Yaliyojiri Mahakama Kuu: Mahakama yatupilia mbali mapingamizi ya Serikali dhidi ya Lissu, Shauri la msingi kuendelea kusikilizwa...

mwanamwana

JF-Expert Member
Aug 1, 2011
782
1,000
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam leo inatarajia kutoa uamuzi endapo maombi yaliyowasilishwa na aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu yanasifa ya kusikilizwa na Mahakama hiyo na kama aliyefungua kwa niaba yake anayo mamlaka ya kufanya hivyo.

Uamuzi unatarajia kutolewa leo mbele ya Jaji Sirilius Matupa,baada ya kusikiliza sababu nane za kupinga maombi hayo ambayo wanadai hayajakizi vigezo vitano kati ya sita.

IMG_20190826_143445.jpg

Kujua mapingamizi yaliyoibuliwa na Serikali, soma
https://www.jamiiforums.com/threads...i-yake-hayakidhi-matakwa-ya-kisheria.1620273/
Kujua kesi ilipoanzia, soma
https://www.jamiiforums.com/threads...-kutoa-uamuzi-siku-ya-agosti-23-2019.1617416/

***UPDATE***
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetupilia mbali mapingamizi ya Upande wa Jamhuri

Tundu Lissu ameshinda pingamizi la Serikali dhidi ya maombi yake ya kibali cha kufungua kesi kupinga kukoma kwa ubunge wake, Mahakama Kuu imekubali kusikiliza maombi yake

****
Zaidi, soma....

Dar es Salaam. Aliyekuwa mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), nchini Tanzania, Tundu Lissu ameshinda pingamizi la awali lililowekwa na Serikali dhidi ya maombi yake ya kibali cha kufungua shauri kupinga kukoma kwa ubunge wake.

Badala yake mahakama hiyo imekubali kuendelea na usikilizwaji wa maombi ya msingi ya Lissu.

Lissu ameshinda pingamizi hilo baada ya Mahakama Kuu Tanzani kutupilia mbali hoja za pingamizi hilo la Serikali na kukubaliana na majibu ya hoja hizo yaliyotolewa na jopo la mawakili wa Lissu, linaloongozwa na wakili Peter Kibatala.

Uamuzi huo umetolewa na Jaji Sirillius Matupa, leo Jumatatu, Agosti 26, 2019, baada ya kupitia na kuchambua hoja za Serikali za pingamizi hilo alilolisikiliza Ijumaa iliyopita ya Agosti 23,2019 na majibu na mawakili wa Tundu Lisuu, dhidi pingamiizi hilo.

Lissu amefungua maombi Mahakama Kuu, Masjala Kuu, Dar es Salaam chini ya hati ya dharura, kupitia kwa kaka yake Alute Mughwai, ambaye amempa mamlaka ya kisheria kufanya hivyo, ikiwa ni hatua ya awali kabisa ya kupigania kurudishiwa ubunge wake.

Katika maombi hayo namba 18 ya mwaka 2019, dhidi ya Spika wa Bunge la Tanzania na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Lissu anaomba kibali cha kufungau shauri la maombi maalum kwa lengo la kupata amri mbalimbali kuhusiana na uamuzi huo wa kuvuliwa ubunge.

Maombi hayo yalikuwa yamepangwa kusikilizwa juzi Ijumaa Agosti 23, 2019, lakini yalikwama baada ya Serikali kupitia kwa AG, ambaye ndiye mjibu maombi wa pili, kuibua pingamizi la awali akiiomba mahakama iyatupilie mbali maombi hayo bila hata kuyasikiliza.

Katika pingamizi hilo la awali, Serikali iliwasilisha jumla ya hoja nane, ikipinga kusikilizwa kwa maombi hayo kwa madai kuwa yana kasoro za kisheria. ambazo zilikuwa zimejikita katika masuala manne, manne kama yalivyobainishwa na Wakili Mkuu wa Serikali (Solicitor General –SG) Dk. Clement Mashamba

Kutokana na pingamizi hilo la awali, mahakama imelazimika kusimamishwa usikilizwaji wa maombi ya Lissu na kusikiliza kwanza, pingamizi hilo la AG, kama ulivyo utaratibu wa kawaida, ambalo lilisikilizwa mpaka saa mbili usiku.

Katika uamuzi wake le Jaji Matupa ametupilia mbali hoja za pingamizi la awali la Serikali isipokuwa hoja moja tu ya kasoro katika viapo vinavyounga mkono maombi ya Lissu.

Kutokana na kasoro hizo Jaji Matupa amesema inapotokea kuwa kuna aya zenye kasoro za kisheria namna pekee ni kuziondoa aya hizo katika kiapo hicho na kuangalia kama aya zinazobaki zinaweza kusimama na kuthibitisha maombi.

β€œNikiangalia hapa aya zinazobaki hapa baada ya kuziondoa hizo zenye kasoro, ninaridhika kabisa kuwa zinaweza kuthibitisha maombi.”, amesema Jaji Matupa na kuongeza:

Hivyo hoja zote za pingamizi la Serikali zimekataliwa isipokuwa hizo zenye upungufu kwenye hati za viapo. Ukiachilia mbali kasoro hizo za viapo, mambo mengine yote yataasikilizwa wakati wa usikilizwaji wa maombi ya msingi.”

Jaji Matupa amesisitiza kuwa pingamizi haliweza kuondoa haki za msingi kuwasikiliza wadaa kama kuna hoja za msingi za kusikilizwa.

Kuhusu hoja ya kusitisha kwa muda kuapishwa kwa mbunge mteule wa Singida Mashariki, Faraji Mtaturu, Jaji Matupa amesema kuwa sasa ni mapema mno kulitolea uamuzi na kwamba atalisikiliza ombi hilo wakati wa usikilizwaji wa maombi ya msingi.

Kwa sasa mawakili wa pande zote wamekutana kujadiliana kama wanaweza kuendelea na usikilizwaji wa ombi hilo la kusitishwa uapishwaji wa Mtaturu.

Lissu yuko nchini Ubelgiji, kwa ajili ya matibabu baada ya kushambuliwa kwa risasi na watu ambao hadi sasa hawajajulikana, tangu Septemba 7, 2017, aliposhambuliwa, katika makazi yake, jijini Dodoma akitokea bungeni.

Juni 28, 2019, wakati akiahirisha mkutano wa 15 wa BungeSpika Ndugai altangaza kukoma kwa ubunge wa Lissu, huku alijitetea kuwa si yeye aliyemvua ubunge bali ni matakwa ya Katiba ya Nchi.

Alitaja sababu za uamuzi huo kuwa ni kutokuhudhuria vikao vya bunge kwa muda mrefu bila kumjulisha Spika kwa maandishi mahali aliko na kutokuja taarifa za mali na madeni kwa mujibu wa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

Chanzo Mwanchi.
 
sweettablet

JF-Expert Member
Nov 16, 2014
5,296
2,000
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam leo inatarajia kutoa uamuzi endapo maombi yaliyowasilishwa na aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu yanasifa ya kusikilizwa na Mahakama hiyo na kama aliyefungua kwa niaba yake anayo mamlaka ya kufanya hivyo.

Uamuzi unatarajia kutolewa leo mbele ya Jaji Sirilius Matupa,baada ya kusikiliza sababu nane za kupinga maombi hayo ambayo wanadai hayajakizi vigezo vitano kati ya sita.

Kujua mapingamizi yaliyoibuliwa na Serikali, soma
https://www.jamiiforums.com/threads...i-yake-hayakidhi-matakwa-ya-kisheria.1620273/
Kujua kesi ilipoanzia, soma
https://www.jamiiforums.com/threads...-kutoa-uamuzi-siku-ya-agosti-23-2019.1617416/

***UPDATE***
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetupilia mbali mapingamizi ya Upande wa Jamhuri

Tundu Lissu ameshinda pingamizi la Serikali dhidi ya maombi yake ya kibali cha kufungua kesi kupinga kukoma kwa ubunge wake, Mahakama Kuu imekubali kusikiliza maombi yake
I like this court "technicality"!
 
Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
85,998
2,000
Hahaha idadi ya watetezi wa serikali haikutosha?! Nyani Ngabu uupate ujumbe huu popote ulipo.
Watu wako wanakata rufaa sasa.
Hilo shauri, kwa mtazamo wangu, lilikuwa ni shauri dogo na jepesi sana na nilitegemea liamuliwe kama lilivyoamuliwa.

Sasa kama kwenye shauri dogo la awali namna hii wanapeleka watu 16, je shauri la msingi litapoanza kusikilizwa, itakuwaje?

Watapeleka idara nzima?

They’re stupid.
 
Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Oct 20, 2014
6,804
2,000
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam leo inatarajia kutoa uamuzi endapo maombi yaliyowasilishwa na aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu yanasifa ya kusikilizwa na Mahakama hiyo na kama aliyefungua kwa niaba yake anayo mamlaka ya kufanya hivyo.

Uamuzi unatarajia kutolewa leo mbele ya Jaji Sirilius Matupa,baada ya kusikiliza sababu nane za kupinga maombi hayo ambayo wanadai hayajakizi vigezo vitano kati ya sita.

Kujua mapingamizi yaliyoibuliwa na Serikali, soma
https://www.jamiiforums.com/threads...i-yake-hayakidhi-matakwa-ya-kisheria.1620273/
Kujua kesi ilipoanzia, soma
https://www.jamiiforums.com/threads...-kutoa-uamuzi-siku-ya-agosti-23-2019.1617416/

***UPDATE***
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetupilia mbali mapingamizi ya Upande wa Jamhuri

Tundu Lissu ameshinda pingamizi la Serikali dhidi ya maombi yake ya kibali cha kufungua kesi kupinga kukoma kwa ubunge wake, Mahakama Kuu imekubali kusikiliza maombi yake
Zis iz interesting.
Kwa hiyo kwaya ya mawakili kwa kuanzia wamegaragazwa?
 
Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
6,934
2,000
halafu hizo kesi za huko nje bora ziendeshwe kwa kiswahili labda wanaweza wakachukua hata siku 2.
ikiwa kwa kiingreza tutapiwa nje ndani saa 3 asubuhi siku ya kwanza!!
Unaonaje wakimpa hizo kesi Tundu Lissu azisimamie!
Pamoja na kwamba huo utakuwa kama muujiza, lakini Tundu ni mTanzania na mzalendo kwelikweli; atapigana kufa kupona Tanzania yetu isipate hasara.

Mpe Tundu Lisuu aisimamie hiyo kesi akishirikiana na jopo lake la wasomi akina Kibatala. Hata Jiwe atafaidika kwa aina yake akifanya hivyo.
 
MISULI

JF-Expert Member
Jan 15, 2014
7,355
2,000
Kwa mikono yangu nmeshika forceps and clamps

Scalpels, (sutures, staples, glue etc)

Zlzotumika kwenye matibabu yake halafu unataka kuongea nini hapa

Hafu hujanijibu swali langu !

Badilika mkuu , na pia Muogope Mungu Wako
Kawaongopee wapuuz wenzio huko. Hakuna anayebisha kupigwa risasi, lkn kufanya exaggeration ya kwamba alipigwa risasi 16 mwilini ni UPUMBAVU.
 
kidamva

JF-Expert Member
Dec 3, 2013
2,584
2,000
Aliyekuwa mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu amewabwaga mawakili wa Serikali waliomwekea mapingamizi ya kufungua kesi ya kupinga kuvuliwa ubunge wake Leo mahakamani
IMG-20190826-WA0034.jpeg
 
Baba Swalehe

JF-Expert Member
Jun 6, 2017
16,396
2,000
Wewe ni MPUMBAVU KIWANGO CHA SGR, Usifikiri wote humu tuna akili za kushikiwa. Kama huna UWEZO WA kureason jambo jua ni MPUMBAVU. Hivi hujawahi kaa hata siku moja kujaribu kujenga kaclip ka mtu kupigwa risasi 16 na ukaona kama inawezekana?
Okay !
 
Nanye Go

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
6,043
2,000
Hilo shauri, kwa mtazamo wangu, lilikuwa ni shauri dogo na jepesi sana na nilitegemea liamuliwe kama lilivyoamuliwa.

Sasa kama kwenye shauri dogo la awali namna hii wanapeleka watu 16, je shauri la msingi litapoanza kusikilizwa, itakuwaje?

Watapeleka idara nzima?

They’re stupid.
Mashauri ya msingi yakianza sitashangaa nikisikia, jaji mkuu, jaji kiongozi, hadi DPP watajiunga upande wa utetezi.
That is who they are, ajira hizi wao wanasema easy money! As always it has been to them.
 
Ambiele Kiviele

JF-Expert Member
Dec 29, 2014
14,907
2,000
Huu uzi nimeupitia kila mahali ila hapa nime Ku quote

Sababu nimeheshim ichi ulicho andika

Respect sana Mh
Hilo shauri, kwa mtazamo wangu, lilikuwa ni shauri dogo na jepesi sana na nilitegemea liamuliwe kama lilivyoamuliwa.

Sasa kama kwenye shauri dogo la awali namna hii wanapeleka watu 16, je shauri la msingi litapoanza kusikilizwa, itakuwaje?

Watapeleka idara nzima?

They’re stupid.
 
Kekofya

Member
May 7, 2018
12
45
Iko wazi
Utakuwa ni ujinga kupoteza muda na gharama kwa mbunge mtoro!
Kumbuka hakufukuzwa bunge, alichofanya ni kutofuata utaratibu wa bunge kwa mujibu wa kanunu zao!
[/QQU] Kilichofanyika ni uhuni na uhalifu dhidi ya watu wa jimbo lake waliomchagua! Haiwezekani tupange foleni kumchagua Mwakilishi kwa maelfu ya makumi ili mlevi mmoja amfutie uwakilishi! Ni Uhaini!
 
Wyatt Mathewson

JF-Expert Member
Dec 22, 2017
9,034
2,000
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam leo inatarajia kutoa uamuzi endapo maombi yaliyowasilishwa na aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu yanasifa ya kusikilizwa na Mahakama hiyo na kama aliyefungua kwa niaba yake anayo mamlaka ya kufanya hivyo.

Uamuzi unatarajia kutolewa leo mbele ya Jaji Sirilius Matupa,baada ya kusikiliza sababu nane za kupinga maombi hayo ambayo wanadai hayajakizi vigezo vitano kati ya sita.

Kujua mapingamizi yaliyoibuliwa na Serikali, soma
https://www.jamiiforums.com/threads...i-yake-hayakidhi-matakwa-ya-kisheria.1620273/
Kujua kesi ilipoanzia, soma
https://www.jamiiforums.com/threads...-kutoa-uamuzi-siku-ya-agosti-23-2019.1617416/

***UPDATE***
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetupilia mbali mapingamizi ya Upande wa Jamhuri

Tundu Lissu ameshinda pingamizi la Serikali dhidi ya maombi yake ya kibali cha kufungua kesi kupinga kukoma kwa ubunge wake, Mahakama Kuu imekubali kusikiliza maombi yake
Weraweraaaaaaa

Mawakili 16 wamelishwa vumbi hatari sana!

Aibu sana aisee!

Nipo na opposition mpaka nitakapokufa!

Sasa,twende kesi ya msingi!

Namuonea huruma sana Spika na yule AG!
 
Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
35,319
2,000
Kawaongopee wapuuz wenzio huko. Hakuna anayebisha kupigwa risasi, lkn kufanya exaggeration ya kwamba alipigwa risasi 16 mwilini ni UPUMBAVU.
Hizi 16 ni Lissu kasema au madaktari waliomshughulikia?
Kwa hiyo kwa akili yako madaktari same exaggerate habari hiyo? Kwa manufaa ya nani? Jee Dodoma hospital, hospitali ya serikali hii na siku ile Katibu mkuu Afya alikuwepo nao ni waongo hakuna risasi Bali alipigwa na mawe?
MTU wa ajabu sana wewe!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom