Nishampigia kura ndugu lissu
IMG_20201028_091903.jpg
 
Hakika Leo nimetimiza wajibu wangu kama Mtanzania ikiwa ni muendelezo toka mwaka 1995, kuna mambo kadhaa nimeona kwenye kituo cha kupigia kura.

1. Watu ni wachache waliojitokeza kupiga kura kwenye kituo changu na hakuna foleni.

2. Nimeona awamu hii every vote count yaani kila karatasi ya kura inakuwa na namba za mpiga kura za kwenye kitambulisho hii imenifikirisha sana.

Kumbe watu wanaweza kudai kura zao mahakamani kama watakuwa hawana uhakika na matokeo,kama ambavyo mwanafunzi anaweza kuomba mtihani wake usahihishwe upya kama akuridhika na matokeo.

3. Ni ngumu kujua wakala wa chama chako pale kituoni
4. Utaratibu wa kupiga kura na hatua zote ziko vizuri mno hongereni tume
5. Ulinzi ni wa kawaida mno sio kivileeeee
6. Wananchi wanaendelea na kazi zao kama kawaida
7. Kuna wakala kanikata jicho baya sana nikastaajabu kunani?

Yote kwa yote zoezi linakwenda vizuri sana Hongereni tume kwa hatua hii ya kwanza hope hata kwenye matokeo mtafanya vizuri
 
Nashukuru Mungu nimetimiza haki yangu kikatiba, Udiwani na Ubunge nimechagua CCM, Urais nimempa Lissu.


Najua Lissu hawezi shinda ila nimempigia kumuonyesha kuwa kuna watu tupo pamoja na yeye ingawa tupo CCM.
 
Nimetembelea maeneo mbalimbali ya vituo vya kupigia Kura, maeneo mengi wasimamizi wanapiga stori tu hakuna watu!!!

Akilini kwangu nikajiuliza, hivi Kwa nini sasa Serikari badala ya kutumia pesa nyiiingi za Kampeni, badala yake hizo fedha zipelekwa kwenye vituo Vyote ili kila mpiga Kura akimaliza kupiga Kura Apewe Tsh 5000 Tu, ili kuwavutia wapiga Kura wengi kujitokeza

Maana Kwa mwelekeo huu, ni Bora Kampeni zote sasa, ziwe zinafanyika kwenye luninga na si kwenye majukwaa na kutembea nchi nzima kupoteza pesa zetu, na badala yake sasa hiyo fedha iwe ni motisha Kwa mtu anayedamka Asubuhi na kuacha shughuli zake kwenda kumchagua mtu ambaye hata hivyo mshahara wake mmoja tu Kwa mwezi, mtu wa kawaida anautafuta miaka mitano yote na haupati

Serikali ijipange kivingine aisee, inachosha na inakatisha tamaa aisee

Nimetembelea vituo zaidi ya 20 mambo ni yaleyale, wasimamizi wanagonga vivyaji na stori nyiiingi!!
 
John Heche, Chadema's Parliamentary Candidate for Tarime reports that homes of many polling agents in his area were invaded at night by the police who then detained them. As a result, there are no opposition agents in many polling centers.
Aache visingizio! Mawakala hawana hela.

Lisu badala ya kufanya organisation ya mawakala kipindi kile amesimamishwa kampeni, badala yake yeye akatumia muda huo kujifanya house girl wa kwenda kununua nyanya kariakoo
 
Reserved: Ajili ya PICHA na video mbalimbali

TUNDU LISSU AELEKEA SINGIDA KUPIGA KURA
View attachment 1614455
Mgombea Urais wa JMT kupitia CHADEMA, Tundu Lissu akiwa Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere, Dar es salaam tayari kuelekea Mkoani Singida kushikiri zoezi la upigaji kura.


BALOZI WA MAREKANI NCHINI TANZANIA AWATAKIA KILA LA KHERI WATANZANIA
Today is the day! Kila la kheri to all Tanzanians as they head to the polls to exercise their right to vote. Providing full access to observers and party agents, along with transparent tallying, will give credibility to this process.
IGP SIRRO APIGA KURA, ATOA NENO
View attachment 1614517
20201028_114009.jpg

Vituoni hamna foleni kabisa kapigeni kura
 
Haya yanatoka wapi tena wakati tulisema mwaka huu hatutalia tena, watalia wao. Mwaka huu hatubiwi tena, wataibiwa wao.
Sasa wewe unaleta tena haya unakuwa unaturudisha nyuma

Unajua unachoongea, kwani watu kupuuza zoezi la kupiga kura ndio kuibiwa kura?
 
Back
Top Bottom