Yaliyojiri Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam: Maadhimisho ya miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara

Petro E. Mselewa

Verified Member
Dec 27, 2012
9,381
2,000

Tutapeana hapa kinachojiri kwenye maadhimisho haya. Viongozi mbalimbali wa kitaifa,wastaafu na wa sasa,wanaendelea kuwasili.

Vikosi vya gwaride viko tayari kwa maadhimisho hayo. Kwasasa anawasili Waziri Mkuu Majaliwa K. Majaliwa

Rais wa Zanzibar,Dr. Ally Mohamed Shein,ndiye anayewasili uwanjani.

Jecha S. Jecha naye yupo uwanjani

Sasa anawasili Makamu wa Rais,Mama Samia Suluhu Hassan

Kumekucha sasa,Rais Dr. John Pombe Joseph Magufuli,Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Tanzania,anawasili sasa uwanjani tayari kuanza kwa maadhimisho haya.

Rais Magufuli yuko kwenye gari maalum kuzunguka uwanjani na kuwasalimu wananchi. Katika gari hilo,yupo na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange.

Rais sasa amepanda jukwaa maalum kupokea salamu toka kwa jeshi. Gwaride liko chini ya Kamanda Luteni Kanali Makanya Eras. Wimbo wa Taifa na mizinga 21 vinarindima.

Rais sasa anakagua gwaride

Ukaguzi umemalizika. Rais anarejea jukwaa kuu. Vikundi vya jeshi vitapita mbele yake kwa heshima,kwa mwendo wa pole na mwendo wa haraka

Sasa vikosi vinapita mbele ya Rais kwa kutoa heshima

Gwaride limekamilika. Linajiweka tayari kuondoka uwanjani kupisha ratiba nyingine kuendelea. Yatafuata maonyesho ya makomandoo na kikosi cha wanamaji wakiwa na kilo 65 migongoni mwao.

Sasa Makomando wanaonyesha uzoefu wao

Komando wanakunja nondo kwa mikono

Komando wanapigana kwa fito hadi kuvunjika

Sasa ni zoezi la kuvuja tofali kifuani na kichwani mwa komando

Komando analalia misumari mgongo wazi

Komando wanasukuma gari lililoharibika hadi kutembea

Kwata ya kimyakimya

Sasa vinafuta vikundi vitatu vya ngoma za asili

Sasa rais Magufuli anahutubia umati uliofika katika viwanja vya uhuru.
Rais anaanza kwa kutoa salamu huku itifaki ikiwa imezingatiwa.

Rais Magufuli: Niliamua kusitisha sherehe za mwaka jana kwa sababu kuu mbili; kwanza Sherehe za mwaka jana zingefanyika kabla sijaapishwa, pili sherehe zingegharimu shiling bilioni 4. Nilielekeza hizo bilioni 4 zitumike kujenga barabara.

Rais Magufuli:
Sherehe za miaka 55 ya uhuru nimeamua zifanyike hapa kwani zitakuwa ndo sherehe za mwisho kufanyika Dar es salaam, Sherehe nyingine zote zitafanyika Makao makuu Dodoma.

Rais anawapongeza wapigania uhuru na marais wastaafu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania na viongozi wote wastaafu.

Rais Magufuli:
Ndugu zangu watanzania katika bajeti ya mwaka 2016/17 tumetenga asilimia 40 ya bajeti yote kwa ajili ya miradi ya maendeleo. Tumeanza miradi mbalimbali ikiwemo kinyerezi I,II na III.

Mpaka sasa tumeshanunua ndege sita kwa ajili ya kujenga uchumi na utalii wa nchi yetu.
Bajeti ya afya imeongezeka kutoka bilioni 31 hadi bilioni 131.
Makusanyo yameongezeka kutoka bilioni 850 mpaka wastani wa trilioni 1.2

Rais Magufuli: Tutaendelea kuchukua hatua kali ktk masuala ya rushwa kwani rushwa ni kansa. Tumepanga kuondoa uonevu hasa kwa wananchi wanyonge
Ombi langu kwenu, tuendelee kudumisha amani yetu. Tudumishe pia umoja na mshikamano wetu tusisahau kuulinda muungano wetu. watanznia pia tuendelee kufanya kazi tuzingatia kauli ya hapa kazi Tuu.

Rais Magufuli: Tutajihidi kutatua kero zenu kwa uwezo wetu wote bila kubagua mtu kwa dini yake, kabila lake au chama chake.

Asanteni sana na Hongereni sana kwa kutimiza miaka 55 ya uhuru
 

Mzee wa hat-trick

JF-Expert Member
Nov 21, 2016
1,737
2,000
Katika watu ambao huwa napata amani nikiwa waona ni firstlady wetu kipenzi mama Janeth . Ila Leo sijamuona uwanjani kitu ambacho kimenipa huzuni ya moyo.
Unapataje amani sasa kwa kumuona mke wa mtu kwny TV...?? Ni kweli kabisa unasema umepata huzuni ya moyo..? Serious...??
 

Masanja

JF-Expert Member
Aug 1, 2007
4,131
2,000
Mi nakwambia huyu first lady ni moja ya wanawake jasiri na mvumilivu, yaan Magufuli yuko madarakani mwaka mmoja tu watu washa mchoka, ila yeye kaish naye miaka 30 nyumba moja, mumuache tuu mama kwa kweli.
Kusema ya wengine ni rahisi. Yako Nani anayajua. It is easy kuweka private life ya Magufuli for public opinion and discussion. What if na sisi tungepata access ya maisha yako private?

Holier than thou!
 

elmagnifico

JF-Expert Member
Jul 7, 2011
8,083
2,000
Acheni uongo wa huyo kimambi, tangu lini mtu akapigwa hadi kuzirai halafu hana majeraha!? Uongo mwingine bwana!
Hata mimi japo mkulu kwa mengine simkubari ila kimambi aliongopa.
Mama hakuwa na majeraha na ingekuwa kweli asingelezwa kwenye wodi public vile angepelekwa wodi private tena kwa usiri mkubwa ili yasivuje..
 

Bulesi

JF-Expert Member
May 14, 2008
7,862
2,000
Kuwa na amani nyumbani kwa kiongozi ni muhimu sana kwani inamuwezesha kutokuwa na msongo wa mawazo na hivyo kutoa maamuzi kwa kupima sana na sio kwa kukurupuka!!
Kwa kauli yake juu ya ushauri alioupata kutoka kwa mzee Ruksa kuhusu siri ya maisha marefu ,inaonekana JPM anapima upepo!!
 

Ndelyaukiwa

JF-Expert Member
Aug 8, 2016
257
500
Mi nawashangaa hawa wanaobweka ooh tuache ndoa za watu, mara tumwachie private life yake, mara tumwachie ya familia yake, Je mtu aliyeshindwa kuimanage familia ataweza kumanage taifa?
 

spinderella

JF-Expert Member
Jul 24, 2016
1,107
2,000
Acheni uongo wa huyo kimambi, tangu lini mtu akapigwa hadi kuzirai halafu hana majeraha!? Uongo mwingine bwana!
Kama wewe sio daktari wake uliemtibu au daktari hajazungumza hilo au hujsona file lake la matibabu basi huwezi kuthibitisha kuwa hakuwa na jeraha
 

DUBULIHASA

JF-Expert Member
Nov 26, 2016
1,858
2,000
Huyu Mama mwenye sura ya upole anapata matatizo makubwa kuliko watanzania weng wanavyofikiri. MUNGU AMSAIDIE
 

mambo

JF-Expert Member
Jun 11, 2007
2,379
2,000
Hii issue ya first lady inavyoongelewa kila pembe inanitia simanzi sana .....hata kama sio kipondo lisemwalo lipo na kama halipo......!!!!!!!Haiwezekaniiii watu wakamuongelea tuuuu daahhh ....[HASHTAG]#BRING[/HASHTAG] BACK OUR FIRST LADY.....PLEASE.Nakumbuka siku mkuu anaapishwa uwanjani yule mama alikuwa na afya nzuriii na alikuwa anatabasamu na kufuta machozi.....
 

koyola

JF-Expert Member
May 20, 2015
2,369
2,000
Humu kila mtu na wake
Wengine hawakumuona mkapa
Wengine jakaya na yote kweli
Tusubiri tena ajitokeze ambae hajamuona wake
 

mambo

JF-Expert Member
Jun 11, 2007
2,379
2,000
Mi nawashangaa hawa wanaobweka ooh tuache ndoa za watu, mara tumwachie private life yake, mara tumwachie ya familia yake, Je mtu aliyeshindwa kuimanage familia ataweza kumanage taifa?
Hiyo ndoa ishakuwa ndoa ya taifa lazima tuiongelee sana tu na inatuhusu wote!!!!!!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom