Yaliyojiri Mkutano wa Edward Lowassa na wanawake wa DSM kutoka Ukumbi wa Millenium Tower

BAWACHA WAMGOMEA LOWASA

Wakiongea kwa nyakati tofauti wanawake wa bawacha wanasema wamefaatilia kwa karibu sana sana hotuba ya mgombea urais kupitia UKAWA aliyoitoa hapa LAPF kwenye kongamano la wanawake BAWACHA na kubaini jambo moja kubwa sana.

Kauli mbiu ya kongamano ni "LOWASA NA HATMA ZA CHANGAMOTO ZA WANAWAKE TANZANIA"

Tumesikitika kuwa tulitegemea kwenye hotuba Yake ataweza kuelezea mikakati ya ukombozi huo wa mwanamke lakini tunasikitika kuwa hakuona mahali popote akiongelea changamoto hizo na jinsi ya kuzitatua.

Ameishia kuimba Wimbo wa Mhe.Dr Magufuli "Alinselema Hadija, mchaka mchaka chinja" na kuzungumza mambo ya MAHABA!

Tumesikitika kusema sisi kama wanawake hatuko tayari kubueuzwa, kura zetu No!!!!!!!!!! Ngoja tumsubiri Dr Magufuli original wa Alinselema na mtu wa kutenda.

Tuna uhakika atatuondolea kiu ya changamoto zinazotukabili ikiwa ni pamoja na kuboresha HUDUMA ZA AFYA.

Tunataka kuona SERA za ukweli za kumkomboa mwanamke kama za Dr Magufuli na sio MAIGIZO.

Kwakifupi babu wetu ni msanii kwelikweli hana uwezo wa kuongoza nchi, tumkatae, tumpinge kwa nguvu zote.

Hahahahahhh hata hajui nani alikuwa mgeni rasmi kwenye mkutano huo.Acha kulialia humu kampigie magufuli kampeni
 
vp kuhusu uzinduzi wa kampen bado msimamo palepale?

Hata kupanda daladala ni kawaida tu lakini alipopanda Lowassa ikawa siyo kawaida.

Subiri leo kama hutamsikia Kova akitoa mapovu.

attachment.php


umhh halima hata aibu haoni..???!
 
Asante sana mkuu newazz.
InshaAllah tukutane hiyo jumamosi Jangwani.

Hakika ni kesho , hakuna kesho nyingine.

Sijapata tshirt .. nataka ile pamba ya nyekundu blue tshirt - form six zinapatikana wapi.

Kesho nataka kuwa ful regalia ....
 
Hakika ni kesho , hakuna kesho nyingine.

Sijapata tshirt .. nataka ile pamba ya nyekundu blue tshirt - form six zinapatikana wapi.

Kesho nataka kuwa ful regalia ....

Hata sijui zinapatikana wapi.
Mie nitavaa dira tu....
 
Akili fupi sana ndio mwisho wako wakufikiria hapo ee?
ya kwako ndefu iko wapi hapo? hatuna nini? ardhi? madini? upepo? maji? yote hayo si mali? au unataka kusema nini sijakuelewa hapo. nimesema muache kudanganya watu wahimizeni wafanye kazi
 
Napitia hapo sasa hivi nikajichukulie.... Nitakuwa mtamu kesho.. nachukulia my whole family.

Utakuwa umefanya jambo laakili sana.....!Ila wakuu pamoja na yote tuhakikishe Tar 25 tunaVote UKAWA angalau kila. Mtu awe na watu japo wa4....kitaeleweka tuu...Manake moto utakaowashwa kesho then GAMBAZ wakishinda uchaguzi haitapendeza cc tuchague UKAWA KURA zitoshe....hata wakitaka kuiba Wawe wanaifikiria ICC
 
umesema vitu vizuri vya watu kufanya kuinua uchumi binafsi bt kumbuka uwekezaji hasa kwenye vitu ulivyo vitaja,upepo,bahari,madini,na ardhi unahitaji mitaji na technolojia ambavyo ndio nguzo muhimu ktk uchumi wa taifa na mtu moja moja.kwa miaka watanzania wengi wamefanya uwekezaji ktk maeneo hayo bila kupata mafanikio ni jukumu la serekali kuwasaidia watu katika maeneo hayo lalkini serekali yetu imelala.unadhani watu watafanyaje sasa
nimekupata mkuu. tunachopaswa kukifanya ni kufanya kazi ktk timu. hata hayo makampuni makubwa km barrick si ya mtu mmoja. baadhi ya makampuni km hayo yalianza na mtaji kidogo tu baada ya watu kujiunga kwa nia ya kufanya kazi pamoja. halafu ngoj nikuulize kipi kinapaswa kua cha mwanzo na kipi kifuate kati ya serikali kusaidia watu na watu kuibua miradi? tunapaswa kua na uthubutu wa kutenda kitu fulani ndio serikali inaweza kuona juhudi zetu na kutuendeleza. tatizo letu kila mtu anataka kufanya lake kitu ambacho tunaishia njiani na kulaumu.
 
sasa ndugu,unaweza kuletewa hela kwa njia tofauti (indirectly) sio lazima iwe direct,kama utachagua mtu unaye amini ktk sera zake zitaleta unafuu ktk uchumi wa nchi hadi kwenye uchumi wa mtu moja moja ni sawa na kupewa hela.ni kama indirect income au indirect tax inavyo fanya kazi ktk uchumi huria.
Pia unasema watu wafanye kazi ni kweli bt unaweza ukafanya kazi 24 hrs bt unacho kipata hakitochelezi kutnkana na bei ya bidhaa na hudtma <tax&inflation) ambayo tunajua vhna athiriwa na uongozi wa nchi hususani kwenye mipango na matumizi ya fedha
kufanya kazi kipato kisitosheleze ni tofauti na watu wanavyolia sasa kwamba wanaletewa umasikini. tatizo nililoliona tunataka tuanze leo na kula matunda leo. nadhani uvumilivu nai muhimu sana katika kufanikiwa. watu wakion matajiri wakubwa au wawekezaji wanadhani wameibuka tu ghafla wakati wengine ni idea za babu zao ndizo zimewafikisha walipo leo. hata km kuna factor zinatuvuta wapo watu ni vijana wadogo tu wametusua maisha balaaa na wameanza from nothing. haya tujiulize hawa wametoka ktk enzi zipi?
 
Kama hujui jambo unauliza ili uelimishwe na si kuhorojoka tu kwani ndiyo maana kwako ni ngumu kujua uhusiano wa CCM na umaskini wako, wa mama zako na ndugu zako wengine huko kijijini kwenu!!

Then, kwa nini au una usaidizi gani wewe wa kuutumia upepo unaovuma tu, maji yanayotiririka tu kuelekea baharini, madini yaliyo lala tu chini, misitu na maliasili zingine lukuki tulizopewa na mwenyezi Mungu zilizozagaa tu kukuondolee umaskini wako na ndugu zako?

Ni kwa nini unafikiri hali iko hivi? Hujui kuwa maeneo ya ardhi karibu yote yenye madini yameuzwa Na serikali ya CCM kwa wawekezaji wa kizungu wa Ulaya na Marekani na sasa Uchina?

Kama unabisha waulize vijana wa Kahama, Nyamongo Mara, Geita na Mtwara kwenye gesi wakuoneshe maiti za vijana wenzio waliouawa na Polisi wa serikali ya CCM wakiwalinda wazungu!!
na hao watz wenye maisha yao wamepata wapi hayo maendeleo? ni ktk enzi ipi ya ukawa? au unabisha hakuna watu wana pesa za kutosha tz hii hii ambayo wengine tunalia humu? fake excuse ni kawaida yetu hebu niambie ni namna gani taratibu zetu za kudeka zimetufikisha hapa.
 
na hao watz wenye maisha yao wamepata wapi hayo maendeleo? ni ktk enzi ipi ya ukawa? au unabisha hakuna watu wana pesa za kutosha tz hii hii ambayo wengine tunalia humu? fake excuse ni kawaida yetu hebu niambie ni namna gani taratibu zetu za kudeka zimetufikisha hapa.

tulia dozi ikuingie

fisadi la ccm
 
Back
Top Bottom