Yaliyojiri wakati wa kipindi cha ana kwa ana na msemaji mkuu wa Serikali Dr. Hassan Abbas redio ya Bomba kuhusu miaka mitatu ya Rais Magufuli

malichi

Member
Nov 7, 2018
79
86
#Katika miaka mitatu hii ya dhamira ya nchi yetu kuelekea kujitegemea kwa kuhakikisha watu wanalipa kodi, takwimu zinaonyesha mapato yameendelea kukua kwa kasi zaidi.

#Hii ilikuwa miaka mitatu ya kuasisi mapinduzi ya fikra kwa wananchi na watumishi wa umma kuelekea utendaji usio wa kimazoea.

#Ni miaka mitatu ya Kuasisi mapinduzi katika sekta ya viwanda ikiwa ni dhamira ya serikali kuelekea uchumi wa kati.

#Ni miaka mitatu ya kuasisi mapinduzi katika sekta ya anga hasa shirika letu la ndege, mpaka sasa tumeleta bombardier tatu, Boeing Dreamliner moja na muda wowote kuanzia sasa tunaleta AIRBUS mbili na baadae mmwakani tutaleta Dreamliner nyingine na mwisho wa siku tutakuwa na ndege 7.

#Ni miaka mitatu ya mapinduzi katika sekta ya afya ambapo tangu uhuru tulikuwa na hospitali 77 tu za Wilaya lakini katika miaka miaka mitatu pekee tumejenga hospitali za wilaya 67, vile vile tumeongeza idadi ya vituo vya afya katika ngazi ya Kata zaidi ya 210 kutoka 115 tu vilivyokuwa vinafanyakazi.

#Sasa hivi nchi yetu tunafanya matibabu ya kibingwa, kwa sasa tunafanya oparesheni ya moyo, upandikizaji wa figo, tunafanya oparesheni kupandikiza vifaa vya usikivu kwa watu wasio sikia.

#Ni miaka mitatu ya mapinduzi katika sekta ya elimu, tumeanza kutoka elimu bure na idadi ya wanafunzi wanaodahiliwa imekuwa ikiongezeka, tunatoa takribani shilingi bilioni 23.83 kwa mwezi.

#Katika miaka mitatu tumetoa ajira za afya zaidi ya 8000 na walimu zaidi ya 6,000 wote hawa na watunishi wengine zaidi sasa wako kazini wanatekeleza majukumu yao.

#Tumeanzisha pia miradi ambayo itatoa ajira kwa watanzania kwa mfano mpaka sasa zaidi ya watanzania 26,000 wameajiriwa kwenye sekta ya viwanda.

#Watanzania tufanye kazi katika maeneo yetu, zile changamoto ambazo zinazojitokeza sisi kama Serikali tutaendelea kuzifanyia kazi.

#Kuhusu uhuru wa habari Tanzania mpaka sasa tuna magazeti zaidi ya 200 na hakuna aliyewahi kuleta maombi ya usajili akakataliwa kama amefuata masharti yote, hiki ni kiwango kipimo muhimu cha Uhuru wa Habari, na tuna redio zaidi ya 150, TV zaidi ya 35. Sasa watu wasichanganye uhuru wa habari na baadhi yao kuvunja sheria za nchi au maadili ya uandishi wa habari.

#Watanzania wanahaki ya kupewa taarifa sahihi na za ukweli lakini si habari za uongo au uzushi.Ni kwa makosa kama haya sisi tutachukua hatua pale ambapo tunaonya, tinashauri maadili yazingatiwe mtu bado anakaidi.

#Tutaanzisha mfumo wa kielektroniki utakaosaidia waandishi wa habari kupata vitambulisho vya uandishi wa habari kwa urahisi.

#Uhusiano wa Tanzania na mataifa mengine pamoja na jumuiya za kimataifa upo vizuri na tunashirikiana na nchi mbalimbali vizuri.

#Tupo vizuri kama Taifa, watanzania tufanye kazi na tutaendelea kuhamasisha maendeleo nchini.
 
mbiki toka mwisho inahitimisha uongo aliotapika hapo
 
Back
Top Bottom