Yaliyojiri Mahakamani kesi ya Mbowe na wenzake: Shahidi wa 13, Tumaini Sostenes Swila kuendelea kutoa ushahidi wake Februari 08/2022

Habari Wakuu,


Leo 07/ 02/ 2022 shahidi wa 13 anatarajiwa kuendelea kutoa ushahidi wake kwenye kesi inayomkabili Mbowe na wenzake 3.

Kujua Kesi ilipoishia fungua kiungo hiki: Yaliyojiri kesi inayomkabili Mbowe na wenzake leo Februari 4, 2022. Kesi imeahirishwa. Shahidi wa 13 kuendelea kutoa ushahidi Februari 7, 2022

Updates:

Jaji ameingia

Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe inatajwa hapa Mahakamani Muda huu

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Ikupendeze naitwa Robert Kidando nipo pamoja na
  • Wakili Pius Hilla
  • Abdallah Chavula
  • Jenitreza Kitali
  • Nassoro Katuga
  • Esther Martin
  • Tulimanywa Majige
  • Ignasi Mwinuka
Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji Ikupendeza naitwa Peter Kibatala nipo Pamoja na

  • Wakili Nashon Nkungu
  • John Mallya
  • Dickson Matata
  • Seleman Matauka
  • Fredrick Kihwelo
Jaji anaita Washtakiwa Wote wanne na wote wanaitika

WS Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Shauri limekuja kwa ajili ya Kusikilizwa na Leo tuna shahidi Mmoja ambaye alishaanza Kutoa Ushahidi Wake, Tupo tayari Kuendelea

Kibatala: Nasisi pia Mheshimiwa Jaji tupo tayari Kuendelea

Jaji: Shahidi nakukumbusha kuwa Ijumaa Ulikula Kiapo na, Leo Utaendelea Kuwa Chini ya Kiapo

Shahidi: Sawa Mheshimiwa

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Sasa Inspector Swila, Siku ile Tulikomea Tarehe 27 October 2020 wakati unampatia DC Goodluck Bastola Baada ya hapo Ulifanya Shughuli gani Nyingine

Shahidi: Niliweza Kupokea Taarifa ya Uchunguzi na SilahaTarehe 27 November 2020 Nilipokea kutoka kwa koplo Azizi wa Kitengo Cha Silaha na Milipuko Nilipokea Silaha, Bastola aina ya Luger A5340, Risasi Moja, Maganda Mawili ya Risasi pamoja na Vichwa Viwili Vya Risasi

Wakili wa Serikali: Wakati unapokea Taarifa ya Risasi Moja pamoja na Maganda Mawawili, Ni wapi ilipokea

Shahidi: Katika Kitengo Cha Uchunguzi Wa Silaha na Milipuko

Wakili wa Serikali: Uliwezaje Kujua kama Ndiyo Silaha uliyopeleka

Shahidi: Niliweza Kuangalia Serial Namba ya Silaha, Nikakuta ni A5340 na Silaha aina ya Luger

Wakili wa Serikali: VIpi Kuhusiana na Risasi Zenyenwe zilikuwa na hali gani

Shahidi: Risasi niliyo pokea ilikuwa ni Moja, Ilikuwa haujatumika, Ilikuwa na Alama A3 na Risasi ambazo zimetumika Nilikuta zimepewa alama ya T1 na T2

Wakili wa Serikali: Nani aliweka alama katika Vielelezo hivyo

Shahidi: Mchunguzi Wa Vielelezo hivyo

Wakili wa Serikali: Baada ya Kuwa umepokea Riport na Vielelezo Ulifanya nini.?

Shahidi: Vielelezo nilipeleka Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam na Kwenda Kuvikabidhi

Wakili wa Serikali: Kitu gani hicho ulienda Kukabidhi Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam

Shahidi: Nilienda Kukabidhi Silaha, Bastola aina ya Luger A5340 na Risasi Moja, Maganda Mawili pamoja na Vichwa Vyake

Wakili wa Serikali: Na Report Ulifanyia nini

Shahidi: Report nilihifadhi na Kufungia katika Kabati langu la Chuma

Wakili wa Serikali: Baada ya Tarehe 27 November 2020, Nataka Kukurudisha Kwanza hapo ambapo unasema Ulikabidhi Risasi Moja, Maganda Mawili na Silaha, Je Ulimkabidhi nani

Shahidi: Nilimkabidhi Sarjent Nuru, ambaye Yupo Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam, ni Mtunza Vielelezo Katika ghala la Kutunzia Silaha

Wakili wa Serikali: Kabla ya kwenda Katika Shughuli Nyingine za Upelelezi, Ni wakati gani tena Ukiweza Kushughulika na Vielelezo hivyo

Shahidi: Nili shughulika tena wakati Wa Kutoa Mahakamani Kwa ajili ya Ushahidi, Ambapo Nilimkabidhi koplo Hafidh Kwa ajili ya Kuja Kutoa Ushahidi Mahakamani

Wakili wa Serikali: Turudi tena Katika Upelelezi Baada ya Tarehe 27 November 2020, kitu gani kiliendelea Wakati wa Kesi hiyo

Shahidi: Niliweza Kupokea Taarifa Kutoka kwa Mrajisi wa Silaha Siku ya Tarehe 18 March 2021

Wakili wa Serikali: Hiyo Taarifa Ilikuwa inahusu nini

Shahidi: Ilikuwa inahusu Mmiliki Wa Silaha Yenye Sirial namba A5340 aina ya Luger

Wakili wa Serikali: Na Ripoti hiyo ilisemaje

Shahidi: Report hiyo ilionyesha Kuwa Silaha hiyo, haina Usajili wowote Katika Ofisi Ya Mrajisi Wa Silaha Hapa Nchini

Wakili wa Serikali: Kitu gani Kingine kiliendelea baada ya hiyo Tarehe 18 March 2021

Shahidi: Tarehe 30 March 2021 Niliweza Kupokea Taarifa Ya Maabara ya Sayansi, Kutoka Kitengo Cha Uchunguzi Wa Maandishi, Kutoka Kwa koplo Khamis, Wa Kutengo cha Uchunguzi Wa Maandishi. Niliweza Kusoma Ripoti hiyo, Ambapo Ripoti hiyo ilionyesha Kuwa Sampuli Za Maandishi yaliyo chukuliwa Kutoka Kwa Mtuhumiwa Khalfani Bwire Hassan, Ni sawa Sawa na Maandishi Yaliyokuwepo Katika Daftari nililoambatanisha katika Uchunguzi ule

Wakili Wa Serikali: Baada ya Kuwa Umesoma, Ukafanya nini

Shahidi: Niliweza Kuhifadhi katika Jalada langu la Kesi na Kufungia Katika Kabati langu la Chuma

Wakili wa Serikali: Baada ya Tarehe hiyo Kitu gani Kingine Ulifanya Kuhusu Kesi hiyo

Shahidi: Mnamo Tarehe 10 July 2021 Niliweza Kupokea Taarifa ya Simu zile Nane Kutoka Kwenye Maabara ya kisayansi Kitengo Cha Uchunguzi Wa Makosa ya Mtandao

Wakili wa Serikali: Ulipokea Kutoka Kwa nani

Shahidi: Nilipokea Kutoka Kwa Inspector Ndowo wa Kitengo Cha Uchunguzi Wa Makosa ya Ki Mtandao Wa Maabara Ya Kisayansi

Wakili wa Serikali: Baada ya Uchunguzi Wa Taarifa hiyo nini Kilitokea

Shahidi: Alijulishwa DC Goodluck ambaye haikuwepo Dar es Salaam, alinijulisha Kwa Uchunguzi umekamilika, Ndipo nilipoenda Kuchukua Taarifa hiyo

Wakili wa Serikali: Ulimkabidhiwa Kwa Utaratibu Upi

Shahidi: Kwa Kusaini Katika Kitabu cha Kitengo Cha Uchunguzi Wa Makosa ya Mtandao

Wakili wa Serikali: Mwanzono Ulisema Kwamba Ulipeleka simu, Sasa unakabidhiwa Riport, Vipi Kuhusu Zile simu

Shahidi: Pia Nilikabidhiwa Simu Nane ambazo niliziandikia Barua

Wakili wa Serikali: Ulijuaje Kama ndiyo Simu ulizopeleka

Shahidi: Niliweza Kuzikagua Wakati na kabidhiwa Wakili wa Serikali Ulifanyia nini hiyo Riport baada ya Kukabidhiwa

Shahidi: Simu Nane nilipeleka Katika Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam, Nilimkabidhi Coplo Charles ambaye ni Mtunza Vielelezo Katika Chumba Cha Kuhifadhia Vielelezo Katika Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam

Wakili wa Serikali: Na Ile Ripoti Ulifanyia nini

Shahidi: Ripoti Ya Uchunguzi Niliweza Kusoma. Na Kuhifadhi katika Jalada la Kesi Kisha Kuweka Katika Kabati langu la Chuma

Wakili wa Serikali: Ripoti hiyo Kwa sababu wewe Ndiye Uliyeomba Uchunguzi, Ni Vitu gani Ukiweza Kupata Kutoka Katika Ripoti hiyo

Shahidi: Katika Report hiyo Niliweza Kugundua Vitu vifuatavyo, Niliweza Kugundua Kuwa palikuwa na Mawasiliano kati ya Shahidi Luteni Denis Urio na Mtuhumiwa Freeman Mbowe ambayo Yalifanyika Katika Mtandao Wa Telegram Pia Kupitia Maelezo Ya Shahidi Luten Denis Urio, aliweza Kusema Kuwa alitumiwa pesa Kutoka Kwa Mtuhumiwa Freeman Mbowe

Ambapo Tarehe 20 July 2020 Namba 0719933386 ambayo ni Ya Mtuhumiwa Freeman Mbowe ilituma Kiasi cha TSh 500,000 Kwenda Kwa namba ya shahidi Luteni Denis Leo Urio ambayo ni 0787 555200.

Pia Tarehe 22 Mwezi huo huo wa July 2020 ilionyesha Kuwa Shahidi Luten Denis Urio Kupitia namba yake ya 0787 555200 ulipokea Kiasi cha TSh 199,000 kutoka Kwenye namba ya Wakala Kama alivyo eleza Luten Denis Urio.

Wakili wa Serikali: Baada ya hapo Nini Kiliendelea

Shahidi: Tuliendelea Kuandika Taarifa Mbalimbali na Kupitia Ripoti hiyo Niliweza Kujiridhisha kuwa ni kweli Mtuhumiwa Freeman Mbowe aliweza Kutuma hizo Fedha Kwa Luten Denis Urio

Wakili wa Serikali: Nini kiliendelea baada ya hapo

Shahidi: Siku ya Tarehe 27 July 2021 Watuhumiwa Justin Kaaya, Khalid na Gabriel Muhina Walifutiwa Shitaka Lao baada ya Kugundulika hawahusiki na chochote

Wakili wa Serikali: Turudi Baada ya Kupokea Ripoti Ya Uchunguzi Wa Kisayansi Kuhusu Simu, Baada ya Hapo Ulifanya nini

Shahidi: Mnamo Tarehe 18 July 2021 Niliandika Taarifa Kwenda Kwa Afande Mkurugenzi Wa Upelelezi wa Makosa Ya Jinai Nchini, Kuwa Kuna Ushahidi Wa Uhusika wa Mtuhumiwa Freeman Aikael Mbowe, nakuwezesha Kumkamata

Wakili wa Serikali: Mwanzoni Wakati Unatoa Ushahidi Wako Ulizungumzia Kuhusu Kufungua Majalada Mawili, Je ni Jalada lipi ambalo wewe Uliandikia Taarifa

Shahidi: Ni lile Jalada la Kesi tulilo fungulia Polisi, ambalo ni CD/IR /2097 /2020 lenye Chama za Kutaka Kufanya Vitendo Vya Kigaidi

Wakili wa Serikali: Wakati Wa Kufungua Jalada la Kesi hili CD /IR /2097 /2020 Ulisema Kwamba Usiandike Jina la Freeman Mbowe Kwa sababu Kama Ungeandika Jina Taarifa zingeweza Kuvunja, na akasitisha Mpango Wake, Je Ulikuwa Unamaanisha Nini

Shahidi: Nilikuwa namaanisha kuwa angeweza Kusitisha Kumtumia Mtoa Taarifa, angeweza Kutumia Watu wengine ambapo Jeshi la Polisi lisingejua Mahali wala Muda, Kitu ambacho. Lingesababisha Jeshi la Polisi Kushindwa Kuzuia Uhalifu

Wakili wa Serikali: Baada ya Kuandika Taarifa Kwenda Kwa DCI Nini Kiliendelea

Shahidi: Nilipokea Taarifa Kutoka Kwa Afande Ramadhan Kingai Kamishina Msaidizi Wa Polisi alinitaka nitunze Jalada hilo na Kwamba Yeye anafanya Jitihada za Kumkamata Mshitakiwa Freeman Aikael Mbowe

Wakili wa Serikali: Baada ya DCI Kukwambia Hatua ambazo angechukua nini Kilitokea sasa

Shahidi: Mnamo Tarehe 22 July 2021 Nilipokea Karatasi Ya Mtuhumiwa Freeman Aikael Mbowe Kutoka Kwa Afande Jumanne Malangahe Mrakibu Wa Polisi, Kimsingi Nilipokea Maelezo hayo Ikionyesha Mtuhumiwa amekataa Kutoa Maelezo Yake Polisi

Wakili wa Serikali: Kwa Kipindi hicho Ulifahamu huyo Mtuhumiwa Freeman Mbowe amepatikanaje

Shahidi: Nilifahamu Kwamba amekamatwa Mwanza na Kusafirishwa Dar es Salaam

Wakili wa Serikali: Umekuwa Ukizungumza Majina Ya Watu Kadhaa Hapa Mahakamani akiwepo, Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe. Hebu ieleze Mahakama Kama Watu hao wapo hapa Mahakamani

Shahidi: Ndiyo Watu hawa wapo hapa Mahakamani

Wakili wa Serikali: Hebu onyesha sasa

Shahidi: Mtuhumiwa Wa Kwanza, Kutoka Upande Wa Kulia ni Khalfani Bwire Hassan, Wapili kutoka Kulia Kwangu ni Adam Hassan Kasekwa, Watatu Kutoka Kulia Kwangu ni Mohammed Abdilah Ling'wenya na Wanne Kutoka Kulia Kwangu ni Freeman Aikael Mbowe

Wakili wa Serikali: Sasa Mwanzoni Wakati Unatoa Ushahidi Wako Ulizungumzia Kuhusu Khalfani Bwire, Adam Kasekwa na Mohamed Ling'wenya Walifikishwa Mahakamani Tarehe 19 August 2020, Mtuhumiwa Freeman Mbowe alifikishwa Mahakamani Tarehe ipi

Shahidi: Mtuhumiwa Freeman Mbowe alifikishwa Mahakamani Tarehe 26 July 2021

Wakili wa Serikali: Ni tofauti gani ipo Kutokana na Kufikishwa Tarehe tofauti na Wale 3

Shahidi: Utofauti unakuja Kutokana na Kusubiri Kwa Taarifa Ya Uchunguzi Wa Makosa ya Mtandao, ambao Kimsingi Nilipokea Tarehe 10 July 2021

Wakili wa Serikali: Sasa na Upelelezi Wa Kesi inayo wakabili, Ni Ushahidi gani ulipata Kwamba Walikula Njama za Kutenda Matendo Ya Ugaidi

Shahidi: Ni Kupitia Maelezo Yao ya Onyo ya Mshtakiwa Wa Pili Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya pamoja na Mshitakiwa Wa kwanza Khalfani Bwire Hassan, Pia Ushahidi Mwingine ambao Unaonyesha walikuwa Njama ni Kupitia Maelezo Ya Shahidi Luten Denis Urio,

Shahidi: Maelezo Ya Askari Walio wa kamata, Askari Walio andika Maelezo Ya Watuhumiwa

Wakili wa Serikali: Kuhusiana na Pesa iloyotumwa, Uliiweza Kubaini nini?

Shahidi: Niliweza Kubaini Fedha hiyo ilitumwa kutoka Kwa Freeman Mbowe Kwenda Kwa Luten Denis Urio, Ambapo Fedha hiyo iliweza Kuwawezesha Watuhumiwa Mshitakiwa Wa Pili na watatu pamoja na Mwingine ambaye hajakamatwa Kuweza Kufika Eneo la Uhalifu ambalo lilikuwa Eneo la Moshi Niliweza Kubaini Kuwa Fedha hiyo ilitumwa iliwezesha Watuhumiwa Kufika Eneo la Utekelezaji Wa Uhalifu

Wakili wa Serikali: Unaposema Kwamba Mshitakiwa Wa Pili, Watatu na Mwingine hajakamatwa, Vipi Mtuhumiwa Wa Kwanza Kuhusiana na Fedha hii

Shahidi: Kuhusu Mshtakiwa Wa kwanza Inaonyesha Pia aliweza Kupokea Pesa kutoka kwa Luten Denis Urio Kwa ajili ya Utekelezaji Wa Vitendo Vya Kigaidi

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Naomba Kukomea hapo Kwenye Examination inchief

Upande wa Utetezi

Wakili Nashon Nkungu: Shahidi Habari za Leo

Shahidi: Njema

Nashon: Shahidi umepona?

Shahidi: Bado

Nashon: Umemeza Dawa zako

Shahidi: Ndiyo

Nashon: nadhani Shahidi unatambua Ukubwa wa hii Kesi

Shahidi: Sahihi

Nashon: Kwamba Ugaidi ni Jambo Serious kwa Nchi na Dunia

Shahidi: Ni sahihi

Nashon: Kutokana na Userious wa Mashitaka, Hata Uchunguzi Wako Ulitakiwa Uwe serious Ku Match na Makosa haya

Shahidi: Sahihi

Nashon: Kupitia Ushahidi Wako uliotoa, Unaweza Kusimama Kifua mbele Kwamba ulitendea Haki Uchunguzi Wa Kesi hii

Shahidi: Ni sahihi

Nashon: Makosa ni Vitu Vinavyotengenezwa na Sheria

Shahidi: Ni sahihi

Nashon: Kuna Sheria ambazo zilikuwa zinawaongoza

Shahidi: Ni sahihi

Shahidi: Tutajie Sheria zipi Mlikuwa Mnazitumia Kuwa Guide

Shahidi: Sheria Mbalimbali

Nashon: Nitajie Sheria Mbili Mlikuwa Mnazitumia

Shahidi: Sheria ya Kuzuia Ugaidi na Sheria ya Mwenendo Wa Makosa ya Jinai

Nashon: Ni nani aliye angalia Sheria akatoa conclusion Kwamba alisema Kwa Story hii, haya ni Makosa ya Ugaidi

Shahidi: Ni Ramadhan Kingai Kamishina Msaidizi Wa Polisi

Nashon: Wewe huku take part katika Kujua haya ni Makosa ya Ugaidi

Shahidi: Hata Mimi Mwenyewe pia nilikuwa najua haya Makosa ni ya Ugaidi

Nashon: Una utaalam wa Kung'amua Kuwa haya ni Makosa ya Ugaidi

Shahidi: Ndiyo

Nashon: Ulisomea wapi

Shahidi: INTERNATIONAL LAW ENFORCEMENT ACADEMY Botswana

Nashon: Kozi gani

Shahidi: FIRST BURST SCENE

Nashon: Kwa hiyo Walimu Wako wakakwambia Kwamba Kozi hiyo ina husika na Ugaidi

Shahidi: Inahusika na Milipuko

Nashon: Shahidi Ulisema Kwamba Mmoja ya Watuhumiwa Katika kesi hii ni Justin Kaaya

Shahidi: Sahihi

Nashon: Uliwahi Kumuandika Kaaya Maelezo Ya Onyo

Shahidi: Hapana

Nashon: Je Unafahamu Kwamba Kaaya alitumiwa pesa na Freeman Mbowe

Shahidi: Ni Kweli

Nashon: Uliwahi Kumuandika Kaaya Maelezo Ya Ushahidi

Shahidi: Sahihi

Nashon: Alikwambia Kwamba aliwahi kutumiwa pesa na Freeman Mbowe

Shahidi: Ni sahihi

Nashon: Ni sahihi Kwamba alitumiwa pesa kama Watuhumiwa Wengine hapa Mbele

Shahidi: Hapana

Nashon: Justine Kaaya, Khalfani Bwire wote Walitumiwa pesa na Freeman Mbowe

Shahidi: Sahihi

Nashon: Wote hawa Wametumiwa pesa na Freeman Mbowe

Shahidi: Sahihi, lakini Malengo ni tofauti

Nashon: Malengo ya pesa ya Khalfani Bwire unayatoa Wapi

Shahidi: Maelezo ya Mtuhumiwa

Nashon: Maelezo ambayo Washtakiwa Wanataka kwamba hawakuyatoa Kwa hiari yao, Bali kwa Mateso ndiyo Ushahidi Wako wa Pekee?

Shahidi: Maelezo ya Washtakiwa Wengine

Nashon: Je Unafahamu Kwamba Kaaya alisema alikuwa anapewa pesa na Freeman Mbowe Kwa ajili ya Kutoa Taarifa Za Sabaya

Shahidi: Lakini alikuwa hafahamu Malengo

Nashon: Je tangu ugundue hakuwa na Nia Mbaya ilikuwa ni Muda gani baada ya Kumkamata

Shahidi: Zaidi ya Miezi 10

Nashon: Ulimkamata lini

Shahidi: Mwezi September 2020

Nashon: Ukaja Kumuachia lini

Shahidi: Mwezi July 2021

Nashon: Baada ya Mwaka mmoja ndiyo Ukajua hakuwa na Melengo Mabaya

Shahidi: Sahihi

Nashon: Ni sahihi Taarifa za Sabaya Freeman Mbowe alizitoa Kwa Kaaya

Shahidi: sahihi

Nashon: Kwamba alilipwa kwa kazi hiyo

Shahidi: sahihi

Nashon: wewe Hukuona Kosa

Shahidi: sahihi

Nashon: Na Kwamba alikuwa anakaa Kikao na Mbowe Kutoa Taarifa hiyo

Shahidi: Sahihi

Nashon: Kwa Kushiriki Kikao hicho Kaaya alikuwa anashiriki Kikao cha Kigaidi

Shahidi: Alikuwa ajui Dhumuni La Kikao, Kwa hiyo ajashiriki Kikao cha Kigaidi

Nashon: Lakini katika Kikao hicho hicho Mbowe alishiriki Kikao cha Ugaidi

Shahidi: Ndiyo

Mahakama: KICHEKO

Nashon: wakati gani ulipokea Bastola

Shahidi: Baada ya Kutoka Maabara

Nashon: Uli label?

Shahidi: Siku Label

Nashon: Lakini Simu za Mshtakiwa Wa kwanza ndiyo Uli Label

Shahidi: Hapana Siku Label

Nashon: Wewe Uli Label Simu za nani

Shahidi: Luten Denis Urio

Nashon: Na uli Label lini

Shahidi: Tarehe 11 na 13 August 2020

Nashon: Je ni sahihi Kwamba Ulichukua Bastola ya A5340 pamoja na Risasi kutoka Kwa Coplo Hafidh

Shahidi: Nilipokea Silaha A5340 aina ya Luger kutoka Kwa Hafidh Ikiwa na Risasi Moja, Maganda Mawili

Nashon: Ulipokea Vielelezo Kutoka kwa koplo Hafidh

Shahidi: Sahihi

Nashon: Naomba Upokeee Simu, Mheshimiwa Jaji ni Kutoka Katika Kielelezo P28

Nashon: hii aina au dizaini la Ku Label unaitolea wapi

Shahidi: Kipo Kwenye Sheria

Nashon: Sheria ambayo unaitumia ni Sheria gani

Shahidi: Ni PGO

Nashon: Mwambie Mheshimiwa Jaji Kama ulijaza Makabidhiano wakati wa Makabidhiano

Shahidi: Humu sijaandika

Nashon: Unafahamu Kwamba Katika Kielelezo, Lebel ya Kielelezo pale Unapo ambatanisha namba ambayo unaambatanisha inatakiwa uwe namba ya Jalada la Kesi

Shahidi: Ni sahihi

Nashon: Unafahamu Kwamba Unatakiwa pia uwe na Exhibit Serial number

Shahidi: Siyo lazima, Kwa sababu hivi Vielelezo Vilikuwa kwenye Mfuko kwa hiyo Exhibit Serial number inakuwa kwenye Mfuko

Nashon: Hiyo PGO Unayosema Ulitumia inataka uwe na Mahala, namba na Tarehe mnayokabidhiana

Shahidi: Ni sahihi

Nashon: Lakini hapa Hakuna hata Moja

Shahidi: Ndiyo hapo Hakuna

Shahidi: SAMAHANI MHESHIMIWA JAJI NAOMBA NIENDE WASHROOM (CHOONI)....

Shahidi karejea

Nashon: Nipo interested na Shahidi ambaye alikuwa Mtuhumiwa akaachiwa

Nashon: Je ni sahihi Katika Maelezo Uliyo Mwandika Wewe, aliandika Kuwa aliwahi Kuwa Msaidizi Wa Katibu wa CCM Wilaya ya Meru

Shahidi: Ni sahihi

Nashon: Pamoja na Kwamba kapokea Fedha, na Kashiriki Vikao ila akaachiwa

Shahidi: Sahihi

Nashon: nani ni Mwamuzi ambaye aliamua kuwa Pesa hizo siyo za Ugaidi

Shahidi: ni Upelelezi

Nashon: Ni nani hasa

Shahidi: Mchakato Wa Upelelezi

Nashon: Ni sahihi Kwamba Uliwahi kuandila Maelezo Yako Mwezi 6 August 2020

Shahidi: Ni sahihi

Nashon: Ni sahihi Kuwa katika Maelezo yako Uliwahi Kusema Kuwa Mbowe ameshiriki Vikao Vya Kigaidi

Shahidi: Ni sahihi

Nashon: Na Katika Maelezo yako Ulisema Kwa, Kuthibitisha hilo ni Kupitia Maelezo ya Onyo ya Washtakiwa Wenzie

Shahidi: Ni sahihi

Nashon: Ni sahihi Kwamba wewe na Wapelelezi Wenzio hamkuwahi Kushuhudia Mbowe akiwa katika Kikao cha Ugaidi

Shahidi: Ni sahihi

Nashon: Ni sahihi Kwamba Wewe na Wapelelezi Wenzio hamkuwahi Kushuhudia Mbowe akiwa katika Kikao Mbeya au Arusha?

Shahidi: Sahihi

Nashon: Ni sahihi Kwamba pia nyie Kama Wapelelezi wa Kesi hii hamna CCTV Camera

Shahidi: Ni sahihi hatuna

Nashon: Ni sahihi Kwamba wewe na Wapelelezi Wenzio hamna hata Sauti ya Mbowe akipanga Ugaidi

Shahidi: Ni sahihi hatuna

Nashon: Ni sahihi Kwamba Jeshi la Polisi lina Vifaa Vya Kurekodi Sauti

Shahidi: Siwezi Kuzungumzia hilo

Nashon: Lakini Unafahamu Kwamba Simu inaweza Kurekodi Sauti

Shahidi: Ndiyo

Nashon: Na Jeshi la Polisi hamkazwi kutumia Simu Kurekodi Sauti

Shahidi: Ndiyo

Nashon: unajua Kuwa Mahakama Inaruhusu Kutumia Video na Sauti katika Ushahidi

Shahidi: Sifahamu

Nashon: Nikumbushe Cheo Chako huko Polisi

Shahidi: Inspector Wa Polisi

Nashon: Na Inspector Wa Polisi Ujui Kuwa Mahakama Inatumika Video na Sauti Katika Ushahidi

Shahidi: Ndiyo

Nashon: Ndiyo Maana hamkuleta Video wala Sauti Mahakamani Kwa sababu ufahamu Ka Inatumika Mahakamani Kama Ushahidi

Shahidi: Ndiyo

Nashon: Nionyeshe Sasa sehemu ambayo Mahakama itaona Mbowe alikaa Vikao Vya kigaidi

Shahidi: Ilikuwa Kwenye Gari, Ukisoma Maelezo Utaona

Nashon: Naomba Sasa Mahakama Ikupatie hizo Meseji Shahidi: Nimeona Meseji ya Tarehe 22 July 2020 Muda wa Saa 7 na Dakika 49 "Kutakuwa na Safari ya kwenda Hai, Leo Usiku au Asubuhi" Mahakama

Nashon: Naomba Sasa Mahakama Ikupatie hizo Meseji

Shahidi: Nimeona Meseji ya Tarehe 22 July 2020 Muda wa Saa 7 na Dakika 49 "Kutakuwa na Safari ya kwenda Hai, Leo Usiku au Asubuhi"

Mahakama: Kicheko

Shahidi:
hii Inaelezea Sasa Kwamba Kutakuwa Kuna Kikao

Nashon: Katika hiyo Meseji wataje Wanaokutana

Shahidi: Mtuhumiwa Wa Kwanza, Wa pili, Watatu na Wanne

Nashon: Kwa hiyo akisoma hiyo Meseji ataona Kwamba Kuna Kikao cha Ugaidi

Shahidi: Ushahidi ni Kuunganisha Dot

Nashon: Kwa hiyo Nikisoma Meseji ipi nitaona nani na nani wametajwa, Saa ngapi na Wapi

Shahidi: Kwenye Meseji Hauwezi Kuona, ila Kwa Kuunganisha Dot

Mahakama: Kicheko

Nashon: Tutoke hapo umesha Sema hatutoona. Meseji Twende Kwingine

Nashon: Ni kweli Kwamba Mlikuwa na Msiri wenu Denis Urio

Shahidi: Ndiyo

Nashon: Baada ya Kuona hiyo Meseji Kwamba wanaenda Hai, nyie Hamku fuatilia

Shahidi: Hatukufutilia

Nashon: Mnafahamu Kuwa Aishi Hotel Ina CCTV Camera

Shahidi: Sifahamu

Nashon: Na hufahamu kwa sababu hujawahi Kufika Aishi Hotel

Shahidi: Kimya

Nashon: Sasa Ulifanya Juhudi zozote za Kwenda Pale Aishi Hotel kama Mpelelezi ambaye Yupo serious, labda Kuandaa Warranty, CCTV CAMERA Kuangalia List ya Wageni

Shahidi: Sikuwahi Kufanya hivyo

Nashon: Kwa ujasiri kabisa Mwambie Mheshimiwa Jaji Kuwa Uliwezaje Kuwaleta Watuhumiwa Mahakamani Kwamba Wamekutana sehemu fulani ambayo wewe na Polisi Wengine hamjawahi Kufika

Shahidi: Mimi nilikuwa sehemu ya Upelelezi tu, Kuna wengine ambao walikuwa Arusha na Kilimanjaro

Nashon: Kwa hiyo Wewe Kwa sababu upo Dar es Salaam hukuona Sababu

Shahidi: Hapakuwa na Ulazima

Nashon: Sasa Pale Aishi Walifanya Nje au Ndani

Shahidi: Nje Kwenye Garden

Nashon: Garden ya upande upi

Shahidi: Sifahamu Sijawahi Kufika

Nashon: Katika Ushahidi Wako Nimekusikia Mahala Kwamba Unasema Ulikuwa unapokea Vielelezo na Kuvitunza, Je Hapa Mahakamani umewahi Kusema Kuwa Uliwahi Kuwa Forensic Beaural

Shahidi: Sijawahi Kusema

Nashon: Wewe Ulikaa na Vielelezo Vipi ambavyo Uliviandaa Kwa ajili ya Ushahidi

Shahidi: Simu za Urio Nashon Simu za Urio tu?

Shahidi: Simu zote Nane

Nashon: za Kwanza

Shahidi: Nilipokea Tarehe 07 August 2020 Mpaka Tarehe 13 August 2020

Nashon: tukumbushe nani alivileta Mahakamani

Shahidi: Hivyo Vielelezo Nilimpa Inspector Ndowo

Nashon: Lini

Shahidi: Sikumbuki

Nashon: Kwa sababu hamkuandikishana

Shahidi: Tuliandikishana

Nashon: Lakini Tukiangalia katika PF 145 Hatuoni sehemu Mliyo kabidhiana

Shahidi: Ni sahihi Hakuna

Nashon: Ulikuwa unafahamu kuwa Sheria inataka uonyeshe Katika PF 145

Shahidi: Nilikuwa nafahamu

Nashon: ila Ukaamua Kupuuza Sheria

Shahidi: Hapana

Nashon: Ni sahihi Uliondoka HQ August 2021

Shahidi: sahihi

Nashon: Ni sahihi Kwamba hujaeleza Mahakama Baada ya Kuondoka Ofisini Kwako Vielelezo ulimuachia nani

Shahidi: Usipotoshe Mahakama, Nilisema Kwamba Vielelezo Vyote nilikuwa nimepeleka Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam

Nashon: Unakumbuka Muda ambao Ulikaa na Vielelezo, Ambapo Vilienda Polisi Kati Dar es Salaam na kukaa navyo katika Kabati la Chuma

Shahidi: Kwa nani? Kwa Tarehe ipi?

Nashon: Je ni sahihi Kwamba Ulichukua Vielelezo Kutoka Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam Yes or No Shahidi Yes

Nashon: Kwanini Sasa unapoteza Muda Wa Mahakama

Nashon: Baada ya Uchunguzi Ulikaa navyo au ulipitiliza Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam

Shahidi: Nilipeleka Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam

Nashon: Kwa hiyo ni sahihi Kwamba Ulikuwa Umekaa na Vielelezo Katika Kabati lako wakati wewe siyo Mtunza Vielelezo

Shahidi: Nilikaa navyo Kwa ajili ya Kuviandikia Barua, Sababu ya Upelelezi

Nashon: Ilikuwa inashindikana Kwa wewe Kuandika Barua Vielelezo Vikiwa Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam

Shahidi: Ilikuwa Haiwezekani

Nashon: Unafahamu Kwamba OC Forensic Beaural ndiye anaye husika Katika Kuandaa na Kutunza Vielelezo Kabla ya Kwenda Kufanyiwa Uchunguzi

Shahidi: OC wa Forensic Beaural anapelekewa na Mpelelezi

Nashon: Je Unafahamu Kwamba OC Forensic Beaural ndiye anaye husika Katika Kutunza, Kuandaa na Kupeleka kwa Expert Examination

Jaji: sijui Mimi Ndiyo sielewi, Naomba Wakili unisaidie

Wakili Kihwelo: Swali lake linahusu Custodian wa Kutunza kabla ya kwenda Kwa Expert Examination

Shahidi: Sifahamu

Nashon: Katika Ushahidi Wako Kuna sehemu Kwamba Ulisema DCI alikwambia pamoja na OC Forensic Beaural ndiyo Mtunza Kielelezo, lakini wewe Kaa navyo

Shahidi: Sikueleza hayo

Nashon: Kwakuwa Umeibuka Mjadala hapo, Na Kwakuwa Mheshimiwa Jaji Shahidi alisema anaifahamu PGO naomba ni Muonyeshe Shahidi PGO hii ambayo alikuwa anaitumia Wakati wa Kufanya Kazi, PGO ya 8 Paragraph ya 9

Jaji: Rudia na uongeze Sauti

Nashon: Soma Kipengele (e)

Jaji: Samahani, Hapa OC anahusika baada ya OC kuwa ameletewa Vielelezo Hapa Sheria inasema Kwamba OC Forensic Beaural, Ndani ya Forensic baada ya Kuvipokea Nataka sasa Kufahamu Premise ya swali lako naandikaje, Inawezekana Unahoja ila namna ya ulivyoliweka ndiyo Unanichanganya

Nashon: labda Kwako Mheshimiwa Jaji, lakini najua siyo sawasawa.

Wakili John Malya: Mheshimiwa Jaji Kwa Kuokoa Muda, wakili aende Kwenye eneo lingine baadae ndiyo arudi kuunganisha hapo

Jaji: Sawa

Wakili wa Serikali Robert Kidando Mheshimiwa Jaji hata sisi tunapata tabu sababu Shahidi Alisha Sema siyo Utaratibu, nilifikiri Kuanzia pale ndiyo tuelezwe Jaji Ndiyo Maana wanasema Watarudi Baadae

Nashon: Shahidi Ni sahihi Kwamba Wewe ndiyo ulimuandika Maelezo Luten Denis Urio

Shahidi: Sahihi

Nashon: Je Hukuona Kosa pale Ambapo Luteni Denis Urio aliposema Kwamba "Mlimkubalia kwa kwenda Kutafuta Watu wa Kufanya Vitendo Vya Kigaidi" alikuwa anatenda Kosa

Nashon: Shahidi Soma yote ndiyo Utaona siyo Kosa

Wakili Abdallah Chavula: Mheshimiwa Jaji naomba hapa Kuweka Sawa, Shahidi anaitwa kwa Sheria tofauti na Kifungu tofauti, Sasa anapoelekea Wakili akatazwe, shahidi awezi Kuwa mtuhumiwa

Wakili Nashon Nkungu: Mheshimiwa Jaji kumsitiri Kaka Yangu Abdallah Chavula PGO 236 Paragraph 08 ambapo inasema During police officers during taking statement.................

Wakili Wa Serikali Abdallah Chavula: Mheshimiwa Jaji Nafikiri aendelee

Nashon: Kwa Ufahamu Wako Kumtafutia Mhalifu Wahalifu Wa Kwenda Kutimiza Uhalifu Siyo Kosa

Shahidi: Inategemea

Nashon: Huyu Luteni Denis Urio alikuwa ni Askari Polisi

Shahidi: Hakuwa Askari Polisi

Nashon: Je huyu Luteni Denis Urio Mlimpa Ulinzi Wa Kisheria

Shahidi: Siyo Mimi niliye pokea Taarifa zake, Mara ya Kwanza alitoa Taarifa Kwa DCI

Nashon: Kwani huyu Luteni Denis Urio alikuwa na Taaluma ya Upelelezi

Shahidi: Siyo Mimi niliye pokea Taarifa

Nashon: Kwani Luten Denis Urio Mlimfundisha Kuhusu Kufanyia Watu Upelelezi

Shahidi: Mimi Sikuwahi Kumuona Luten Denis Urio kabla

Nashon: Umesikiliza Ushahidi Wa Luten Denis Urio

Shahidi: Wapi

Nashon: alipokuwa hapa Mahakamani

Shahidi: Sikuwepo Mahakamani

Nashon: Sawa, Ngoja ni kwambie sasa, Urio Mada aliwatafuta Watuhumiwa lakini hawakuwa wanajua Kuwa wanaenda Kufanya Ugaidi

Nashon: Je Muda gani sasa Khalfani Bwire alipata Guilty Mind

Shahidi: anafahamu Mwenyewe

Nashon: Je ni muda gani Adam Kasekwa alipata Guilty Mind

Shahidi: anajua yeye Mwenyewe

Nashon: Je ni Muda gani Mohammed Ling'wenya alipata Guilty Mind

Shahidi: Sifahamu

Nashon: Katika Ushahidi Wako Ulisema Uliitwa Tarehe 14 July 2020 kwa Mkurugenzi, Je ni sahihi

Shahidi: Siyo Sahihi

Nashon: Wacha nisome... Wakili anasoma

Shahidi: Ni sahihi

Nashon: Kwa hiyo Tarehe 14 July 2020 Taarifa zimekuja tayari Kuna Kundi

Shahidi: Ni sahihi

Nashon: Unafahamu Kwamba Pesa zimeanza kutumwa Tarehe 20 July 2020

Shahidi: Ndiyo

Nashon: Je hilo Kundi lililkuwepo Kabla halijakutana Tarehe 20 July 2020

Shahidi: Lilikuwepo Kabla

Nashon: Je Unafahamu Kwamba Kundi Lilianza kutengenezwa na Luteni Denis Urio Tarehe 20

Shahidi: Kundi Lilikwepo Mara baada ya Luteni Denis Urio Kukutana NA Freeman Mbowe

Nashon: Kwani hilo Kundi ni hili au Kundi lingine

Shahidi: Ni hili

Nashon: Kwa hiyo Wewe na Luteni Denis Urio Mahakama iangalie nani anasema Kweli

Shahidi: Mahakama ndiyo itajua

Nashon: Shahidi Ni sahihi Ulisema Kwamba Hamkuandikisha Jina la Freeman Mbowe Kwa sababu Taarifa zingevuja

Shahidi: Ni sahihi

Nashon: Kwa hiyo Kuna Askari siyo Waaminifu

Shahidi: Tulihofia Kwamba Kile Kitabu kinasomwa na kubadilishana Taarifa Kwa Polisi

Nashon: Kwani wewe Unafahamu sheria yoyote inayoruhusu Kufungua Kwa Jalada bila Kujaza Jina

Shahidi: Hakuna

Nashon: Lakini Unafahamu Sheria ambayo Inaelekeza Majina yajazwe

Shahidi: Nafahamu

Nashon: Shahidi Wakati Unaenda Kule Coco beach, Kumtafuta Khalfani Bwire, Hukuona haja ya Kuwa chukua Watuhumiwa Wenzake Kwenda pamoja Kumtafuta Khalfani Bwire Kwa sababu wangemtambua hata Kama kawapa Mgongo

Shahidi: Hapakuwa na haja hiyo

Nashon: Shahidi, Ulisema Kuna Kidaftari

Shahidi: Ni sahihi

Nashon: Ulisema Kile Kidaftari Kina Michoro Ya Ramani

Shahidi: Sahihi

Nashon: Kwani wewe Unataaluma Ya Ramani

Shahidi: Hapana, ila naweza Kusoma Ramani

Nashon: Kwani Nikochora Duara Utajua ni Kisima

Shahidi: Hapana

Shahidi: waliandika Majina ya Barabara, na Mishale ya Kuingia na Kutoka

Nashon: Kwani Walitaja Mikoa

Shahidi: Hapana

Nashon: GBP na Bigbon

Shahidi: sahihi

Nashon: Kilicho Kufanya Ujue ni Kariakoo na Morocco uliyokwenda ni ipi

Shahidi: Sababu palikuwa na Majina ya Barabara

Nashon: Ulisema Kwamba Khalfani Bwire alikataa Sampuli ya Maandishi

Shahidi: Ndiyo

Nashon: Unafahamu Kwamba Unapokuwa unuhoji Mtuhumiwa Kuna Haki zake ikiwemo Kuandika Maelezo Ya Onyo

Shahidi: Nafahamu

Nashon: Maelezo ya Kukataa hapa Mahakamani yapo Wapi

Shahidi: Hakuna

Nashon: Kwani Hakuna Majina ya Barabara yanayo Fanana, Kama Morocco zipo mbili Kinondoni

Shahidi: Nafahamu zipo Mbili

Nashon: Hicho Kidaftari Kipo hapa Mahakamani

Shahidi: Hapana

Nashon: Unasema Ulikuwa Unawatoa Watuhumiwa Mahabusu Kuwachukua sampuli Je huo Muda Ulifanyika Kisheria

Shahidi: Ndiyo

Nashon: Umeleta Detention Register ambayo Inaonyesha Walitoka Saa ngapi na Kurudi Saa ngapi

Shahidi: Hapana

Nashon: Nikikataa kuwa Hukuwa toa Kisheria unaushahidi gani

Shahidi: Maelezo yangu

Nashon: Mheshimiwa Jaji naomba Kuishia hapa Kwa Shahidi huyu

Wakil John Mallya: Mheshimiwa Jaji Nina Maswali Kadhaa, Ila naona Muda wa Health Break Umefika, Naomba tuairishe Kwa sasa

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Kwa Dakika 45

Jaji: naahirisha mpaka saa 7 na Dakika 45

Jaji anatoka 07:30


*************************


Jaji amerejea 08:30

Kesi inatajwa


Wakili wa Serikali Robert Kidando:
Mheshimiwa Jaji Shauri limekuja kwa ajili ya Kusikilizwa Quorum ipo Kama awali tupo tayari Kuendelea

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji na sisi tupo kama awali tupo tayari Kuendelea

Jaji: Malya karibu

John Malya: Mheshimiwa Jaji naomba Kielelezo

Malya: ile namba ya Kesi CD /IR /2097/2020 Ipo sahihi

Shahidi: Sahihi

Malya: ina Maana yoyote hapa

Shahidi: Inafanya Reference Kwenye kesi ambayo ipo Mahakamani

Malya: Je hiyo namba imepangwa Kwa Mtiririko wa Kesi au Hapana

Shahidi: Ni Mtiririko Wa Kesi zilizopo

Malya: Mheshimiwa Jaji naomba Kielelezo namba 39

Malya: by The way Mhe Kielelezo kimeandikwa Namba 29 nafikiri ni Makosa ya Karani wa Mahakama, Ilitakiwa Kuwa Kielelezo namba 39

Malya: Shahidi namba hii Ndiyo tunayoiona hapa

Shahidi: Sahihi

Malya: Kwa hiyo Hakuna namba Nyingine ambayo Inafanana na hii namba hapa Mahakamani

Shahidi: Sahihi

Malya: na hizi feature zote ni za Muhimu Katika Kuandika namba ya Kesi katika hili faili

Malya: Naomba Mheshimiwa Kielelezo namba P 37

Malya: Tazama katika Karatasi hii, Je ni sahihi Hakuna Mkwaju.?

Shahidi: Ni sahihi, Hakuna Mkwaju katika Kielelezo namba 37

Jaji: huo Mkwaju unamiss wapi

Malya ANAMUELEKEZA

Malya: Wakati Mnakabidhiana Simu na Denis Urio Ulikuwa wapi

Shahidi: Ofisi Ndogo ya Mkurugenzi wa Upelelezi Makosa Ya Jinai

Malya: Ni sahihi Kwamba Ofisi ile ndiyo Ofisi Kubwa ya Upelelezi Kuliko zote kwa Dar es Salaam

Shahidi: Ni sahihi

Malya: Je Ofisi Ya DCI Dar es Salaam ina uhaba wa Vifaa.?

Shahidi: Inategemea

Malya: Wakati Wa Shauri Kubwa kama la Kesi ya Ugaidi, Utakubali Kuvunja Sheria au utasubiri Vifaa

Shahidi: Nitasubiri Vifaaa

Malya: Sasa hii Fomu hapa iliyojazwa hivi, Ni Just for Cosmetics au inatakiwa Kujazwa kama. Inavyotakiwa

Shahidi: Inatakiwa inajazwe Kama inavyotakiwa

Malya: hizo features zilitakiwa Zijazwe au zisijazwe

Shahidi: Zilitakiwa zijazwe

Malya: Ni sahihi hizo fomu Mlitakiwa Makabidhiane Askari Polisi Kwa Askari Polisi

Shahidi: Ni sahihi

Malya: Sasa wewe ulikabidhiana kwa fomu hiyo na Askari

Shahidi: Hapana

Malya: Je Denis Urio alikuwa ni Askari Polisi.?

Shahidi: Hapana, Kwa sababu yeye ni shahidi

Malya: Mwambie Mhe Jaji akisoma wapi atajua yeye ni Shahidi

Shahidi: Hapa haionyeshi

Malya: fomu yenyewe inajieleza Kuwa anayekabidhi, Jina na Sahihi anaye kabidhi

Shahidi: Mtu anayekabidhi,Hakuna Jina

Malya: Mhe Jaji naomba nipatiwe Kielelezo D4 Maelezo Ya Bwana Denis Urio

Malya: Shahidi tumeukizana Habari ya Jina, Kujiridhisha kama. Kweli huyo Mtu alikuwa ni Urio, Je katika Signature Ya Denis Urio Kuna features zipi ambazo zinaonyesha

Shahidi: anaye weza Kuitambua hii ni Mtaalamu Wa Maandishi

Malya: Kwahiyo Hauwezi Kuitambua

Shahidi: anayeweza Kuitambua hii ni Luteni Denis Urio Malya: Sijauliza kama Unaitambua au huitambui Shahidi: Kuna Mkorogo tu, anaye weza Kuitambua hii ni Mtaalamu Wa Maandishi

Malya: Sasa hapa pia Nina Maelezo Ya Denis Urio, Yana Signature pia, Je Kwa Macho yako Zinafanana au hazifanani Shahidi zinafanana

Malya: Sawa Nenda pale Kwa Ruhusa Ya Mheshimiwa Jaji, Muonyeshe zinavyofanana

Malya: Mheshimiwa Jaji naomba nipatiwe Kielelezo P 30

Mallya: Je Shahidi Katika Simu ya Bwire wewe ndiye uliye andika Exhibit Label

Shahidi: Nilimjibu siyo Mimi

Malya: Maana ya Kuhamisha Faili Maana yake ni nini

Shahidi: Namba ya Faili inabakia Vile vile

Malya: Je Unasema Kwamba Shughuli zinafanyikia wapi

Shahidi: Inategemea

Malya: Ulielezea Kwa Mheshimiwa Jaji

Shahidi: Hapana

Malya: Bwire alikamatwa wapi

Shahidi: Chang'ombe

Malya: Unajua aliyejaza simu za Bwire alijaza wapi

Shahidi: Sijui

Malya: Wakati Wa Kingai na Goodluck wamemkamata Bwire wewe Ulikuwa Central.?

Shahidi: Sahihi

Malya: Hii Simu ambayo nimeshika ni ya Bure, Je ilijaziwa wapi

Shahidi: Sijui

Malya: Lakini Kingai na Goodluck Walikukuta Central

Shahidi: Sahihi

Malya: msomee Mheshimiwa Jaji Sehemu Iliyo andikwa Station

Shahidi: Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam

Malya: na Simu ya Urio Ulichukua wapi

Shahidi: Ofisi ya DCI

Malya: Shahidi Nakuonyesha Kielelezo P28, Simu ya Urio imeandikwa wapi

Shahidi: Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam

Malya: Kielelezo P 29 Msomee Mheshimiwa Jaji Sehemu ya Station

Shahidi: Polisi Kati Dar es Salaam

Malya: Shahidi Tarehe 11 August 2020 ndiyo Urio alikuja Ofisini Kwako, akakuachia Simu Moja

Shahidi: Sahihi

Malya: Wewe ni Mpelelezi Wa aina gani, Anaye Jipanga au Kukurupuka

Shahidi: anayeJipanga

Malya: Kama amayejipanga, Urio alipokwambia Kesho anakuja, Ulikuwa umejipanga au Hukuwa umepanga

Shahidi: za Makabidhiano nilikuwa nazo ila PF 145 sikuwa nazo

Malya: Kwa hiyo Ulijipanga kuwa na fomu za Makabidhiano ila za PF 145 Hukuwa nazo

Shahidi: Ndiyo Nilivyo Eleza

Malya: haya Shahidi Muonyeshe Mheshimiwa Jaji Sehemu ya Station Imeandikwaje

Shahidi: Polisi Kati Dar es Salaam

Malya: Shahidi Umeeleza wewe Ulikuwa Mjumbe wa Kikosi X, Je Wajumbe wa Kikosi X Wanafamika na Jamii?

Shahidi: Wanafahamika

Malya: Jumanne alikuwa Katika Kitengo hicho

Shahidi: Hapana

Malya: Kingai

Shahidi: Hapana

Malya: Goodluck

Shahidi: Hapana

Malya: Mahita

Shahidi: Hapana

Malya: Mwenzako wa Kitengo X alikuwa nani

Shahidi: Afande MSANGI

Malya: Mwingine nani

Shahidi: Ni huyo tu

Malya: Kumtukana Rais Mtandaoni ni Kuhatarisha Usalama wa Nchi

Shahidi: Hapana

Malya: Ugaidi ni Kuhatarisha Usalama wa Nchi

Shahidi: Ndiyo

Malya: Kwa sasa upo Ofisi ya RCO Temeke

Malya: Ni sahihi Kwa Mlalamikaji kuteua Mpelelezi Wangu

Shahidi: Hapana

Malya: katika kesi hii Mlalamikaji ni nani

Shahidi: Afande DCI

Malya: wewe alikuteua nani

Shahidi: Afande DCI

Malya: Kwa hiyo sisi haturuhusiwi Kuchagua Mpelelezi ila Kwa DCI analalamika na kuteua Wapelelezi

Shahidi: Kwa hili Mazingira ni tofauti

Malya: Ulimweleza Mheshimiwa Jaji Hayo Mazingira tofauti

Malya: Nilisikia Umeandika Barua Kwa DCI wakati huo Wambura Tarehe 18 July 2021

Shahidi: Ni sahihi

Malya: Wakati Unatoa Riport Kwa DCI ulikuwa unamdangamya au Ulikuwa serious

Shahidi: Nilikuwa Nipo Serious

Malya: Wakati Unaandika Ripoti kwa DCI Watuhumiwa Wengine Walikuwa tayari Upelelezi Wao tayari au bado

Shahidi: Ilikuwa tayari Katika Ripoti hiyohiyo

Malya: Wakati Unaandika Ripoti hiyo ya Kutaka Sasa Mbowe akamatwe ulikuwa na Ushahidi au Ulikuwa unataka Mbowe akae ndani Kidogo

Shahidi: Nilikuwa na Ushahidi Wa Kutosha

Malya: Mheshimiwa Jaji naomba Kielelezo D1

Malya: Tarehe 18 July 2021 umemuandikia DCI una ushahidi Wa Kutosha

Shahidi: Ndiyo

Malya: Ni sahihi Kwamba Maelezo Ya Justine Kaaya Uliyachukua Tarehe 30 July 2021 Kuhusu Ugaidi wa Mbowe Wakati huo Umeshamkamata Mbowe tayari

Shahidi: Ndiyo lakini, Huo ni Ushahidi Wa ziada

Malya: Una taarifa Mwaka huu Kuna Masoko yameungua

Shahidi: Ndiyo

Malya: na Moshi na Kwingine Kote Masoko yameungua

Shahidi: Ndiyo

Malya: Masoko hayo yameungua Wakati hawa wapo ndani, Mnasema Kwamba Walipanga Kuchoma,masoko, Je nikisema Yanaungua Sababu ya laana ya Kumsingizia Mbowe nitakuwa Nakosea

Shahidi: Ni Uongo, hilo ni Kosa Moja, lakini Wanashitakiwa na Makosa ya Kukata Miti Barabarani, Kupanga Njama za Ugaidi, Kutaka Kudhuru Viongozi

Malya: Wakati Unaandika Taarifa ya Kwenda Maabara Ya Kisayansi, Simu ya Kaaya na wenzake ulikuwa nazo

Shahidi: Ndiyo

Malya: Uliambatanisha katika Maombi ya Uchunguzi?

Shahidi: Hapana Walikamatwa baada ya Kuwapeleka hawa Mahakamani, Nilipeleka Simu za Watu wa tatu tofauti

Malya: Wakati Wa Ushahidi Wako Ulizungumzia hilo

Malya: katika Maelezo Ya Kaaya, Kaaya anasema alikuwa anapigiwa Simu na Mbowe

Shahidi: Sahihi

Malya: Je finding za Kaaya zipo hapa Mahakamani

Shahidi: Hapana

Malya: Ushahidi Wa Utaalamu Wa Uchaguzi wa Simu ya Kaaya Mnayo Jeshi la Polisi

Shahidi: Taarifa zimeanza Kufanya Tarehe 10 August 2020

Malya: Kwa hiyo Mbowe na Kaaya waliwasiliana baada ya hawa Mabwana Kukamatwa

Shahidi: Hakuendelea Kuwasiliana naye

Malya: Conlusion Naiachia Mahakama

Malya: Kuna Simu Ulipewa na IMEI namba yake Ilikuwa Imefutika

Shahidi: sahihi

Malya: Ulipewa Katika hali gani

Shahidi: Ikiwa Imezimwa na Ukiwasha inakuwa katika Flight Mode

Malya: Simu ya nani hiyo

Shahidi: Mohamed Abdilah Ling'wenya

Malya: Wakati Unakabidhwa Ulikuwa wapi

Shahidi: Nilikabidhiwa Nikiwa Katika Kituo Cha Polisi Kati Dar es Salaam

Malya: Umepewa su Ukaambiwa IMEI namba zake zimefutika, Wakati Unapewa simu ulikuwa wapi

Shahidi: Nilikuwa Ofisi Ndogo ya DCI

Malya: Ulikuwa na nani aliye shuhudia

Shahidi: DC Goodluck

Malya: Mohammed Ling'wenya alikwepo

Shahidi: Hakuwepo

Malya: Anita Mtaro

Shahidi: Hakuwepo

Malya: Esther Nduguuru

Shahidi: Hakuwepo

Malya: na Ukasema Ukabonyeza namba fulani fulani Ukapata Taarifa Uliyokuwa unatafuta katika Ile simu

Shahidi: Ni sahihi

Malya: turudi tena Pale Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam

Mallya: Ni sahihi Ulisema Kwamba siku ya Tarehe 07 August 2020 ulipigiwa Simu Kuwa Uje Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam

Shahidi: Ni sahihi

Malya: Ni sahihi Ulikabidhiwa Simu

Shahidi: Ni sahihi

Malya: Baada ya hapo Mlitoka Kwenda Sinza na Coco beach

Shahidi: Ni sahihi

Malya: Mpaka hapo Hukusema zile simu Ulihifadhi wapi

Shahidi: nilirudisha

Malya: Uliyasema hayo Wakati anakuongoza Kaka Yangu Kidando

Shahidi: Hapana

Malya: Vifaa Simu na Computer, Vilivyokamatwa Kuhusu Kesi hii Vilikuwa Vinakuja kwako

Shahidi: Siyo Sahihi

Malya: Unafahamu Kwamba Computer, Rooter za Watoto na Mke wake Vilikamatwa

Shahidi: Ni nacho fahamu Mimi, Mtuhumiwa alikamatwa na Simu na Laptop

Malya: Simu Ngapi

Shahidi: Si zaidi ya Moja

Malya: Aina gani ya Simu

Shahidi: Sikumbuki

Malya: Computer

Shahidi: Zaidi ya Moja

Malya: angalau zilikuwa Mbili

Shahidi: Sikumbuki

Malya: Vitu hivi ulipeleka wewe Maabara Ya Uchunguzi

Shahidi: Ndiyo

Malya: Wakati Wakili wa Serikali Robert Kidando anakuongoza ulitoa Ushahidi huo wa Kupeleka Vifaa hivyo

Shahidi: Hapana Sikusema

Malya: Uchunguzi huo unasemaje

Shahidi: Leo Ndiyo nimejulishwa kuwa Matokeo ya Uchunguzi yamekamilika

Malya: Kwa hiyo Leo Ndiyo Upelelezi Wa Kesi Ya Mbowe Umekamilika

Shahidi: Sahihi

Malya: Kuna tuhuma hapa, Line za Simu za Denis Urio hazifahamiki zilipo, Je Umepeleka Wapi

Shahidi: Zipo Katika Simu zake

Malya: Denis Urio alikuja hapa akawasha Simu zake akasema hazioni line zake, Kwa hiyo Jaji atapima Maelezo Yako wewe na Denis Urio

Malya: Ni sahihi Kwamba Madawa ya Kulevya yanaongeza hali ya uhalifu

Shahidi: Ni sahibi

Malya: Je Mbowe anaweza Kuwapa hawa Vijana Madawa ya Kulevya ili Wakafanye Uhalifu

Shahidi: Inategemea

Malya: Shahidi Je Tuhuma Za Ugaidi na Madawa ya Kulevya Yanaunganika.?

Shahidi: Inategemea

Malya: Ni sahihi Kwamba Kukuta kwa Madawa ya Kulevya Kungeweza Kuongeza Hali ya wao Kutenda Ugaidi Sasa

Shahidi: Madawa ya Kulevya hayahusiani na Ugaidi, Kwa sababu Ugaidi ni Kesi Nyingine na Madawa ni Kesi Nyingine

Malya: Kesi ya Madawa ipo wapi

Shahidi: Ilifunguliwa Moshi

Malya: Inaanza lini,kmi Wakili wake Adamoo ni jiandae

Shahidi: Siwezi Kufahamu

Malya: Wakati DC Goodluck anakukabidhi Vielelezo alikwambia anatoka wapi

Shahidi: alisema Anatoka Moshi

Malya: Kwamba alienda nazo Kwa Mama Mtilie Kunywa Supu na Kupiga Mswaki Hakukwambia

Shahidi: Hakuniambia

Malya: hivi Malalamiko kuja Kitengo X yalikuwa Ofisi za DCI ila wewe Ukaenda Kufungua Kesi Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam

Shahidi: Malalamiko yalianzia Kwa DCI

Malya: nani alisema Ukafungue Kesi Kituo Cha Polisi Kati Dar es Salaam

Shahidi: Ni Kingai

Malya: alikwambia kwanini hakukwambia Ukafungue Kituo cha Temeke au Oysterbay

Shahidi: Hakuniambia

Malya: Je angekwambia Ukafungue Oysterbay Ingekuwa Tofauti?

Shahidi: Kwa Nature ya Kesi Yenyewe Isingewezekana, Kwa sababu Kuna Mikoa inahusika

Malya: Kwa nini, Hamku Fungua Moshi, Kilimanjaro

Shahidi: Kwa Nature ya Offense Yenyewe

Malya: Je Kitengo X Kinaweza kutoa Amri kwa Polisi Wa Mkoa wa fulani Wamkamate Mtu fulani

Shahidi: Inawezekana

Malya: Tarehe 14 July 2020 Kidando alitoa Wapi hii Tarehe

Wakili Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Mimi nilikuwa nuongoza Shahidi, Sasa sijui wakili ana Lengo gani

Malya: Sawa Nitarudia Swali, Je Tarehe 14 July 2020 aliyokuwa anakuuliza alitoa wapi

Shahidi: Alitoa Kwangu

Malya: Maelezo Yako ninayo hapa, Hakuna Sehemu Umeandika Kuhusu Tarehe 14 July 2020

Shahidi: Ni sahihi Hakuna Tarehe 14 July 2020

Malya: huyu Mtu alitoa Wapi sasa hii Tarehe 14 July 2020

Shahidi: Mimi Ndiyo nimetoa wakati wa Kukumbushia Maelezo Yake

Malya: wewe Ulimweleza Mheshimiwa Jaji, kuwa Ulitoa wapi hizo Memory

Shahidi: Sikumueleza

Malya: Unasema Tarehe 07 August 2020 Kingai alikupigia Simu Kwamba Wale Watu weshapatikana

Shahidi: Ni sahihi

Malya: Maelezo Ya Kingai umeshawahi Kuyaona

Shahidi: Ndiyo Malya: Sasa....... Sauti ya Shahidi inamkatisha

Shahidi: MHESHIMIWA JAJI NAOMBA NIENDE WASHROOM (CHOONI)

Shahidi Karejea Malya: Je Shahidi Unajua Kuwa Kingai alipopata Taarifa

Shahidi: Nilikuwa najua

Malya: na Unaamini Kuwa alikuwa hadanganyi na Hamuonei Mbowe.. Simu ya nani ilikuwa Ina Coordinate

Shahidi: Simu ya Mbowe

Malya: kwenda Kwa nani

Shahidi: Kwa Luten Denis Urio

Malya: wale ambao Sasa Tarehe 14 mnaosema Kuwa Wale Watu wamepatikana, Je Hapa Mahakamani Wapo

Shahidi: Hawapo, Siku ambayo Luteni Denis Urio alikutana na Freeman Mbowe, Ndiyo Ulisoma Mbowe anasema Kwamba mimi na Chama Changu Chadema Kimedhamiria Kuchukua Nchi

Malya: kwa hiyo Kundi lake mlilofungulia Kesi ni Chama Chake

Shahidi: Sijui sasa Kama Chama Chake

Malya: Kwa hiyo hao anaosema Chama Changu wewe huwajui

Shahidi: Siwajui

Malya: Unafahamu Kwamba 2020 Ulikuwa Mwaka Wa Uchaguzi

Shahidi: Nafahamu

Malya: Unafahamu Kwamba Mbowe na Wenzake Walikuwa wanagombea nafasi Mbali mbali

Shahidi: Nafahamu

Malya: Je unafahamu Kwamba Vyama Vya siasa Vimeundwa Kwa Dhumuni la Kuchukua Dola

Shahidi: Ni sahihi kama utafuata Sheria

Malya: Ni sahihi Kwamba Vyama Vingine Vimeundwa kwa Lengo la kushiriki Uchaguzi la Kuchukua Dola

Shahidi: Lengo Kubwa la Chama ni Kuchukua Dola

Malya: Unafahamu Kwamba Mwenyekiti Freeman Mbowe ni Kiongozi wa Chama gani

Shahidi: CHADEMA

Malya: Chama Cha Mheshimiwa Mbowe Mwaka 2020 kilishiriki Uchaguzi au hakikushiriki

Shahidi: Kilishiriki

Malya: Wewe Kama Mpelelezi Uliwahi Kumuhoji Lengai Ole Sabaya

Shahidi: Sijawahi

Malya: Je Kama Hiyo Mipango Ingetimia angedhurika

Shahidi: Ndiyo

Shahidi: Malya hata Kingai Mwenyewe hajawahi Kumuhoji Sabaya

Shahidi: Hajawahi

Malya: hujawahi Kusikia Kauli ya Afande Siro Kwamba Kesi ya Kupigwa Risasi Tundu Lissu wanashindwa Kufanya Upelelezi Kwa sababu Wameshindwa Kumuhoji Lissu

Shahidi: Sijawahi Kusikia

Malya: haya Sabaya sasa ambaye ni Victim, hajawahi Kuhojiwa lakini Upelelezi Wake Umekamilika, Je hii siyo Double Standard?

Shahidi: Sabaya bado Siyo Victim

Malya: Kuna Mtu kapiga Risasi Upelelezi wake haujakamilika, lakini Kunatu hata hajaguswa na Upelelezi Umekamilika

Shahidi: Siwezi Kuzungumzia Suala ambalo sijapeleleza

Malya: Lengo la Kwenda Tigo na Airtel ilikuwa Kuleta Mahakamani kama ni kweli.?

Shahidi: Ni sahihi

Malya: Sasa Kilichokushinda Kuandika Barua Kwenda EWURA Kuthibitisha Kwamba kweli Kuna Kituo cha Mafuta oe Morocco

Shahidi: Sikuona haja hiyo

Malya: Je ulithibitisha Vipi Kama Kituo kama Kinauza Mafuta kweli, ulinunua hata Mafuta ya TSh 5000?

Shahidi: Hapana

Malya: haya Ulienda Kuthibitisha Masoko Katika Vyama Vya Ushirika kwa Kuandika Barua

Shahidi: Sikuona haja hiyo

Malya: Mimi nikibisha Kwamba Hakuna hayo Masoko sasa, Utathibitisha kwa Lipi

Shahidi: Kwa Ushahidi Wangu

Malya: Shahidi Mnataka Kujenga Picha Kwamba Mlifahamu Mbowe alitaka Kutenda Ugaidi na Nyie Mkamuwezesha Kufikia Lengo lake

Shahidi: Si Kweli

Malya: Kufanya Kikao cha Ugaidi ni Kosa au siyo Kosa?

Shahidi: Kosa

Malya: Kama Kukaa Kikao cha Ugaidi ni Kosa, Je hao waliokaa Kikao cha Ugaidi Walitoka wapi

Shahidi: Sifahamu

Malya: hao Watu ambao Mbowe anashitakiwa Kufanya nao Kikao cha, Mbowe aliwapata wapi

Shahidi: alitafutiwa kwa Lengo la Kuku Sanya Taarifa

Malya: Kwa hiyo Wakati Wanafanya Kikao Walikuwa wanafanya Ugaidi au Wanakusanya Taarifa

Shahidi: Walikuwa wameshashawishiwa

Malya: Kwani Kikao cha Ugaidi Walikuwa wamekaa Wapi na wakina nani

Shahidi: Washtakiwa wanne katika Hotel ya Aishi

Malya: Kwani Tarehe ngapi Walikuwa wamebadirika Kuwa Magaidi

Shahidi: Tarehe 25 July 2020

Malya: Swali langu Tarehe 20 July 2020 wakati wanatumiwa pesa Walikuwa Magaidi au siyo Magaidi

Shahidi: Hawakuwa Magaidi

Malya: Kama Mbowe Tarehe 20 July 2020 Mbowe anatuma Pesa Kwa Wale Watu zilikuwa Safi au Chafu

Shahidi: Ilikuwa Chafu kwa sababu Mbowe alikuwa anajua Lengo

Malya: na Muamala Wa Tarehe 22 July 2020 zile pesa ambazo Walitumiwa Siku hiyo na zenyewe Safi au Chafu

Shahidi: Pesa chafu

Malya: Tarehe 25 July 2020 Kama Wangekataa zile pesa Wangekuwa na Hatia

Shahidi: Wasingekuwa na Hatia

Malya: Mbowe Katika hicho Kikao cha Watu Wanne angekuwa amekaa Kikao cha Ugaidi au Siyo

Shahidi: Angekuwa amekaa Kikao cha Ugaidi

Malya: Je Shahidi Kama Upo Ofisini Kwako akasema anataka Kwenda Kuiba Benki, utakuwa na Wajibu wa Kuzuia au Utamuacha

Shahidi: Hilo haliwezekani, Mhalifu akupe Taarifa

Malya: Je nikija Kwako Kwamba nataka Kuiba Benki, Je utanizuia au Utaniacha

Shahidi: Nitakuzuia

Malya: Sasa DCI kapata Taarifa Kutoka kwa Luten Denis Urio (Msiri wake) kwamba Mbowe anataka Kufanya Uhalifu Wa Kigaidi, Je alikuwa ana wajibu wa Kuzuia au lah?

Shahidi: Ndiyo Maana alizuia

Malya: Vipi Kikao Kilifanyika au hakikufanyika.?

Shahidi: Kilifanyika

Malya: Sasa Luteni Denis Urio anasema alimpatia DCI Taarifa Kwamba Mbowe anatafuta Watu akae nao Kikao cha Kigaidi, lakini DCI Haku fanya lolote Kikao Kika fanyika, DCI katika hili hakuwajibika

Shahidi: Si Kweli

Malya: Unafahamu Kwamba Kuna Njia ya Kuweka Mamluki ambao Mtu anakuwa nao akizani ni wenzake halafu Kumbe wanatoa Taarifa

Shahidi: Nafahamu

Malya: Je Katika Ushahidi Wako Ulizungumzia Kuhusu Kuweka Mamluki au Kutokuweka

Shahidi: Sikueleza

Malya: Unasema Kwamba Mbowe alikaa Vikao Kuanzia May Mpaka July Kula Njama za Kutenda Ugaidi

Shahidi: Sahihi

Malya: Kuna sehemu Umetaja Vikao Vilifanyika wapi

Shahidi: Hapana

Malya: Wewe ndiye ulikuwa Mpelelezi Katika hili Shauri, Je wewe Uliwahi Kumwambia Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kuwa Kuna watu Wemeshafungwa katika Shauri hili

Shahidi: Sijawahi Kumwambia, Na Ndiyo nasikia Leo

Malya; Je Shahidi Unafahamu Kwamba Wakati Mheshimiwa Mbowe anakamatwa alikuwa Mwanza Katika Kongamano la Katika

Shahidi: Sifahamu

Malya: Kuna tuhuma dhidi yako Kwamba Ulipokuwa Tazara Ulishiriki Kumpiga, Kwa Kusema Mshusheni Chini tumshughulikie

Shahidi: Si Kweli, Mtuhumiwa Ni kutana naye Chang'ombe Polisi

Malya: Kwani Kituo cha Polisi Chang'ombe ni Cha Ghorofa

Shahidi: Hapana

Malya: Kwanini Sasa Useme Mshusheni Chini tumshughulikie

Shahidi: Si Kweli

Malya: Mheshimiwa Jaji naomba Kielelezo namba P 36

Malya: Unaulizwa Maswali na Wakili Msomi Nashon Nkungu Ulifanya Reference katika hii

Shahidi: Ndiyo

Malya: soma tena

Shahidi: Watakuwa tena na Safari ya kwenda Moshi Leo au Kesho Asubuhi

Malya: Kuna Meseji Yoyote inasema Kwamba Wamefika Hai

Shahidi: Hakuna

Malya: Mheshimiwa Jaji naomba nipatiwe Kielelezo P 15, 16, na 17

Malya: Ni Kuuliza Swali Mwanzo Kwamba wewe ni Mpelelezi Unaye Jipanga au Kukurupuka, Ukasema Unajipanga, Ni sahihi Kwamba Uliomba Taarifa za Namba 3

Shahidi: Ni sahihi

Malya: Ni sahihi Wakati Airtel wanajibu Walijibu namba 2

Shahidi: Ni sahihi

Malya: namba ipi Taarifa zake Zina Miss

Shahidi: Ni Namba 0782 237913

Malya: unataka Nikuulize Miamala ya Denis Urio, Wacha Nikuulize Shahidi

Mallya: Mheshimiwa Jaji namuuliza Extraction Ya Denis Urio, Kielelezo namba P 20, Mhamala Kutoka Kwa Wakala

Malya: Muamala Wa Tarehe 22 July 2020, TSh 199,000 imeingia

Shahidi: Ni sahihi Kuwa Mhamala Wa TSh 199,000 umeingia Kwenye namba ya Simu ya Luten Denis Urio

Malya: Unafahamu hii namba ya Chini Mhamala Wa TSh 7000 alipewa nani Kwenda namba 0787000027

Shahidi: Sifahamu

Malya: Shahidi Ulisema Kwamba Ulimruhusu Shahidi Kwa Sababu Hata Ulitoa line ya Simu Mawasiliano Yatabakia Kwenye Simu

Shahidi: Ndiyo

Malya: Unafahamu au Ulikuwa unajiongeza

Shahidi: Nilikuwa nafahamu

Malya: Mheshimiwa Jaji naomba Kielelezo P 22 Mpaka Kielelezo namba P 27 nimpatie Mtaalamu Wa Telegram

Malya: Nakuonyesha Kielelezo namba P 26, Kielelezo ameleta Bwana Ndowo

Shahidi: Nilicho kuwa nasema Mimi, Kwamba hata Ukitoa line Kwenye Simu bado Extraction Riport ya Simu na Simu Taarifa zitafanana

Malya: haya Namba ya Bwana Denis Urio katika Ripoti ya Bwana Ndowo Hebu itaje Sasa

Shahidi: 1130138344

Malya: Ulitoa Explanation Wakati Unaongozwa na Wakili Msomi Kidando, Kuhusu hii Variation iliyopo katika Simu na Extraction Riport

Shahidi: Sikutoa

Malya: Wewe na Goodluck Ndiyo Mlibadilishana Vielelezo, Je ulitoa Maelezo Kuhusu Mvunjiko vunjiko wa Simu pembeni Katika Kielelezo namba 27 na 35

Shahidi: Sikueleza

Malya: Ulihifadhi hizi Simu, Kuna simu iliwashwa Ilikuwa na Chaji na Zingine Hazikuwaka, Je Unaweza Kueleza Kwanini Simu Moja tu ya Denis Urio iliweza Kuwaka Hapa Mahakamani

Shahidi: Siwezi Kujua, mimi Nilikabidhi Siku Nyingi

Malya: Wewe lakini unatabia za Kuchungukia Simu za Watu, Unakumbuka ulichungulia Simu ya Ling'wenya

Shahidi: Siyo Kuchungulia, Bali niliangalia IMEI namba

Malya: Ni sahihi Kwamba hii namba ya Jalada la Kesi, Inawashtakiwa zaidi ya Hawa wanne

Shahidi: Ndiyo

Malya: Je Katika Wingi huo naweza Kutaja Kitu cha Mtu bila Kufafanua

Shahidi: kama Kuna Jina au Namba unaweza Kujua

Malya: Sasa Katika Maelezo Yako Kuna sehemu Unasema Pia Uchunguzi Wa Cyber Unaonyesha Waziwazi na Jinsi Mtuhumiwa Freeman Mbowe aliwaelekeza Wenzake Jinsi ya Kutekeleza Mipango yake

Shahidi: Ni sahihi

Malya: Sasa Umeonyesha Mahakamani Wakati Wa Ushahidi Wako Kuwa hapa Ndiyo alikuwa anawaelekeza Watuhumiwa Cha Kufanya

Shahidi: Ndiyo nimeonyesha

Malya: Ulipata Kujua Sasa Wakala aliyetuma Pesa ni Yupo wapi

Shahidi: Hapana

Malya: Umeeleza ni Wakala wa Mtandao gani

Shahidi: Kama Nilivyo Jibu awali, Sikueleza

Malya: Kuhusiana na Taarifa ya Ballistic, Ni kweli Wewe Ndiye uliyempa Ruhusa koplo Hafidh Kuharibu zile Risasi

Shahidi: Hakuziharibu alizichunguza

Malya: Ulipompelekea Wewe koplo Hafidh zile Risasi, zilikuwa ngapi

Shahidi: Zilikuwa Tatu

Malya: zilikuwa na Hali gani

Shahidi: Zilikuwa Moja ni Nzima na Mbili zilikuwa zimetumika

Malya: hizi Mbili ambazo ulipeleka zilikuwa Sawa na Wakati unazipeleka?

Shahidi: Zilikuwa katika Hali ya Kutumika

Wakili John Malya: Mheshimiwa Jaji Sina Swali la zaidi. Naomba Kurudisha Vielelezo

Wakili Fredrick Kihwelo: Mheshimiwa Jaji Tumebakia na Dakika 5 sababu ya Muda tunaomba airisho Kwa sababu hizo Dakika hazitoshi

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Hakuna Pingamizi

Jaji:Kufuatia Maombi yaliyoletwa na Wakili Wa Mshtakiwa Wa tatu, Juu ya Muda, Na-airisha Shauri Mpaka Kesho Saa 3 Asubuhi. Shahidi Naomba Kesho Tarehe 08 urudi Kutoa Ushahidi wako. Washtakiwa wataendelea Kuwa Rumande chini ya Magereza Mpaka Kesho Asubuhi Saa 3 Asubuhi.
Kumbe hii kesi wanajaribu kumwondoa Urio. Halafu Akina Khalidi, Kaaya na Gabriel Muhina wakfutiwa kesi baada ya kumaliza mchezo??
 
Nadhani huyu comte angependa Mbowe anyongwe kabisa.

Kwa ushahidi huu, ni wale "wanaoijua sheria tu" kama comte ndiyo wanaweza kusema Mbowe atakutwa na kesi ya kujibu. Sisi wengine tusioijua sheria, tusubiri tuone matokeo ya haya mapishi ya kina Kingai.
Kesi ililpikwa vibaya mpaka inakera. Risasi tatu zilikamatwa Pale Rau zikiwa nzima lakini mpaka zinafika Dar kwa Swila mbili zilitumika. Ikabaki moja. Sasa hao watuhumiwa walizitumiaje wakati walishang'anganywa?
 
Kesi ililpikwa vibaya mpaka inakera. Risasi tatu zilikamatwa Pale Rau zikiwa nzima lakini mpaka zinafika Dar kwa Swila mbili zilitumika. Ikabaki moja. Sasa hao watuhumiwa walizitumiaje wakati walishang'anganywa?
Mkuu- Sifa ya uongo ni kukosa kumbukumbu- risasi mbili zilitumiwa na mataalam wa milipuko aliyekuwa anajaribu kuona kama hiyo silaha ni nzima na alishatoa ushahidi huo mahakamani
 
DPP kakimbia kaacha vumbi tuuu, mapolisi waliomba kwenye haja kubwa bila aibu kwenye huu music
 
Back
Top Bottom