Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,196
- 25,516
Tutapeana hapa kinachojiri kwenye maadhimisho haya. Viongozi mbalimbali wa kitaifa,wastaafu na wa sasa,wanaendelea kuwasili.
Vikosi vya gwaride viko tayari kwa maadhimisho hayo. Kwasasa anawasili Waziri Mkuu Majaliwa K. Majaliwa
Rais wa Zanzibar,Dr. Ally Mohamed Shein,ndiye anayewasili uwanjani.
Jecha S. Jecha naye yupo uwanjani
Sasa anawasili Makamu wa Rais,Mama Samia Suluhu Hassan
Kumekucha sasa,Rais Dr. John Pombe Joseph Magufuli,Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Tanzania,anawasili sasa uwanjani tayari kuanza kwa maadhimisho haya.
Rais Magufuli yuko kwenye gari maalum kuzunguka uwanjani na kuwasalimu wananchi. Katika gari hilo,yupo na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange.
Rais sasa amepanda jukwaa maalum kupokea salamu toka kwa jeshi. Gwaride liko chini ya Kamanda Luteni Kanali Makanya Eras. Wimbo wa Taifa na mizinga 21 vinarindima.
Rais sasa anakagua gwaride
Ukaguzi umemalizika. Rais anarejea jukwaa kuu. Vikundi vya jeshi vitapita mbele yake kwa heshima,kwa mwendo wa pole na mwendo wa haraka
Sasa vikosi vinapita mbele ya Rais kwa kutoa heshima
Gwaride limekamilika. Linajiweka tayari kuondoka uwanjani kupisha ratiba nyingine kuendelea. Yatafuata maonyesho ya makomandoo na kikosi cha wanamaji wakiwa na kilo 65 migongoni mwao.
Sasa Makomando wanaonyesha uzoefu wao
Komando wanakunja nondo kwa mikono
Komando wanapigana kwa fito hadi kuvunjika
Sasa ni zoezi la kuvuja tofali kifuani na kichwani mwa komando
Komando analalia misumari mgongo wazi
Komando wanasukuma gari lililoharibika hadi kutembea
Kwata ya kimyakimya
Sasa vinafuta vikundi vitatu vya ngoma za asili
Sasa rais Magufuli anahutubia umati uliofika katika viwanja vya uhuru.
Rais anaanza kwa kutoa salamu huku itifaki ikiwa imezingatiwa.
Rais Magufuli: Niliamua kusitisha sherehe za mwaka jana kwa sababu kuu mbili; kwanza Sherehe za mwaka jana zingefanyika kabla sijaapishwa, pili sherehe zingegharimu shiling bilioni 4. Nilielekeza hizo bilioni 4 zitumike kujenga barabara.
Rais Magufuli: Sherehe za miaka 55 ya uhuru nimeamua zifanyike hapa kwani zitakuwa ndo sherehe za mwisho kufanyika Dar es salaam, Sherehe nyingine zote zitafanyika Makao makuu Dodoma.
Rais anawapongeza wapigania uhuru na marais wastaafu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania na viongozi wote wastaafu.
Rais Magufuli: Ndugu zangu watanzania katika bajeti ya mwaka 2016/17 tumetenga asilimia 40 ya bajeti yote kwa ajili ya miradi ya maendeleo. Tumeanza miradi mbalimbali ikiwemo kinyerezi I,II na III.
Mpaka sasa tumeshanunua ndege sita kwa ajili ya kujenga uchumi na utalii wa nchi yetu.
Bajeti ya afya imeongezeka kutoka bilioni 31 hadi bilioni 131.
Makusanyo yameongezeka kutoka bilioni 850 mpaka wastani wa trilioni 1.2
Rais Magufuli: Tutaendelea kuchukua hatua kali ktk masuala ya rushwa kwani rushwa ni kansa. Tumepanga kuondoa uonevu hasa kwa wananchi wanyonge
Ombi langu kwenu, tuendelee kudumisha amani yetu. Tudumishe pia umoja na mshikamano wetu tusisahau kuulinda muungano wetu. watanznia pia tuendelee kufanya kazi tuzingatia kauli ya hapa kazi Tuu.
Rais Magufuli: Tutajihidi kutatua kero zenu kwa uwezo wetu wote bila kubagua mtu kwa dini yake, kabila lake au chama chake.
Asanteni sana na Hongereni sana kwa kutimiza miaka 55 ya uhuru