Yaliyojiri mjadala wa Sekta ya habari, Mawasiliano na TEHAMA ulioongozwa na Waziri Nape

N'yadikwa

JF-Expert Member
Aug 10, 2014
6,825
9,528
WALIOHUDHURIA MKUTANO HUO WA ZOOM ULIOFANYIKA JUMAMOSI TAR. 19 FEB. 2022
1. Waziri wa Habari, Mawasiliano na TEHAMA NAPE NNAUYE
2. DG wa TCRA Dkt Jabiri Bakari
3. Mkurugenzi wa ITV/Radio One Bi. J. Mhavile
4. Mkurugenzi Mtendaji Multichoice Tanzania- Bi. J. Woiso
5. Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania- Deodatus Balile
6. Askofu wa WAPO MISSION - Gamanywa
7. DG wa TBC - Dkt Rioba Chacha
8. MwanaDiaspora - Mubelwa Bandio
9. Balozi wa Tz Nigeria- Benny Banna

WALICHOJADILI KWA MUKHTASARI

- Mhaville: Ni jambo jema kwamba Free to Air Channels i.e. Chaneli za kutazama bila kulipia, zimerudi kwenye Satelaiti decoders DtH (Direct to Home) kv DSTV;

- Balile: Tunadhani hatua ya kufungulia magazeti ni ya kuungwa mkono inatupa sura mpya ya Serikali iliyopo madarakani;

- DG wa TCRA: Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye gharama nafuu ya data duniani ikishika nafasi ya 21 kati ya 155...pia Tanzania inashika nafasi ya PILI miongoni mwa nchi 43 za Afrika kwa usalama mtandaoni kwa mujibu wa utafiti wa ITU....Aidha Tanzania inashika nafasi ya 6 kwa unafuu wa gharama ya DATA barani Afrika kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na taasisi ya British Technology Research Firm...Huyu bwana yeye aliongea zaidi kwenye hii online symposium.

- Ayub Chacha Rioba: TBC tunataka kuweka kipaumbele kwenye TEHAMA katika uwasilishaji wetu wa taarifa....watu hawaelewi TBC ni chombo cha kuzungumza POSITIVES za nchi.....TBC tunampango wa kuanzisha Chaneli ya TV ya Kiingereza kuwahudumia hadhira ya Kimataifa na local isoelewa Kiswahili...

- Woiso wa Multichoice: Tunawashukuru TCRA na serikali wamekuwa mstari wa mbele kutukutanisha kujadili masuala yenye manufaa kwetu

- Benson Bana: TBC tunaamini itafanya vema Rioba na timu yake walikuja huku Nigeria kujifunza na kuona wanavyoweza kuendeleza zaidi TBC...Tunaenda vizuri kama nchi.

- Mubelwa Bandio wa Marekani: Vitengo vya habari/ Kurugenzi za Habari serikalini zijitanue zaidi anasema 'sio kweli kwamba anachofanya Rais au Waziri kinatosha kuweka kwenye Press release ya ukurasa mmoja...anashauri vitengo vya Mawasiliano Serikalini viwezeshwe viwe kama media ndogo vitunze Text, video na audio na kuweka kwenye portal maalum mahali ambapo Waandishi wa habari au wananchi watapata taarifa kwa KINA juu ya nini viongozi Waandamizi wa nchi wanafanya...amesisitiza urasimu wa upatikanaji wa habari unapaswa kuondolewa.

Gamanywa: Maaadili yatiliwe mkazo ndiyo nguzo ya jamii thabiti.

WAZIRI NAPE: Tunatanua uhuru wa habari ila hiyo isiwe 'fungulia mbwa'[haya yangu] kwa wanataaluma kutenda makosa.

Nape anasema sasa hivi Mwandishi akipiga janga atakula na wa kwao badala ya adhabu kutolewa kwa Chombo chote cha habari kwa sababu ya mzembe mmoja aleshindwa kuzingatia maadili ya kazi.

Mratibu wa hii Symposium alikuwa jamaa mmmoja anaitwa H. Makundi ameendesha mjadala vizuri sana kwa mtazamo wangu.

MY TAKE:
Vijana tujitahidi kufuatilia mijadala hii ni muhimu kwa mustakabali mwema wa nchi yetu na vizazi vyetu.

Nawasilisha

N'yadikwa
 
Tanzania tuna idadi kubwa ya vijana wa hovyo sana. Wanaguswa na kuumizwa sana na maisha binafsi ya watu wa hovyo kuliko maisha yao wenyewe na maslahi yao.

Si rahisi kuwakuta wakijadili mambo kama haya.
 
Tanzania tuna idadi kubwa ya vijana wa hovyo sana. Wanaguswa na kuumizwa sana na maisha binafsi ya watu wa hovyo kuliko maisha yao wenyewe na maslahi yao.

Si rahisi kuwakuta wakijadili mambo kama haya.
Ndiyo bahati mbaya tuliyonayo huwezi kukutana na idadi kubwa ya vijana kwenye mijadala kama hii wengi wapo kwenye maisha binafsi ya artists yasiyokuwa na manufaa yoyote kwenye maisha yao ya kila siku...tofauti ya wenzetu Wanaijeria, wakenya na waghana huwa inatokea hapo...kwa kijana wa kitanzania ZAMA za leo ni taboo kujadili hard news wao mkazo upo kwenye soft news sports, entertainment, socialites nk
 
TBC ijitanue kwa nini BBC, CNN, DW, VOA, n.k zipo dunia kwa lugha tofauti tofauti.
Kwa nini na sisi wasiweke hata channel kwa matangazo ya lugha tofauti tofauti mfano kingereza, kifaransa,n.k ifike mahali na sisi tu expand sasa
 
Back
Top Bottom