Yaliyojiri viwanja vya JMK Park kwenye Maadhimisho ya #SikuYaMtoto wa Afrika, 2017

Sema Tanzania

JF-Expert Member
May 18, 2016
251
465
Ndugu WanaJF,

Mnakumbuka tuliwaalika kujumuika nasi kwenye kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika? >> Je, unaishi Dar? Una mtoto wa umri kati ya miaka 3 na 15? Mlete kwa Jakaya M. Kikwete

Hatimaye ile siku imewadia na tuko viwanjani muda huu tayari kuanza sherehe hizi zinazofanyika mara moja tu kwa mwaka.

Kwa niaba ya wenzetu wa JamiiForums ambao tuko nao hapa kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa, tunakukaribisha uungane nasi kwenye uzi huu ili kujua kinachojiri moja kwa moja kutoka katiika viwanja vya Jakaya M. Kikwete Youth Park jijini Dar es salaam.

Pia unaweza kufuatilia kwenye kurasa zetu zote za mitandao ya kijamii kwa matukio zaidi na picha;

Twitter | JamiiForums na SemaTanzania (hashtag [HASHTAG]#SikuYaMtoto[/HASHTAG])

Instagram: | SemaTanzania na @jamiiforums_events

Facebook: | Facebook.com/SemaTanzania

Usibanduke!
---------

Updates..

Shughuli imeanza sasa..

Mtt.jpg


Hapa ni hatua za awali kabisa mapema leo. Wadau wetu wakiandaa bango la kupigia picha kunako zulia jekundu..

ssk.jpg

Na zoezi la picha limeanza kwa kasi..
-------

Tunawaletea zaidi matukio katika picha kwa kadri yanavyotokea..

Mvua ya ghafla imejitokeza na kufanya washiriki wawahishe zoezi la kwenda kupata chakula kabla ya kurudi kuendelea kufurahia siku hii ya kipekee hapa...

Baada ya zoezi la kupata chakula, kinachoendelea muda huu ni zoezi la upigaji picha, kuchora nyuso za watoto (face painting) pamoja na michezo mbalimbali..
 
Tuko pamoja tupe kinachojiri....
Tuwathamini,tuwalinde na tuwapende watoto wetu

[HASHTAG]#sikuyamtotowaafrika[/HASHTAG]
 
Siku ya mtoto wa Afrika huadhimishwa kimataifa kote duniani kwa lengo la kutambua thamani, utu , na umuhimu wa mtoto duniani. Maadhimisho haya hufanywa kila juni 16 tangu ilipotangazwa kuwa siku rasmi mwaka 1991 na jumuiya ya umoja wa Afrika. Elimu kwa watoto ndio imekuwa mada kuu kwa nchi nyingi katika kumuinua mtoto wa Africa.
 
Historia siku ya mtoto wa Afrika

Siku ya mtoto wa Afrika – au kwa kimombo Day of African Child (DAC), ikiwa ni kumbukumbu ya mwaka 1976 ambapo waandamaji wanafunzi wa shule za Soweto Afrika ya Kusini waliandamana kupinga elimu iliyokuwa inatolewa kwa manufaa ya utawala wa kibaguzi wa makaburu. Maandamano hayo yalipok elewa na mikono isiyo na huruma na masikio yasiyo sikivu ya utawala wa kibaguzi na kusababisha vifo vya mamia ya wanafunzi ambao hawakuwa na silaha,idadi halisi ya waliouwawa haijulikani lakini inakadiliwa ni watoto 176 mpaka 700.

Hector Pieterson 13 anayejulikana kama ishala ya waandamanaji (The Symbol of the Protest) alikuwa ni mmoja wa watoto wa shule aliyepigwa risasi na askari,alikimbizwa kwenye Dispensari ya kijiji na kujulikana alifariki mda mfupi baada ya kupigwa risasi. Alipopigwa risasi Hector alibebwa na Mbuyisa Makhubo 18 akisaidiana na dada yake Hector aliyeitwa Antoinette 17,walikimbilia gari la mpiga picha Sam Nzima ambaye aliwapiga picha.
img_7944-1.jpg

Hata leo imekuwa ni picha ya kumbukumbu(Iconic image) ya machafuko hayo. Siku ya kumbukumbu na jumba la maonyesho ya Hector Pieterson yalizinduliwa juni 16,2002
260px-HectorPieterson1030626.JPG

“Watu wangu, leo nipo huru kwa kuwa sitosahaulika kabisa, siku itatimia ambapo kila mmoja wetu atakuwa huru, huru kutokana na unyanyasaji, huru kutokana na woga,huru kutokana na kuuwawa,nyinyi ni vijana wadogo mtaishi hadi kujiona siku hiyo na hata kama sintofanikiwa kuiona siku hiyo ninyi mnatakiwa kusadiki tu mimi nitakuwepo siku hiyo,hapa ni nyumbani kwangu pahala pa kuishi.”

Hayo ni maneno yaliyotamkwa na Sarafina katika filamu iliyoigiza mauaji hayo ya juni 16,1976 huko Soweto.Inaaminika kuwa maandamano hayo yaliyofanyika miaka 41 iliyopita yalikuwa mwanzo wa kuangusha utawala wa kibaguzi nchini humo.

Juni 16,ilitangazwa rasmi mwaka 1991 na Jumuiya ya Umoja wa Afrika kuwa siku ya mtoto wa Afrika.Siku hii inatoa nafasi kwa wadau wote wa haki za watoto,zikiwamo serikali mbalimbali,mashirika yasiyo ya kiserikali na hata jumuia za kimataifa kuyatazama kwa kina matatizo yote yanayowakabili watoto katika bara letu la Afrika.
 
Tunawaletea zaidi matukio katika picha kwa kadri yanavyotokea..

Mvua ya ghafla imejitokeza na kufanya washiriki wawahishe zoezi la kwenda kupata chakula kabla ya kurudi kuendelea kufurahia siku hii ya kipekee hapa...

Baada ya zoezi la kupata chakula, kinachoendelea muda huu ni zoezi la upigaji picha, kuchora nyuso za watoto (face painting) pamoja na michezo mbalimbali..


day.jpg


mtttt.jpg
 
Kutana na mtoto anaitwa Ethan mwenye umri wa miaka 6 akitambulisha App yake inayoitwa EthanMan hapa viwanjani.

ethan.jpg

ethan2.jpg
ethn.jpg
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom