Yaliyojiri tamasha la tisa la jinsia Dar....Mashoga, makahaba watetewa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Yaliyojiri tamasha la tisa la jinsia Dar....Mashoga, makahaba watetewa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Dr. Chapa Kiuno, Sep 26, 2009.

 1. Dr. Chapa Kiuno

  Dr. Chapa Kiuno JF-Expert Member

  #1
  Sep 26, 2009
  Joined: Sep 11, 2009
  Messages: 445
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Padri Privatus Karugendo  KATIKA makala yangu ya juma lililopita kuhusu Tamasha la tisa la Jinsia nilimaliza kwa kusema kwamba Changamoto kubwa anayoiona Profesa Tamale, ni jinsi ya kupambana na fikra zote duni zinazoendeleza fikra za kutawaliwa kifikra.
  Kukosoa vitu tulivyojifunza siyo rahisi; kwani inahitaji kuachana na fikra tulizozikumbatia hapo awali kwa muda mrefu, na kujenga upya uelewa wetu katika mambo yale yale tunayoyapinga. Kujifunza upya kunahitaji kuwa na mtazamo tofauti, na mara nyingi changamoto tunayokumbana nayo ni ya jinsi gani ya kuachana na tabia za kale tulizozoea.
  Profesa Tamale anafikiri kwamba safari hii ya kujifunza mambo mapya siyo tambarare. Mara nyingi inakumbwa na mitikisiko mikubwa; hususan itokanayo na misingi na mihimili tuliyokuwa tumejiwekea tangu mwanzo. Safari hii inamtoa mtu kutoka kile alichokiamini ni ukweli na kuanza safari nyingine ambayo ni vigumu kufahamu mwisho wake.
  Ni bora mtu kufahamu hivyo mapema, ili aweze kujiandalia safari hii ngumu ambayo ina hisia za hasira, kuumia, kutengwa na wakati mwingine kunyanyapaliwa.
  "Kukosoa na kujifunza upya kunatulazimu kuchambua kiyakinifu, na kuuliza maswali nyeti kuhusu yale tuliyoyaamini. Safari hii ni safari ya kukua inayokuwezesha kufungua milango, kuondoa mipaka na kutamani kufanyia kazi mabadiliko.
  "Kukosoa na kujifunza upya ni sehemu ya maisha. Inatuwezesha kuendeleza kujadili, kuuliza maswali na kukataa kumilikiwa kifikra na kimwili. Inahitaji kujitolea mhanga, lakini hii ndiyo njia pekee ya kuleta mabadiliko katika dunia ya leo," alisema Profesa huyo.
  Ili kueleweka vizuri, Profesa Tamale alitoa mfano wa makundi mawili ya wanawake yaliyowekwa pembezoni. Hawa ni wanawake mashoga na wale wanaohusika na biashara ya ngono. Alieleza ukweli ulio bayana kwamba wanawake wengi wanaofanya biashara ya ngono hufanya hivyo sio kwa kuchagua, bali ni kutokana na mahitaji ya kiuchumi.


  Profesa Sylvia Tamale


  Sheria zilizopo zinaweka taswira kwamba wanawake hawa hawana maadili mema, na adhabu zinalenga tu wale wanaouza; kwani wanaonunua ngono hawaadhibiwi. Kwanini jamii inaamua kumuadhibu tu yule anayeuza, na inamwacha mnunuzi?, alihoji Profesa Tamale.
  Pia alionyesha ukweli tunaoufahamu kwamba biashara ya ngono hapa Afrika inaandamana na ukatili dhidi ya wanawake, na hatimaye kuwaadhibu. Wanawake wengi hapa barani Afrika wanachagua kufanya kazi moja au nyingi zenye manyanyaso, na zisizolipa jasho lao.
  Kazi hizo zinaweza ziwe ni kazi za majumbani, hotelini au biashara ya ngono. Kwa mfano, wanawake wanaofanya kazi katika viwanda vya nguo wanafanya kazi takribani saa 14 hadi 18 kwa siku.
  Kwa bahati mbaya, mawaziri wetu wa fedha wanapotoa hotuba bungeni, hawataji kabisa michango ya kina mama itokanayo na kazi ya kuendeleza kizazi inayofanyika katika ngazi za kaya. Kazi hizi - iwe biashara ya ngono au kazi za majumbani, zinaongeza pato la taifa. Unapoadhibu kazi hizi inalazimu wafanya biashara ya ngono kufanya kazi hii kwa usiri na kuhatarisha zaidi maisha yao ambayo tayari yako hatarini.
  Mkutano wa kwanza wa wanawake wanaofanya biashara ya ngono kule Johannesburg, Afrika ya Kusini ulipitisha azimio kwamba kila mwanamke anayefanya biashara ya ngono ni mtetezi wa haki za binadamu.
  Mkutano huo uliwakusanya wanawake 153 wanaofanya biashara ya ngono. Walitoka nchi zaidi ya kumi za Afrika zikiwemo Afrika ya Kusini, Senegal, Zambia, Zimbabwe, Botswana, Malawi, Uganda, Kenya, Namibia na Nigeria.
  Mkutano huo uliunda umoja wa kuzishinikiza serikali za Kiafrika kuitambua biashara ya ngono kama chanzo cha kipato na kukomeshwa kwa manyanyayo na unyanyapaa dhidi ya biashara hiyo. Nchi ya Senegal, iliyohalalisha biashara ya ngono kwenye miaka ya sitini ni nchi inayongoza kwa kuwa na maambukizo madogo ya UKIMWI.
  Kuhusu mashoga, Profesa Tamale alieleza kwamba hakuna kundi linalonyanyapaliwa kama kundi la mashoga. Wanawake wanaovutiwa na wanawake wenzao wanaonekana kama wenda wazimu, na wanahitajiwa kutibiwa kwa kuwabaka au kuwanajisi.
  Kimantiki, kuna imani kwamba wanawake kama hawa wakifanya mapenzi na wanaume, basi tatizo lao linatatuliwa. Suala la ngono sahihi ni suala la tafsiri za jamii kuhusu jinsi na jinsia, na vile vile tafsiri hizi zimejikita kati mfumo dume.
  Pia kwamba tamaa za ngono zinajumuishwa tu na kazi ya kuzaa, na wala siyo vinginevyo. Hiki ndicho kinachohalalisha mahusiano ya ngono sahihi. Sheria zinapotumiwa kutafakari ngono sahihi, zinaendeleza mfumo dume katika tafsiri ya jinsi na ujinsia.
  Ujinsia wa mwanamke unahusishwa tu na kazi yao ya kuendeleza kizazi. Tamaduni zetu zinasisitiza tu ngono ya starehe kwa wanaume ambapo kwa mwanamke ngono inahusishwa tu na uzazi. Kunapotokea kundi kama la mashoga, basi linatingisha mhimili wa kwanza wa mfumo dume na mahusiano ya jinsia.
  Profesa Tamale alitoa mfano wa Uganda: " Mwaka huu, Mahakama Kuu ya Uganda ilitoa uamuzi wa kihistoria uliowatetea mashoga ambao walivamiwa na polisi, kupigwa na kunyang'anywa mali zao. Katika hali ambayo haikuwa ya kawaida, Jaji Stella Arach aliitia hatiani serikali kwa kukiuka haki za wahusika za kimsingi ikiwa ni pamoja na haki ya faragha na haki ya kutokuumizwa. Huu ulikuwa ushindi wa kwanza wa mashoga huko Uganda".
  Profesa Tamale alielezea pia juu ya mtandao wa mashoga wa Afrika ambao ni asasi isiyo ya kiserikali inayotetea haki za mashoga Afrika. Mtandao huo uliundwa mwaka 2003 na ni asasi ya kwanza katika ngazi ya kanda inayotetea kwa wazi haki za mashoga.
  Ilizinduliwa rasmi huko Namibia katika mkutano uliowakilishwa na wanachama kutoka Sierra Leone, Ghana, Nigeria, Rwanda, Kenya, Uganda, Tanzania, Zimbabwe, Botswana, Afrika ya Kusini, Msumbiji na Namibia.
  Hii inamaanisha kwamba kuna vuguvugu la vikundi vinavyotetea haki za ujinsia kwa kukosoa kile kinachojulikana kwamba ndio njia sahihi. Hata hivyo tutambue kwamba vuguvugu hili lina changamoto nyingi, ikiwa ni pamoja na kunyanyapaliwa.
  Juu ya suala la kutoa mimba, Profesa Tamale alifafanua vizuri juu ya Itifaki ya Maputo kwamba ibara ya 14 ya Itifaki ya Maputo kuhusu makubaliano ya Nchi za Kiarika kuhusu haki za binadamu na haki za wanawake, imeweka bayana haki za wanawake katika eneo la afya na uzazi.
  Kati ya mambo mengi, kifungu hicho kinatoa wito kwa wanachama wa nchi huru za Afrika kulinda haki za wanawake za uzazi. Kinaidhinisha haki za kutoa mimba itokanayo na kubakwa na vile vile pale ambapo mimba hiyo inahatarisha afya ya mwanamke au maisha ya kiumbe.
  Na kwamba hata kabla ya Itifaki ya Maputo, Tunisia, Cape Verde, Afrika ya Kusini na Zimbabwe zilishatoa haki za mwanamke za kutoa mimba katika mazingira yaliyotajwa katia Itifaki ya Maputo. Nchi nyingine zilizokwisha ruhusu jambo hili ni pamoja na Togo, Mali, Benin, Burkina Faso, Guinea na Chad.
  Ingawa, kwa kutumia busara tu, mwanamke yoyote hapaswi kulazimishwa kubeba mimba itokanayo na kubakwa, zipo nchi nyingi zinazoruhusu utoaji wa mimba zitokanazo na kubakwa. Kundi moja linalopinga vikali Itifaki ya Maputo linasema:
  "Itifaki ya Maputo ilitokana na msukumo wa chama cha International Planned Parenthood kinachoshinikiza serikali zetu ziruhusu kutumiwa kwa dawa za kuzia mamba. Jambo hili haliruhusu tu mauaji ya watoto, bali vilevile inaathiri afya za kina mama kisaikolojia. Itifaki hii inahalalisha utoaji mimba katika bara hili letu la Afrika. Hii ni njia ya kuhalalisha utoaji mamba katika bara hili la Afrika"
  Upinzani mkali unaojidhihirisha katika maneno haya ni ishara ya upinzani mkubwa wa mapinduzi ya kumkomboa mwanamke wa Kiafrika. Lakini mawazo haya hayazingatii ukweli kwamba kumekuweko na utoaji mimba kwa njia za siri, jambo lililoashiria kupoteza maisha ya wanawake wengi hapa barani Afrika.
  Kujenga mazingira yanayowalazimisha wanawake kuzaa au kubeba mimba na kutunza watoto bila ridhaa yao, ni kuendeleza fikra zinazohalalisha kwamba kazi kuu ya mwanamke ni ya kuendeleza kizazi, bila kujali rasilimali iliyowekezwa kwenye kazi hii, ikiwa ni pamoja na nguvu kazi inayohitajika katika kuendeleza kizazi.
  Changamoto kubwa ya hotuba ya Profesa Tamale, ni pale alipoelezea ujinsia ulivyotumika kama chombo cha kupinga unyanyasaji. Kwamba katika jamii nyingi za Kiafrika, ujinsia ulitumika kama ishara ya mwisho ya kupinga utawala wa mabavu. Matumizi ya ishara za jinsi, kwa mfano wanawake wakikaa uchi, kama njia ya mwisho ya kupinga mifumo kandamizi.
  Njia hizo ziliweza kuleta mabadiliko kwa wakati husika. Harakati za wanawake za mwaka 1929 Kusini mwa Nigeria, na harakati za Waingereza huko Cameroon ya mwaka 1958-59 (wakati wanawake walipokaa uchi kupinga utawala wa mabavu wa kikoloni), ni mifano michache tu.
  Katika mapambano hayo, wanawake hao walionyesha hisia zao kwa njia za matumizi ya nyimbo, dansi na kufanya ishara za kuashiria ngono:
  "Wanawake wenzangu tusisahau ni jinsi gani ujinsi wetu unavyotumika kama alama ya taifa. Mataifa yetu husema, mama, sheria mama, mama kanisa, hata pale ambapo wanawake wamewekwa pembezoni. Tutumie nafasi hii, kudai mataifa yetu kutuenzi; hususan kuenzi kazi tunazofanya kuendeleza kizazi.
  "Ni lazima tudai haki zetu kama wanawake wa Kiafrika ili tuweze kutambulika kama raia huru wa bara hili. Haki za kusikika, haki za kushiriki, haki za kushiriki, haki za elimu haki za kutobaguliwa, kutonyanyaswa, n.k. Haki hizi zote zinahusiana na ujinsia wetu.
  "Jamii sharti itambue, pamoja na tofauti zetu, za kidini, kitabaka, siasa, na ulemavu, sisi kama wanawake, tunayo haki ikiwa ni pamoja na haki ya ujinsia wetu. Tunadai usawa katika taasisi zetu, katika matabaka tuliyomo, na haki za ujinsia, ikiwa ni pamoja na wanawake wanaonyonyesha, mashoga, wafanyakazi, wenye kuishi na virusi vya UKIMWI, wenye kufanya biashara ya ngono, nk", alisema Profesa Tamale.
  Profesa Tamale alimaliza hotuba yake kwa kusisitiza kwamba ujinsia ni nguvu. Na kwamba nguvu hii ni raslimali ambayo wanawake wa Kiafrika sharti waitambue, waidai na kuitumia ili kuleta ukombozi wa wanawake wa kimapinduzi.
   
 2. M

  Magezi JF-Expert Member

  #2
  Sep 26, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  rekebisha bandiko lako linachosha kusoma, weka paragraphs.
   
 3. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #3
  Sep 26, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  Inawezekana kuchosha kusoma ila kilichoandikwa hapo kinahitaji uzito wa pekee kujadiliwa. Haya mambo ya usenge na usagaji na haki sawa kupitiliza yakiachiwa, tz itaangukia pua. Kinachosikitisha ni wasomi wanasapot hii dhoruba kwa kisingizio eti 'sasa tufanyeje'. SHAME ON THEM! Kupata xposure isiwe kigezo cha kuridhia hizi kadhia za magharibi. Kumkubali ****** au msagaji ni kumpa kichwa kuwa anachofanya ni sawa. Tena MODS msijaribu kumodify chochote. Anayepigia chepuo ufirauni ni mpumbavu. Upumbavu sio tusi. Where we dare to talk openly
   
Loading...