Yaliyojiri uwanja wa Jamhuri Dodoma: Rais Kikwete kukabidhiwa Rasimu ya Katiba Mpya

jambo linaloshangaza kwani Dodoma hakuna askofu Wa katoliki? huyu padri ni Wa parokia gani hapa Dodoma?
 
Suala sio Bavicha. Kwa Tukio la leo umati Huu sio mkubwa. Pia Viongoz wote wakuu wangeshriki.
 
Kweli mijitu mingine hamnazo kabisa,yani yameingia uwanjani saa 2 asubuhi halaf mgeni rasmi anaingia saa kumi,ukiuliza kisa...eti makabidhiano ya rasimu ya katiba!kesho yanaanza kulalamika oooh maisha magumu,serikali haitujali wananchiii...pambaf kabisaaa..
Hao police wenye wamechomeshwa jua tangu asubuhi
 
Sio kawaida kwenye hafla ya kitaifa namna hio asalishe Padre. Huyo Padre anaweza kuwa ni mtu wa kawaida tu au kweli ni Padre lakini kuwepo kwake ni kwa nafsi yake na walipomjua basi wakamtafdhalisha asalishe. Huwezi ukakataa kusalisha kama wewe ni kasisi au sheikh. Tusimhukumu kwanza.

Askofu wa Jimbo Kuu la Dodoma ni Mh Thadei Ruwaichi, yule gwiji msomi aliyebobea katika faslafa sio tu ya kanisa bali ya elimu dunia. Sio rahisi akawa katika hafla kama ile!
 
jambo linaloshangaza kwani Dodoma hakuna askofu Wa katoliki? huyu padri ni Wa parokia gani hapa Dodoma?

Mkuu hukumsikia Askofu Ngalalekumtwa na Niwemugizi hapo jana? Kuna uzi unazungumzia juu ya msimamo wao na Kanisa jwa ujumla. Kwahakika kabisa ccm wahesabu kukosa kura za Wakatholic nchi nzima.

BACK TANGANYIKA
 
Ninachoona ni kwamba ccm ni kama wameshakuwa na uhakika wa kura za maoni za wananchi hata kabla kura hazijapigwa.
 
jambo linaloshangaza kwani Dodoma hakuna askofu Wa katoliki? huyu padri ni Wa parokia gani hapa Dodoma?

Kiti cha kiaskofu cha Dodoma kipo wazi baada ya mhasham Nyaisonga kuhamishiwa jimbo la Mpanda.
 
kumekuwa na nyaraka mbalimbali ambazo zimetolewa na makundi tofauti tofauti hasa viongozi wa dini yaani maaskofu kuupinga mchakato wa upatikanaji wa katiba mpya katika hatua ya bunge maalum. Jambo hili lilipelekea mwenyekiti wa lililokuwa bunge hilo mh. Samwel sitta kutoa maneno yasiyofaa kwa viongozi wa dini nchini.
Jambo linalonshangaza mimi ni kuona viongozi wa dini haohao wamejazana dodoma bila kujali matusi na fedhea zilizotolewa na sitta. Hii inaonesha namna ambavyo watanxania wengi tulivyowaoga na wanafiki, kwani viongizi hawa hawa wamekuwa wakiipinga katika ibada zao. Sasa nashindwa kuamini kwamba kuna askofu kutoka cct na padre wa kanisa katoliki pia yupo. Ifike wakati watanzania wenzangu tuwe wakweli na wenye misimamo bila kujali umesimama mbele ya nani.
Nawasilisha.

huwezi kukuta padre au askofu wa kanisa katoliki ktk upumbafu wa leo
wanajitambua sana wale
watakuwepo wachungaji na maaskofu njaa kali tu!
 
Chenge asema kuwa katiba wanayokabidhi leo dodoma imechukua mahudhui 81% kutoka kwenye katiba ya Warioba.....duuu mbona naona malupe lupe?
 
Sio kawaida kwenye hafla ya kitaifa namna hio asalishe Padre. Huyo Padre anaweza kuwa ni mtu wa kawaida tu au kweli ni Padre lakini kuwepo kwake ni kwa nafsi yake na walipomjua basi wakamtafdhalisha asalishe. Huwezi ukakataa kusalisha kama wewe ni kasisi au sheikh. Tusimhukumu kwanza.

Askofu wa Jimbo Kuu la Dodoma ni Mh Thadei Ruwaichi, yule gwiji msomi aliyebobea katika faslafa sio tu ya kanisa bali ya elimu dunia. Sio rahisi akawa katika hafla kama ile!

Dodoma haina askofu kwa sasa kwani alihamishiwa Mpanda
 
Katiba ya Chenge inataka Watanzania wakope kwa miaka 50 mbele.Sasa lini tutajitegemea wanafanya mambo ya aibu katiba inataka nchi ikope only katiba ya CCM inapendekeza Mikopo duniani.
 
Back
Top Bottom