Yaliyojiri Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam: Maadhimisho ya miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara

Halafu watangazaji wa ITV wapunguze kuongea!...wawe wanatupia maneno ya hapa na pale, si kuwa kama wao ndio wenye shughuri. Mf. wakati wa mizinga na hata ukaguzi wa vikosi wanabwabwaja tu hata muziki wa brass band hausikiki!
Kweli kabisa jamaa walikuwa wanaongea sana.!
 
Naomba kukuuliza hivi Mkuu wa Mkoa Paul Makonda siku hizi na yeye amekuwa Mtu wa Itifaki? Kwani namwona anafanya Kazi za Watu wa Protocol na kimsingi yeye anatakiwa tu kumpokea mgeni, kupeana nae mkono kisha kuwaachia Watu wa ( Kazi Maalum / Itifaki ) kuendelea na majukumu yao waliyosomea na kubobea nayo lakini cha kusikitisha yeye huyo huyo RC Makonda anaenda kumpokea Mgeni kisha yeye huyo huyo tena anawasindikiza karibu na kupanda ngazi tena huku akitoa maelekezo. Huyu Mkuu wenu wa Mkoa aache kuwa na sifa na kimbelembele na nina uhakika hata Watu wa Itifaki alionao pale anawakwaza. Kwanini hajifunzi na habadiliki?
Exactly, ameingilia majukumu yasiyo yake, pia alikuwa anachagua, Jaji Mkuu hakumsindikiza. Kamfanya hata Chief Protocal yule mama asionekane.
 
Wanao jf nimekuwa nahudhulia Mara nyingi sherehe za Uhuru zaidi ya miaka 40. Lkn kwa Mara ya kwanza Leo nimeona tofauti kubwa kati ya sherehe zilizopita na ya Leo.

Sherehe za Leo zimekosa msisimko kabisa, hata ukiwaangalia watu usoni unaona ile bashasha hapo kabisa ya kutamani kuona jambo lolote jipya.

Mahudhurio ya watu wenyewe yamekuwa ya kawaida mno tofauti kabisa na hali halisi tulioizoea. MF upande wote wa kasikazini mwaka uwanja wa Uhuru ni watu wachache sana waliopo.

Shamrashamra zenyewe hakuna, wala husikii zile kelele na vigeregere ambazo tulikua tumezizoea ktk Siku kama hii kila MTU anaonekana mwenye mawazo YAKE binafsi licha ya kwamba huko ktk eneo LA tukio.
Hakika ninacho ona hali ni ngumu kiasi kwamba kila MTU anaisoma namba.
 
Naomba kuuliza kati ya Waziri na Mkuu wa mkoa nani yupo juu kwenye itifaki katika sherehe ya Taifa?
 
JK vipi au hasira za bibie bado zinawaka! Simuoni hapa.
Yani mpaka leo JK hujamjua tu, hana hayo mambo kabisa. Kama kweli hiyo stori basi mwingine asingesema watii maagizo ya Mkuu. JK yupo Ethiopia majukumu ya UN, Mkapa yupo Burundi. Na kama kususa angesusa Mama mwenyewe, lakini yupo. Usiwaze kipumbav
 
Jecha leo lazima atoke na tuzo ya heshima kwa sababu ya uchaguzi uliofanyika Zanzibar. Ngoja tusubiri Mkuu aanze kuhutubia!
 
Nashukuru kama na wewe umeliona!

lazima itifaki izingatiwe!

Mkuu nimebarikiwa na Mwenyezi Mungu kuwa na macho ya dhahabu na vipaji vingi vilivyotukuka ILA nina bahati mbaya mno kuwa huwa ninachukiwa kwa kusema ukweli hata hivyo wengi ambao husikiliza na kufuata kile ninachowashauri leo hii wamefanikiwa sana na hawaishi kunishukuru. Kuna makosa mengine kadhaa nimeyaona nitakujuza baadae kadri tunavyozidi kutiririka ngoja kwanza niandae uji wangu wa ulezi ninywe huku nikikodoa mubashara. Ila all in all Jamaa ana mapungufu makubwa mno ya Kiitifaki na naomba wahusika walione hili na wamsaidie tafadhali.
 
Nilimuona Kigwangallah akipiga selfie na Wambura. Mwijage alikuwa busy na simu mda mrefu, Kairuki alikuwa yuko alert sana na yanayomzunguka, akachungulia kwenye simu ya Mwijage anachokifanya, kwa ufupi amem-snoop
 
Jecha leo lazima atoke na tuzo ya heshima kwa sababu ya uchaguzi uliofanyika Zanzibar. Ngoja tusubiri Mkuu aanze kuhutubia!
acha tuone kama atatangaza na ajira mupya!
Yani mpaka leo JK hujamjua tu, hana hayo mambo kabisa. Kama kweli hiyo stori basi mwingine asingesema watii maagizo ya Mkuu. JK yupo Ethiopia majukumu ya UN, Mkapa yupo Burundi. Na kama kususa angesusa Mama mwenyewe, lakini yupo. Usiwaze kipumbav
Nimemuona Mama Jk,full tabasamu,full kicheko!
 
Back
Top Bottom