Yaliyomkuta Abdul Jumbe yatamkuta Mwanasheria mkuu wa Zanzibar Mh Othman ?

kwani kura maana yake nini?

"Mwanasheria Mkuu ndiye atakayekuwa Mshauri Mkuu wa kisheria kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, na atatekeleza shughuli nyengine zozote za kisheria zitazopelekwa kwake au atakazoagizwa na Rais au kwa mujibu wa Katiba hii au Sheria nyenginezo zozote.".....katiba ya zanzibar sehemu ya madaraka ya serikali kifungu cha 56..inaweka wazi kuwa anatakiwa kuheshimu katiba na kufuata directions za rais kama mamlaka iliyomteua la sivyo angejiuzulu
 
"Mwanasheria Mkuu ndiye atakayekuwa Mshauri Mkuu wa kisheria kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, na atatekeleza shughuli nyengine zozote za kisheria zitazopelekwa kwake au atakazoagizwa na Rais au kwa mujibu wa Katiba hii au Sheria nyenginezo zozote.".....katiba ya zanzibar sehemu ya madaraka ya serikali kifungu cha 56..inaweka wazi kuwa anatakiwa kuheshimu katiba na kufuata directions za rais kama mamlaka iliyomteua la sivyo angejiuzulu

Sasa pale kaingia kama mjumbe au mwanasheria mkuu?
 
Huyu mwanasheria ni mbmumbumbu sijawahi kuona, NAKUMBUKA THE ORIGINAL COMEDY walipokwenda Zanzibar walikuwakuta wakazi wengine kule ni "MNDEMBWEDO" huyu mwanasheria atakuwa mmoja wao

Eti nini? Kwa kipi unacholingana nae? hata ..............!
 
ameingia kutokana na wadhfa wake hivyo angechagua kutenda kama wadhfa wake unavyomuelekeza kwenye katiba au angejiuzulu
Kama ameingia kwa wadhifa wake basi yuko sahihi kuzikataa hizo ibara kwa sababu zinaivunja katiba ya znz ambayo yeye ndo mlinzi wake mkuu.
 
Hivo kwa nini wanasiasa wa bara wanaingangania Znz? Kwa ninj wasiwaache waamue fate yao? Kama wakitaka kuwa na devolution sawa wakitaka kuwa huru wapewe referendum waamue.
 
Kamanda doreen

Maneno makubwa haya...well articulated Mkuu.

tatizo tangu mwanzo ni jinsi wajumbe wa bunge hili walivyopatikana hata hivyo naomba mwenye majibu anipe huyu mwanasheria alikuwa anapiga kura kwa niaba ya nani serikali ya mapinduzi zanzibar au ccm zanzibar au kama mjumbe binafsi kama alivyo ona yeye katiba ni ya serikali au ya wananchi?
 
Last edited by a moderator:
Kama ameingia kwa wadhifa wake basi yuko sahihi kuzikataa hizo ibara kwa sababu zinaivunja katiba ya znz ambayo yeye ndo mlinzi wake mkuu.

katiba ya jamhuri ya muungano ndo katiba mama...na1964 zanzibar na tanganyika zili-surrender sovereignty..hivyo huwezi sema inavunja katiba ya zanzibar bali katiba ya zanzibar ndo inavunja katiba mama ya jamhuri ya muungano wa tanzania
 
katiba ya jamhuri ya muungano ndo katiba mama...na1964 zanzibar na tanganyika zili-surrender sovereignty..hivyo huwezi sema inavunja katiba ya zanzibar bali katiba ya zanzibar ndo inavunja katiba mama ya jamhuri ya muungano wa tanzania

warioba aliyaona haya ndio maana alipendekeza 3 bomba. wale,wapuuzi wakamuona mjinga ag wa zanzibar kawarudisha kujifunza heshima kwa nchi yake as a free sovereign state of zanzibar.
 
Ilikuwa "April 1972" Mh: Alhaji Abdul Jumbe Mwinyi alipotwaa madaraka ya Zanzibar na kuwa Rais wa awamu ya pili wa serikali ya SMZ mara baada ya Mh: Abeid Aman Karume kuuwawa, Septembar 5, 1975 Mwalimu Nyerere akiwa kama Mwenyekiti wa Tanu na Rais wa Tanganyika aliwasilisha wazo kwenye kamati kuu ya "TANU" juu ya kuunganisha chama cha "TANU" na "ASP" suala lilijadiliwa na hatimae "OCTOBER 1976" "ASP" na "TANU" zilifikia muafakha juu ya kuungana na kuzalisha chama cha "CCM" ambacho uzinduzi wake ulikiwa Tarehe 5/2/1977, Mwendendo wa Abdul na Nyerere kwa wakati huu ulikuwa mzuri japo Abdul Jumbe alijisahau sana juu ya Taifa lake la Zanzibar lakini yote haya yalisababishwa na tamaa ya madaraka! Kwan alitamani awe rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Abdul jumbe safar yake ilianza kuwa mashakhani pale tu mara baada ya ujio wa "Edward Sokoine" ndipo alipo amua kuanza kudili na Taifa lake la Zanzibar kwa kuangalia maslahi ya Zanzibar na watu wake na kuona kuwa swala la Muungano limekaa vibaya na kuanda taarifa mbalimbali ili awasilishe mahakamani, Bila shakha wana jamvi mutakuwa munakumbuka nn kilimkuta Rais huyu wa Zanzibar Shekhe Abdul Jumbe Mwinyi kwani alipigwa kibuti na CCM mnamo mwaka 1984 kwa kisingizio cha kuvunja katiba hivo kupoteza nafasi zake zote alizokawa nazo yaani Rais wa Zanzibar, Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pia na makamo mwenyekiti wa "CCM" japo nchi yake ilikuwa na katiba……!

Mwanasheria mkuu wa zanzibar (Mh: Othman Masoud Othman) ikumbukwe alijiulu katika kamati ya uandishi wa katiba pale BMK, Mwanasheria huyu huyu hakuonekana siku nyingi katika mara baada ya kujiuzulu pale kwenye kamati ya uandishi japo kwa upande wa "CCM" hawakuona kama ni tatizo kuto kuwepo kwake, wachambuzi wa masuala ya siasa hawakupenda juu ya kuendelea mchakato wa katiba huku kukiwa na makundi makubwa yanayo pingana juu ya namna ya kuandika katiba hiyo, Makamu Mwenyekiti wa wa "JUKATA" akihojiwa katika kipindi cha HOT MIX kinachoenda heweni chanel 5 alidokeza juu ya kile kilichomtoa mwanasheria huyu wa SMZ katika kamati ya undishi kuwa ni "kulingana na mjadala unavyoendelea BMK haoni maslahi ya Zanzibar ili katika Rasimu ya Tume ya mabadiliko ya katiba maslahi ya Zanzibar yalikuwepo kwa 100%" , ikiyaeleza haya makamo huyo wa mwenyekiti alisema kuwa yeye alipata nakala ya barua ya kujiengua ktk kamati hiyo ya uandishi, cha kushangaza ni leo mwanasheria huyu wa SMZ alipokuja BMK na kupiga kura ya HAPANA katika ibara na sura zote ambazo hakuzihafikhi…!!! Na kura ya NDIO kwa ibara ambazo hakuwa na tatizo nazo…!

Ya moyoni mwanangu;- Mwanasheria huyu hata undiwa zengwe kama alivyofanyiwa mzee Abdul Jumbe Mwinyi…??

Je kweli Mwanasheria huyu halifanya haya bila kumshirikisha Rasi wa SMZ…??

Je kuundwa kwa kamati ya mashauliano pale BMK jana alishajua wajumbe waliopiga kura hapana watarubuniwa na kubadiri misimamo yao na yeye akaamua kujitosa ili waone kama wako pamoja na yeye na kuwapa nguvu ya kusimamia yale wanayo yaamini…???

Je mwanasheria kashaona kuwa sasa si wakati wa kwaheri ukoloni, kwaheri uhuru…???

katika haya kuna moja au mawili lazima mwanasheria huyu aliyaona…………!!

Inauma historia ya muungano huu pale utaposoma kitabu cha kwaheri ukoloni, kwaheri uhuru……!

Kisharia Mh Othman Masoud yeye aliapa kuilinda katiba ya Znz na alichofanya ni kuhakikisha maslah na ustawi wa Znz unapatikana katika katiba mpya. Na pale alipoona kuna kuminywa kwa haki hizo na matakwa hayo alikuwa na haki zote kupinga kwa kula hali na aliposhindwa alijiondosha katika kamati ya Uandishi kwa kutoa sababu zake..

Na hata alipopiga kura amevikataa vifungu vyote visivyo na maslahi kwa Znz. Huyu ni jasiri sana na mkweli na anasimamia haki na maslahi a katiba ya Znz. watu hawa ndio wale wa kupongezwa.

Si kama alivyokuwa mh Kessy amejitahidi kuinanga na kuitetea Tanganyika lakin katika kupiga kure AMEUFYATA na kupiga kura ya NDIO kwa katiba nzima. Watu wa aina hii tunawaita WANAFIKI


 
Back
Top Bottom