Yaliyojiri Ubungo Plaza: Prof. Lipumba ametangaza nia ya kuchukua fomu ya kugombea Urais wa JMT

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
46,870
143,921
Kwa wasio na taarifa. Prof. Lipumba leo anatarajiwa kuchukua fomu ya kugombea urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ticket ya CUF/UKAWA na shughuli hiyo itaanza saa 4 asubuhi ya leo na itapofika saa 7:30 mchana.

Tukio hilo litarushwa live na ITV kutoka Ukumbi wa Blue Pearl Hotel pale Ubongo Plaza.

NOTE:
Mchakato unaanzia kwenye vyama kwanza kabla hajapatikana mgombea mmoja wa UKAWA.

Kaa mkao wa kula.

============

Updates
:
attachment.php

Mkutano ndo umeshaanza kurushwa Live ITV na muda huu 13:54GMT. Sasa ni dua kutoka kwa Madhehebu ya dini.

Viongozi waliopo jukwaa kuu pamoja na Lipumba ni;

Juma duni haji

Magadalena Sakaya

Simba wa nyika Maalim Seif.

CUF wanasema Mwaka huu ni mwaka wa maamuzi

Sasa anaye ongea ni katibu mkuu wa CUF Mh.Seif.

=Anasema bado Miezi mitatu ya hakuna kulala.

= Anaomba radhi kwa kuchelewa. Anasema alikua Pemba, akasema pamoja na shughuli hii hawezi muacha mwenyekiti wake.

=Anasema Tanzania Ipo tayari kwa Mageuzi. Watanzania wamechoka na utawala kandamini, Utawala wa Mabavu wa CCM. Wananchi Wanataka waishi katika nchi isiyo na ubaguzi, yenye haki sawa, isiyo na matabaka yenye tofauti kubwa sana ya kipato

=Anasema wote waliotangaza nia CCM, hakuna hata mmoja ambaye ni msafi.

=Tanzania inatakiwa impate rais asiye mbinafsi, ambaye anaguswa na matatizo ya watu, anayeweza kukaa na wananchi kwenye mvua au jua, mwenye uwezo wa kuona mbali mwenye kutujengea uchumi madhubuti, mwenye mawazo mapya. Rasilimali zitumike kwa manufaa ya Watanzania. Na mtu huyo sio Mwingine isipokua Prof. Lipumba.

UKAWA tulikubaliana kwamba kila chama kikae kimteue Mgombea ndani ya chama ili akashindanishwe na wengine wa UKAWA. Sisi tumemchagua Prof. Lipumba akatuwakilishe UKAWA. Ambapo UKAWA ndo watachagua Rais wa Kutuwakilisha kama Taifa,

Juma Duni Haji anasema;

=Huu ni Mwaka wa Uamuzi.

Prof alifukuzwa kazi chuo kikuu kisa kagombea Urais 1995 nami nikia mgombea mwenza, tulizunguka na gari moja Tanzania nzima. Nmekua mwenza wa Prof. Lipumba mara tatu.

Kila kipindi tulikua tukiwaambia watanzania wazinduke. CCM hata ukiwapa miaka mia, hawawezi kututoa hapa tulipo.

=Wezi wapo mitaani lakini Polisi wanampiga Lipumba. Walioiba eti hadi tufanye utafiti.

=Prof. kila mtu anajua Elimu yake. anao uwezo wa kuwasaidia watanzania

=Prof dunia inamtamani CCM wanampiga madongo

Prof. Ibrahim Lipumba Anasema;
=Haki?

=Haki sawa kwa nani?

=Asiependa haki?

Wanaumeeeeeeeeeeeeeeeeeeee??,

Wanawakeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee??,

CCM!!..Kwisha kwisha kabisa, nyang'anyang'a, ndembwe ndebwe, mlalo wa chali kifo cha mende .Asanteni sana.

=Nawashukuru wote mliokuja.

(Anaonyesha picha ya wasisi wa TANU iliyopigwa 1957. MMoja wa hao wazee waliopo kwenye hiyo picha leo yupo hapa Ukumbini).

=Nachukua fomu kwa mara ya tano kwa sababu;


1. Kuhakikisha tunapata Katiba mpya.
Hili jina la (UKAWA)Umoja wa Katiba ya Wananchi mimi ndo nlilibuni. UKAWA ni ummoja wa vyama vilivyo sajiliwa.

2.Nina uwezo na nia ya kuwaondosha hawa mafisadi ambao badala ya kua jela wanachukua fomu ya kugombea urais wa CCM. Wanahitajika kuwa jela na mali zao zirejeshwe

-Kidato cha tano nlisoma masomo ya hesabu uchumi na Geografia. Na chuo nliweka rekodi ya kufaulu Vizuri ambapo chuo kiliniomba nibakie shuleni nafundisha.

-Nilienda Marekani kusoma na Kurudi kufundisha chuio kikuu cha Dar. Nilikua mshauri wa Mwinyi katika maswala ya Uchumi

-Nlichaguliwa kua mshauri wa katibu mkuu wa Umoja wa mataifa katika maswala ya uchumi.

-Bunge la marekani walinikaribisha niwafunde kwanini nataka madeni ya Afrika yafutwe.

Bunge la Marekani nlikaribishwa kuwashauri kuhusu mahusiano kati ya shirika la fedha na Afrika. Ushauri ulikubaliwa. Nmefanya ushauri wa Wizara ya fedha Namibia, Swazland, Uganda. Katika maswala ya Ushauri nmefanya kwa muda mrefu.

Unapozungumzia maswala ya Uchumi nayaelewa sana.

-Umasikini wa Tanzania unasababishwa na Siasa mbovu za Seikali ya CCM.

-Nliulizwa umeoa? Ninaye mmoja ambaye anafanya kazi Umoja wa Mataifa ambapo yeye haruhusiwi kufanya shughuli za Kisiasa. Hata hivo mimi ndo nagombea urais sio familia ndio inagombea. Kama anataka siasa aingie kwa uwezo wake sio aingie kwenye ubawa wa mume au mke.

-Tunahitaji wakina mama waingie kwenye siasa kwa uwezo wao sio kwa kofia za familia kama ngazi. Hata Nyerere kwenye shughuli kubwa ulikua humuoni Mama Maria. Lakini sasa hivi wanabeba na familia zao.

3. Nataka wakina mama na Watoto wapate lisha bora na huduma za Msingi za Uzazi kwa kila Mtanzania. Watoto wanazaa wakiwa watoto, watoto wamedumaa, watoto wapewe Fursa za kusoma. Jambo la kuwekeza kwa watoto ndo msingi Imara

4. Kumaliza tatizo la ajira. Geografia yetu ni nzuri ambayo ninzuri katika kujenga ajira. Mtwara kuna badari asilia ya kina kirefu. Hapo kuna fursa ya Biashara kwani kuna gesi, Tanga kuna bandari na kunakubali kila aina ya mazao. Vilevile sekta ya kilimo ni sehemu nzuri sana ya kutengeneza ajira.

=Ujenzi wa miundo mbinu imara, sio tu tunaongeza ajira bali usalama pia kwani nchi nane tulizopakana nazo zinategemea bandari za Tanzania.

5. Hali ya Afya.
Tunatakiwa tuwe na hifadhi ya jamii kwani wazee wanateseka kwa kuwa hakuna huduma.

6. Ufisadi.
Kama nikichaguliwa kupeperusha bendera ya UKAWA, sitakuwa na huruma na mafisadi

=Kama UKAWA watanipendekeza kupeperusha bendera, Nikiwa rais ntaunda Serikali ya Umoja wa kitaifa kupambana na ufisadi.

=Nipo tayari Kumuunga mkono na Kumpigia debe Mgombea yoyote ambaye atapitishwa ndani ya UKAWA
. Ninacho waomba wananchi, Nendeni kujiandikisha ili tupige kura na kulinda kura pia, kwani miaka ya kuchakachuliwa imeshapitwa na wakati. Asanteni sana.

Kamaliza kuhutubia 15:15GMT

Asanteni.
 

Attachments

  • lipumba.png
    lipumba.png
    75.3 KB · Views: 12,646
safiiiiiiiiiiiiiiiiiii UKAWA mjue mkivurugana hampati hata robo ya viti mlivonavo wananchi tutawaadhibu
 
Kipyenga kinapulizwa kuashiria zamu ya upinzani.....tunataraji upepo kubadilika humu JF
 
Raisi Mkapa hakuwa Mchumi ila alizuia mfumuko wa bei na kuongeza thamani ya Shillingi.

Kinachohitajika ni utashi wa Kisiasa na kukubalika kwa wananchi.... Itakuwa tabu kumnadi Lipumba.

Kama Lowasa akipitishwa na CCM, Lipumba atashindwa asb mapema...

Hata CCM ikipitisha MKristo, Lipumba atashindwa Vibaya ...

CUF someni alama za nyakati..... Ijapokuwa sio rasmi ila mawazo ya Watanzania wanajua ni zamu ya MKristo... CCM wanajua hili

Hatuna haja na Raisi Mchumi......

Raisi hawezi kuamua mambo ya uchumi mwenyewe....

Ipo Tume ya mipango na wapo wachumi wa kumshauri Raisi vizuri.....

Kikwete ni mchumi ila uchumi ndo umedorora, shillingi kwishney.... mfumuko wa bei
 
I wish Viongozi wotee waandamizi wa vyama shiriki vya UKAWA kuhudhuria tukio hili i.e Mh.Mbowe, Mbatia, Makaidi< Mwalimu, Seif na wengineo wengii
 
Kwa wasio na taarifa,mh.Lipumba leo anatarajiwa kuchukua form ya kugombea urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ticket ya CUF/UKAWA na shughuli hiyo itaanza saa 4 asubuhi ya leo na itapofika saa 7:30 mchana,tukio hilo litarushwa live na ITV kutoka Ukumbi wa Blue Pearl Hotel pale Ubongo Plaza.

NOTE:
Mchakato unaanzia kwenye vyama kwanza kabla hajapatikana mgombea mmoja wa UKAWA.

Kaa mkao wa kula.

Dr. silaa Njoo utangaze na wewe, ....hahahaaaa
 
Yaani Cuf inataka kusmamisha wagombea zanzibar na bara? Hiyo haitakuwa sawa.
 
Ila msururu wa magamba haujamalizika.
Sasa hivi wanajaa bus tatu
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom