Yaliyojiri Tuzo za EATV kutoka Dar es Salaam

Miss Natafuta

JF-Expert Member
Sep 16, 2015
25,525
45,743


Leo Desemba 10, 2016 katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam zimetolewa tuzo kwa wasanii mbalimbali wa muziki na wa filamu kutoka nje na ndani ya Tanzania.

Jumla ya tuzi 9 zilizotelewa kwa wasanii mbalimbali waliofanya vizuri kwa mwaka 2016 ambapo tuzo moja ya heshima ilitolewa kwa mtu aliyekuwa na mchango mkubwa katika saanaa ya Tanzania na hivyo kufanya jumla ya tuzo 10.

Tuzo hii ilitolewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye.

Hapa chini ni orodha ya washindi wa tuzo mbalimbali zilizotolewa usiku wa Desemba 10.

Tuzo ya Filamu Bora ya Mwaka- Safari ya Gwalu

Wimbo Bora wa Mwaka- Aje wa Ali Kiba

Video Bora ya Mwaka- Aje ya Ali Kiba

Tuzo ya Mwigizaji Bora wa Kiume- Salim Ahmed maarufu Gabo

Tuzo ya Mwigizaji Bora wa Kike- Chuchu Hans

Kundi Bora la Muziki- Navy Kenzo

Mwanamuziki Bora Chipukizi- Amani Khamis maarufu Man Fongo

Tuzo ya Heshima- Dj Bonny Love

Mwanamuziki Bora wa Kike- Judith Wambura maarufu Lady JayDee

Mwanamuziki Bora wa Kiume- Ali Kiba

Mwanamuziki Ali Kiba ameweka rekodi katika tuzo hizi zilizotolewa kwa mara ya kwanza baada ya kutwaa tuzo tatu ikiwa ni Video Bora ya Mwaka, Wimbo Bora wa Mwaka, na Msanii Bora wa Kiume.
 
Kitendo walichofanya Clouds Kupitia XXL kuweka Tamasha Lao siku moja na EATV Awards ni Kuendeleza ule ule Upuuzi wa Ruge/Mwana FA vs Vinega,XXL Kama wadau wa Burudani ilitakiwa wakae na EATV wapeane mda kama wasanii wanavyopeana mda kwenye kutoa wimbo au kuingiza album sokoni.
 
Kitendo walichofanya Clouds Kupitia XXL kuweka Tamasha Lao siku moja na EATV Awards ni Kuendeleza ule ule Upuuzi wa Ruge/Mwana FA vs Vinega,XXL Kama wadau wa Burudani ilitakiwa wakae na EATV wapeane mda kama wasanii wanavyopeana mda kwenye kutoa wimbo au kuingiza album sokoni.

Acha ukichaa wewe,tamasha la after school bash ni la wanafunzi na limeisha saa 12 jioni. Usijitoe ufahamu tena.
 
Hii EATV AWARDS itabamba sana... naangalia hapa kwa channel yke ni noma sna
 
  • Thanks
Reactions: dtj
Acha ukichaa wewe,tamasha la after school bash ni la wanafunzi na limeisha saa 12 jioni. Usijitoe ufahamu tena.
Ficha Upumbavu wako,Hilo xul Bash mbona Le Mutuz miaka ya nyuma aliudhuria na yeye ni mwanafunzi? Nachozungumza kuweka ratiba siku moja na EATV Awards,Sidhani hao watu walioudhuria xul bash wakitoka huko waende mliman city kwenye Awards maana watakuwa wameshachoka.
 
Haiya haiya leo ndo leo , asiye na mwana abebe jiwe , zile tuzo za kwanza na za aina yake , zinazopenya bila promo kama Muziki ya darasa zinazofanyiwa figisu na wale jamaa kwa nao kulazimisha kuweka show mav.i leo huku wakiwatishia baadhi ya wasanii mamburura kususia show ya tuzo hizo, inafanyika katika ukumbi wa kimataifa hapa Mlimani city .Burudani mbalimbali zitaporomoshwa .Karibuni team wastaarabu wote wenye roho nyeupeeee kupata burudani nzuri na kuwaunga mkono watu wetu....

Wasanii watakao wania tuzo ni hawa wafuatao..

MWANAMUZIKI CHUPUKIZI.

Amani Hamisi (Man Fongo) - Hainaga Ushemeji
Feza Kessy - Sanuka
Rukia Jumbe (Rucky Baby) - Give me some more
Mayunga Nalimi (Mayunga) - Nice Couple
Rashid Said (Bright) - Nitunzie

MUIGIZAJI BORA WA KIUME
Meya Shabani Hamisi
Salim Ahmed (Gabo)
Daudi Michael (Duma)
Dotto Hussein Matotola
Saidi Mkukila

MUIGIZAJI BORA WA KIKE
Chuchu Hansy
Rachel Bithulo
Frida Kajala Masanja
Khadija Ally

FILAMU BORA YA MWAKA
Facebook Profile
Safari ya Gwalu
Mfadhili Wangu
Hii ni Laana
Nimekosea Wapi

KUNDI BORA LA MWAKA
Navy Kenzo
Mashauzi Classic
Team Mistari (Kenya)
Sauti Sol (Kenya)
Wakali Wao

VIDEO BORA YA MWAKA
Namjua - Shetta
Njogereza - Navio
Aje - Ali Kiba
Don't Bother - Joh Makini
NdiNdiNdi - Lady Jay Dee

MWANAMUZIKI BORA WA KIUME
Gnako
Shetta
Mwana FA
Ben Pol
Alikiba

MWANAMUZIKI BORA WA KIKE
Lilian Mbabazi (Uganda)
Ruby
Lady Jay Dee
Linah
Vanessa Mdee

WIMBO BORA WA MWAKA
Don't Bother - Joh Makini
NdiNdiNdi - Lady JayDee
Kamatia Chini - Navy Kenzo
Aje - Alikiba
Moyo Mashine - Ben Pol



Nimeshindwa weka picha atakayeweza kuweka picha aweke na mods watasaidia kuzipandisha

Show inaonyeshwa live channel 5 a.k.a eatv saivi red carpet na watu mbali mmbali wanaendelea kuingi ukumbini
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom