Yaliyojiri Mahakamani kesi ya Mbowe na wenzake: Upande wa Utetezi waanza kutoa ushahidi. Kesi yaahirishwa mpaka 26 Novemba, 2021

mulwanaka

JF-Expert Member
Feb 19, 2017
5,138
2,000
Kumbe Kibatala ni dhaifu kiasi hiki- INFERIORITY COMPLEX

Peter Kibatala: Hatari ninayoona hapa Kwamba Kuna watu wanajiona wao ni bora Kuliko Wengine, Kesi Ya Mtobesya Vs DPP hawa waendesha Mashtaka Walishapewa Agizo kuwa sisi wote ni Mawakili hakuna aliye Juu Mahakamani..

Kibatala: Mahakama hapa Imeshatoa Rulling ndiyo Maana Hapa Mtobesya ameacha Kufanya Submission kwa Maelekezo Yako, halafu anasimama Mtu Mbele yako akijua Kuna Amri ya Mahakama na Kuanza Kuku' challenge wewe wakati Mahakama Yako ipo Funtus Officio..
Nimesha gundua we ni shabiki tu huna hoja, kabisa hapo kabatali alicho ongelea kina mashiko.
 

FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
25,604
2,000
Wakili FREDRICK kihwelo: Mheshimiwa Jaji tutapinga anachokifanya

WS: Mheshimiwa Jaji naongelea Kuhusu Competence ya Barua, Wanaogopa nini na wao Walikuwa wanafanya

Jaji: Nilisema Nini Kuhusu Content,

Mtobesya: Mahakama Ilisema Kwamba tunaweza Kuangalia Jina na Force Namba,

Mtobesya: Lakini Siyo Kwenda Kwenye Content
ha ha ha, yamewakuta nao kuhusu Content.
 

Lyamber

JF-Expert Member
Jul 24, 2012
10,591
2,000
Kesi imeisha
1. wamekiri kukusanywa na kumfahamu Mbowe
2. wamekiri kwenda Moshi
3. wamekiri kufanya mikutano na Mbowe kwenye maeneo yanayomilikiwa na Mbowe
Hizo ni ingridient za kesi ya Jamhuri
Kwaio hizo ingridients ndo zinaleta nia ya kufanya ugaidi? Intent to commit terrorism mdogo wangu umesoma chuo gani?
 

ostrichegg

JF-Expert Member
Jun 30, 2013
11,507
2,000
shahidi kafundishwa kuja kusema maneno ya kutia huzuni mahakamani akifikiria yatamuokoa yaani hata aseme alilishwa mavi jela iko palepale hao ni magaidi
Hiyo ni lugha ambayo imekuwa ikitumiwa sana na watesi/madhalimu na HASA mawakala wao, ILI kutisha wapigania haki.
Ninaamini kuwa hilo ni SWALA la muda tu, kwani ukweli na haki ndio vitakujashinda na hatimae kutawala taifa hili. AMEN
 

comte

JF-Expert Member
Dec 11, 2011
4,405
2,000
Mawakili wa Mbowe na wenzake wamepelekewa moto wanakula matapishi yao

Jaji: endelea tu, Nimesha andika hicho Ulichosema

WS Abdallah Chavula: Asante Mheshimiwa Jaji

WS: Mheshimiwa Jaji Shahidi amesema Kwamba alimuelekeza Wakili Wa Mshtakiwa Wa Tatu, Wakili wa Mshtakiwa wa Nne akaalikwa na Wakili wake

WS: Akayatoa Yale ambayo alitaka Yafanywe na Wakili wake, Katika Hali ya Kustaajabisha, Katika Uandishi wa Barua ambayo yeye alielekeza Haikuandikwa na yeye wala Wakili wake Bwana Fredrick Kihwelo, Ikaenda Kuandikwa na Bw. Kibatala, Wakili wa Mshtakiwa Wa Nne

WS: Mheshimiwa Jaji Sote tunafahamu, Awali Kaka zetu na Dada zetu Wasomi MAWAKILI Walikuwa wanawatetea washtakiwa Wote wanne Kwa umoja wao, Waliacha Kuwatetea Washtakiwa wote kwa Umoja wao Baada ya Kuonekana Kuna Mgongano wa Kimaslahi..

Kwamba Hivyo hawawezi Kuwatetea Washtakiwa Wote Kwa Pamoja bila Kuacha Athari..

Wakili Fredrick Kihwelo: Mheshimiwa Jaji Tunamuomba Kama ana meneno Mengine ya Kutumia atumie, Hicho anachokisema Siyo Jambo Letu....

Wakili Peter Kibatala: Kama ana submit Pingamizi Jipya hapo Lisajiliwe kuwa ni Pingamizi Jipya, kwa sababu Sisi tunaguswa Kama Upande wa Mshitakiwa Wa Nne....

WS: Mheshimiwa Jaji Hakuna Pingamizi Jipya Hapo, Na Amri ya Mahakama ipo wazi Kwamba palikuwa na Mgongano Wa Maslahi ya Haki za wateja
 

MASHANJARA

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
284
500
Jaji ni Mpumbavu toka siku ya kwanza ona anasimama Kama shahidi wa mashitaka. Alioni aibu anasema mtuhumiwa AMEFUNDISHA kujibu Kisa atetemeki kujibu au? Anajibu kwa ufasaha sababu yeye ndiyo aliyepigwa anaeleza kitu halisi. Siyo mashahidi wake wa kufundishwa.
Inasikitisha Judge anavyoonyesha waziwazi kuwagandamiza kina Mbowe! Inasikitisha kwamba kumbe askari wa JWTZ, tena makomandoo wanaweza kusingiziwa, kunyanyaswa, kuonewa na hata kudhulumiwa na polisi wenye rekodi chafu ya utumishi kama Mahita baba na sasa kwa bahati mbaya sana, Mahita mtoto, kina Jumanne na wengine bila consequence? Hivi polisi wanaoweza kutenda uovu huu kwa wanajeshi kwa raia wa kawaida itakuwaje? Kuna lutakalofuata stay tuned.
 

Kohelethi

JF-Expert Member
Mar 8, 2013
2,481
2,000
Inasikitisha Judge anavyoonyesha waziwazi kuwagandamiza kina Mbowe! Inasikitisha kwamba kumbe askari wa JWTZ, tena makomandoo wanaweza kusingiziwa, kunyanyaswa, kuonewa na hata kudhulumiwa na polisi wenye rekodi chafu ya utumishi kama Mahita baba na sasa kwa bahati mbaya sana, Mahita mtoto, kina Jumanne na wengine bila consequence? Hivi polisi wanaoweza kutenda uovu huu kwa wanajeshi kwa raia wa kawaida itakuwaje? Kuna lutakalofuata stay tune.

Inasikitisha Judge anavyoonyesha waziwazi kuwagandamiza kina Mbowe! Inasikitisha kwamba kumbe askari wa JWTZ, tena makomandoo wanaweza kusingiziwa, kunyanyaswa, kuonewa na hata kudhulumiwa na polisi wenye rekodi chafu ya utumishi kama Mahita baba na sasa kwa bahati mbaya sana, Mahita mtoto, kina Jumanne na wengine bila consequence? Hivi polisi wanaoweza kutenda uovu huu kwa wanajeshi kwa raia wa kawaida itakuwaje? Kuna lutakalofuata stay tuned.
Mkuu kila anayependa haki na kulitakia taifa mema anajiuliza Hilo swala ulilojiuliza hapo. Ni Mambo ya Aibu na kusikitisha sana. Alafu wanajiona wanaweza kufanya chochote wanachotaka. Na kwamba wanaweza kujitawala pasipo MUNGU. Ndiyo maana wanapanga Maovu. Kutesa .kuteka na kuuwa watu.
 

MIGNON

JF-Expert Member
Nov 23, 2009
3,884
2,000
Kesi imeisha
1. wamekiri kukusanywa na kumfahamu Mbowe
2. wamekiri kwenda Moshi
3. wamekiri kufanya mikutano na Mbowe kwenye maeneo yanayomilikiwa na Mbowe
Hizo ni ingridient za kesi ya Jamhuri
Haswaaaa,kesi imeisha kabisa,ni mvua za kutosha tu!
 

Freyzem

JF-Expert Member
Jun 29, 2013
8,967
2,000
Kesi imeisha
1. wamekiri kukusanywa na kumfahamu Mbowe
2. wamekiri kwenda Moshi
3. wamekiri kufanya mikutano na Mbowe kwenye maeneo yanayomilikiwa na Mbowe
Hizo ni ingridient za kesi ya Jamhuri

Wamekiri kufanya ugaidi...!?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom