YALIYOJIRI SADC: Rais Magufuli awa M/kiti SADC. Tanzania yawa nchi pekee ya SADC ambayo uchumi wake unakua

MIMI BABA YENU

JF-Expert Member
Mar 1, 2019
295
679
Rais wa Tanzania, John Magufuli leo Jumamosi Agosti 17, 2019 amekabidhiwa uenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na Rais wa Namibia, Dkt Hage Geingob

Uteuzi wa Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo hudumu kwa mwaka mmoja, na huzunguka miongoni mwa Marais wa nchi wanachama

=========

Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya SADC Dr. Stergomena Lawrence Tax ameipongeza Tanzania kuwa nchi pekee ambayo imeongoza kwa kukidhi vigezo vya ukuaji wa uchumi, kwa kufikia asilimia 7, ikiwa ni tofauti na nchi nyingine.

Kauli hiyo ametoa wakati wa mkutano wa kwanza wa SADC uliofanyika jijini Dar es salaam, ambapo viongozi mbalimbali wa jumuiya hiyo wakiwemo viongozi wastaafu na Mawaziri wamehudhuria.

Dk.Tax amesema kwa nchi za jumuiya hiyo pamoja na mambo mengine kwenye eneo la uchumi kuna malengo ambayo yamewekwa kwa nchi wanachama na Tanzania ni nchi pekee ambayo uchumi wake unakuwa kwa asilimia saba na hivyo wanastahili kupongezwa.

"Uhimilivu wa uchumi ni nyenzo muhimu katika maendeleo, nchi wanachama zimekidhi vigezo vya SADC kiuchumi, takwimu zimeonesha Tanzania inafanya vizuri, na kwa vigezo pekee Tanzania ndiyo nchi pekee ambayo imefikia ukuaji wa asilimia 7, mjipongeze." Amesema Dr Tax na kuongeza;

"Katika kufikia uchumi wa Viwanda nchi wanachama hawana budi kukuza uzalishaji wa umeme, kwa kuwa ni kitu muhimu kwenye ujenzi wa viwanda, nashukuru katika wiki ya Viwanda hata Tanzania , tumeona mradi mkubwa wa umeme katika maporomoko ya mto Rufiji ambao ujenzi wake unaendelea"
 
Write your reply...uchumi unapimwa kwa interchange hiyo moja ya Tazara? au kwa kipi? kuwa na ngozi nyeusi ni laana au ni mkosi? utapeli mtu 7% kwa maisha haya, au kuna mengine?
 
uchumi unakua kwa 7% huko chato, the rest of the country uchumi unasinyaa
 
Rais wa Tanzania, John Magufuli leo Jumamosi Agosti 17, 2019 amekabidhiwa uenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na Rais wa Namibia, Dkt Hage Geingob

Uteuzi wa Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo hudumu kwa mwaka mmoja, na huzunguka miongoni mwa Marais wa nchi wanachama

=========

Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya SADC Dr. Stergomena Lawrence Tax ameipongeza Tanzania kuwa nchi pekee ambayo imeongoza kwa kukidhi vigezo vya ukuaji wa uchumi, kwa kufikia asilimia 7, ikiwa ni tofauti na nchi nyingine.

Kauli hiyo ametoa wakati wa mkutano wa kwanza wa SADC uliofanyika jijini Dar es salaam, ambapo viongozi mbalimbali wa jumuiya hiyo wakiwemo viongozi wastaafu na Mawaziri wamehudhuria.

Dk.Tax amesema kwa nchi za jumuiya hiyo pamoja na mambo mengine kwenye eneo la uchumi kuna malengo ambayo yamewekwa kwa nchi wanachama na Tanzania ni nchi pekee ambayo uchumi wake unakuwa kwa asilimia saba na hivyo wanastahili kupongezwa.

"Uhimilivu wa uchumi ni nyenzo muhimu katika maendeleo, nchi wanachama zimekidhi vigezo vya SADC kiuchumi, takwimu zimeonesha Tanzania inafanya vizuri, na kwa vigezo pekee Tanzania ndiyo nchi pekee ambayo imefikia ukuaji wa asilimia 7, mjipongeze." Amesema Dr Tax na kuongeza;

"Katika kufikia uchumi wa Viwanda nchi wanachama hawana budi kukuza uzalishaji wa umeme, kwa kuwa ni kitu muhimu kwenye ujenzi wa viwanda, nashukuru katika wiki ya Viwanda hata Tanzania , tumeona mradi mkubwa wa umeme katika maporomoko ya mto Rufiji ambao ujenzi wake unaendelea"

Aisee huu uongo jamani!

Mnatia huruma wazee wa mapambio!

Mpaka mnaonekana watoto sasa!
 
Uchumi upi unaokuwa!? 😳😳😳😳

sadc.JPG

RAIS John Magufuli amekabidhiwa rasmi uenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) leo, Jumamosi, jijini Dar es Salaam. Rais Magufuli anachukua madaraka hayo kutoka kwa Rais wa Namibia Dk Hage Geigob na ataongoza jumuiya hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Makabidhiano hayo yamefanyika katika Mkutano wa 39 wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika, jijini Dar es Salaam ambao umewaleta pamoja marais na viongozi wa serikali kutoka nchi 16 za jumuiya hiyo. Akizungumza katika mkutano huo Rais Magufuli amesema kuwa masuala ya viwanda yatapewa kipaumbele katika kipindi hiki cha uongozi wake.

“Tuna changamoto pia ya kutokuwa na mifumo mizuri ya uchumi wa viwanda, na hii ni sababu inayodumaza uchumi wetu kwenye jumuiya hii ya SADC,” ameongeza. Hata hivyo Dk Magufuli ameitaka #Sadc kusimama pamoja na kuitetea Zimbabwe ili vikwazo vya kiuchumi dhidi yake viondolewe. Katika makabidhiano hayo, mwenyekiti anayemaliza muda wake ametumia fursa hiyo kutangaza Kiswahili kuwa lugha ya nne rasmi ya #Sadc. Mbali na Kiswahili chenye mizizi yake, Tanzania, lugha nyingine rasmi katika mawasiliano ya #Sadc ni Kiingereza, Kireno na Kifaransa ambazo zinazungumzwa katika baadhi ya nchi wanachama.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom