Uchaguzi 2020 Yaliyojiri Tabora: Tundu Lissu (CHADEMA), azindua Kampeni Kanda ya Magharibi katika viwanja vya Chipukizi

Wakati JPM Yuko Nzega Lissu alikuwa shinyanga, alipitia wapi misafara haijakutana? Wakati hamna njia mbadala?
 
Kwa Mujibu wa ratiba ya kampeni iliyotolewa na Chadema inaonyesha kwamba Mh Tundu Lissu leo atakuwa Tabora

=====

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia
CHADEMA TUNDU LISSU leo Septemba 3, 2020, atazindua kampeni kwa Kanda ya Magharibi, uzinduzi ambao utafanyika katika viwanja vya Chipukizi mkoani Tabora.
View attachment 1557624
View attachment 1557627
Msafara wa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chadema, Mhe. Tundu Lissu, aliyeambatana na Mgombea wa Kiti cha Makamu wa Rais, Mhe. Salum Mwalim Juma Mwalim, ukiingia na kupokelewa katika Uwanja wa Chipukizi, mjini Tabora baada ya kufika mkoani humo akitokea Mkoa wa Shinyanga.
View attachment 1557623
View attachment 1557631
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chadema, Mhe. Tundu Lissu akiwasalimia maelfu ya wananchi wa Mkoa wa Tabora waliofika kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni za mgombea huyo kwa Kanda ya Magharibi (Kigoma, Tabora na Katavi) uliofanyika katika Uwanja wa Chipukizi, mjini Tabora leo Alhamis, Septemba 3, 2020.
View attachment 1557625View attachment 1557626View attachment 1557628View attachment 1557630
Umati wa maelfu ya wananchi wakimsikiliza Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chadema, Mhe. Tundu Lissu, kwenye Mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni za Chadema, Kanda ya Magharibi (Tabora, Kigoma na Katavi) uliofanyika leo Alhamis, Septemba 3, 2020, katika Uwanja wa Chipukizi, mjini Tabora.

Nilikuwepo kwenye mkutano huu....

Huyu jamaa siyo wa kawaida.....

Watu kwa hiari yao walijazana kwenye uwanja huu wa wazi na kumsikiliza kwa makini mgombea...

Hoja na sera zake anazifafanua ktk lugha rahisi kueleweka...

Watu walikuwa wanafurahia kila dakika...

Alitumia dakika kama 58 hivi kuhutubia...

Lakini watu walikuwa na hamu ya kuendelea kumsikiliza zaidi na zaidi...

Hoja ya ujenzi wa uwanja wa ndege kimataifa Chato itamtesa sana Magufuli na watetezi wake...

Kwa hakika kabisa Chato International Airport ni 100% pure example ya ufisadi wa Magufuli...!!
 
Mradi wa maji toka ziwa victoria umeshammaliza. Ccm wanazoa kura zote Tabora. Maana huu mradi umewapa credit kubwa sana ya kisiasa Ccm. Akina mama wa kinyamwezi hawawezi kumsikiliza mtu anaesema kuletewa maji tabora ni maendeleo ya vitu.
Amepeleka maji kwa kodi zetu wananchi, si kwa pesa zake wala za ccm. Ni wajibu wa serikali kutumia kodi inayokusanya kupeleka huduma kwa walipakodi. Si jambo la kupongezwa wala kusifiwa. Hata farao alikusanya kodi na kutoa huduma kwa raia wake, lakini hakuwa kiongozi mzuri.
 
Na atabaki madarakani kwa nguvu ya kodi yenu
 
Amepeleka maji kwa kodi zetu wananchi, si kwa pesa zake wala za ccm. Ni wajibu wa serikali kutumia kodi inayokusanya kupeleka huduma kwa walipakodi. Si jambo la kupongezwa wala kusifiwa. Hata farao alikusanya kodi na kutoa huduma kwa raia wake, lakini hakuwa kiongozi mzuri.
Pumbavu huna akili. Je kama angezitafuna maana hakuna wa kumzuia.
 
Polisi nasikia walimpitishia barabara za ukimyaaa, ili watu wasione kama Lissu kaingia. Ila imeshindikana kuzuia. Watu waliposikia tu wakajumuika kumsikiliza mkombozi wao.

Lissu hazuiliki jamani ‍♀️. Muwe wapole tu. Chaguo la wananchi huyo.
 
Nilikuwepo kwenye mkutano huu....

Huyu jamaa siyo wa kawaida.....

Watu kwa hiari yao walijazana kwenye uwanja huu wa wazi na kumsikiliza kwa makini mgombea...

Hoja na sera zake anazifafanua ktk lugha rahisi kueleweka...

Watu walikuwa wanafurahia kila dakika...

Alitumia dakika kama 58 hivi kuhutubia...

Lakini watu walikuwa na hamu ya kuendelea kumsikiliza zaidi na zaidi...

Hoja ya ujenzi wa uwanja wa ndege kimataifa Chato itamtesa sana Magufuli na watetezi wake...

Kwa hakika kabisa Chato International Airport ni 100% pure example ya ufisadi wa Magufuli...!!

You nailed it Mkuu. Kila herufi yako imejaa ukweli mtupu.
 
Mke wa Lissu sasa ananifurahisha sana. Hivyo hivyo anavyoongea ndio inatakiwa.
 
Dodoma watu walikuwa wengi Sana
Acha kutumikaView attachment 1558534
IMG_20200904_190825.jpg

Sent from my CPH1803 using JamiiForums mobile app
 
Mradi wa maji toka ziwa victoria umeshammaliza. Ccm wanazoa kura zote Tabora. Maana huu mradi umewapa credit kubwa sana ya kisiasa Ccm. Akina mama wa kinyamwezi hawawezi kumsikiliza mtu anaesema kuletewa maji tabora ni maendeleo ya vitu.
Maji ya ziwa Victoria ni kaa la moto. Bei yake ni kubwa. Kwa sasa mambo ya bei yamefunikwa ili uchaguzi upite. January inakuja.
 
pouplation au kwa kanda? sasa mbona unabwabwaja uongo kuwa mnazindua kwa kanda? Lakini turudi nyuma kama kweli mnazindua kwa population mbona mlipata watu wachache mbagala,kawe na segerea Dar es salaam kuliko Arusha au Mwanza? hiyo logic ya population mbona haieleweki?
Utaielewa tu October 28
 
Back
Top Bottom