Zanzibar 2020 Yaliyojiri Tibirizi, Pemba mkutano wa kufunga kampeni ya Maalim Seif. Tundu Lissu ahudhuria

Mgombea Urais wa Tanzania anayeelekea kushinda Tundu Lissu leo atatikisa visiwa vya Pemba.

Pemba ngome Kuu ya ACT wanatarajiwa kumlaki kwa kishindo mgombea huyo wa Urais ambaye chama chake na ACT Wana urafiki wa Damu.

ACT Wazalendo imetangaza kumuunga mkono Tundu Lissu nafasi ya Urais wa Muungano huku CDM ikitangaza kumuunga mkono Maalim Seif nafasi ya Urais Zanzibar

Updates saa 2.30 asubuhi

Tayari mgombea urais wa Zanzibar kupitia ACT Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad, amewasili kisiwani Pemba hivi sasa tayari kwa mkutano wa kampeni za mgombea Urais Chadema ambao utahudhuriwa pia na viongozi mbalimbali wa ACT

========



Sheikh PONDA: Huu uchaguzi msingi wake ni kuhakikisha haki inapatikana lakini haki haipatikani kwa kuomba, haki inachukuliwa. Huu ndio mkakati katika uchaguzi huu. Mko tayari kuchukua haki zenu?

Mmesikiliza dua aliyoiomba baba Askofu, imezungumza lugha hii ninayoizungumza mimi, hii ndio lugha ya wakristo Tanzania, ndio lugha ya Waislamu Tanzania. Ndio lugha ya viongozi wa vyama vikubwa vya siasa Tanzania kwamba tunachukua haki yetu safari hii.

Tutahakikisha yule ambae aloshinda kwa kura za wananchi huyo ndie ambae anatangazwa.

JUSSA: Langu la kwanza, mara hii kama walidhamiria kuifisidi Pemba basi CCM itaangushwa Unguja. Waliengua wagombea
wakadhani watawavunja moyo wana-ACT wazalendo na wazanzibari lakini nikupeni habari za Kisiwandui?

Kisiwandui wanalizana vilio mtindo mmoja, uchaguzi huu hausimamiwi na ZEC na NEC kama tulivyozoea miaka ya nyuma. Mara hii kuthibitisha ukoloni wao wameletwa maafisa usalama kutoka Tanganyika kuja kusimamia uchaguzi wa Zanzibar.

Lakini ambalo hawakulikumbuka afisa usalama hawawezi kubadili msimamo wa wananchi wa Unguja na Pemba katika tunalolitaka.


=======

Pichani ni mgombea Urais Zanzibar kupitia chama cha ACT Wazalendo ndugu, Seif Sharif Hamad akimuombea kura mgombea Urais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania ndugu, Tundu A. Lissu leo 22 Oktoba 2020 katika Viwanja vya TIBIRINZI Pemba.

#ZanzibarYenyeMamlakaKamili

yajayo yanafurahisha
 
upinge muungano kivipi umetoa ajira maelfu kwa wazanzibari wizara ya mambo ya ndani na jeshini

Wazanzibari wapenda muungano ni wengi kuliko wasioupenda

Wazanzibar wasioupenda muungano ni viongozi wa kisiasa wa zanzibar wa upinzani ambao hutafuta tu kura wakishinda huwasikii tena wakiongelea muungano.Seif alikuwa makamu wa Raisi wa ZANZIBAR alipopata umakamu akaufyata kimya hakuongelea muungano tena

Pia kwa Tanzania bara wasiotaka muungano ni viongozi wa upinzani tu akina Lisu wakitafuta tu gia ya kura kwa wanasiasa wenzao wa Zanzibar .Mtanzania bara wa kawaida wala hana shida na muungano

Lisu na maalim seif muungano wao ni wa viongozi wa siasa sio wanachama asubiri tarehe 28 october aone atakavyonyolewa

Asikilize hii clip ndio atajua zanzibar atanyolewa asikilize kuanzia mwanzo hadi dakika ya tatu hivi

Hakuna mzanzibat anaependa muungano olá wanaopata manufaa yao tu.
 
Ndio ushangae Tanzania bara wengi wanataka muungano Zanzibar pia halafu utashangaa kuona upinzani wanaongelea kupinga muungano nawanagombea uraisi wa muungano fikiria mtu kama Lisu akili zimo kweli anagombea uraisi wa muungano Halafu anasema haitaki muungano kuna kura za wapenda muungano atazipata kweli
Tanzania bara wanataka muungano lakni visiwani hawautaki hat kuuona usitusemee.
 
Pemba huijui ni ngome ya vyama vinne kuna CCM Pemba ndiko alikozaliwa Raisi Mohamed Shein na ndiko alikozaliwa mama Siti Mwinyi mama yake mgombea uraisi wa sasa wa Zanzibar Hussain Mwinyi pili Pemba ni ngome ya chama cha CUF cha Lipumba tatu Pemba ni ngome ya chama cha ADC cha Hamad Rashid Mohammed kimeshatoa hadi waziri wa serikali ya Zanzibar Kule cha nne ni ACT Maalim Seif Pemba atashindwa mapema tu asubuhi
Wewe ndiyo huijui pemba.

Hatumtaki kibaraka WA tanganyika. Amba bibiye kibaraka atoka pemba. Cheeee. Hebu tu one she mkutano WA cuf uliofanyika pemba mwaka huu
 
Shein na mbarawa wote wapemba Maalim Seif ndie mwarabu wa kuja Pemba ngome ya CCM ya raisi aliyepita Abeid Amani Karume mama yake Mpemba ndio maana Seif kipindi cha Karume alibwagwa na cha Shein mpemba akabwagwa mara mbili na sasa ajiandae Pemba hana mtelemko wa ushindi kule Unguja ndio kabisa hapati kitu ni ngome kuu ya CCM na CUF tu ndio maana kutwa anakimbilia Pemba kama Lisu ambaye kutwa anakimbilia Singida akirudi mara mbilimbli kampeni
Huna adabu.
 
Leo CCM Nchi Nzima Masikio Ni Pemba Kujua Nini Kinakwenda Kuongelewa, Kesho Utasikia Pole Pole Anaongea Na Wana Habari Kupooza Joto
Sijui Mwinyi yupo kwenye hali gani anapoona haya mambo na uungwaji mkono mkubwa kama huu kwa Maalim Seif Hamad Sharif
 
Shein na mbarawa wote wapemba Maalim Seif ndie mwarabu wa kuja Pemba ngome ya CCM ya raisi aliyepita Abeid Amani Karume mama yake Mpemba ndio maana Seif kipindi cha Karume alibwagwa na cha Shein mpemba akabwagwa mara mbili na sasa ajiandae Pemba hana mtelemko wa ushindi kule Unguja ndio kabisa hapati kitu ni ngome kuu ya CCM na CUF tu ndio maana kutwa anakimbilia Pemba kama Lisu ambaye kutwa anakimbilia Singida akirudi mara mbilimbli kampeni
Ccm haijwahi kushinda uchaguzi Zanzibar tangu mwaka 1995.
 
CCM antena zote ni Pemba !! Kweli Lissu wewe ni game changer.....
Nimeonja onja kachumvi, nitakuambia kwa kuvutia wanapotoa mada yupo Mwalimu na Lissu. Yaani bundle inaliwa na unaomba jamaa aendelee. Mkoloni mweusi na vibaraka wao leo wamekaangwa ile mbaya. Thank you/Akhsante TAL may... GOD bless you.
 
Back
Top Bottom