumbe na wewe
unashuka hapa?
YEYE : so what?
MIMI : ok umekataa karanga zangu, basi twende hapo kwa Mama ntilie tukagonge chai,andazi maharage,
YEYE : khaa! Unikome, mimi huwa natumia vitu kama Burger,Kuku, sausages,Pizza, Egg Chops na Chipsi Mayai, yaani Uzuri Wangu woote
unilishe kwa Mama ntilie? KOMA!,
Dah Mrembo akasepa zake, nikaona hakuna Noma nikaagiza zangu Maharage ya 200,maandazi mawili 200 na Chai ya 100, nikaacha kajero
hapo nikasepa, Nimefika Kwa Shangazi akafurahi kweli kuniona.
SHANGAZI : mwanangu
Chogomundu Karibu Baba!,
MIMI: asante Shangazi
SHANGAZI: yule mwanangu wa Mwisho unamkumbuka?
MIMI : Si yule Kipandauso?
SHANGAZI: huyo huyo!
MIMI : namjua vizuri,wakati anakuwa namuona,hata nepi nimembadili teh!, yupo wapi siku hizi?
SHANGAZI : amekuwa mkubwa kweli, anasoma Hapo Chuo Cha Kodi TRA pale karibu na ITV, ila yupo alienda Chuo akahisi homa
kaona arudi,ngoja nimuite,
Kipandausooooo!!!
KIPANDAUSO : beeee Mama!
SHANGAZI : Njoo mwanangu,kuna Mgeni!
Hamad! Ndipo Macho yangu
yakakutana na Yule Mrembo wa
Kwenye daladala, kavaa vitenge vya zamani vya Shangazi, hana Wigi tena,muda huu komwe la ukoo linaonekana, komwe la babu yetu!,
mrembo kashika sahani ya Maboga na kikombe cha uji wa Mchele!,
Aliponiona Almanusura azimie!!!, huyu ndiye Kipandauso, Mtoto wa Mwisho wa Mjomba Dindoyogo!, ukipenda Muite Kipandauso Dindoyogo!
SHANGAZI : Njoo na Maboga ya kutosha na kikombe kingine cha uji uje unywe na Kaka yako!
Dah! akarudi ndani kinoma noma kainamisha sura chini, mi nikawa najiuliza wapi Pizza? Wapi Burger? Wapi Sausage?,
anyway hayo ndio ya dada zetu wakiwa huko mabarabarani.


Sent from my iPhone using JamiiForums app
 
Aisee in fact kakukela sana, hata hivyo haikuwa saizi yako. Yaani unakula kalanga utegemee kingast.
 
Back
Top Bottom