tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
37,322
2,000
Si mlisema mwaka huu ccm watajua hawajui? Kumbe mlikuwa mna maananisha kususia zoezi?

Nakuambia watanzania ww unasema habari za ccm! Idadi ya wapiga kura ni ndogo sana ukilingabisha na hiyo idadi ya kupika ya 29m+. Ukiwa mshabiki si lazima uwe mjinga.
 

900 Inapendeza zaidi

JF-Expert Member
Nov 19, 2017
3,110
2,000
Niko naangalia TBC1 hapa, nimecheka hili igizo, eti waziri naye kapanga mstari na mkewe wanasubiri wapige kura! Hivi karne hii wanamdanganya nani wakati kila siku huwa tunasimamishwa barabarani zaidi ya masaa mawili kusubiri wapite?
ukiona hivyo ujue anakwenda kumfyekelea mbali magu
 

Polite

JF-Expert Member
Apr 12, 2011
1,166
2,000
D,,,D,,,,D,,wamefunga funga ipi sasa,kwaresma au mweze wa ramadhani?
Ha ha ha ha ha wamefunga mfungo wa kibeberu,nimeshangaa Sana

Chadema wameshidwa hata kuwapelekea uji,wamekaa Kama wapo msibani,

Na hii ni dalili jioni Kuna mazishi
 

ofisa

JF-Expert Member
May 15, 2011
2,658
2,000
20201028_121330.jpeg
 

tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
37,322
2,000
Dereva wake yupo wapi?

Huna hoja kaa kimya, hakuna uchunguzi maana muhusika yuko juu ya sheria. Hata hivyo nakusalimu maana hujaonekana hapa jukwaani muda.

Nenda kaangalie idadi ya wapiga kura ilivyo ndogo tofauti na ile idadi ya kupika ya 29m+. Huo ni udhibitisho kuwa wananchi wamedharau zoezi la kupiga kura, maana ni upuuzi kama upuuzi mwingine. Hiyo itatoa viongozi walioko kisheria lakini wasio na uhalali wa umma.
 

MISULI

JF-Expert Member
Jan 15, 2014
7,359
2,000
Huna hoja kaa kimya, hakuna uchunguzi maana muhusika yuko juu ya sheria. Hata hivyo nakusalimu maana hujaonekana hapa jukwaani muda.

Nenda kaangalie idadi ya wapiga kura ilivyo ndogo tofauti na ile idadi ya kupika ya 29m+. Huo ni udhibitisho kuwa wananchi wamedharau zoezi la kupiga kura, maana ni upuuzi kama upuuzi mwingine. Hiyo itatoa viongozi walioko kisheria lakini wasio na uhalali wa umma.
So Dereva hatakiwi kuhojiwa?
 

mbenge

JF-Expert Member
May 15, 2019
1,775
2,000
Nilichokishuhudia hii leo wakati nikitimiza wajibu wangu wa kiraia wa kupiga kura, niliweza kuziangalia vyema fomu za kupigia kura kwa nafasi ya uraisi, ubunge na udiwani.

Wakati fomu za wagombea wa nafasi za ubunge na udiwani, majina yalipangwa kufuatia mpangilio wa alphabeti za vyama vyao, hii ya uraisi ilikuwa ni tofauti. Mpangilio wa alphabeti haukuzingatiwa bali ni kama vile ambavyo NEC ilikuja na sababu zake zisizokuwa na kichwa wala miguu.

Huu uchaguzi unaweka rekodi mpya kutokana na woga wa chama tawala ktk kukabiliana na vyama vya upinzani ktk sanduku la kura. Toka awali inaonyesha walijipanga kupata ushindi kwa njia za hila za kifedhuli, badala ya kutumia uhuru wa wapigakura na njia iliyokuwa ya uwazi na haki. Hii ni aibu na fedheha kubwa kwa chama hiki kikongwe na kilichopitwa na wakati.
 

Stan Mashamba

JF-Expert Member
Apr 22, 2020
1,856
2,000
Mimi ni msimamizi wa uhaguzi kituo flani naona kila mpiga kura anaweka tiki mwanzoni kabisa mwa karatasi ya kupigia kura. Wachaaaaache ndiyo nawaona wakiweka tiki mwishoni mwa karatasi hiyo.
Naona una macho ya X-ray kumuona mtu akifanya yake chumba cha siri cha kupigia kura. Kwani kituo hicho watu wanapiga kura hadharani? Wee acha uhuni.
 

BUSH BIN LADEN

JF-Expert Member
Mar 16, 2019
3,428
2,000
Nakuambia watanzania ww unasema habari za ccm! Idadi ya wapiga kura ni ndogo sana ukilingabisha na hiyo idadi ya kupika ya 29m+. Ukiwa mshabiki si lazima uwe mjinga.
Hivi unafanyaje tathmini ya uwingi au uchache wa wapiga kura kwa kituo kimoja tu ulichopigia kura?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom