Yaliyojiri siku ya mauaji ya Karume

Uzi mtamu huu sijui kwanini sikuuona tangu ulivyoanza mwaka jana.
Mimi nilisoma habari za kifo na nadharia zake nikiwa bwana mdogo sana.
Mengi ni kama nimesahau na sikujishughulisha tena kuyajua.

Ila n'nakumbuka wakati fulani kuna mzanzibar aliwahi kusema kuna wakati kaburi la marehemu Karume lilikua likifuka moshi. Na baada ya dua nyingi mfululizo likaacha na ikawa ndi sababu ya kulizungushia ukuta. Je, ni ya kweli haya au hadithi za gahawa?

Cc: Pohamba, FaizaFoxy, Mohammed Said
 
Ni takribani miaka 44 sasa tokea kuuawa kwa aliyekuwa rais wa kwanza wa Zanzibar marehemu sheikh Abeid Karume.

Tukio hilo lililotokea katika ofisi za makao makuu ya A.S.P huko kisiwa Ndui mjini Zanzibar.

Katika makala haya tutajadili yaliyotokea siku hiyo na haswa tutaangalia yaliyomsibu aliyekuwa mkuu wa operesheni na mafunzo wa JWTZ kanali Ali Mahfoudh.

Ilikuwa mida ya jioni ambapo kikosi cha askari wasiozidi nane wakiongozwa na kapteni Ahmada pamoja luteni Humud walipovamia ofisi za makao makuu ya A.S.P na kumshambulia hayati sheikh Abeid Karume kwa risasi na hatimaye kusababisha kifo chake. Mmoja kati ya wauaji hao Luteni Humud aliuawa na walinzi wa Karume huku wenzake wakifanikiwa kutoroka.

Muda mchache baada ya tukio hilo kutokea aliyekuwa mkuu wa operesheni na mafunzo wa JWTZ kanali Ali Mahfoudh alifika eneo hilo akiwa ameambatana na askari mwenzake na mara moja wakaichukua miili ya Sheikh Karume pamoja na Humud na wakaipeleka hospitali kuu ya mnazi mmoja kwa uchunguzi zaidi.

Kwa mujibu wa Dr Harith Ghassan katika kitabu chake cha Kwa heri ukoloni kwa heri Uhuru ameeleza kuwa haraka sana taarifa zilifika kwa aliyekuwa mkuu wa maswala ya usalama Zanzibar kanali Seif Bakari na mara moja akatangaza hali ya hatari na kutoa amri kwa askari wote kukusanyika katika kambi ya migombani.

Harith Ghassan ameeleza kuwa kanali Seif Bakari pamoja na kanali Ali Mahfoudh waliweka askari wote kuwa tayari kwa mapambano.

Kanali Seif Bakari alipeleka kikosi cha askari kuwasaka kina kapteni Ahmada na wenzake na aliamuru kuwa endapo watawakamata wawalete mara moja ili wahojiwe. Katika hali ya kushangaza kanali Ali Mahfoudh alipinga swala hilo na aliwaamuru askari pindi watakapowakamata kina kapteni Ahmada wawaue mara moja na wasiwalete kuwahoji.
Muda mchache baadae askari hao kwa kutumia redio maalum za kijeshi waliripoti kuwa tayari wameshawakamata kina kapteni Ahmada na walikuwa tayari kuwaleta wahojiwe.

Kanali Ali Mahfoudh alipinga swala hilo na akawaamuru wawaue mara moja na wasiwalete kuwahoji hivyo askari wale wakatii amri hiyo na wakawaua kapteni Ahmada na wenzake.

Pia msako uliendelea kwa washukiwa wengine ambapo walikamatwa mmoja baada ya mwingine.

Mji wa Zanzibar ulitaharuki kwa tukio hilo na mara moja watu walianza kukimbia sehemu za mjini na kukimbilia sehemu za mashambani kwa hofu ya vita.

Kitendo cha kanali Ali Mahfoudh kutoa amri ya kuuawa kwa kapteni Ahmada na wenzake badala ya kuwaleta wahojiwe kiliwashangaza sana askari wenzake na viongozi wengine waliokuwepo eneo hilo na isitoshe taarifa za kiintelijensia zilionesha kanali Ali Mahfoudh alikuwa anahusika katika mpango huo wa mauaji ya sheikh Abeid Karume lakini hakuna aliyethubutu kumkamata kwani kwa kipindi hicho kanali Ali Mahfoudh alikuwa ni komandoo aliyekuwa akisifika kwa uhodari wake aliokuwa anaouonesha katika vita vya kuikomboa nchi ya Msumbiji na hivyo askari wenzake walikuwa wakimuogopa sana.

Muda mchache baadae aliyekuwa mkuu wa maswala ya usalama Zanzibar kanali Seif Bakari aliwasiliana na viongozi waliokuwa Dar es salaam na akawaelezea hali halisi ilivyokuwa na ikatolewa amri kutoka Dar es salaam kuwa kanali Ali Mahfoudh pamoja na kanali Seif Bakari waende mara moja Dar es salaam kuhudhuria kikao maalum cha ulinzi lengo ikiwa ni kumkamata kanali Ali Mahfoudh.

Aliyekuwa mnadimu mkuu wa JWTZ mwaka 1972 kanali kashmiri anaikumbuka vyema sana siku hiyo na anaeleza kama ifuatavyo;
Siku hiyo mimi na mkuu wa majeshi General Sarakikya tulikuwa tupo ofisini ghafla tukapata taarifa za kilichotokea Zanzibar.
Ndipo ghafla tukapokea simu kuwa mkuu wa majeshi anahitajika kwa waziri mkuu kwa kikao maalum na hivyo akaondoka na kuniacha mimi peke yangu.

Nikiwa nipo ofisini huku nikitafakari yaliyotokea Zanzibar nikapokea simu iliyopigwa na mkuu wa majeshi Jenerali Sarakikya akaniambia kuwa kanali Mahfoudh yupo ndani ya makao makuu ya jeshi amefika muda huu na hivyo nifanye mpango wa kumkamata mara moja kwani alikuwa ni mmoja wa washukiwa na wao wamemuelekeza aje hapo ili mimkamate.
Nikaanza kujiuliza nitamkamata kwa njia gani ndipo nikaona niite askari ofisini kisha nijifanye kama kuna kikao ili akiingia ndani wale askari wamkamate. Nikaita askari kisha nikawapanga kwenye viti kana kwamba kuna mkutano na nikawapa amri kuwa atakapoingia kanali Ali Mahfoudh pamoja na kanali Seif Bakari fanyeni haraka mumkamate kanali Ali Mahfoudh.

Wakati naendelea kuwapa maelekezo askari wale ndipo kanali Mahfoudh na kanali Seif Bakari wakawa washafika nje ya ofisi. Nakumbuka kabisa kanali Seif Bakari alikuwa amevaa sare za kijeshi bila ya silaha zozote lakini kanali Mahfoudh alikuwa amevaa sare za kijeshi na bunduki mbili kiunoni na visu viwili ameviweka ubavuni. Kanali Mahfoudh akachungulia akanisalimia " Kashimiri habari". Nikamwambia "salama kabisa njooni tulikuwa tunawasubiria nyinyi tuanze kikao".
Ndipo yeye na kanali Seif Bakari wakaingia ndani kwenye kikao.

Nilikuwa nimeshatayarisha viti vyao watakavyokaa na nilikuwa nimeweka kanali Mahfoudh akae pale katikati ya wanajeshi ili iwe rahisi kumkamata.
Walipoingia wakakaa katika viti vile vile nilivyopanga wakae kisha wakaanza kunieleza kuwa hakuna yaliyotokea Zanzibar na wakaniambia kuwa hakuna haja ya kupeleka askari wengine kwani wao wenyewe tayari wamesha tuliza hali ya vurugu na utulivu ulikuwa umesharejea Zanzibar na kama itawezekana wapelekwe askari wachache ili kusaidiana na wale wa Zanzibar kutuliza amani.

Unajua wao waliambiwa waje kwenye kikao na wakadhania kuwa kikao chenyewe ndio hichi kumbe hapakuwa na kikao wala nini. Ilikuwa Ni mpango wangu wa kumkamata kanali Mahfoudh.
Muda wote wakati kikao hicho kinaendelea nilikuwa nawapa ishara kwa siri wale askari kuwa wamkamate lakini cha ajabu hakuna hata mmoja aliyethubutu kumsogelea.
Wakati huo kila Mara mkuu wa majeshi General Sarakikya alikuwa anapiga simu pale ananiuliza kama tayari nishamkamata nikawa sasa namjibu kimkato mkato ili kanali Mahfoudh asinishtukie wakati huo nakazana kuwapa ishara kwa siri askari wamakamte lakini kwa muda wa nusu saa hakuna aliyemsogelea kanali Mahfoudh.

Mwisho sasa kanali Seif Bakari akaniambia mkuu "sie sasa tunaondoka zetu bwana" nikawaambia sawa mie ngoja nibaki hapa ofisini kidogo.
Kina kanali Mahfoudh na kanali Seif Bakari walivyoondoka nikawaambia wale askari " nyie kwa nini hamjamkamata". Mmoja wao akaniambia "mkuu una arrest warranty ya kumkamata" nikamjibu nikamwambia "nyie vp kwani jeshini napo pana arrest warranty embu nendeni mkamlete hapa" nikawa mkali sana nawafokea wale askari nawaambia "hii Ni amri ya serikali na maoni yangu binafsi embu nendeni bwana".

Niliona dhahiri walikuwa wanamuogopa. Unajua kanali Mahfouz alikuwa ni pande la mtu tena komandoo aliyefuzu Cuba. Na kwa kipindi kile alikuwa akisifika sana kwa uhodari wake wa kivita aliokuwa akiuonesha katika vita vya kuikomboa nchi ya Msumbiji na kumbuka pia kuwa alikuwa na silaha pale. Mie nikazidi kuwa mkali nikiwafokea huku nikiwaona dhahiri wakionesha wasi wasi wao.
Ghafla askari mmoja akaniambia "mkuu mie ninaenda kumkamata" kwa bahati walikuwa bado wapo ofisini kwa kamisaa wa siasa jeshini. Alipofika akamwambia kanali Mahfouz " Kanali jamhuri ya muungano wa Tanzania imeamuru ukamatwe tafadhali fuatana nami mpaka kwa kanali Kashimiri ukajisalishe".
Katika hali ya kushangaza sana kanali Mahfouz akawa mnyonge sana na wala hakuleta pingamizi.
Akaja nae mpaka ofisini pale kwa mkuu wa majeshi nikamwambia kanali Mahfouz asalishe silaha zake zote kisha akakabidhi kwa wale askari kisha nikawaambia askari wote watoke nje watuache peke yetu. Hivyo tukabaki pale ofisini wawili peke yetu. Nikamuuliza una maagizo yoyote unayotaka kunipa ili niyafikishe kwa familia yako akanijibu ndio. Akaniomba nimpe karatasi aandike barua, kiuhalisia kwa kesi nzito kama ile nilikuwa na matumaini madogo sana kama atatoka salama na kwa kweli sikutaka maisha ya askari mwenzangu yapotee hivi hivi bila ya kutoa maagizo kwa familia yake. Kanali Mahfouz akaandika barua ndefu kwa mke wake na nikamuahidi kuwa itamfikia mke wake bila shaka yoyote.

Muda mchache baadae akaja kuchukuliwa na mkurugenzi wa makosa ya jinai kipindi hicho CID Sawaya.

Muda mchache baadae mkuu wa majeshi general Sarakikya akanipigia kuniuliza kama nimeshamkamata kanali Mahfouz nikamjibu tayari kanali Mahfouz yupo mikononi mwa serikali.
Ndivyo ilivyokuwa bwana kumkamata yule jamaa ilikuwa shughuli pevu kweli kweli.

Nilikuja kugundua baadae kuwa hata yeye mwenyewe aliona ni salama kukamatiwa huku Dar es salaam kuliko Zanzibar ndio maana hakufanya fujo wala kuleta pingamizi.

Kanali Mahfouz na wenzake walihukumiwa adhabu ya kifo lakini kutokana na shinikizo kutoka kwa mashirika ya kutetea haki za binadamu washukiwa wote waliachiwa huru mwaka 1978 na kanali Mahfouz alipewa sharti la kutokukaa wala kukanyaga tena nchini Tanzania.
Ndio akachukuliwa na Aliyekuwa Rais wa Msumbiji hayati Samora Macheli na huko akafanywa kuwa mshauri mkuu wa maswala ya usalama.

Kanali Mahfouz na kanali Kashimiri walikutana tena mjini Maputo miaka ya baadae na yeye mwenyewe kanali Kashimiri anasimulia kuwa walivyokutana kanali Mahfouz alimpokea na kumchangamkia vizuri kabisa na akamwambia kuwa wala hana kinyongo na yeye ingawa baadhi ya watu walikuwa wanamwambia kuwa eti mbaya wake ni kanali Kashimiri.
Kanali Mahfouz aliniambia " Kashimiri unajua kabisa kuwa pale ulikuwa unatekeleza amri ya serikali na sheria kuu ya uaskari ni kutii amri unayopewa hata ningekuwa Mimi ningefanya hivyo hivyo kama ulivyofanya wewe na si vinginevyo".
Kanali Mahfouz na kanali Kashimiri waliendelea na urafiki wao hadi kanali Mahfouz alipofariki dunia.

Mwaka 1978 wakati nduli Idi Amin alipoivamia Tanzania alipeleka ombi maalum kwa serikali ya Msumbiji ili akaitetee nchi yake. Alisema nchi yangu imevamiwa na Amin anaua ndugu zangu nipeni ruksa nikaitetee nchi yangu.
Lakini ombi lake halikukubaliwa kwani ilionekana itakuwa hatari sana kwake endapo angeenda vita ya kagera kwa sababu bado kuna waliokuwa na machungu na kifo cha Karume na wangeweza kumdhuru vitani. Hivyo kanali Mahfouz hakupigana vita ya kagera

Kanali Mahfouz alifariki dunia nchini Msumbiji na amezikwa katika makaburi ya mashujaa wa nchi iyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
nzuri sana hii
 
Col Ali Mahfudh akivishwa nishani na Mwalimu JK Nyerere
1581541525570.jpeg
 
Kifo cha Karume kilisababishwa na Seif Bakari na Khamis Hemed Nyuni hawa ndio waliokuwa na dhamana ya kikosi maalum cha kumlinda Rais Karume. Tayari aseif Bakari ameshapata taarifa ya kutibiwa kwa silaha na hakuchukuwa hatua ya kulinda Karume angalau mpka zitakapo kamatwa silaha zilizoibiwa. Hakuchukuwa hatua yoyote kwa tamaa ya yeye kukamata nafasi ya Karume. Ndio maana Ali Mahfudh statement yake haikuweza kusomwa Mahkamani. Ameeleza yote wazi wazi tokeo hili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na sio kweli kwamba yeye kaamrisha askari wawauwe wa husika. Hali ilikua hivi: Baada ya taarifa ya kuuwawa kwa Mzee Karume na wauwaji kuikimbia mashamba. Baraza la Mapinduzi walikutana ili kufanya nashauri ya kuwakamata wa husika. Ukweli wengi wa viongizi hao waliziduwa na matumbo kuwa makubwa na khofu imewajaa. Waliogopa wao kwenda na wakamuagiza Ali Mahfudh aende kuwakamata na wakamtaka awalete wakiwa hai ndipo hapo Ali Mahfudh akawakatalia kwa vile wale wauwaji walikuwa na silaha na wakotayari kumuuwa mtu yeyote. Ndipo hapo Ali Mahfudh akadai kwamba kama wameamua kumpelekea yeye basi iwe kufa kupona adha wakamatwe wakiwa hai au waletwe wakiwa maiti. Ndipo akapewa barua ya kwenda kuwakamata wakiwa hao au maiti.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nalaila Jidawi alikuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia CUF ile yenyewe ya 1995-2000 bahati mbaya Sana akatamani cheo Cha Seif Sharif Hamad Cha ugombea Urais wa kudumu wa CUF Znz, akapigwa Fitna akafukuzwa CUF

Akahamia NCCR Mageuzi Na kutangaza kugombea Urais wa Znz kupitia Chama hicho Mwaka 2000

Baada tu ya kuchukua form kupitia NCCR Mageuzi Hotel zake Za kitalii Visiwani Znz zikaanza kuchomwa Moja Baada ya nyingine mpaka Familia yake ikamshinikiza aachane Na Siasa Na Hotel zikapumzika kuchomwa
Duh, siasa hizi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Historia ina tabia fulani hivi ya kujirudia rudia, sasa ipo siku sehemu ya hayo matukio yatajirudia tena.

Bahati mbaya sana historia rasmi ya matukio ya siasa za Zanzibar kuanzia mapinduzi mpaka leo hii imechakachuliwa mnoo. Sijui kwanini historia ya siasa Zanzibar haiwagi wazi na kunyooka?

Mpaka leo bado tunajiuliza kwanini Karume aliuwawa na nani walikuwa nyuma ya hilo tukio, jibu ni tata. Lakini ukichunguza kwa karibu na kuunganisha mambo basi utagundua kisa ni Muungano na mzee Mchonga ndio mhusika mkuu, wengine wote ni watekelezaji tu.
 
Hapa kutakuwa kuna kitu mkuu. Ndio maana Wazanzibar hawataki kabisa hii maneno ya Rais kutoka Chamwino Dodoma.

Naanza kuelewa kwanini wanamtaka sana Maalim Seif. Lakini nasikia Deep State ilishasema Maalim hatokuwa na hatakiwi kuwa Rais za SMZ.
Watu hawajui. Seif yuko upande wa sultan wa Zanzibar aiyepinduliwa. Ambaye mpaka sasa yuko hai anaishi Uingereza. Na kule anahesgimika.kama sultani wa zanzibar. Ukimpa seif tu. Sulta anarudi.
Ndio maana pia piga ua tanzania haikubali uraia pacha kwa sababu ikiukubali nasi sultan atakuwa raia pacha wa Tanzania mwenye haki ya kurudi Tanzania.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aliwekwa ndani kwa Kuwa waliomtuma kumsaliti Aboud Jumbe walimuahidi akitoka Jumbe atapewa Yeye Urais Lakin akapewa Mwinyi then Idrissa Abdul wakeel sasa akapanik Na kuanza kusambaza sumu Pemba kuhusu Rais Wakeel
Sio kweli. Yeye nanpinga mapinduzi. Ndio kinachomponza. Mkimoa anarudisha uhuru wa 1963. Na kumrudisha sultan

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu hawajui. Seif yuko upande wa sultan wa Zanzibar aiyepinduliwa. Ambaye mpaka sasa yuko hai anaishi Uingereza. Na kule anahesgimika.kama sultani wa zanzibar. Ukimpa seif tu. Sulta anarudi.
Ndio maana pia piga ua tanzania haikubali uraia pacha kwa sababu ikiukubali nasi sultan atakuwa raia pacha wa Tanzania mwenye haki ya kurudi Tanzania.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hizo unazowaza ni akili za kitoto sana.
Zama za usultani na Ukoloni wa uingereza kwa Zanzibar zilikoma mwanzoni mwa miaka ya 1960.

Ni hadithi za kutunga kusema au kuwaza kuwa Sultani ana mpango tena wa kurejea Zanzibar. Kufanya nini?
Ana uwezo kiasi gani?
Ana ushawishi kwa nani?
Hivi unajua umri wake kwa sasa utakuwa miaka mingapi ikiwa kama bado yuko hai?
Sultani alikuwa na athari gani kwa Tanganyika mpaka watanganyika wawe wanamuwaza na kumuota kuliko wazanzibar wenyewe ambao walitawaliwa naye kwa mateso kwa miaka zaidi ya 100?

Kilichotokea wakati wa Mapinduzi, baada ya mapinduzi, ujio wa Muungano, kuuwawa kwa Karume na chaguzi zote zilizofanyika wakati wa mfumo wa vyama vingi bado zipo vichwani mwa wazanzibar karibu wote mpaka leo, na hizo hisia huwezi kuzifuta daima.

Wazanzibar wengi wanajitambua kisiasa na wanajua nani anayefaa kuwaongoza, kama wanaona Seif anawafaa, tuwaache waamue wenyewe.

Historia ina tabia fulani hivi ya kujirudia, huenda ipo siku mapinduzi yatajirudia tena Zanzibar maana watawala wa sasa wanayaimba, kuyapenda na kuyaabudu sana.

Muda ni mwalimu mzuri sana.
 
Col. Mahfudhi ni nani? Kwanini alizikwa Mozambique na sio Tanzania?
Ni Nani mahfouz hili halijawekwa wazi ila sisi wanafasihi twishajua ni nani huyu!
Ili kumuepusha na madhara ya alichofanya ili bidi akina JK wa mwanzo azuge kumfunga kwa miaka takribani mi5.. na kwa usalama zaidi coz alikuwa mwamba was Vita ikabidi Jk amtafutie usalama huko ugenini nsumbiji.. Alifia huko

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni Rahisi Raila Odinga Au Makongoro Mahanga Kuwa Rais wa Znz Kuliko Seif kupata Urais wa Znz

Seif analipia gharama Za kumsaliti Jumbe

Akipata Urais itakuwa funzo baya kwa Wazanzibari kwa Kuwa itaaminika Usaliti unalipa

Lazima akose Na akoseshwe Urais Kama Funzo kwa Vizazi vijavyo vya Wazanzibari
Mkuu pohamba!unaonaje membe atachomoza ndani ya chama???Huyu mama samia nae kule zanzibar watamkubali???
 
Nilikuwa natafuta Picha ya huyu Mwamba.
Duu kweli ni Pande la Mtu.

Pichani ni Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akimvisha medali ya Ushujaa wa Vita vya Ukombozi wa Nchi za Afrika Mwanajeshi Mkakamavu, Komandoo aliyeogopwa na Maadui wa Tanzania na Afrika na Mpiganaji Shupavu aliyejitolea kupigania Ukombozi, Kanali Ali mahfoudh, Picha hii ilipigwa mwaka 1969.
 

Attachments

  • 318958_475211132523925_68544832_n.jpg
    318958_475211132523925_68544832_n.jpg
    10.8 KB · Views: 5
Back
Top Bottom