Mathayo Fungo
JF-Expert Member
- Nov 13, 2018
- 319
- 510
YALIYOJIRI LEO JUNI 14, 2019 WAKATI WA MKUTANO WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, DKT. JOHN POMBE MAGUFULI NA RAIS WA JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA CONGO, MHE. FELIX TSHISEKEDI
Aliyoyazungumza Rais Felix Tshisekedi
#Tumekubaliana kuwa hatuwezi kufanya jitihada zozote bila kuwa na amani itakayosaidia watu wa nchi hizi mbili ili waweze kunufaika.
#Tumekubaliana pia katika ujenzi wa miundombinu pamoja na kushughulikia changamoto ya vizuizi vya kibiashara.
Aliyoyaongea Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
#Tumekubaliana kuwa Rais wa DRC aimarishe Bandari upande wa DRC ili tusiwe na matatizo wakati wa kusafirisha bidhaa.
#Naomba ukashughulikie shida za watu wa DRC kwa ajili ya kuikomboa nchi hiyo kwa sababu nchi hiyo haikutakiwa uchumi wake kukua kwa asilimia nne (4%).
#Tumekubaliana Mamlaka zetu husika na Wafanyabiashara kufanya vikao vya ujirani mwema kwa ajili ya maendeleo yetu.
Aliyoyazungumza Rais Felix Tshisekedi
#Sababu ya ziara hii ni kwa ajili ya kukuza mahusiano baina ya nchi zetu hivyo tumejadili na kukubaliana masuala ambayo yataelekezwa katika kukuza mahusiano haya.
#Tumekubaliana kuwa hatuwezi kufanya jitihada zozote bila kuwa na amani itakayosaidia watu wa nchi hizi mbili ili waweze kunufaika.
#Tumekubaliana pia kuna umuhimu wa kukuza fursa za kiuchumi ili kukuza uchumi wetu, tumegundua kuwa biashara kati yetu ni ndogo hivyo lazima Tume ya Pamoja lazima ikae kwa haraka ili kuchambua sababu zinazosababisha hali hiyo.
#Tumekubaliana pia katika ujenzi wa miundombinu pamoja na kushughulikia changamoto ya vizuizi vya kibiashara.
#Nashukuru kwa mualiko katika mkutano wa SADC na niko tayari kuja katika mkutano huo.
Aliyoyaongea Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
#Ziara hii inatoa fursa kwa nchi zetu mbili kukuza zaidi uhusiano na ushirikiano hasa kwenye masuala ya kiuchumi kwani licha ya uhusiano wa muda mrefu ushirikiano wetu wa kiuchumi sio mkubwa sana.
#Tumekubaliana kuwa Rais wa DRC aimarishe Bandari upande wa DRC ili tusiwe na matatizo wakati wa kusafirisha bidhaa.
#Tumezungumza pia juu ya ujenzi wa barabara mbalimbali nchini pamoja na suala la usafiri wa anga ili kwa kupitia mashirika haya mawili ya ndege, Air Tanzania iweze kwenda kwenye baadhi ya miji ya DRC.
#Naomba ukashughulikie shida za watu wa DRC kwa ajili ya kuikomboa nchi hiyo kwa sababu nchi hiyo haikutakiwa uchumi wake kukua kwa asilimia nne (4%).
#Kwa lengo la kuimarisha ushirikiano wetu, tumeamua kuifufua Tume ya Pamoja ya Ushirikiano kwani haijakutana tangu mwaka 2002.
#Tumekubaliana Mamlaka zetu husika na Wafanyabiashara kufanya vikao vya ujirani mwema kwa ajili ya maendeleo yetu.
#Tumebadilishana mawazo kuhusu masuala ya kimataifa kwani ni vizuri kutetea maslahi ya Ukanda wetu pamoja na Bara letu kiujumla.