Watu wanasoma. Tizama “views”.Yani Bavicha wamemsusa kabisa Mbowe?
Inakuwaje uzi wake una coments 30 tu?
... una maslahi gani na hii kesi?Asizengue kama last time out
Hapa sasa jamaa lazima aende haja.. Maswali yameanza sio ule ushuzi wa HilaKesi ya Ugaidi inayomkabili Freeman Mbowe na wenzake 3 inaendelea leo 18, Jan 2022 katika mahakama ya Uhujumu Uchumi na Rushwa.
Kufahamu ilipoishia, soma hapa:Yaliyojiri Mahakama Kuu kwenye Kesi ya Ugaidi inayomkabili Mbowe na wenzake watatu. Kesi imeahirishwa hadi Januari 18, 2022
Ungana nami katika uzi huu ili kujua kila kinachojiri Mahakamani.
UPDATES
Jaji ameingia Mahakamani, Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe inatajwa hapa Mahakamani
Wakili wa Serikali Robert Kidando: Ikupendeze Mheshimiwa Jaji naitwa Robert Kidando nipo pamoja na
wakili wa Serikali Pius Hilla
Abdallah Chavula
Jenitreza Kitali
Nassoro Katuga
Esther Martin
Ignasi Mwinuka
Tulimanywa Majige
Wakili Peter Kibatala: Mahakama hii Tukufu ikipendezwa, Majina yangu naitwa Peter Kibatala, Nipo Pamoja na;
Michael Lugina
Michael Mwangasa
Faraji Mangula
Nashon Nkungu
John Mallya
Fredrick Kihwelo
Alex Massaba
Khadija Aaron
Maria Mushi
Jaji anaita Washtakiwa Wote wanne na wote wanaitika wapo Mahakamani
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Shauri limekuja kwa ajili ya Kusikilizwa na Shahidi tukiyekuwa naye Jana, Amefika na yupo Tayari Kuendelea
Shahidi: anapanda Kizimbani
Jaji: Utetezi
Kibatala: tupo tayari kuendelea
Jaji: Shahidi nakukumbusha tangu Jana Uliapa na Leo Utaendelea Kuwa Chini ya Kiapo hicho
Wakili wa SerikaliPius Hilla: Mheshimiwa Jaji naomba Kukumbushwa tulipoishia Jana
Jaji: uliishia ambapo alisema Kuwa Mihamala ambayo ilihusika ni Kuanzia Tarehe 1 June 2020 Mpaka 31 July 2020
Na akasema aliringanisha report yake na Ile aliyopata Kutoka kwa Service Provider
Wakili wa Serikali: Shahidi Eleza report Yako Kwenda kwa wapelelezi iliambatana na Vitu gani
Shahidi: Vielelezo pamoja na Cover letter
Shahidi: Kutoka Forensic Beaural kwenda Kule ambapo Kesi Imetoka
Wakili wa Serikali: Cover letter inaandaliwa na nani
Shahidi: Inaandaliwa na Kamishna wa Uchunguzi, Kama hayupo inaandaliwa na kusainiwa na Wasaidizi Wake Kwa Niaba
Wakili wa Serikali: Madhumuni ya Barua hiyo, Covering Letter ni nini?
Shahidi: Ni Kutambulisha ile kazi niliyofanya kama Imetoka Kwa Kamishina Wa Forensic Beaural
Wakili wa Serikali: Shahidi Nikuulize, Katika zile Extraction Report ambazo Uliandaa, Unasema Zinatokana na Vielelezo Vipi
Shahidi: Vielelezo Vilivyo kuja Maabara ambazo ni Simu zilikuwa Ni Nane, Kwa Maana ya Vielelezo Vyenye Positive Results ni Simu Nne ambazo Ndiyo niliandalia report
Wakili wa Serikali: Ifahamishe Mahakama kati ya hizo su Nane, hizi Nne unazo Sema ni zipi
Shahidi: Simu ya Kwanza Nilikuwa Nimeipa Alama "E" Ilikuwa Stika Ya Rangi Ya Kijani ambayo tunatumia Maabara Ku label Vielelezo, Juu Nimeandika Kwa Mwandiko wangu, Ilikuwa ni simu aina ya Tecno
Wakili wa Serikali: Simu Nyingine Shahidi
Shahidi: Simu Nyingine Miliipa Alama "F" na Pia ni Stika ya Kijani, Niliandika Mimi Mwenyewe Kwa Mkono Wangu
Wakili wa Serikali: Ilikuwa Simu ya aina Gani
Shahidi: Ilikuwa ni Simu aina ya Itel
Wakili wa Serikali: Simu ya tatu Shahidi,
Shahidi: Niliipa Alama "G" na Yenyewe Ni Stika ya Kijani na Niliandika hiyo Herufi Kwa Mkono Wangu Mwenyewe
Wakili wa Serikali: Ni simu ya aina gani?
Shahidi: Ni simu aina ya Tecno
Wakili wa Serikali: Simu ya Nne Shahidi
Shahidi: Simu ya Nne Niliipa Alama "H" Pia ipo katika Stika ya Kijani na Niliandika Kwa Mkono Wangu Mwenyewe
Wakili wa Serikali: Ni simu ya aina gani
Shahidi: Ni Tecno pia
Wakili wa Serikali: Alama hizi ulikuwa unaziweka Sehemu gani?
Shahidi: Nilikuwa naweka Upande wa Nyuma ya Simu na Kwa zile Zenye Cover nilikuwa naweka Upande wa Nyuma na Kwenye Cover la Simu
Wakili wa Serikali: Kwanini kuwa unaweka alama hizo
Shahidi: Kwa ajili ya Utambuzi Wangu Mwenyewe
Wakili wa Serikali: Barua uliyoambatanisha na Vielelezo Utaweza Kuitambua
Shahidi: Ndiyo itakuwa na Sahihi yangu
Wakili wa Serikali: Nasemea Barua, Sisemei report Senior assistant Commissioner Of police NAFTALI JOSEPH
Wakili wa Serikali: Kitu Kingine
Shahidi: Pia itakuwa na Muhuri Kwa Niaba ya Kamishina
Wakili wa Serikali: Twende kwenye Nyaraka Nyingine, Report yako uliyotuletea wewe Mwenyewe, Ukiona Leo hii utaitambuaje
Shahidi: Ina Logo ya Jeshi la Police, Ina Majina Yangu, Ina sahihi Ya Kwangu, Ina Muhuri Ambao Umeandikwa Tanzania Police Forensic Beaural Dar es Salaam
Wakili wa Serikali: Kingine
Shahidi: Itakuwa na Kumbukumbu ya Maabara ambayo ni FB/CYBER /2020 /LAB/ 479
Wakili wa Serikali: Namna Nyingine ya Kutambua Report yako
Shahidi: Pia itakuwa na namba ya Kesi ambayo ni CD/IR/2027/2020
Wakili wa Serikali: Kingine?
Shahidi: Hizo ndiyo Features Kuu
Wakili wa Serikali: Twende Katika zile Extraction Report, Ieleze Mahakama Je Extraction Riport ya Simu Yenye alama E Ukiona Leo hii Utaitambuaje
Shahidi: Nitaitambua Kwa sababu Nakumbuka Baadhi ya IMEI
Wakili wa Serikali: Unakumbukaje
Shahidi: Kwanza Naomba Mahakama Inielewe Kuwa IMEI ni 14 Mpaka 16 Digits Kwa hiyo siyo Rahisi Kushika namba zote, Kwa hiyo Nilichofanya ni Kushika Namba za Mwanzoni na Mwishoni Kwa baadhi ya Vielelezo
Wakili wa Serikali: Ni Vyema Je Kwa Simu ya Alama E Ikoje
Shahidi: Ilikuwa ni simu ya TECNO nitataja Moja ambayo ni 35 na Namba Mbili za Mwisho ni 15
Wakili wa Serikali: Kigezo Cha Pili cha Kutambua Extraction Report ni Kipi
Shahidi: Ni Kutokana na Taarifa zilizopo Katika Report ambazo ni Kwanza Lazima Report itakuwa na Sahihi Ya Kwangu na Itakuwa na Muhuri Wa Tanzania, Forensic Beaural, Dar es Salaam, Itakuwa na Laboratory Namba
Wakili wa Serikali: Lab Namba Ngapi
Shahidi: LAB CYBER /2020 /479
Wakili wa Serikali: Kigezo Kingine katika simu hii
Shahidi: itakuwa na Majina yangu pia Kwa Maana ya Mchunguzi.. Kwa kuwa zile Documents Zinatokana na Mashine ya CELEBRITE, pia Itakuwa na Maneno CELEBRITE
Wakili wa Serikali: Twende Kwenye Extraction Report ya Simu uliyoipa alama F,
Shahidi: Niliona naweza Kuitambua Kwa Alama za IMEI, ambayo ni 35 na Inaishia na 05
Wakili wa Serikali: Kigezo Kingine Cha Kutambua Extraction Report ya Simu F
Shahidi: Ni sahihi ya Kwangu, Muhuri Wa Polisi Tanzania, Forensic Beaural Dar es Salaam, Itakuwa na Laboratory Namba
Wakili wa Serikali: Lab Namba Ngapi
Shahidi: LAB/CYBER /2020, 479 Wakili wa Serikali_ Kigezo Kingine
Shahidi: Itakuwa na Majina Yangu, Na Kutoka Imetoka na Mashine ya CELEBRITE itakuwa na Maneno CELEBRITE
Wakili wa Serikali: Twende Kwenye Extraction Report ya Simu uliyoipa alama G Shahidi: Report hii niliona Nitaitambua Kwa IMEI namba Mbili za Mwanzo no 35 na Mwisho Zilikuwa ni 40 Wakili wa Serikali: Namna Nyingine ya Kutambua Report yako
Shahidi: Kupitia sahihi ya Kwangu, Muhuri Wa Tanzania Police, Forensic Beaural Dar es Salaam, Kuwa na Laboratory Namba ambayo ni FB/CYBER/2020/479 Kwa kuwa Imetoka na Mashine ya CELEBRITE Itakuwa na Maneno CELEBRITE
Wakili wa Serikali: Na Extraction report ya Simu uliyoipa alama F Utaitambuaje
Shahidi: Kupitia IMEI namba ya 35 na Mbili za Mwisho ni 27
Wakili wa Serikali: Vigezo Vingine
Shahidi:,.Itakuwa na Sahihi yangu, Muhuri Wa Tanzania Police Forensic Beaural Dar es Salaam
Shahidi: Itakuwa na Majina yangu, itakuwa na Neno CELEBRITE sababu Imetoka kwenye Mashine ya CELEBRITE
Wakili wa Serikali: Elezea Mahakamani Uhalisia Wa Taarifa zilizopo Katika Report
Shahidi: Uhalisia wa Taarifa Zipo kama ambavyo zimetoka Katika Mashine, Kwa sababu Ya Mifumo ya Vifaa Vya Uchunguzi Inaruhusu Ku Read tu na siyo Tu kutoruhusu Bali ina Teknolojia ya WRITE BROCA
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Shahidi amesema anao uwezo wa Kutambua Nyaraka
Wakili wa Serikali anakusanya Nyaraka
Wakili wa Serikali: Shahidi Naomba utazame Nyaraka hizi
Shahidi anazichambua Moja Moja
Shahidi: Kwanza Ina Muhuri Kwa Niaba ya Kamishina Wa Uchunguzi wa Kisayansi, Ina sahihi Ya Kimishna Msaidizi wa Polisi NAFTALI JOSEPH, Ina Kumbukumbu ya Maabara, Ambayo ni FB /HQ/CYBER/R. 38/2021/VOLUME 21/300,
Wakili wa Serikali: Twende Kwenye Taarifa Yako
Shahidi: Ina Logo ya Police, Ina Kumbukumbu namba Kwa Maana ni Laboratory Namba ambayo ni FB/CYBER/LAB /479, Pamoja na Kesi namba CD IR 2097 2020, Ina Muhuri Wa Tanzania Police, Forensic Beaural Dar es Salaam, Pia Ina Majina Yangu Pamoja na Sahihi Yangu
Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama Kwa Ujumla Wake ni Kitu gani
Shahidi: Nyaraka hizi Mheshimiwa Ni Nyaraka ambazo niliziandaa Mwenyewe na Ninazitambua
Wakili wa Serikali: Kwa Jina La Jumla Unaziitaje
Shahidi: Report Ya Uchunguzi Niliofanya
Wakili wa Serikali: Katika Report hiyo Kuna Nyaraka zipi
Shahidi: Kuna Taarifa ambayo niliyoiandaa, Kuna Extraction Report ya Simu Nne Kama Nilivyo Eleza
Wakili wa Serikali: Jana Ulielezea Viambatanisho Katika Taarifa Yako Je ni Viambatanisho Vipi ambavyo havipo hapo
Shahidi: Taarifa Ya Airtel na Taarifa Ya Tigo
Wakili wa Serikali: Vipo wapi
Shahidi: Jana Vilitolewa Mahakamani Hapa
Wakili wa Serikali: Kwenye hizi Nyaraka ambazo zipo Mbele Yako, Covering Letter Umeitambuaje
Shahidi: Kwanza Ina Muhuri Kwa Niaba ya Kamishina Wa Uchunguzi wa Kisayansi, Ina sahihi Ya Kimishna Msaidizi wa Polisi NAFTALI JOSEPH, Ina Kumbukumbu ya Maabara, Ambayo ni FB /HQ/CYBER/R. 38/2021/VOLUME 21/300,
Wakili wa Serikali: Twende Kwenye Taarifa Yako
Shahidi: Ina Logo ya Police, Ina Kumbukumbu namba Kwa Maana ni Laboratory Namba ambayo ni FB/CYBER/LAB /479, Pamoja na Kesi namba CD IR 2097 2020, Ina Muhuri Wa Tanzania Police, Forensic Beaural Dar es Salaam, Pia Ina Majina Yangu Pamoja na Sahihi Yangu
Wakili wa Serikali: Twende Kwenye Extraction Riport ya Simu uliyoipa alama E
Shahidi: Ni IMEI 335 KWA Maan ya 35 na Mwisho ni 45
Wakili wa Serikali: Vigezo Vingine,
Shahidi: Ina Muhuri Wa Tanzania Police Forensic Beaural Dar es Salaam Ina Sahihi Yangu, Majina Yangu, Laboratory Namba
Wakili wa Serikali: Lab Namba Ngapi
Shahidi: FB/CYBER /2020 /LAB /479
Wakili wa Serikali: Twende Kwenye Extraction Riport ya Simu uliyoipa alama F
Shahidi: Ni hii hapa na part ya IMEI namba ni 35 na Mbili za Mwisho ni 05
Ina signature ya Kwangu, Muhuri Wa Tanzania Police Forensic Beaural Dar es Salaam, Ina Majina Yangu, Ina laboratory Namba ambayo ni FB /CYBER /2020 /LAB /479
Wakili wa Serikali: ina kitu gani Kingine
Shahidi: Neno CELEBRITE
Wakili wa Serikali: Linaonekana Sehemu gani
Shahidi: Kulia juu
Wakili wa Serikali: Twende Kwenye Extraction Riport ya Simu uliyoipa alama G
Shahidi: Ni hii hapa na Ina Features za IMEI namba za Mwanzoni ni 35 na Mwishoni ni 40
Wakili wa Serikali: Vigezo Vingine
Shahidi: ina sahihi ya Kwangu, Tanzania Police Forensic Beaural Dar es Salaam na Majina yangu, Sahihi Yangu na Lab Namba FB/CYBER /2020 /LAB /479
Wakili wa Serikali: Twende Kwenye Taarifa Nyingine
Shahidi: Ni hii Extraction Report ya Simu niliyoipa alama G
Wakili Peter Kibatala: MHESHIMIWA JAJI, Nimewanong'oneza mawakili wa serikali lakini naona Wa naendelea tu, Shahidi anasoma content za ndani ya nyaraka badala ya utambuzi
WS Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji labda Kama Wakili afuatilii
Kibatala: Inawezekana Kweli Nilisinzia, Lakini Mheshimiwa Jaji Ndiyo Shahidi anasoma na Kumbukumbu namba na Lab Namba Kweli? ndiyo Utaratibu huo?
WS Pius Hilla: Mheshimiwa Jaji naelewa Concern Yake, Lakini Nature ya Content katika hili linataka ataje alama ambazo ni Namba
Kama Lab Namba na IMEI namba, Hii ni description Ya Nyaraka hizi, Mheshimiwa Jaji Ukiangalia Kwa Maana hii siyo Content, Kwa Kutaja Namba za IMEI za Kwanza na Mwisho sidhani kama ina Violates na Kuzuia Admission ya Vielelezo
Jaji: Namna nzuri ya kwenda Ni Kwamba anachokisema ni Kile alichosema Wakati wa Identification, Kitu ambacho Mahakama Ingekuwa Karibu angeonyesha..Kilichopo katika Documents ni Reference Ya Kile alichokitaja..
Kibatala: Kwa Ruhusa Yako Wacha tu aendelee
Jaji: Kama naona Sawa Sawa alikuwa anaelekea Kwenye Kielelezo Cha Mwisho
Wakili wa Serikali: Shahidi Tulikuwa kwenye Nyaraka ya Mwisho, na Vigezo Uliyotumia Kutambua
Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama Unaiomba Kufanya Nini katika hizi Nyaraka ulizotambua
Jaji: Nyaraka zipo Ngapi
Wakili wa Serikali: Zipo Sita
Jaji: H bado hajaitambua
Wakili wa Serikali: Hebu ieleze Mahakama Kwamba Sasa Extraction Report ya Simu uliyoipa alama H Kama Ipo
Shahidi: Ndiyo ipo
Wakili wa Serikali: Unaitambuaje
Shahidi: Part ya IMEI namba zipo hapa Kwa Maana ya 35 Mwanzoni Pamoja na 27 Pia kuna sahihi ya Kwangu, Kuna Muhuri Wa Tanzania Police Forensic Beaural Dar es Salaam, ina Majina yangu, Ina Lab Namba FB/CYBER /2020 /LAB /479
Kingine ni Mwonekano wa CELEBRITE
Wakili wa Serikali: baada ya Utambuzi wa Nyaraka hizi Unaiomba nini Mahakama
Shahidi: Naomba Nyaraka hizi zipokelewe Kama USHAHIDI wangu
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji naomba Kukabidhi Vielelezo Shahidi amenyoosha Mkono wake
Jaji: Ndiyooo
Shahidi: Mheshimiwa Jaji nilinyoosha Mkono, Naomba Kwenda Chooni
Kibatala: Mhe Jaji Hatuna Pingamizi Kwa hilo ni katika hali ya Ubinadamu, ila kwa kuwa Yupo Katika Kizimba naomba asindikizwe na Askari Polisi Pamoja na Magereza
Jaji: Sawa Nenda Lakini Utasikindikizwa na Askari Magereza, pamoja ni Inspector lakini ni Inspector ambaye ni Shahidi
Wakati huo Jopo la mawakili wa utetezi wameizunguka nyaraka zilizotolewa na shahidi... Wanazikagua.
Shahidi amesharejea kutoka chooni na sasa amepanda tena kizimbani tena
Wakili Nashon Nkungu: Mheshimiwa Jaji Kwa niaba ya Mshtakiwa wa kwanza Sina Pingamizi Wakili
John Mallya: Kwa niaba ya Mshtakiwa Wa Pili sina Pingamizi
Wakili Fredrick Kihwelo: Mheshimiwa Jaji Kwa niaba ya Mshtakiwa wa tatu Sina Pingamizi
Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji Kwa niaba ya Mshtakiwa wa Nne hatuna Pingamizi Nyaraka zinachukuliwa na Makarani na Kupandishwa Kwa Jaji
Jaji: tuliishia Kielelezo Namba Ngapi? 21 siyo?
Jaji: Kwenye hizi Report, Nitumie IMEI namba au nini Sababu hizo Mark za E au F zina Appear Kwenye hizi report?
Shahidi: Hapana
Jaji: Kila Moja tunapata Namba Yake atuwezi Ku admits as a group
Wakili wa Serikali: Kwa IMEI Mheshimiwa Jaji
Jaji: Samahani Shahidi Naomba Usogee hapa
Shahidi: anaenda Mezani Kwa Jaji na Kushika Nyaraka
Jaji: Tuanze na E
Shahidi: E Ilikuwa 35 na 40 Mwisho
Jaji: ya F?
Shahidi: ilikuwa 35348.. 05
Shahidi: G ilikuwa 35........
Shahidi: na H ni 35.....27
Naona kama sauti hazitoki kwa Ufasaha Zoezi halisikiki kwa uzuri, Kidogo pana Ugumu Jaji na Shahidi Wapo Pale Mbele Mezani Kwa Jaji wanaseana IMEI namba huku Mbele Hatusikii Chochote... Tunaendelea kusubiri..
Shahidi amemaliza zoezi aliloitiwa Kwa Jaji anashuka Kutoka Mbele Mezani anarejea kizimbani
Jaji: Kuna Karatasi Hapa, Tusaidie Ipo kwenye Nyaraka ipi? Shahidi anatoka Kizimbani anaenda Mezani Kwa Jaji Kuchambua Makaratasi Amemaliza na kurudi, Karani anabana na stapler
Jaji: Baada ya Kusikiliza Pande zote Mbili, Nyaraka zinapokelewa kama ifuatavyo Report ya Uchunguzi Kutoka Forensic Beaural ni Kielelezo namba 22 Report ya Uchunguzi Kielelezo namba 23 Extraction Report ya Simu IMEI 365029115930845 Kielelezo namba 24
Extraction Report ya SIMU IMEI 353487133305 Kielelezo namba 25 Extraction Report ya SIMU IMEI namba 358821101132040 Kielelezo namba 26 Extraction Report ya SIMU IMEI namba 352386071165127 Kielelezo 27
Shahidi anasoma sasa Nyaraka zote Kama Ulivyo Utaratibu Wa Mahakama Kupitia Sheria ya Ushahidi
Jaji: Kwa sababu ya Muda mnaonaje asome sehemu pekee ambazo aliomba na Barua badala ya Kusoma kila kitu?
Wakili wa Serikali Pius Hilla: Shahidi Umesikia Maelezo ya jaji?
Jaji: Soma kwenye reference za Barua
Shahidi: Nikiwa nasoma Mawasiliano yaliyokuwa yanaingia na kutoka
Je ni some yote au in summary?
Jaji: Soma in summary
Shahidi amemaliza kusoma Kielelezo namba 26 bado kielelezo kimoja..
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji naomba tupumzike, maana ni saa saba sasa
Jaji: Mnasemaje
Kibatala: Kibatala ni bora tuvumilie, tu' break Kwa ajili ya Cross Examination baadae..
Jaji: Basi amalizie kielelezo namba 27
Shahidi amemaliza sasa kusoma kielelezo cha 27, na amemaliza kusoma vielelezo vyote
Wakili wa Serikali: Mhe Jaji naomba tuhairishe turudi kuendelea baadae
Jaji: turudi saa ngapi?
Kibatala: turudi saa 1:55
Jaji: basi tunaenda break ya dakika 45 na tutarejea saa saba na dakika 55
=======
Jaji amerejea Mahakamani Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe inatajwa
Wakili wa Serikali: Mhe Jaji Quorum ya Uoande wa Serikali Ipo Kama awali
Wakili Kibatala: Mhe Jaji sisi tupo Kama tulivyo kuwa hapo awali na tupo tayari Kuendelea
Jaji: Kwa Mara Nyingine tena nakukumbusha upo chini ya kiapo
Wakili wa Serikali: Shahidi nitaendelea Kukuuliza Maswali.. Zile simu kabla ya Kurejesha Kwa Mpelelezi ililiwaje
Shahidi: Nili hifadhi Kwenye Roka Langu
Wakili wa Serikali: Ulihifadhi Kwenye Kiwango gani
Shahidi: Nili hifadhi Kwenye plastic Bag, Na kuseal, Kwa Juu nikaandika Majina yangu na Tarehe
Wakili wa Serikali: uli Seal Kwa Kutumia nini.?
Shahidi: Kwa Kutumia Tape
Wakili wa Serikali: Kwanini Uli seal, Elezea Mahakama
Shahidi: Nilitaka ziwe Intact (Salama)
Wakili wa Serikali: Jana pia Ulielezea Kuwa Ulihifadhi, Je ni lini tena Ulikuja Kuziona
Shahidi: Nilikuja Kuziona Siku ya Jana Tarehe 17
Wakili wa Serikali: Ifahamishe Mahakama Ilikuwaje
Shahidi: Ijumaa wiki iliyopita nilipigiwa simu na Inspector Swila, Kwamba nahitajika kuja Kutoa Ushahidi, Kutokana na Uchunguzi niliofanya, Na Baadae Katika Kumuuliza ni Uchunguzi unaotokana na Lab Namba Ngapi akaniambia 479 ya 2020
Wakili wa Serikali: baada ya kukutajia namba Ukafanya nini
Shahidi: Nilienda Kuangalia kwenye Register Ya Maabara Kuhusu Kesi Inayo toka Kwa DCI Baadae simu ya Jumatatu, nikawasiliana naye akawa kaniletea Vielelezo
Wakili wa Serikali: alikuletea Vielelezo wapi
Shahidi: Forensic Beaural
Wakili wa Serikali: ieleze Mahakama sasa hiyo Jumatatu ya Jana Swila alikuletea Vielelezo Vipi
Shahidi: Ni simu
Wakili wa Serikali: Simu Ngapi
Shahidi: Simu Nane
Wakili wa Serikali: Uliweza Kuvionaje
Shahidi: Sababu niliweka Kwenye Bag ambalo Transparent
Shahidi: Niliangalia Zile Stika na Attachment Fomu yake ambayo ni PF 109
Wakili wa Serikali: Baada ya Kukabidhiwa na Swila Ulifanya nini
Shahidi: Nili hifadhi Kisha Nikaja navyo Mahakamani
Wakili wa Serikali: Hali ya seal Ilikuwaje
Shahidi: Ilikuwa kama Nilivyo weka, Niliona Majina yangu Bado yapo pamoja na Tarehe, Niliona Pia Maandishi yaliyoongezwa Juu ya Bahasha Yameandikwa Kwa Maker pen
Wakili wa Serikali: Ulihifadhi Kwenye nini
Shahidi: Bag langu
Wakili wa Serikali: Kwa nini kwenye Begi lako
Shahidi: Ili viwe Kwenye Possession yangu
Wakili wa Serikali: Ukaenda navyo wapi
Shahidi: Ni kaja navyo Mahakamani
Wakili wa Serikali: Kwa Makusudi ya kutolea Ushahidi
Wakili wa Serikali: Ilikuwaje sasa hiyo Jana
Shahidi: Kutokana na Changamoto za Ki Afya Zoezi halikukamilika
Wakili wa Serikali: Baada ya Zoezi Kutokamilila ilikuwaje
Shahidi: Nilirudi navyo Ofisni nikavihifadhi kwenye Roka Langu
Wakili wa Serikali: Ofisini Wapi
Shahidi: Forensic Beaural, Ofisi Ndogo za Dar es Salaam Kitengo Cha Cyber Crime
Wakili wa Serikali: Ulihifadhi Mpaka Lini
Shahidi: Mpaka Leo Asubuhi ambapo Nilivichukua wakati Nakuja Mahakamani
Wakili wa Serikali: Hivi sasa Vielelezo hivyo Vipo wapi
Shahidi: Ni navyo Kwenye Begi langu
Wakili wa Serikali: Begi lipo wapi
Shahidi: Begi ninalo hapa
Wakili wa Serikali: Endapo Utatoa Vielelezo Kutoka Kwenye Begi lako vitakuwa na Alama zipi
Shahidi: Zitakuwa na Alama A, B, C, D, E, F, G, na H
Wakili wa Serikali: Alama hizo ni za Namna gani
Shahidi: Alama ambazo zipo Kwenye Stika ya Kijani ambapo Niliandika Kwa Mkono Wangu
Wakili wa Serikali: Hebu ieleze Mahakama endapo Unakumbuka Ni simu za aina gani
Shahidi: Techno zilikuwa Nne, Itel Mbili, Samsung Moja na Moja ni Bundy
Wakili wa Serikali: Kwenye Kila simu Ala ulizo weka wewe ni zipi
Shahidi: zilikuwa na Kikaratasi Kilichoandikwa PF 145
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji naomba Sasa Shahidi apewe Begi lake aweze Kutuonyesha Vielelezo
Wakili wa Serikali: Shahidi Ieleze Mahakama Parcel Unayo Fungua ni Vitu gani
Shahidi: Hizi ni simu mbalimbali
Wakili wa Serikali: Nini kinachokutambulisha
Shahidi: Kuna Majina Yangu Sehemu ambayo Imeandikwa" SEALED BY" Na Tarehe, 09 July 2021
Wakili wa Serikali: Kitu gani Kingine
Shahidi: Ni Vile Vikaratasi ambavyo vilikwepo tangu Siku ya Kwanza PF 145 ambapo Vina namba ya Kesi, Vyote Vilikuwa na namba ya Kesi CD IR 2097 2020
Wakili Kibatala: Mheshimiwa Jaji Samahani, Hebu turudi Nyuma Kama Kuna sehemu alitaja Kwa Kifupi hiyo Kumbukumbu namba ya Kwenye stika
Jaji: Wewe Kumbukumbu zake Zinasemaje
Kibatala: alitaja zote full FB/CYBER /2020 /LAB..
Jaji: Kama nimesikia Vizuri amezungumzia Kwenye Ile Green Label Aliandika tena hiyo LAB Namba Kwa Ufupi, Hoja Yangu sasa Je Wakati anafanya Identification alitaja hiyo Kwa Kifupi?
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji shahidi anatoa simu nane VIELELEZO (SIMU) zinakwenda kwenye Jopo la mawakili wa utetezi kuziangalia vizuri Jopo la mawakili wa utetezi wamezunguka vielelezo kwa pamoja
Wakili wa Serikali: Shahidi Sasa Unaiomba nini Mahakama Kuhusiana na Vielelezo Hivi
Shahidi: Naiomba Mahakama Kwamba Hivi Ndiyo Vielelezo Nilivyo fanyia kazi na Taarifa niliyotoa Imetokana na Vielelezo Hivi, Naomba Mahakama Ipokee Kama Ushahidi Wangu
Wakili Nashon Nkungu: Kwa Niaba ya Mshtakiwa Wa Kwanza Mheshimiwa Jaji Hakuna Pingamizi
Wakili John Mallya: Kwa niaba ya Mshtakiwa wa Pili Hakuna Pingamizi
Wakili Fredrick Kihwelo: Kwa Niaba ya Mshtakiwa wa tatu Hatuna Pingamizi
Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji Kwa niaba ya Mshitakiwa Wa Nne hatuna Pingamizi
Karani anachukua Kifurushi cha Simu Kwenda Mezani Kwa Jaji
Jaji: tunapokea Jaji anamuita shahidi Kwenda Mezani Kwake Kuviorodhesha
Shahidi anamueleza Jaji Kuwa vielelezo vina seal Karani wa mahakama amekuja na mkasi, Wanakata Seal na kumkabidhi shahidi Vielelezo vyake
Jaji: Mahakama inapokea simu aina ya Tecno yenye stika ya Green A Kama Kielelezo Namba 28 Simu aina ya Samsung yenye Green B Kama Kielelezo namba 29 Simu aina ya Bundy Green C Kama Kielelezo namba 30 Simu ya Itel yenye Green D Ka Kielelezo namba 31
Simu aina ya Techno Yenye Stika ya Green E Kama Kielelezo namba 32 Simu aina ya Itel yenye Stika green F kama Kielelezo namba 33 Simu aina ya Techno Yenye Stika ya Green G kama Kielelezo namba 34
Simu aina ya Techno Yenye Stika ya Green H kama Kielelezo namba 35 Wakili wa Serikali Pius Hilla: Mheshimiwa Jaji sina Swali zaidi Kwa Upande wangu
=======
Nashon Nkungu: Shahidi Nilikusikia Sawasawa Kwamba Unamiaka 37. Kwani Jeshi la Polisi Una Staafu Ukiwa na Miaka Mingapi
Shahidi: Sifahamu
Nashon: Wewe ni Mstaafu wa Jeshi la Polisi
Shahidi: Hapana
Nashon: Juzi Ijumaa Tuliambiwa wewe Shahidi Unayefuata ni Mstaafu na Unamuuguza Mzazi wako Handeni
Shahidi: Si Za Kweli
Nashon: Je wewe Ndiyo Utakuwa Ulitoa Taarifa za Uongo?
Shahidi: Sijawahi Kutoa Taarifa za Namna hiyo
Nashon: Ulisoma Kitu gani IFM
Shahidi: Advanced Diploma in Computer Since
Nashon: Ni sahihi Kuwa Umesomea Hacking
Shahidi: Mimesomea Ethical Hacking
Nashon: Ulitaja Jina la Uliposomea Hacking
Shahidi: Nilitaja
Shahidi: Nitakuwa Sahihi nikisema Hacking ni Udukuaji wa Taarifa Za Mtu Mwingine
Shahidi: Kwa Maneno Yako
Nashon: Jibu ni yes au No
Shahidi: Jibu siyo Yes au No inategemea
Nashon: Je ni Kweli Hacker anaweza Kuingilia Taarifa na Kuzibadili,
Nashon: Je Hacker anaweza Kuingilia Kifaa hata Kama Kina Password
Shahidi: Possible
Nashon: Je inawezekana Kifaa hicho kikawa Kina Version ambayo ni latest
Shahidi: Sijaelewa Swali
Nashon: Ulimwambia Mheshimiwa Jaji ulinzi wa kile chumba?
Shahidi: Hapana
Nashon: Ulimwambia Mheshimiwa Jaji kwamba kifaa hata kikiwa na Password unaweza kupata Access na ukaingia
Shahidi: hapana
Nashon: Ni sahihi kuwa ulikaa na taarifa hadi 2.7.2021 ndipo ukaaanza kufanyia uchuguzi?
Shahidi: sikusema hivyo
Nashoni: Kwa majibu wa Ushahidi wako ulipopokea 13.8.2020 ukaweka kwenye locker lako hadi 1.7.2021?
Shahidi: sio kweli
Nashoni: Kutokana na Ushahidi kuacha 1.7.2021 ambayo ndio ulijibiwa barua ni kitu gani ulifanya hapo katikati?
Shahidi: Mheshimiwa 1.7.2021 ndio nilianza kuomba taarifa
Nashoni: Ni muda gani tangu umepokea taarifa?
Shahidi: miezi 10
Nashon: Kwanini hukutoa taarifa ya kutofanyia kaz hivyo vifaa?
Shahidi: nilitoa
Nashon: Unajua kutofanyia kazi kwa muda wote inasababisha Vielelezo kuwa na mashaka?
Shahidi: Sifahamu
Nashoni: Hatua ya kwanza kuchukua ni kuomba data.. ilifanyika tarehe 1 majibu yakaja tarehe 2 kaz ilifanyika siku moja?
Shahidi: tarehe 1 na mbili nilifanya kazi
Nashoni: Ni kawaida Upelelezi kufanyika ndani ya siku1?
Shahidi: Uchunguzi wa nini?
Nashon: wa kile mlichokua mnachunguza
Shahidi: kimya
Nashon: wewe ni Askari unafahamu PGO?
Shahidi: HAPANA
Nashon: unafahamu PGO imeweka utaratibu wa ku label Vielelezo?
Shahidi: Nafahamu
Nashon: PGO imeweka utaratibu wa ku' label Vielelezo kutoka afisa mmoja kwenda mwingine?
Shahidi: sahihi
Nashon: Mheshimiwa Jaji naomba package ya Exhibit from 28_33
Nashon: Shahidi unafamu PF 135
Shahidi: nafahamu kwa kuona
Mboe lazima atalipia kwa matendo yake maovu ya kuvuruga amani ya nchi yetu.Acha upungufu wa matumizi ya akili wakunyooshewa kidole ni wale Kwa makusudi walihatarisha usalama wake, ili kumdhoofisha na kushindwa kuhakikisha usalama wa maisha yake na mali zake.
Masaburi akili zake ni mavi! amka acha kutumia masaburi . Au ubongo ulimkabithi aliyelala futi sita kule chatoDhamira ya mboe ilikuwa ni kuvuruga amani na utulivu wa nchi kwa kuwatumia watu waliopata mbinu za kijeshi.
vitendo vya kuvuruga amani ya nchi ni ugaidi.Kwa hiyo sasa umebadili siyo ugaidi tena. Duu!
Kama ulidhani utanufaika na matendo maovu ya mboe basi unapaswa ujue kuwa mwisho wake umefika, wewe uliye ponea chupu chupu ni bora kwa sasa utubu maovu yako.Masaburi akili zake ni mavi! amka acha kutumia masaburi . Au ubongo ulimkabithi aliyelala futi sita kule chato
Una akili timamu- ok kwa kifupi ni hivi wazazi wake na Mbowe walihamia kutoka Malawi baada ya kuwadhurumu wazazi wangu mali na kuhamia Moshi.... una maslahi gani na hii kesi?
Tulia kwanza kwa muda kidogo .....sasa andika vizuri jina la Mbowe...ni hilo tu sina la ziada..Mboe lazima atalipia kwa matendo yake maovu ya kuvuruga amani ya nchi yetu.
Asizengue ndio nini warundi mpo wengi humu.Asizengue kama last time out
Wa kutubu ni wewe uliyezoea kuua na kupoteza watu! Your days are numbered!kama ulidhani utanufaika na matendo maovu ya mboe basi unapaswa ujue kuwa mwisho wake umefika, wewe uliye ponea chupu chupu ni bora kwa sasa utubu maovu yako.