Yaliyomtokea Kiongozi wa (UVCCM) Masauni ni Mtego uliokuwa unasubiriwa kufyatuliwa. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Yaliyomtokea Kiongozi wa (UVCCM) Masauni ni Mtego uliokuwa unasubiriwa kufyatuliwa.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sonara, May 21, 2010.

 1. Sonara

  Sonara JF-Expert Member

  #1
  May 21, 2010
  Joined: Oct 2, 2008
  Messages: 730
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kabla ya uchaguzi wa Umoja wa vijana kulizuka mvutano,wa makundi yanayotaka kuwepo kwa mtu wao hususan kutoka bara. Ndipo Rais akaleta mamuzi kiongozi apatikane kutoka zanzibar ili kutuliza hali ile na bila kuonekana kuwa Rais anapendelea kundi fulani ijapokuwa analo kundi lake.

  Sasa nitamnukuu masauni, juzi katika mahojiano kabla ya kujiuzulu aliuliwa jee ni kweli umebuni cheti cha kuzaliwa? Akanena laa, nitabunije? kauliza

  Akaendelea kusema kuwa vyombo vyote vya chama na serekali,vikiwemo vya Usalama wa taifa wameridhika na profile yangu ,na ndio nikapewa nafasi hii ,sasa tujiulize hivi ni kweli Usalama wa taifa walikuwa na maruwi ruwi kiasi hchi
  ?

  Wachilia mbali hizo tasisi nyingine kama utazingatia kwa undani na kama ni kweli aliyosema masauni kuwa usalama wa Taifa wameridhia ya profile yake kwa maaana hiyo ilipangwa wampe huyu kijana uongozi wa muda mfupi na itafikapofika wakati fulani hii kashifa itolewe, alazimishwe kujiuzulu na yule ambae anatokana na moja kati ya yale makundi yanyovutana ashike madaraka.
   
 2. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #2
  May 21, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,804
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Sikio la KUFA ....
   
 3. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #3
  May 21, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,589
  Likes Received: 18,573
  Trophy Points: 280
  Hoja yako sii kweli, hao vijana wa under 30 wa kuongoza UV-CCM hata Zanzibar wapo wengi tuu. Nafasi itakapotangazwa i wazi, wenye busara watamshauri Malisa na Riz1 wake wasijitokeze.

  Hii issue ya mwaka wake wa kuzaliwa ni udhaifu tuu wa vyombo husika, kule tuendako, utakuwa huna tena hata haja ya kutaja, DNA itamaliza kila kitu.
   
 4. HeartBreak

  HeartBreak JF-Expert Member

  #4
  May 21, 2010
  Joined: Apr 21, 2008
  Messages: 346
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  kumbe ndio tatizo..je moyo...tatizo ni nini? jamani chama cha mapinduzi...kuna shida
   
 5. u

  ulijualo New Member

  #5
  May 21, 2010
  Joined: May 21, 2010
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Kwa sasa nipo nje ya TZ.Hii habari ya Masauni nimeisikkia kijuu juu tu kuna mtu anaweza kunieleza kwa undani zaidi ?
   
 6. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #6
  May 21, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Pitia ile threa ya mwenyekiti wa uvccm kungatuka
   
 7. M

  Mafuchila JF-Expert Member

  #7
  May 21, 2010
  Joined: Apr 29, 2006
  Messages: 752
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Sasa tumeiona ni jinsi gani chama kinavyosimamia kanuni yake, "nitasema ukweli daima, fitina kwangu mwiko." Bila shaka baada ya kumalizana na Masauni, sasa wataelekeza macho kwa waliofoji vyeti, waliodanganya mali zao na ......
   
 8. Scientist

  Scientist JF-Expert Member

  #8
  May 21, 2010
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 392
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mh sidhani... hii iliandaliwa ndio maana imewekwa wazi..hizo nyingine, sahau. Inawezekana hata muungwana naye kafoji vyeti na watu wanajua ndio maana hawezi kuwaumbua wengine!
   
 9. Andrew Nyerere

  Andrew Nyerere Verified User

  #9
  May 21, 2010
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 3,025
  Likes Received: 1,206
  Trophy Points: 280
  Kuhusu swala la Masauni,sijui wameamua nini,kumchagua Mzanzibari mwingine,au kufanya uchaguzi ambao ni free for all.
   
 10. B

  Baba Ubaya Senior Member

  #10
  May 21, 2010
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 127
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Thubutu!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 11. Che Guevara

  Che Guevara JF-Expert Member

  #11
  May 21, 2010
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 1,178
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 145

  Kaimu Mwenyekiti ni Makamu Mwenyekiti Beno Malisa, rafiki wa Ridhiwani Kikwete. Ndiye alikuwa mgombea wa kundi la Mzee Jakaya na Ridhiwani Kikwete kwenye uchaguzi ule.
  Masauni alikuwa ametangulizwa kwa baiskeli ya mbao, ili akiwa figure-head wamwache, vinginevyo hokohuko njiani apigwe mtama na wachukue wenyewe, kama ilivyokuja kutokea.
   
 12. G

  Godwine JF-Expert Member

  #12
  May 22, 2010
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Kuna viongozi wengi ndani ya chama na serikali na bunge ambao wamedanganya au kojitambulisha na sifa zisizo zao, kuna wabunge mawaziri na makatibu wakuu lakini cha kushangaza ni kijana huyu wa UVCCM akumbwe na mkasa huu , kwanini na sababu ya kuenguliwa kwake au kuna wakubwa wanataka kuweka vijana wao? au sababu ametoka zanzibar? nini kinaendelea ? viongozi wote walifoji na kudanganya waenguliwe si kwa kumnyanyasa kijana huyu pekee au kuna sheria zinazoshambulia baadhi ya watu, nchi yetu haina sheria na taratibu za kibaguzi kwa hiyo ni wakati wa kulitazama kwa kina
   
 13. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #13
  May 22, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Siku zote baridi humpata kondoo mwenye manyoa haba, CCM kuna mafisadi, waliofoji vyeti kujitafutia vyeo "vihiyo", wezi n.k hawajaguswa, hichi chama chote kimeoza yaliyobaki yanatokea tu.
   
 14. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #14
  May 22, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Kwa nini msiwataje hao vigogo waliofoji vyeti, umri ili muone kama hawatachukuliwa hatua? Au tuseme kwa kuwa kuna kesi mahakamani kuhusu ubakaji na wakati huo huo kuna wabakaji ambao hawajafikishwa mahakamani ni kwa sababu ya upendeleo na si mambo ya ushahidi? Does two wrongs make a right, anyway?
   
 15. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #15
  May 22, 2010
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,680
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Bado tusubiri tu
   
 16. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #16
  May 22, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  [​IMG] Wahoji kama umri ni kosa, ufisadi je?  [​IMG]
  Aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana (VCCM) Taifa, Hamad Yussuf Masauni, akisakata ngoma.  Uamuzi wa kujiuzulu viongozi wa Jumuiya ya Vijana ya Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) umechukua sura mpya Zanzibar, baada ya kupokelewa kwa kinyongo na kuhusishwa na mbio za mgombea urais wa Zanzibar kumrithi Rais Amani Abeid Karume, ambaye atamaliza muhula wake Oktoba, mwaka huu.
  Wakizungumza na Nipashe kwa nyakati tofauti, baadhi ya vijana wa CCM na makada wa chama hicho Zanzibar, walisema aliyekuwa Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Hamad Yusuf Masauni, ameponzwa kutokana na kuwa karibu na mgombea mmoja anayetajwa kuwania kiti hicho, jina tunalisitiri kwa sasa.
  Walisema kwamba tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa UVCCM mwaka 2008, vijana wa chama tawala wamekuwa wakionekena wamoja katika hadharani, lakini kulikuwepo na mivutano.
  Aliyekuwa Katibu wa CCM Wilaya ya Tanga na kiongozi mwandamizi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Baraka Shamte, alisema viongozi wa Jumuiya hiyo wameshindwa kujenga umoja kutokana na makundi ya wagombea urais kuwagawa tangu makundi hayo kuanza kuitumia kufikia malengo yao binafsi ya kugombea urais wa Zanzibar.
  Alieleza kwamba viongozi wa Jumuiya hiyo wamekuwa katika mazingira magumu baada ya kuibuka viongozi kadhaa ndani ya UVCCM wanaomuunga mkono kada mmoja mashuhuri wa CCM awe mrithi wa Karume wakati baadhi ya vigogo kadhaa wa SMZ wakipinga.
  “Nafasi ya urais wa Zanzibar ndiyo inayowatesa vijana na kuanza kuchafuana kisiasa wenyewe kwa wenyewe,” alisema Shamte.
  Alisema kwamba makundi ya wagombea urais Zanzibar ndio yanayosababisha Jumuiya hiyo ishindwe kujenga umoja kutokana na siasa za chuki na kufafanua kuwa suala la kudanganya umri limetumika kama njia ya kufikia lengo la kummaliza Masauni kisiasa.
  Mkereketwa wa CCM, Said Ali Said, kutoka maskani ya Ndiyo alisema kwamba amepokea kwa mshtuko uamuzi wa Masauni na Naibu Katibu wa UVCCM Zanzibar, Mohamed Moyo, wakati Zanzibar ikiwa katika maandalizi ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 31, mwaka huu.
  “Waswahili husema tonge zuri halifiki kinywani, tumepoteza kijana mkimya na mchapa kazi,” alisema Said.
  Naye Suleiman Mfaume Suleiman, mkazi wa Michezani, alidai kuwa anaamini kujiuzulu kwa Masauni kumetokana na fitna za kisiasa za viongozi wenzake kutoka Tanzania bara, ambao wamekuwa na kinyongo kutokana na nafasi hiyo kuchukuliwa na Mzanzibari.
  Alidai kuwa Masauni alianza kupigwa vita tangu uchaguzi ulipomalizika kwa kuwa baadhi ya viongozi wenzake walipokea kwa kinyongo uamuzi wa nafasi ya mwenyekiti kugombewa na wanachama kutoka Zanzibar pekee.
  Alieleza kwamba uamuzi wa Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, kuamua nafasi ya Mwenyekiti UVCCM igombewe na wanachama kutoka Zanzibar pekee ulipokelewa kwa kinyongo na baadhi ya wagombea kutoka Tanzania Bara.
  Hata hivyo, alisema Masauni ataendelea kukumbukwa kutokana na kazi nzuri aliyoifanya kwa muda mfupi ikiwemo kufufua matembezi ya kuwaenzi waasisi wa Muungano na Mapinduzi ya Zanzibar, kuanzisha mashindano ya soka ya wilaya pamoja na chuo cha makada wa CCM mkoani Iringa.
  Mwanachama mwingine wa CCM, Mwanahija Seif Kombo, alisema Masauni amejiuzulu kutokana na majungu ya viongozi wenzake na sio kudanganya umri kwa sababu kuna viongozi ndani ya CCM wanakabiliwa na tuhuma kubwa za ufisadi, lakini bado wanashikilia nyadhifa za juu za uongozi ndani ya chama hicho.
  “Wametuumizia mtoto wetu kwa chuki, kwanini wanaotuhumiwa kwa ufisadi hawajajiuzulu nyadhifa zao katika chama, awe mtoto wetu Masauni peke yake,” alisema Mwanahija huku akifuta machozi.
  Aidha, alisema ameshangazwa na Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba, kuwa mstari wa mbele kuzungumzia suala la Masauni na kusahau viongozi ndani ya chama wanaohusishwa na ufisadi wa mali za umma.
  Hata hivyo, Katibu Mwenezi wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai, aliwataka wanachama wa Jumuiya hiyo Zanzibar kuwa wavumilivu kufuatia uamuzi wa Masauni na Moyo kujiuzulu mapama wiki hii katika kikao cha Baraza Kuu la UVCCM mjini Iringa.
  Vuai alisema kuwa viongozi hao hawakulazimishwa kujiuzulu kama inavyodaiwa, isipokuwa waliandika barua za kujiuzulu kwa hiari yao.
  “Nawaomba vijana waendelee kuwa wastahamilivu kutokana na maamuzi mazito yaliyofanywa na viongozi wao. Jambo la msingi ni kujenga umoja ndani ya Jumuiya” alisema Vuai.
  Suala la Masauni na Moyo kujiuzulu limezua mjadala mkali Zanzibar na kusababisha vijana kukaa katika vikundi wakijadili uamuzi uliofikiwa na viongozi hao.
  Rais Jakaya Kikwete alisema juzi kuwa uamuzi wa Masauni kujiuzulu ulikuwa sahihi kwa kuwa hakusema ukweli kuhusu umri wake.
  Alisema kilichomponza ni kudanganya umri na kwamba asitafutwe mchawi kuhusiana na kilichotokea.  CHANZO: NIPASHE
   
 17. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #17
  May 22, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  Yaliyo mtokea Kiongozi wa (UVCCM) Masauni ni Mtego uliokuwa unasubiriwa kufyatul

  shida yangu hapa ni kusahihisha hiki kichwa cha habari. Ungeandika hivi: Yaliyomtokea (kiongozi wa uvccm) Masauni ni mtego uliokuwa unasubiriwa kufyatuka/fyatuliwa. Maneno ya kwenye mabano ni ufafanuzi wa zaidi wa kile unachozungumzia. Kwa maneno yako ni swa na kama umeandika; "Yaliyomtokea kiongozi wa Masauni", kitu ambacho hakileti maana kabisaa. Ni hayo tu
   
 18. G

  Godwine JF-Expert Member

  #18
  May 22, 2010
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  wametajwa katika kitabu cha mafisadi wa elimu na wengine kama wabunge watu wameshafikisha malalamiko lakini hakuna hatua yeyote inayochukuliwa na katika uhakiki wa vyeti unaoendelea TCU waligundua watu wengi lakini hakuna kinachoendelea
   
 19. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #19
  May 22, 2010
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kwani malalamiko dhidi ya Masauni si kuna yalikoanzia? Kwa nini tunampa jukumu zito huyo aliyefichua kashfa hii afanye hivyo katika kila tukio? Suala hili liibuliwa huko UVCCM na waoa wamelichukulia hatua. Hatuwezi kuwatwisha mzigo wa kufichua na kuchukua hatua kila kashfa.

  Haya maskandali mengine yana mkondo wake na wanaowajibika kuyalipua wapo. Kwa hili tupongeze maana huyu bwana angeachiwa angeweza hata kufoji na mengine hata elimu yake. Wacha atiwe adabu!
   
 20. Tatu

  Tatu JF-Expert Member

  #20
  May 22, 2010
  Joined: Oct 6, 2006
  Messages: 1,081
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Mbayuwayu ni mtoto wako au mke wako tu, wengine si Mbayuwayu.

  So go figure why these people took action only on this particular person.
   
Loading...