Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,805
- 11,965
Leo mgombea wa Urais kupitia chama cha mapinduzi (CCM), Dkt. John Magufuli yupo jijini Mwanza baada ya kuwasili jana ambapo yeye na chama chake wanatarajia kuzindua kampeni zao jijini humo kwenye uwanja wa CCM Kirumba kuomba ridhaa ya wananchi kuendelea kuongoza serikali.
Mwaka 2015, Dkt Magufuli na chama chake walipata ushindi mnono jijini Mwanza na viunga vyake. Je, wapiga kura wataendelea kuwaamini na kuwapa ridhaa? Kuwa nami kukujuza yatakayojiri leo kwenye uzinduzi wa kampeni za chama cha Mapinduzi jijini Mwanza.
=====
Yaliyojiri
Dkt. Magufuli amesema: Tumefanya ukarabati wa Meli 5 na tumejenga Meli mpya kwa gharama ya Bil 152. Tumejenga vivuko vya MV Mwanza na MV Ilemela kwa Bil 2.7
"Nataka Meli zetu za MV Mwanza, MV Victoria na nyingine ziwe zinasafiri hadi Bukoba, Uganda, Musoma na kuja Mwanza"
Tumeanza kujenga Reli ya umeme na ili ikamilike ndiyo maana tumekuja tena kuwaomba kura. Mnaona Ndege kubwa za abiria na mizigo zinaondoka moja kwa moja hadi Ulaya.
"Inawezekana mkachagua wengine tutakuwa tumepoteza mipango ya kuiendeleza Mwanza"
Zamani maeneo ya huku ikiwemo Chato ilikuwa ukitaka kwenda DSM lazima upite Bukoba hadi Uganda, ukazunguke Kenya ndio uende DSM
"Yaani unaenda Makao Makuu ya Nchi yako ila lazima uzungukie Nchi mbili za jirani, haya sasa hayapo. Ukiona vyaelea vimeundwa"
Tunaupanua uwanja huu wa Mwanza, ndege yoyote kutoka nchi yoyote itatua hapa, tuongeze watalii, tukuze uchumi wetu.
Wapo wanaobeza atapigiwa kura na madaraja, watu wanaopita kwenye hayo madaraja, wanaotibiwa kwenye hospitali tulizojenga watanipigia kura Okt. 28.
======
Mgombea wa Urais kupitia Tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM, Dkt. John Pombe Magufuli akimvalisha kofia Msanii wa Bongo Flavor Nasib Abdul Diamond ambaye alikuwa akitumbuiza katika Mkutano ya Kampeni ya Chama cha Mapinduzi CCM uliofanyika leo tarehe 7 Septemba, 2020 jijini Mwanza