Kwa namna yoyote, uchaguzi uliofanyika jana ni kilele cha kiburi cha hali ya juu cha watawala kuonyesha dharau mbele ya wananchi.

Watawala kwa kutumia TISS, NEC, Polisi, Jeshi wamefanya kila aina ya uhuni dhidi ya wananchi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Wamepiga risasi na kuua watu Zanzibar, Wameondoa mawakala wa upinzani kwenye vituo vya kupigia kura, kabla ya hapo tangu kipindi cha kampeni wamevamia wagombea wa vyama vya upinzani na kuharibu mali zao na kuwaharass kwa kila namna, Wameingiza kura feki kibao katika sehemu mbalimbali za nchi.

Sasa ndugu zangu, kuna uchaguzi hapo?

Mimi nivipongeza vyama vya upinzani, Vimetimiza wajibu wao wa kuwa sauti mbadala katika nchi kwa tabu, mauivu na machungu mengi.

Kushiriki kwenu kwa tabu nyingi, kumesaidia kutuonyesha na kuuonyesha uimwengu aina ya utawala wa kidhalimu tulio nao

Nawaonea huruma Polisi wetu, Uslama wa Taifa na hata Wanajeshi wanadhani kwa kuwalinda watawala na udhalimu wao basi wao maisha yao yatakuwa bora. Masikini laiti wangalijua, Wanalinda mfumo wa kidhalimu utakaowaumiza hata wao wakiwa waevua hayo magwanda na bunduki zao zibazowafanya wajihisi wako juu mbinguni.

Ndugu zangu, CCM kamwe haitong'oja kwa vikaratasi hivi viitwavyo kura katika set up tuliyonayo hivi sasa. The Next step ya action ya vyama vya upinzani, mwananchi mmojammoja, taasis binafsi, lazima wajue kuwa CCM ilishakataliwa na wananchi atleast kuanzia mwaka 2010, Kilichofanyika kuanzia hapo ni uhuni, ghiliba, ulaghai, uonevu, hongo. Kwa hiyo uchaguzi huu uwe ni Jaribio la kuhitimisha(conclusive test) kuwa kamwe KATIKA MFUMO HUU TULIONAO, CCM KAMWE HAWATOKUBALI KUONDOKA KWA KURA. Wapanga strategy kwa ajili ya Tanzania mpya lazima mlitilie maanani hili jambo!

Kwa hiyo ndugu zangu Watanzania, puuzeni huu ujinga wanaosema ni uchaguzi umefanyika jana, Ule siyo uchaguzi ni uhuni mtupu!
 
Kutokana na hali inayokwenda kwa sasa kuhusu huu uchaguzi Bunge letu limetekwa na ccm na wataligeuza kuwa ni vikaoo vya chama.

Nna uhakika hakuna kuwa na hata Mbunge wa upinzani hata mmoja bunge. Nchi imelazimishwa kurudishwa kwenye utawala wa chama kimoja.

Kila mtu anajua uchaguzi ulikuwa na mapungufu, wizi wakura kila kona ya nchi.

Nakutakieni Vikao vyema vya chama, katika Mkutano mkuu wa Bunge la chama cha ccm lijalo kama watanzania wakikubali ujinga huu.
 
Hakika kama ni wakati wa kufurahi kwa shangwe kuu ilikuwa ni wakati huu. Kuweza kuzisambaratisha ngome kubwa za upinzani hasa Hai, Arusha, Mbeya mjini, Tarime, Bunda, Kawe nk sio mchezo hata kidogo!

Lakini ajabu ni kuwa pamoja na huo "ushindi" mbona wanaccm wamenyong'onyea na kujiinamia kwa aibu? Kitu gani kinasababisha hayo? Jee wamejigundua kuwa heshima ya chama kikongwe imepotea kutokana na WIZI na UBABAISHAJI?
 
Wengi wataona kwamba CCM pekee ndio wenye furaha kwa wakati huu baada ya majimbo yote kupora wao na pia vyombo vya dola kumrudisha tena mgombe wa Ccm ikulu kwa style ya kimabavu, lakini hakuna chochote utakachofanya duniani bila ya gharama, lazima utalipa gharama kutegemea na Ukubwa wa jambo ulilofanya.

Ukiangalia kwa undani kutokana na chaguzi hizi utagundua kuwa Upinzani umefanya kazi kubwa katika kuionyesha dunia mauchafu yanayofanywa na vyombo vya dola kuanzia mauaji, kujeruhi, wizi, udhalilishaji na hata umafia wa kiwango chajuu sana, na hata kufikia kufunga kabisa njia za mawasiliano. Kwangu mimi huu ni ushindi mkubwa sana kwa upinzani.

Kwa vile kutakuwa hakuna upinzani tena Bungeni sasa, hii itasaidia sana kuondoa visingizio kwamba ‘hakuna maendeleo hapa maana mmechagua upinzani’. Uchaguzi huu umetoa picha pana kabisa kwa watanzania (hata wale wa vijijini) kuelewa hali halisi ya nchi yetu na mustakabali wa vyombo vyetu vya dola. Watanzania wote kwa pamoja tujiandae sasa kulipa gharama za kilichofanywa na vyombo vyetu vya dola na washirika wao.

Upinzani umeshinda kwa kishindo kikuu.
 
Matokeo yameendelea kutangazwa na kila kunapotangazwa ushindi unakwenda kwa Madiwani wa CCM na Wabunge wa CCM. Tofauti ya Kura kati ya wagombea wa CCM na Wapinzani ni kubwa sana kiasi kwamba hauwezi kusikia kuwa yapo malalamiko kuwa wagombea wa CCM wameiba kura ama wameshinda kwa ujanja ujanja.

Iliwahi kusemwa kuwa Uchaguzi ni akili, maarifa na mipango na kwamba CCM kama Chama kilijipanga katika kila hatua ya kuelekea ushindi huu ambao umeendelea kutangazwa kwa wanaCCM, wakati CCM wakijiandaa na kufanya ground work ya kuhakikisha wanachama wao wanajiandikisha, wanakuwa na vitambulisho na wanapiga kura.

Wakati hayo yakiendelea CUF walikuwa na mgogoro uliopelekea kuvunjika kwa Chama chao na Maalim Kujiunga ACT Wazalendo ambayo nayo ilikuwa na mgogoro wa kiuongozi na kusababisha wanachama wake na viongozi wake wengi kukihama chama hicho na kujiunga na CCM hali ya kuwa CHADEMA ikiongozwa kuhamwa na wanachama wake na Viongozi wake hasa wabunge kutokana na matatizo ya kiuongozi yaliyokikumba Chama hicho yaliyotokana na Uchaguzi wa Ndani wa Chama hicho na hasa NAFASI YA UENYEKITI wa Chama.

Ninachokisema ni kuwa Wapinzani wanayo nafasi ya kujifunza na hasa wakiwa tayari kufanya hivyo, walipofanya uamuzi wa kugomea uchaguzi wa Serikali ya Mitaa walikuwa wanapaswa kutambua kuwa walikuwa wanajivunja miguu na kuwafanya washindwe kusimama tena.
 
Naomba kukutaarifu kuwa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa tiketi ya Chadema, Mhe. Tundu Lissu atazungumza na vyombo vya habari vya kitaifa na kimataifa, Alhamis, Oktoba 29, 2020.

Mkutano huo utakaoanza saa 3.00 asubuhi, jijini Dar es Salaam ambapo Mhe. Lissu pamoja na Viongozi Wakuu wa Chama, atazungumzia mwenendo na hali ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 28, mwaka huu, uliotawaliwa na kila aina ya uharibifu, uvurugaji na ukiukwaji mkubwa wa taratibu zinazosimamia Uchaguzi Mkuu

Chombo chako kinapewa taarifa na kualikwa katika mkutano huo muhimu.

Tunatanguliza shukrani zetu,

Makene, Tumaini.
 
Back
Top Bottom