Yaliyojiri Mikutano ya Dr. Magufuli, Dar es Salaam (Kigamboni, Mbagala, Temeke, Ubungo, Kinondoni)

R.B

JF-Expert Member
May 10, 2012
6,296
2,573
Mikutano ya Dkt. Magufuli leo Dar Es Salaam.

Kigamboni: Saa 3-4
Mbagala: Saa 5-6
Mwembeyanga: Saa 7-8
Ubungo: Saa 9-10
Biafra: Saa 10:30-12
=========
BIAFRA
Anaeongea kwa sasa ni Warioba na anasema utaratibu haujakiukwa, amesema hata yeye aligombea mwaka 95 na walikuwa 16 na utaratibu ulikuwa kutoa majina matano kutoka halmashauri kuu lakini kutokana na mazingira ikawekwa watu watatu na yeye alipunguzwa kwa sababu alikuwa namba nne, huo ndio utaratibu unaotumika hadi leo.

Anasema mgombea anaegombea kupitia UKAWA ni CCM na wanaomnadi ni CCM sasa iweje ameishiwa pumzi. Sasa anatoa sananu za kumpigia kura Magufuli.

Amesema kwanza anaifahamu Tanzania tofauti na wale wanaosema miaka 54 hakuna kilichofanyika, anajua mafanikio yake na matatizo yake na ameyafafanua. Pili amani na anatakiwa mtu ataeweza kutuimarisha.

Nyingine ni anahitajika mtu atakaedhibiti ufisadi, anapenda kutawala kwa sheria, amesema atampigia kura John Magufuli na anawaomba wampigie kura.

Magufuli: Anasema maisha yake yote ya kuwa waziri amekua mkazi wa Kinondoni, anasema laeo amepita majimbo matano lakini mapokezi ya Dar es Salaam ni makubwa na ya aina yake. Kubwa ni mji ulipambwa kwa benderea ikiwemo za CCM, CHADEMA na CUF na nyingi ni mpya kuashiria wanampokea Rais wa watanzania wote.

Anawapongeza CHADEMA ambao wameweka bendera na anaungana nao hivyo wampe power awe kiongozi wa awamu ya tano na anawapongeza CUF wampe haki Magufuli awe Rais wa awamu ya tano.

Kigamboni
k1.jpg k2.jpg

Mbagala

Mwembeyanga

Ubungo


Kinondoni
 
Aliwaambia wapige mbizi,leo na yeye aende Kigamboni kwa kupiga mbizi na zile pushapu zake azipigia kwenye maji kimo cha pua,analeta usanii na dhihaka!!

maCCM yalitupa msanii wa Bagamoyo na Msoga,sasa wanatuletea msanii wa Geita na Chato!!

******** eti hapa kazi tu wakati wahitimu wa vyuo hawana kazi na mitaani pia vibarua hakuna,kupiga pushapu ni kazi??!! kila pushapu moja kiasi gani??!!
 
sumaye ni mkorofi,,hata sura yake tu imekaa kikorofi korofi,,,,anapanga pia kwenda mwanza kuvuruga mkutano wa magufuli wa kuhitimisha kampeni....
 
Magufuli bhanaaaaa!!!!! Baada ya kutwambia wakazi wa Kigamboni, kama hatuna nauli, tupige mbizi; huna hata aibu kuja tena kutuomba kura! HATUDANGANYIKI!!!!!!!! Rais wetu ni Lowassaaaaaaaaa!!!!!!!!




lowassa anataka bandari iwe ya karamagi kama akiwa rais kwa sababu karamagi kamchangia hela za kampeni, sh 200 ya nauli ni kwa ajili ya maendeleo ya kivuko na hakuna aliyeshindwa kulipa, magufuli atapigiwa kura na wengi zaidi subiri uone, ukasimulie kwenu
 
Anakuja kweli kwa wapiga mbizi....??? Ingekuea nchi inayojielewa kama kenya wakazi wote kigamboni bila kujali chama wangemkataa adhalani....
 
Back
Top Bottom