Yaliyojiri Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam: Maadhimisho ya miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,188
25,493

Tutapeana hapa kinachojiri kwenye maadhimisho haya. Viongozi mbalimbali wa kitaifa,wastaafu na wa sasa,wanaendelea kuwasili.

Vikosi vya gwaride viko tayari kwa maadhimisho hayo. Kwasasa anawasili Waziri Mkuu Majaliwa K. Majaliwa

Rais wa Zanzibar,Dr. Ally Mohamed Shein,ndiye anayewasili uwanjani.

Jecha S. Jecha naye yupo uwanjani

Sasa anawasili Makamu wa Rais,Mama Samia Suluhu Hassan

Kumekucha sasa,Rais Dr. John Pombe Joseph Magufuli,Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Tanzania,anawasili sasa uwanjani tayari kuanza kwa maadhimisho haya.

Rais Magufuli yuko kwenye gari maalum kuzunguka uwanjani na kuwasalimu wananchi. Katika gari hilo,yupo na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange.

Rais sasa amepanda jukwaa maalum kupokea salamu toka kwa jeshi. Gwaride liko chini ya Kamanda Luteni Kanali Makanya Eras. Wimbo wa Taifa na mizinga 21 vinarindima.

Rais sasa anakagua gwaride

Ukaguzi umemalizika. Rais anarejea jukwaa kuu. Vikundi vya jeshi vitapita mbele yake kwa heshima,kwa mwendo wa pole na mwendo wa haraka

Sasa vikosi vinapita mbele ya Rais kwa kutoa heshima

Gwaride limekamilika. Linajiweka tayari kuondoka uwanjani kupisha ratiba nyingine kuendelea. Yatafuata maonyesho ya makomandoo na kikosi cha wanamaji wakiwa na kilo 65 migongoni mwao.

Sasa Makomando wanaonyesha uzoefu wao

Komando wanakunja nondo kwa mikono

Komando wanapigana kwa fito hadi kuvunjika

Sasa ni zoezi la kuvuja tofali kifuani na kichwani mwa komando

Komando analalia misumari mgongo wazi

Komando wanasukuma gari lililoharibika hadi kutembea

Kwata ya kimyakimya

Sasa vinafuta vikundi vitatu vya ngoma za asili

Sasa rais Magufuli anahutubia umati uliofika katika viwanja vya uhuru.
Rais anaanza kwa kutoa salamu huku itifaki ikiwa imezingatiwa.

Rais Magufuli: Niliamua kusitisha sherehe za mwaka jana kwa sababu kuu mbili; kwanza Sherehe za mwaka jana zingefanyika kabla sijaapishwa, pili sherehe zingegharimu shiling bilioni 4. Nilielekeza hizo bilioni 4 zitumike kujenga barabara.

Rais Magufuli:
Sherehe za miaka 55 ya uhuru nimeamua zifanyike hapa kwani zitakuwa ndo sherehe za mwisho kufanyika Dar es salaam, Sherehe nyingine zote zitafanyika Makao makuu Dodoma.

Rais anawapongeza wapigania uhuru na marais wastaafu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania na viongozi wote wastaafu.

Rais Magufuli:
Ndugu zangu watanzania katika bajeti ya mwaka 2016/17 tumetenga asilimia 40 ya bajeti yote kwa ajili ya miradi ya maendeleo. Tumeanza miradi mbalimbali ikiwemo kinyerezi I,II na III.

Mpaka sasa tumeshanunua ndege sita kwa ajili ya kujenga uchumi na utalii wa nchi yetu.
Bajeti ya afya imeongezeka kutoka bilioni 31 hadi bilioni 131.
Makusanyo yameongezeka kutoka bilioni 850 mpaka wastani wa trilioni 1.2

Rais Magufuli: Tutaendelea kuchukua hatua kali ktk masuala ya rushwa kwani rushwa ni kansa. Tumepanga kuondoa uonevu hasa kwa wananchi wanyonge
Ombi langu kwenu, tuendelee kudumisha amani yetu. Tudumishe pia umoja na mshikamano wetu tusisahau kuulinda muungano wetu. watanznia pia tuendelee kufanya kazi tuzingatia kauli ya hapa kazi Tuu.

Rais Magufuli: Tutajihidi kutatua kero zenu kwa uwezo wetu wote bila kubagua mtu kwa dini yake, kabila lake au chama chake.

Asanteni sana na Hongereni sana kwa kutimiza miaka 55 ya uhuru
 
Maalim Seif ametinga hapo uwanjani...!?

Kutaka kujua tu...!
 
Tutapeana hapa kinachojiri kwenye maadhimisho haya. Viongozi mbalimbali wa kitaifa,wastaafu na wa sasa,wanaendelea kuwasili.

Vikosi vya gwaride viko tayari kwa maadhimisho hayo. Kwasasa anawasili Waziri Mkuu Majaliwa K. Majaliwa

Naomba kukuuliza hivi Mkuu wa Mkoa Paul Makonda siku hizi na yeye amekuwa Mtu wa Itifaki? Kwani namwona anafanya Kazi za Watu wa Protocol na kimsingi yeye anatakiwa tu kumpokea mgeni, kupeana nae mkono kisha kuwaachia Watu wa ( Kazi Maalum / Itifaki ) kuendelea na majukumu yao waliyosomea na kubobea nayo lakini cha kusikitisha yeye huyo huyo RC Makonda anaenda kumpokea Mgeni kisha yeye huyo huyo tena anawasindikiza karibu na kupanda ngazi tena huku akitoa maelekezo. Huyu Mkuu wenu wa Mkoa aache kuwa na sifa na kimbelembele na nina uhakika hata Watu wa Itifaki alionao pale anawakwaza. Kwanini hajifunzi na habadiliki?
 
Hata mimi nashangaa sana. Hakupaswa kufanya hivyo
 
Hamna viongozi wageni wa nchi nyingine .i.e kenya, uganda, rwanda, etc:(:(, au wapo angani wanakuja?
 
Back
Top Bottom