Yaliyomtokea Kawambwa bungeni: Matatizo ya uswahiba wa rais wetu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Yaliyomtokea Kawambwa bungeni: Matatizo ya uswahiba wa rais wetu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by OkSIR, Jul 5, 2009.

 1. O

  OkSIR Senior Member

  #1
  Jul 5, 2009
  Joined: Jun 3, 2009
  Messages: 108
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu wapendwa leo hii ...nimefurahi sana kuona wabunge wa CCM wanasimamisha budjet ya wizara ya miundo mbinu kana kwamba ni sinema ya alinacha....nimewiwa leo hii kusema yaliyotokea kwa waziri kawambwa iwe ni sehemu tu ya somo kwa RAIS jakaya mrisho KIKWETE kwa kuchagua watu kuhodhi madaraka makubwa yaliyo juu ya uwezo wao just sababu ni ndugu ama mjomba/rafiki shemeji/ama mates wa shule kama nilivyosikiwa walivyojazana kwenye wizara
  Kuna wakati mwingine unaweza fikiria RAIS anapochagua anakuwa anachaguliwa na mkewe ama anakuwa kaamaka usingizini na kutoa majina...siitaji kutaja rundo la binadamu na maswahiba wa rais kikwete walioshika uongozi wa juu kama mawaziri na kwingineko....
  Kawambwa ni mtu mmoja mzuri ila nilipenda na ntaendelea kusema kuna wizaraa inabidi ziongozwe na watu proffessional else madhara yake ni makubwa mno mno....mmeona kitendo cha kumuweka swahiba wake mkulo kwenye wizara ya fedha anaamua kutoa fedha ovyo hata kama bunge alijapitisha.......akuna ubishi kama kuna bajeti inayotalkkiwa kulaaniwa ni hii ya wizara ya miundo mbinu/tatizo moja na ambalo ndugu yetu amekumbana nalo...ni kwamba kawambwa ana mchezo wa kuwaamini watu na kutofwatilia jambo ndio maana mwisho wa siku anakutana na upuuzi kwenye maswala nyeti kama bajet....hakuna ubishi mmeona upuuzi alioufanya kwa kumchagua WAZIRI CHENGE KUONGOZA WIZARA HII..
  kisa tu anajua upuuzi wote wa mikataba michafu na pesa walizochota EPA..matatizo mengi yanaitaji kuangaliwa mifano ni kama ifuatavyo

  ATCL

  Shirika hili limekuwa likifwanywa kama mchezo wa kidalipo kila mwenye kuchuma achume haraka na kuondoka...mwanzoni nilihisi kama serikali na rais wake wameamua kulitupa nikaona akapita mwandosya akala na nsouthafrican airways akapelekewa wanae south kwa bil ya SAA..baadae akapewa jukumu hilo chenge;nae akaiba akajikimbilia...akaletwa mjomba...mara akapewa ukurugenzi swahiba ama mates chumba kimoja jamani??leo hii mates kaaribu kammkibizia N.I.C ati akalifufue.....mi bado nina wasiwasi na RAIS.....Leo hii waziri husika analitengea shirika la TALC BILLION MOJA kwenye budget,jamani watanzania inatuingia akilini huyu kweli ni waziri ama is he serious na kazi zake????

  TRL

  HIILI NI VITUKO NAOMBA NIANDIKE KWA HERUFI KUBWA;HII KAMPUNI IMEBINAFSISHWA NA WAHINDI WALIOLETWA NA JEETU PATEL MKONO KWA MKONO KWA RAIS WETU KIKWETE....WAKAAHIDI MENGI TU...GAFLA TUKAAMBIWA WANACHUKUA VYUMA AMA ENGINE ZETU WALIZOZINUNU NYERERE ...ATI WANAPELEKA INDIA...BAADA YUA HAPO MNA TAARIFA WAMELETA ENGINE 25 AMBAZO ZIMEFUNGWA 15 NA KATI YA HIZO KILA MOJA TUNALIPIA LAKI NANE KWA SIKU....800,000....SIDHANI KAMA HUYU WAZIRI ANAIPENDA HII WIZARA YAKE...JAMANI.SAMAHANI KWA HILO....UKIACHA HILO ATCL HAINA HATA MTU WA KUWABEBA AMEENDA KUIPA TRL SH BILLION 80 KWENYE BAJETI....HIZI ZOTE NI KWA AJILI YA UCHAGUZI WANATUFANYA WAPUMBAVU...WATANZANIA TUAMKE TUACHANE NA UPUUUZI

  TUME YA ATCL

  NDUGU WAPENDWA ATCL ILIUNDIWA TUME ILIOONGOZWA NA MAPROFESA NA WENGI WAKALALAMIKA MAGAZETI WAKAANDIKA WANAYOWEZA .....MWISHO ILE TUME WAMETUMIA MILION 47,KWA MUDA WALIOPEWA HALAFU KILA MWANAKAMATI AKATUNUKIWA LAPTOP MPYA UKIACHA ZILE PER DIEM ZA KILA SIKU NA OVERTYM...
  MWISHO WAMEKABIDHI MH WAZIRI AKADAI ANASUBIRI AKIKABIDHIWA ANAWATANGAZIA WANANCHI SABABU ZA KUSIMAMISHA SAFARI ZA ATCL;ALIPOKABIDHIWA AKALIPELEKA KWENYE DROO ZA OFISI ZAKE PALE UJENZI NA KUFUNGA DROO......ALIPOBANWA SANA AKADAI ANAMSUBIRI MWENYEKITI WA BODI ,YALIPOTOLEWA MAJIBU YA MWENYEKITI WA BODI HAKUNA KILICHOFANYIKA MPAKA SASA .......HUU NI UPUUUZI KABISA HATUYITAJI KUWA NA MAWAZIRI WA KUJUANA KWENYE OFSI NYETI KAMA HIZI LEO HII WANAOLITAFUNA TRL NA ATCL NI WALELWALE NA WANAENDELEA NA MBINU ZAO CHAFU....HATUJUI LAKINI IPO SIKU WANANCHI WATASEMA BASIIIIIIIIIIIIIIII IMETOSHA

  KILA LA KHERI KAWAMBWA.......
   
 2. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #2
  Jul 5, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Wizara ya fedha na hii ya miundo mbinu "zinatakiwa kuongozwa na mbuge wa kuteuliwa asiye na Jimbo maana wamezidi kujineemesha na miradi ya serikali kwenye maeneo ya majimbo yao.
   
 3. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #3
  Jul 5, 2009
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Hili nalo la ufisadi mpaka wapande ndege waende Marekani na kuonana na watu mashuhuri n.k. na kuomba msaada? Jamani mbona wote hawa wezi wameapa kwa BIBLIA au QURUAN au KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA kuwa watailinda nchi na kuitumikia na sii kuitumia. Nasema OLE wao, OLE wao walao chakula cha mayatima na wajane na masikini na kuwadanganya na kuwapumbaza huku watoto, jamaa na rafiki zao wakiishi kwa mkate, siagi, maziwa na asali. Yatawafika siku ya mwisho na kamwe hamtauona ufalme wa Mungu. Ni motoni milele na watoto wenu, na jamaa zenu, na rafiki zenu walishiriki kunyang'anya haki ya wanyonge. Maisha ya raha mwisho wake ni hapa hapa bali milele mtaishi kwa kilio na kusaga meno na mwenyekiti wenu LUCIFER. Let those who hear this, turn around and confess to the public so that may inherit the kingdom of heaven. It is your last chance!
   
 4. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #4
  Jul 5, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,320
  Likes Received: 1,785
  Trophy Points: 280
  Dr. Kawambwa ni mmoja wa walimu waliokuwa makini na waungwana pale faculty ya engineering. Sijui vizuri uwezo wake wa kuwa kiongozi kama waziri, lakini inawezekana kabisa tatizo likawa ni ule upole wake akiwa anadili na watu wajanja wajanja kama wanasiasa wazoefu. Ni rahisi kumfix.
   
 5. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #5
  Jul 5, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135

  Mkuu, hapo majibu unayo yote. Otherwise is very good academically
   
 6. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #6
  Jul 5, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Aende kufundisha darasani au kule UDOM na siyo siasa
   
 7. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #7
  Jul 5, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Chizi kakabidhiwa rungu kila naye kutana naye halali yake, sasa hii mada ina uhusiano gani na ibada ya Kadhi?
   
 8. U

  Utatu JF-Expert Member

  #8
  Jul 6, 2009
  Joined: Dec 31, 2008
  Messages: 436
  Likes Received: 111
  Trophy Points: 60
  Vikaragosi kila mahali....
   
 9. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #9
  Jul 6, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,305
  Likes Received: 5,640
  Trophy Points: 280
  Ipo siku watanzania wataamka kama watanzania...wamechoka.....
   
 10. J

  JokaKuu Platinum Member

  #10
  Jul 6, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,747
  Likes Received: 4,967
  Trophy Points: 280
  ..kwa mtizamo wangu fedha za kujenga barabara za Singida,Tabora,Rukwa,Mwanza,Sinyanga, zipo kinachokosekana ni dhamira na uzalendo.

  ..sidhani kama ni lazima kupunguza fedha za barabara za jimboni kwa Mkulo,Kawambwa,na Kigoda na kuzipeleka kwenye majimbo ya kina Samuel Sitta na Lucas Selelii.

  ..wabunge, mawaziri, na serikali nzima kwa ujumla, waanze kubana matumizi yao yasiyokuwa ya lazima, kama posho kubwa-kubwa, magari ya anasa, pamoja safari zisizokuwa na tija kama zile za kwenda vijijini kuelimisha wananchi kuhusu bajeti
   
  Last edited: Jul 6, 2009
 11. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #11
  Jul 6, 2009
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,640
  Likes Received: 2,872
  Trophy Points: 280
Loading...