Yaliyojiri Uwanja wa Uhuru: Kuapishwa kwa Dr. Pombe Magufuli kuwa Rais wa Tanzania

wabungenjaa

JF-Expert Member
Feb 21, 2014
1,782
336



Ndugu mtanzania. Leo ni siku ya kihistoria katika nchi yetu ambapo rais mteule John Joseph Magufuli ataapishwa na kukabidhiwa Nchi rasmi.

Maandalizi yote muhimu yamekamilika.

Fuatilia uzi huu kwa live updates mwanzo mwisho.
Tukio hili la aina yake litarushwa mubashara na Tbc1,star tv,channel ten,Azam tv na clouds tv pamoja radio mbalimbali ikiwemo tbc fm.

Stay updated. Stay tuned

*******updates********

- Wageni mbalimbali wanaendelea kuwasili hapa uwanjani.

- Wameingia marais wastaafu akiwemo Benjamin Mkapa,Ally Hassan Mwinyi na wake zao,mawaziri wakuu wastaafu Msuya na wengineo,Jaji Augustino Ramadhan na sasa jaji mkuu Othman Chande anaingia na ndio atamuapisha rais mteule.

- Marais saba wa nchi mbalimbali wanahudhuria tukio hili. Pia waziri mkuu mstaafu wa Kenya Raila Odinga yupo

- Wapo mabalozi wa nchi mbalimbali na wawakilishi wa jumuiya za kimataifa na mashiriki ya UN.

- Spika wa bunge Anne Makinda na naibu spika Job Ndugai wamo.

- Rais wa Zanzibar na delegation yote ya Zanzibar akiwemo Pandu Ameir Kificho wamehudhuria.

- Watu ni wengi kweli kweli.



RAIS MTEULE KATIKA KILA TUKIO MUHIMU MVUA ILINYESHA IKIWEMO LEO. ISHARA YA BARAKA NA UTAWALA HALALI WA RIDHAA YA WANANCHI.

- Vikosi vya majeshi ya wananchi ya tanzania viko tayari kwa gwaride maalum.

- Wabunge wateule wa Jamhuri ya Muungano wameshaketi tayari.

- Jaji Mkuu Othman Chande ndio anawasili sasa hivi.

- Bendera ya Rais wa sasa itashushwa na kuashiria ukomo wa serikali ya awamu ya nne na Rais wa awamu ya tano atakapoapishwa bendera ya taifa itapandishwa.

- Anaingia mke wa Rais Mteule Mama Janet Magufuli

- Wapo viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa

- Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe amewasili hivi punde.

- Rais Jakob Zuma wa Afrika Kusini pia naye amefika.

-Maandamano rasmi ya kuelekea Jukwaa Maalum la Kuapishwa Rais mteule yataongozwa na Jaji Mkuu,Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano na Katibu Mkuu Kiongozi.

- Tukio linalofuata ataingia Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi yote ya Tanzania, Mh. Jakaya Mrisho Kikwete.

- Rais mteule Dr. Magufuli ameelekea jukwaa maalum la kiapo.

- Rais anakagua gwaride kwa mara ya mwisho kisha ataenda jukwaa la kuapisha na mizinga 21 inapigwa, kisha bendera ya serikali ya awamu ya nne itashushwa.

-Wimbo wa taifa unaimbwa.

Bendera ya serikali ya awamu ya nne inashushwa kuashiria mwisho wa utawala wa awamu ya nne.


TUKIO LA KUAPISHWA MAGUFULI LINAENDELEA.

- Rais anayemaliza muda wake akiwa na makamu wake wanasaini kukubali kwao kukaa benchi na kukabidhi nchi rasmi kwa Rais wa Awamu ya Tano.


***UPDATES***

- Rais wa awamu ya Tano na makamu wake wameshakula kiapo, sasa ni sala kutoka kwa viongozi mbalimbali wa dini.

****updates*****

Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mh. Magufuli anapigiwa mizinga 21 ya Utiifu ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ)

Rais John P Magufuli anakagua gwaride la Tanzania likiwa katika umbo la ALFA kuashiria mwanzo wa Serikali Mpya. Rais amemaliza kukagua gwaride na sasa amepanda jukwaa kuu



******Updates****

Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania, Mh. John Pombe Magufuli kwa ufupi

Anawashukuru wote waliojitokeza kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwake,anashukuru tendo la kubadilishana madaraka kwa njia ya amani na anasema anatambua changamoto na majaribu yaliyopo katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Anawapongeza wapinzani walioonyesha ushindani na kuwaomba ushirikiano. Kwamba uchaguzi umepita sasa turudi katika umoja wetu tujenge taifa.

Sasa ni kazi tu.

Anaishukuru tume ya uchaguzi na wote waliofanikisha uchaguzi.

Anawapongeza jeshi kwa ukakamavu walioonesha kwenye gwaride na kwamba anafarijika na kuona ataongoza jeshi lenye afya.

Anawashukuru marais wastaafu mawaziri wakuu wastaafu na watanzania wote waliompa ushirikiano na kumuamini.

Anasema sio siku ya kutoa hotuba. Uchaguzi umekwisha. Rais ni John Magufuli. Wapinzani tufanye kazi sasa. Naenda kufanya kazi. Tunaenda kufanya kazi. Tupeni ushirikiano
 
Last edited by a moderator:
Picha na video kutoka Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam Tanzania



attachment.php
attachment.php
attachment.php
attachment.php
attachment.php
attachment.php
attachment.php
attachment.php
attachment.php
attachment.php
attachment.php
attachment.php
attachment.php
attachment.php
attachment.php
attachment.php
attachment.php
attachment.php
attachment.php
attachment.php
attachment.php
attachment.php
attachment.php
 

Attachments

  • 1.jpg
    1.jpg
    30.2 KB · Views: 11,548
  • 2.jpg
    2.jpg
    24.2 KB · Views: 11,412
  • 3.jpg
    3.jpg
    26.2 KB · Views: 11,272
  • 4.jpg
    4.jpg
    23.5 KB · Views: 11,186
  • 5.jpg
    5.jpg
    38.6 KB · Views: 11,188
  • 6.jpg
    6.jpg
    38.2 KB · Views: 10,988
  • 8.jpg
    8.jpg
    33.6 KB · Views: 10,948
  • 11.jpg
    11.jpg
    33.6 KB · Views: 1,120
  • 12.jpg
    12.jpg
    29.8 KB · Views: 10,793
  • 13.jpg
    13.jpg
    28 KB · Views: 11,546
  • 14.jpg
    14.jpg
    31.3 KB · Views: 11,528
  • 15.jpg
    15.jpg
    29.6 KB · Views: 11,409
  • 16.jpg
    16.jpg
    28.9 KB · Views: 10,585
  • 17.jpg
    17.jpg
    14.6 KB · Views: 11,444
  • 18.jpg
    18.jpg
    27.2 KB · Views: 10,375
  • 19.jpg
    19.jpg
    29.2 KB · Views: 11,159
  • 20.jpg
    20.jpg
    30.5 KB · Views: 11,122
  • 21.jpg
    21.jpg
    20.2 KB · Views: 10,282
  • 22.jpg
    22.jpg
    31.3 KB · Views: 11,154
  • 23.jpg
    23.jpg
    30.6 KB · Views: 10,269
  • 24.jpg
    24.jpg
    35.7 KB · Views: 11,106
  • 25.jpg
    25.jpg
    34.2 KB · Views: 10,223
  • 26.jpg
    26.jpg
    37.3 KB · Views: 10,201
Last edited by a moderator:
Picha na video kutoka Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam Tanzania
attachment.php
attachment.php
attachment.php
attachment.php
attachment.php
attachment.php
attachment.php
attachment.php
attachment.php
attachment.php
attachment.php
attachment.php
attachment.php
attachment.php
attachment.php
attachment.php
attachment.php
attachment.php
attachment.php
attachment.php
attachment.php
attachment.php

 

Attachments

  • 27.jpg
    27.jpg
    37.8 KB · Views: 10,596
  • 28.jpg
    28.jpg
    39.5 KB · Views: 9,812
  • 29.jpg
    29.jpg
    34.2 KB · Views: 10,534
  • 30.jpg
    30.jpg
    25.9 KB · Views: 9,705
  • 31.jpg
    31.jpg
    33 KB · Views: 10,604
  • 32.jpg
    32.jpg
    22.1 KB · Views: 9,635
  • 33.jpg
    33.jpg
    35.5 KB · Views: 10,497
  • 34.jpg
    34.jpg
    34.2 KB · Views: 9,565
  • 35.jpg
    35.jpg
    25.3 KB · Views: 9,594
  • 36.jpg
    36.jpg
    10.3 KB · Views: 9,614
  • 37.jpg
    37.jpg
    23.5 KB · Views: 9,739
  • 38.jpg
    38.jpg
    25.2 KB · Views: 9,542
  • 39.jpg
    39.jpg
    21.1 KB · Views: 9,531
  • 40.jpg
    40.jpg
    24.3 KB · Views: 9,401
  • 41.jpg
    41.jpg
    26.6 KB · Views: 9,625
  • 42.jpg
    42.jpg
    27.7 KB · Views: 10,025
  • 43.jpg
    43.jpg
    27.7 KB · Views: 11,595
  • 44.jpg
    44.jpg
    24.8 KB · Views: 10,217
  • 45.jpg
    45.jpg
    27 KB · Views: 9,927
  • 46.jpg
    46.jpg
    26.2 KB · Views: 9,708
  • 47.jpg
    47.jpg
    25.4 KB · Views: 11,298
Haimaanishi chochote.

Mvua kila mwaka zinanyesha na zina msimu wake.

Na sasa hivi ni msimu wa mvua za vuli.

Hivyo siku ya leo kunyesha mvua hakuashirii chochote kile kuhusu huyo jamaa.

Bali kunyesha kwake kuna uhusiano wa moja kwa moja na msimu uliopo.
 
Kwa Mila na Desturi za Kiafrika, kunyesha kwa mvua wakati wa shughuli kama hii ya leo ya kumuapisha Mhe. John P. Magufuli, ni ishara na dalili njema kwa kiongozi huyo.

Wenye hisia za kisiasa na wale wenye MAHABA hawatokubaliana na hili.
 
Back
Top Bottom