Yaliyojiri wakati Rais akizindua hoteli ya nyota tano ya Verde leo Januari 11, 2020 Zanzibar

Cybercrime

JF-Expert Member
Feb 14, 2014
3,248
2,000
Leo ni siku muhimu kwa maendeleo ya taifa letu hasa kwa uwekezaji huu mkubwa uliozalisha ajira zaidi ya 200.

Miradi kama hii inadhihirisha tunajikomboa kiuchumi. Hoteli hii yenye hadhi ya nyota tano inachochea kukua kwa uchumi, hongera muwekezaji

Umenifurahisha umelipa kodi toka ulipoanza umelipa Bilioni 4 na ushee hongera Bakhresa

Kwa sasa Sekta ya Utalii inachangia asilimia 80 ya fedha za kigeni Zanzibar. Uwepo wa Hoteli hii utaongeza fedha za kigeni

Mmiliki wa hoteli hii ni Mtanzania mwenzetu ndio maana wakati wote nawaambia watanzania sisi sio maskini tukiamua tunaweza. Nampongeza Mzee Bakhresa kwa uwekezaji katika sekta mbalimbali

Naipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuweka mazingira bora kwa uwekezaji. Kwa uwekezaji huu mkubwa uliogharimu Bilioni 65

Mzee Bakhresa hakuzaliwa tajiri amezaliwa maskini amefanya kazi kwa bidii na kuwa mvumilivu mpaka ametajirika. Wawekezaji sio lazima watoke nje wawekezaji wanaweza kutoka ndani na kuleta tija kwa taifa.

Niwaombe viongozi waweke mazingira mazuri ili kuwatengeneza wawekezaji wazawa kwa maendeleo ya taifa

Watanzania na wanasiasa wenzangu msifiche mali zenu hata kama mlizipata kwa kificho wekezeni ili kulijenga taifa

Tutaendelea kulinda usalama wa wawekezaji na Watanzania ili Tanzania ibaki kuwa yenye neema na sehemu nzuri ya kukimbilia
 

Pakawa

JF-Expert Member
Mar 11, 2009
6,109
2,000
Kufungua Hotel na Head of State ni upoyoyo
Kuna Hotel zinajengwa duniani za kisasa kushinda huu uchafu wenu umewahi ona Head of State anatumia pesa za walipa kodi kuhangaika na ushamba huu
Ni ushamba uliopitiliza period!
 

KENZY

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
11,851
2,000
Vichwa panzi wameshaanza kusagana humu! Fanyeni kazi mpate hela na nyinyi mje mmualike rais kwenye miradi yenu,watu wanahangaika na wanaotoa Kodi za mabillion na si wanaopiga mikelele humu.. na hili limesimama kibiashara linapaisha hotel husika kwa kuzinduliwa na rais kenge tutaendelea kung'aka wengine wanapiga hela..
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom