Uchaguzi 2020 Yaliyojiri mkutano wa kampeni za Mgombea wa CCM Dkt. Magufuli akiwa Bukoba, Kagera

Hakika nyie waongo na mnatafta Kiki huu umati wote unang'aa kwa nguo Safi za kijani et unatuambia wameropoka hawamtaki. Walai nawaambia watanzania wamemchagua Dr John P Magufuli na wamemchagua CCM.

Na wale waliokuwa wanatumia Kiki ya tetemeko povu leo limewatoka baada ya kuona umati Mkubwa ukimshangilia jemedari wao na Rais wao anayesubilia kuapishwa
Check umati huu
View attachment 1571640
Sina mlengo na siasa, ila nimejaribu kutoa tetesi, plz acha kuhemkwa.
 
Wananchi wa Bukoba wameelewa umuhimu wa tarehe 28 Oktoba kwenda kumchagua Dkt Magufuli.
Kilichobaki sasa ni kusubiri siku ifike tukamchague Mgombea wa CCM na Rais DK MAGUFULI
Mimi Nitapiga Kura na Kumchagua ✅
Wewe Je??!
 
Chadema waliishiwa zamani saaana
Yaani ccm wacheni vichekesho mnawakusanya wanafunzi kibao ndiyo mnajisifu mafuriko? Shame on you guys
FB_IMG_1600274388329.jpg
 
Aisee bado sana ,yaani taa za barabarani ati ni agenda ya kuombea kura ....dah
Magufuli ana upeo mdogo sana. Kwake kila kitu anakiangalia kwa jicho la ujenzi hadi anachosha. Hajui kuwa maisha ya watanzania yana mambo mengi zaidi ya hayo mataa yake anayowaza kujenga. Bure kabisa huyu Mhutu
 
Jamani watu kama misukule vile wamesombwa usiku kucha na malori ya ng'ombe kutoka Karagwe, Bukoba Vijijini, nk. tuseme watu walilala uwanjani.

Hii imejionyesha baada ya hotuba.

Vipi waliokamatwa kwa kutonyoosha mikono ya kukiri kuichagua CCM?

Tutafika hiyo 28/10/2020?
 
Yaani ccm wacheni vichekesho mnawakusanya wanafunzi kibao ndiyo mnajisifu mafuriko? Shame on you guysView attachment 1571667
Hizo ndio Kiki ambazo mnatumia ili muelewele. Hizo picha ni za Jana je mbona hujatuma picha zote za Jana je kulikuwa na watoto? But also watu wanampenda Mheshimiwa Rais na baadhi ya sehemu watu hawajawahi kumwona Rais so Kama watu wamesikia Rais anakuja kwa Nini wasije kumwona????

Jana Lissu alituma picha za sehemu alipokwenda na kuambiwa katika kata ile hajawahi kumwona Mgombea urais so hata Jana watu hata Kama ni wanafunzi wanaenda kumwona Rais anayewasomesha bure
 
Watu wanampenda Magufuli Hadi basi na tarehe 28 utashuhudia Kama upinzani mtapata hata Jimbo moja Kagera
Kwanin unateseka kiasi hicho?Angalia usijeanguka kwa pressure!Mpaka tar 28 bado mbali sana,huu moto wa kampeni angalieni usijewaacha na maradhi ya moyo!
 
Hizo ndio Kiki ambazo mnatumia ili muelewele. Hizo picha ni za Jana je mbona hujatuma picha zote za Jana je kulikuwa na watoto? But also watu wanampenda Mheshimiwa Rais na baadhi ya sehemu watu hawajawahi kumwona Rais so Kama watu wamesikia Rais anakuja kwa Nini wasije kumwona????

Jana Lissu alituma picha za sehemu alipokwenda na kuambiwa katika kata ile hajawahi kumwona Mgombea urais so hata Jana watu hata Kama ni wanafunzi wanaenda kumwona Rais anayewasomesha bure
Ccm mmekwisha jiandaeni kisaikolojia maana Lissu ndiye rais wako ajaye
 
Mimi silalamiki ila nakushangaa kujifanya Chizi wa kutokuwa unaangalia matukio ambayo yanakushika na unaangalia tu matukio unayotolea pumba zako za kutuletea hapa
Duh....chizi...pumba....huna maneno mengine kujenga hoja yako zaidi ya maneno haya....chizi...pumba?? Unaelewa maana ya neno chizi?! Unaelewa maana ya kumwambia mtu kuwa 'maneno yako ni pumba' ? Hebu Kwanza kamwambie Kwanza baba yako aliyekuzaa na mama yako kwamba 'baba wewe ni chizi....mama wewe ni chizi na maneno yako ni pumba' tu..'. Majibu utakayopata kutoka kwa wazazi wako uje utujulishe humu JF...
 
Magufuli ana upeo mdogo sana. Kwake kila kitu anakiangalia kwa jicho la ujenzi hadi anachosha. Hajui kuwa maisha ya watanzania yana mambo mengi zaidi ya hayo mataa yake anayowaza kujenga. Bure kabisa huyu Mhutu
Upepo wa JPM ni wa kuotea mbali
Check
IMG-20200916-WA0148.jpg
 
Kwanin unateseka kiasi hicho?Angalia usijeanguka kwa pressure!Mpaka tar 28 bado mbali sana,huu moto wa kampeni angalieni usijewaacha na maradhi ya moyo!
Hatuna pressure maana ushindi wa Magufuli Mwaka huu ni wa kihistoria. Mwenye shida ni Lissu maana juzi kaanza kuanguka na pressure mufindi
 
Nakuona unateseka kwenye nyuzi humu JF,angalizo ni kuwa angalia usijepata maradhi ya moyo!
Maana utaendelea kuumia tu kwani kampeni hata nusu bado!
 
MGOMBEA Urais kwa tiketi ya CCM, Dkt John Pombe Magufuli, leo Septemba 16, 2020 ameendelea kupiga kampeni, ambapo baada ya kumaliza wilayani Chato, mkoani Geita, Muleba leo yupo Bukoba Mjini mkoani Kagera Uwanja wa Gymkana.

MGOMBEA Ubunge jimbo la Bukoba Mjini Stephen Byabato amewaomba wananchi wa jimbo hilo katika Uchaguzi Mkuu mwaka huu kuhakikisha wanajenga mnara wa mawasiliano kati yao na Rais Dk.John Magufuli kwa kuchagua Rais, Mbunge , madiwani kutoka Chama Cha Mapinduzi( CCM).

Akizungumza mbele ya maelfu ya wananchi wa Mkoa wa Kagera waliohudhuria mkutano wa kampeni za mgombea urais kwa tiketi ya CCM Dk.John Magufuli kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 28 mwaka huu, Byabato amesema katika uchaguzi hakuna sababu ya hao kufanya makosa kama yaliyofanyika uchaguzi wa mwaka 2015 kwa kuchagua mbunge na madiwani wa upinzani.

"Bukoba Mjini tulikosea mwaka 2015 kwa kuchagua upinzani , na hivyo kukata mawasiliano kati yetu na Rais Magufuli.Huu ni mwaka wa kujenga mnara wa mawasiliano,naomba wote tumchague Dk.Magufuli kwa nafasi ya urais,mnichague mimi kwenye ubunge jimbo la Bukoba Mjini pamoja na wabunge wote wa CCM,"amesema Byabato.

Amefafanua kuwa ni kweli maendeleo hayana Chama na ndio maana Rais Magufuli amefanya maendeleo makubwa bila kuombwa na mtu yoyote lakini kwa upendo wake mkubwa kwa wananchi wa Bukoba Mjini na Kagera Mjini ameleta maendeleo.

Ameongeza katika miaka mitano iliyopita chini ya uongozi wa Rais Magufuli wananchi wa Bukoba Mjini kunamaendeleo makubwa yamefanyika na kwamba Sh.bilioni 158 zimetumika kwa maendeeleo."Tunatambua kwamba yote hatukuomba lakini tumezipata fedha hizo kwa upendo mkubwa alionao kwa ajili yetu."

Amesisitiza Bukoba Mjini kuna taa za barabarani wamepata kilometa 13 za lami, wamepata mradi mkubwa wa maji wenye kuzalisha lita milioni 18 wakati mahitaji ni lita milioni 15 kwa siku na hivyo kubaki na ziada ya lita milioni tatu na kwamba yote hayo yamefanyika sio kwasababu waliomba bali yametokana na Rais Magufuli na mapenzi yake kwa wananchi.

Pia Sh.milioni 500 zimetolewa na Rais Magufuli kwa ajili ya vituo vya afya na leo, miundombinu katika sekta ya afya imeboreshwa na kuimarika sana."Hayo yote hatukuomba katika miaka mitano lakini tumepewa.Nawaombeni wana Bokoba, tusifanye makosa tena.Tumchague Dk.Magufuli kwanza jina lake ni kubwa hata ukilitaja unasikia raha.

"Tujenge mnara wa mawasiliano ambao utakuwa rasmi kwa ajili ya kupeleka mawasiliano kati ya wananchi na Rais wetu.Tunataka tukipiga simu kwa Rais tunaambiwa mawasiliano yapo na tunayoomba yanafanyiwa kazi, Bukoba iwe na mawasiliano mazuri na sio ukipiga unaambiwa Not reachable,"amesema Byabato.

----
Sehemu ya Wanachama na Wananchi wa Mkoa wa Kagera waliohudhuria mkutano wa kampeni za mgombea urais kwa tiketi ya CCM Dk.John Magufuli kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 28 mwaka huu.

WhatsApp%2BImage%2B2020-09-16%2Bat%2B8.54.24%2BAM.jpeg

WhatsApp%2BImage%2B2020-09-16%2Bat%2B8.54.25%2BAM%2B%25281%2529.jpeg
Wanakagera hatujasahu ujue ewe john.

Ulituambia twafa Tetemeko halikuletwa na sirikali yako
 
Attachments

  • ca0a7ed7-88a4-4755-9c5f-7ad4d167985a.JPG
    ca0a7ed7-88a4-4755-9c5f-7ad4d167985a.JPG
    90.4 KB · Views: 1
  • 2d9824ad-7868-4cb8-a34f-b52a4944f717.JPG
    2d9824ad-7868-4cb8-a34f-b52a4944f717.JPG
    147.4 KB · Views: 1
  • a701581f-6182-4acd-8872-dcea7dd48bd8.JPG
    a701581f-6182-4acd-8872-dcea7dd48bd8.JPG
    121.9 KB · Views: 1
Back
Top Bottom