Yaliyojiri Mkutano wa waandishi wa habari na wakurugenzi wa TRC na NHIF

Shigganza

Senior Member
May 24, 2018
160
412
YALIYOJIRI LEO DESEMBA 12, 2019 KWENYE MKUTANO WA MKURUGENZI MKUU WA SHIRIKA LA RELI TANZANIA (TRC), MASANJA KADOGOSA NA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU MAFANIKIO YA TAASISI HIYO KATIKA MIAKA MINNE YA SERIKALI YA AWAMU YA TANO

#TRC ilianza kazi rasmi mwezi Machi 2018 na iliundwa kupitia Sheria Na. 10 ya mwaka 2017 ili kuendeleza kazi zilizokuwa zikifanywa na RAHCO na TRL

#TRC imefanikiwa kuanzisha huduma ya usafiri wa treni za mjini (Dar es Salaam) kutoka Posta kwenda Pugu na kutoka Posta kwenda Ubungo

#Kuanzia Julai 2018 TRC imerejesha safari kwa treni za mizigo kutoka Dar es Salaam hadi Kampala nchini Uganda na kusafirisha tani 52,709 za mizigo

#Kuanzia Julai 2019 TRC imerejesha huduma ya treni za mizigo kutoka Dar es Salaam-Tanga-Moshi na kusafirisha tani 4,800 za mizigo

#TRC imeongeza idadi ya abiria kwa treni za mikoani kutoka 411,172 mwaka 2014/15 hadi 578,439 mwaka 2018/19

#Kuanzia 6 Desemba 2019, TRC imerejesha huduma ya usafiri wa abiria kutoka Dar es Salaam kwenda Kilimanjaro

#TRC inatekeleza mradi mkubwa wa ujenzi wa reli ya kisasa "Standard Gauge Railway" awamu ya kwanza kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza yenye kilometa 1,219

#TRC inaboresha reli ya kati kutoka Dar es Salaam hadi Isaka yenye kilometa 970 ambapo mradi huo umetoa zaidi ya ajira 1600

#TRC imeongeza mapato yake kutoka shilingi bilioni 17.4 kwa mwaka 2014/15 hadi bilioni 30 mwaka 2018/19 kwa treni ya mizigo

*Imetolewa na Idara ya Habari-MAELEZO*

*YALIYOJIRI WAKATI WA MKUTANO WA MKURUGENZI MKUU WA MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA (NHIF) BW. BERNARD KONGA NA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU MAFANIKIO YA MFUKO HUO KATIKA KIPINDI CHA MIAKA 4 YA SERIKALI YA AWAMU YA TANO LEO DESEMBA 12, 2019*

# NHF imetumia jumla ya Shilingi Bilioni 13.7 katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Tano kuwezesha ukarabati na ununuzi wa vifaa vya matibabu kama MRI, CT SCAN na uanzishwaji wa viwanda vidogo vya kuzalisha maji na gesi

#Baadhi ya Hospitali zilizonufaika ni Hospitali ya Taifa Muhimbili, Bugando, KCMC, MOI, Ocean Road na Hospitali ya Rufaa Mbeya

# NHIF imetoa fedha kuwezesha uwekezaji wa awamu ya pili katika Hospitali ya Benjamin Mkapa na ununuzi wa vifaa tiba vya kisasa kuwezesha huduma za kibingwa kama upandikizaji figo

#Shilingi Bilioni 32.10 zimetolewa kwa ajili ya ujenzi na Bilioni 43.12 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma

#Uwekezaji wa majengo pacha ya MOI umesaidia kuongeza uwezo wa kulaza wagonjwa na kuboresha huduma za Kibingwa

#Majengo mengine yaliyojengwa kwa uwekezaji wa NHIF ni Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya, Hospitali ya Rufaa Dodoma, Hospitali ya Rufaa Bugando na KCMC.

#Wanachama wa NHIF wanapata huduma katika vituo 7,606 nchi nzima vikiwemo vya Serikali na Binafsi kwa ngazi zote ikilinganishwa na vituo 6,185 vya mwaka 2014/2015 ,Ongezeko hili ni sawa na vituo 1,421 kwa kipindi cha miaka minne.

#Katika kipindi cha miaka minne, NHIF imelipa jumla ya shilingi trilioni 1,283,109,701,067 kwa vituo vyote vinavyohudumia wanachama wake nchini

# Mwaka 2018/2019 Mfuko umelipa kiasi cha Shilingi Bilioni 444.1 ambayo ni ongezeko la asilimia 64 ikilinganishwa na malipo yaliyofanyika mwaka 2014/2015 ya shilingi bilioni 157.9

#Jumla ya Shilingi Bilioni 43.12 zilitolewa kwa ajili ya vifaa katika Hospitali ya Benjamin Mkapa

#Mradi wa Tumaini la Mama ulilenga kuwapatia wanawake wajawazito bima ya Afya na umewanufaisha jumla ya akina mama 1,044,000.

#Katika kipindi cha miaka minne mradi huu umewanufaisha akina mama 796,404 sawa na ongezeko la la asilimia 76 kutoka wanufaika 247,596 wa mwaka 2014/2015

#Mradi wa Tumaini la mama umesaidia kupunguza vifo vya uzazi, umewezesha wakina mama kujifungulia Hospitali

#Serikali kupitia Wizara ya Fedha na NHIF imesaini mkataba wa awamu ya tatu na KfW wenye thamani ya EURO milioni 13 sawa na Shilingi Bilioni 32.7 na utekelezaji utakamilika mwaka 2020.

#NHIF imethibitishwa kwa utoaji wa huduma bora kwa viwango vya kimataifa na kukabidhiwa cheti cha ubora (ISO 9001:2015) mwaka 2018.

#Ndani ya kipindi cha miaka minne ya Awamu ya Tano, mfuko umeimarisha mawasiliano na wanachama na wadau wake kwa kuanzisha Kituo cha Huduma kwa Wateja

#Watumishi wa umma ambao mpaka sasa takribani asilimia 99 ni wanachama wa NHIF, Watumishi wa Sekta binafsi

# Mfuko unahudumia wanachama 966,792 swa na wanufaika 4,025,693 ikilinganishwa na idadi ya wanufaika 3,237,434k kwa mwaka 2014/15 sawa na ongezeko la asilimia 20

Imeandaliwa na Idara ya Habari MAELEZO
 
Naipongeza sana TRC chini ya Masanja Kadogosa na siyo NHIF kwa sababu wagonjwa wengi hawapati madawa kutokana na magonjwa yao. Utaambiwa kuwa Kituo hiki hakina uwezo wa kutoa dawa aina fulani.
 
Back
Top Bottom